Mbunge CCM akerwa na Kikwete kuwapa ulaji rafiki zake

We have to ask Hon. Kigwa, what is his priority? His party, his nation or his conscious?

Mwenyekiti JK anatakiwa arudi kuwa Mwana CCM kwa vitendo na sisi makada wenzake tumuone akifanya hivyo, si kutujazia watu wasiokijua chama wala wasio na machungu na chama, matokeo yake ni wao sasa kuwa wakamilishaji wa ndoto zao na familia zao, na wala si za chama hawana machungu hata kidogo na CCM,"
....angetakiwa kuchagua makada kutoka kwenye chama chake.....
... ili kilinde maslahi yake
.
Unaweza kuona kuwa anajaribu kuonyesha kuwa anaweka CHAMA mbele....
Kwa namna anavochanganya hoja injionyesha kuwa ni maslahi yake ndo kwanza, then yanafuata maslahi ya yeyote anayempa kula.
 
Dr. Kigwa atakuwa katumwa na mzee wa magogoni ili apate maoni ya wana JF. kama sio hivyo basi Dr. Kigwa sio raia kama ilivyokuwa kwa Bashe. Membe alishasema ubalozi una kigezo kimoja tu. ''INAVYOMPENDEZA RAISI'' Na sisi CCM Magamba wallishampa madaraka yote raisi sasa analalamika nini?
 
Dr. Kigwa atakuwa katumwa na mzee wa magogoni ili apate maoni ya wana JF. kama sio hivyo basi Dr. Kigwa sio raia kama ilivyokuwa kwa Bashe. Membe alishasema ubalozi una kigezo kimoja tu. ''INAVYOMPENDEZA RAISI'' Na sisi CCM Magamba wallishampa madaraka yote raisi sasa analalamika nini?


....Wanaweza kabisa kumwambia huyu kwamba sio raia, hivyo akaadhirika. Usicheze kabisa na magamba, chama twawala.
 
Ulilosema ni la kweli haya matamko hatukuyaona kipindi cha BWM, hapo kuna lao jambo na yanaonyesha ni chuki zaidi za kidini kuliko dhamira ya kweli ya kumkomboa mtanzania


tusiwe wavivu wa kufikiri. Hizi dini zipo siku zote tangu enzi za mwinyi?, kwani enzi za mzee ruksa yalikuwepo? Ama naye alikua mkristo? Tuwe wakweli, uongozi wa bwm na jmk ni vitu tofauti sana. Japo bwm naye hakuwa mkamilifu ila huyu amezidi kuharibu by far. Call a spade a spade bwn
 
Kikwete ashambuliwa
• Mbunge CCM akerwa kuwapa ulaji rafiki zake

na Mwandishi wetu
Tanzania Daima


MWENENDO wa uongozi wa serikali ya Rais Jakaya Kikwete umedaiwa kutowaridhisha Watanzania wengi na kwamba iwapo hakutachukuliwa hatua madhubuti za kurekebisha kasoro nyingi zilizopo, wananchi watapoteza matumaini.

Hayo yamebainishwa na Chama cha Wakristo Wanataaluma (CPT) katika tamko lao lililosambazwa kwa vyombo vya habari, ikiwa ni sehemu ya sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru zilizohitimishwa Desemba, 9 mwaka huu.

Wakati CPT ikibainisha hayo, Mbunge wa chama chake (CCM), Dk Hamis Kigwangala wa Nzega, amemshambulia akimtaka aache kuteua watendaji wa serikali kwa kuangalia urafiki na kwamba anashukuru Mungu hatagombea tena urais 2015, kwani kipindi chake kikatiba kitakuwa kimekwisha.

Kwa upande wao, wanataaluma wa CPT wamesema viongozi sharti waulizwe jinsi walivyotumia nafasi walizoaminiwa na watu, kwani mambo yanazidi kwenda hovyo ndani ya nchi.

Wakichambua hatua kwa hatua juu ya mwenendo wa utawala, wanataaluma hao wamedai kuwa taifa limekumbwa na mambo mengi ya kusikitisha na kufedhehesha.

Baadhi ya mambo hayo ni pamoja na kuzuka kwa tabia ya kulaumiana na kushutumiana baina ya makundi ndani ya vyama vya siasa, baina ya viongozi binafsi juu ya tabia mbaya na upotoshaji wa maamuzi miongoni mwao na kwa umma pasipo wahusika kuchukuliwa hatua au kuthibitisha ukweli na usahihi wa mambo.

Wamesema hatua hiyo ya kufumbia macho mambo imesababisha Watanzania wengi kukata tamaa na kujawa hofu kwa kujua kuwa hata kama kiongozi akifanya ovu la aina gani hakuna kitakachofanywa kudhibiti au kuwajibisha wahusika.

Wanataaluma hao wamesema hata hatua ya kukaa kimya kwa idara za serikali katika kufuatilia tuhuma za uhalifu mkubwa dhidi ya wenye madaraka, wakati taarifa zote za uhalifu zikiwa zimebainishwa, ni ukatili wa kimuundo dhidi ya wananchi.
Wameonyesha kuchukizwa kwao na suala zima la mchakato wa uundwaji wa Katiba lilivyopokewa na kutekelezwa katika namna ambayo haikuwafurahisha.
“Hivi karibuni tumeshuhudia mabishano makali bungeni juu ya kusomwa kwa muswada wa kuongoza mchakato wa uundaji wa Katiba mpya ya Jamhuri ya Tanzania. Masuala muhimu kwa uhai wa taifa kama hili la katiba si tukio la kubishania kisiasa -ni utovu mkubwa wa uwajibikaji na ni aibu kwa wahusika wote katika mchakato wa uundaji wa sheria mama ya nchi,” wamesema wanataaluma hao.

Aidha, CPT wamekosoa waziwazi uamuzi wa Ofisi ya Bunge kuongeza posho za vikao kwa wabunge na kudai kuwa hatua hiyo imewaudhi wananchi wengi.
“Vitendo vya kutumia pesa za walipa kodi kwa posho za vikao–kazi na kukirimiana bila kujali mahitaji ya msingi ya umma ni vya kuchukiza sana.

“Si wana CPT tu wasioridhishwa na uongozi wetu, pia Watanzania wengi wamepoteza imani kwa uongozi kutokana na matukio na mienendo mingi inayo shuhudia kasoro,” imesema sehemu ya tamko la wanataaluma hao.

Wameongeza kuwa hata kukosekana kwa uwazi na umakini katika usimamizi wa uchimbaji wa madini na kukataa kutekeleza mapendekezo ya kamati teule mbalimbali kwa masuala muhimu ya usimamizi wa mali za umma, ni ufujaji na usaliti wa mamlaka na dhamana ya uongozi.
“Cha kushangaza mno ni kwamba wageni wanapewa masharti na taratibu za upendeleo wa umiliki wa ardhi kuliko wazawa waliopigania uhuru wao ili wazipate fursa za maendeleo endelevu nchini mwao,” wamesema.

Waomba msaada kwa viongozi wa dini

Wanataaluma hao wamesema kuwa kwa vile viongozi wengi wa serikali wamewageuka wananchi walioahidi kuwapigania, wametoa ombi kwa viongozi mbalimbali wa dini kuungana kwa pamoja kupinga kila aina ya uovu unaowaumiza wananchi.

“Tunafahamu kuwa imani na dini nyingine zina misingi yao ya maadili inayofanana katika kupinga mienendo miovu katika jamii. Kwa unyenyekevu tunawaalika viongozi wa dini zote kuinuka na kubakia viongozi wa kiroho wakiunganisha nguvu zao na za kanisa, pamoja na wale wote walio na mapenzi mema na wazalendo, kusimama imara kiadilifu na kukemea kwa dhati maovu ya uroho na ubinafsi katika usimamizi na uendeshaji wa shughuli za utawala wa nchi yetu,” wamesema.
Wamewataka viongozi wa dini kutoruhusu nguvu za fedha za viongozi waroho ziwatawale katika utendaji kazi zao.
“Tafadhalini msiruhusu fedha na nguvu za kisiasa kuwatawala. Bakieni viongozi wa kiroho bila hofu ya uwezo wa kiulimwengu au kushawishiwa na mialiko ya wenye uwezo wa kidunia. Msiwaangushe waamini wenu.“Mwito wa uhuishaji wa maadili kitaifa unatolewa kwa dini zote na asasi za kijamii katika moyo wa kumpenda Mungu na jirani kwa kuweka mbele masilahi ya wote,” wamesema wanataluma hao katika tamko lao lililosainiwa na mratibu wa taifa, Mariam Kessy.

Mbunge CCM amshambulia

Kwa upande wake, Dk. Hamis Kigwangala, akichangia mjadala kupitia mtandao wa Wanabidii, kuhusu uteuzi wa mabalozi wapya, alimponda Kikwete kwamba amefanya uteuzi huo kwa kuzingatia urafiki zaidi, tena kwa watu wasio na uchungu na chama wala serikali.

“Tony, ni kweli. Mwenyekiti JK anatakiwa arudi kuwa Mwana CCM kwa vitendo na sisi makada wenzake tumuone akifanya hivyo, si kutujazia watu wasiokijua chama wala wasio na machungu na chama, matokeo yake ni wao sasa kuwa wakamilishaji wa ndoto zao na familia zao, na wala si za chama na serikali yao...hawana machungu hata kidogo na CCM,” alisema Dk. Kingwangala.

Kwa mujibu wa mbunge huyo, Rais Kikwete ameteua watu wa serikali wengi ambao hana uhakika nao kuhusu itikadi yao ya moyoni kama inaendana na ile ya CCM.

“Nadhani katika siasa za vyama vingi angetakiwa kuchagua makada kutoka kwenye chama chake. Nadhani tunalazimika kumwambia hilo. Katika competitive politics, ambapo chama kimoja kinaongoza serikali baada ya kushinda uchaguzi, ili kilinde maslahi yake, katika kuharakisha utekelezaji wa dhati wa sera za chama chake, inabidi itumike strategy moja muhimu na ya lazima sana inayoitwa 'Cadre deployment.'

“JK anakwamishwa sana kwa sabotage inayofanywa na watu aliowaweka kwenye nafasi nyeti serikalini, mashirika ya umma na wakala mbalimbali, watu ambao si wanasiasa ama makada wa chama chake! Hili ni kosa kubwa sana ambalo analifanya kila mara.

“Anafanya hivi eti kwa kuwaogopa CHADEMA na wanaharakati, ambao hata akiwasikiliza namna gani hakuna siku wamewahi kumkubali,” alisema mbunge huyo.

Dk. Kigwangala alienda mbali kwa kusema kuwa aina hii ya uteuzi unaofanywa na Rais Kikwete, imekuwa ikiwaudhi sana makada wa CCM na anashukuru Mungu kwamba mwaka 2015 hagombei tena, vinginevyo wangemyima uteuzi.

Mchangiaji mwingine anayependa kujitambulisha kwa jina la Tony, alisema wananchi wengi hivi sasa wamekata tamaa naye kabisa kwenye duru za siasa ndani ya chama na hata nje ya chama.

Tony ambaye hakujitambulisha itikadi yake, aliungana na Dk. Kigwangala kwa kusema kuwa serikali ya Rais Kikwete, imejaa watendaji wa Serikali badala ya wanachama wake.

“ Hata baraza la mawaziri limejaa watu waliopitia CCM badala ya wana- CCM. No wonder ndo maana baadhi yao hawajui hata jinsi ya kujibu tuhuma za wapinzani wake. It is very unconventional,” alisema.

Wiki iliyopita, Rais Kikwete alifanya uteuzi wa mabalozi wapya. Walioteuliwa ni pamoja watendaji wa serikali waliokuwa mawaziri wa awamu iliyopita, lakini walishindwa kwenye uchaguzi wa ubunge.
Walioteuliwa ni pamoja na Phillip Marmo, ambaye anakuwa Balozi wa Tanzania nchini China.
Kabla ya hapo Marmo alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge.

Mwingine ni Dk. Deodorus Kamala, ambaye anakwenda Ubelgiji. Kabla ya hapo Kamala alikuwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Dk. Batilda S. Burian, ambaye ameteuliwa kuwa Balozi nchini Kenya.
Kabla ya hapo, Burian alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira).

Wengine na nchi wanazokwenda kwenye mabano ni Ladislaus Komba (Uganda). Kabla ya hapo Dk. Komba alikuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii.
Shamim Nyanduga, (Msumbiji). Kabla ya hapo alikuwa Naibu Mkuu wa Itifaki, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano, Grace Mujuma, (Zambia), ambaye awali alikuwa Kaimu Mkurugenzi, Ushirikiano wa Kikanda (Regional Co-operation), Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Yumo pia Mohamed Hamza (Misri) ambaye awali alikuwa Mkurugenzi wa Mambo ya Nje, Zanzibar, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Ali A. Saleh (Oman).
Kabla ya hapo Saleh alikuwa Balozi Mdogo (Consul General) nchini Dubai. Uteuzi wa mabalozi hao walioapishwa juzi, ulianza Desemba 12, mwaka 2011.


h.sep3.gif

sitarajii positive altitude kutoka kwa hocho kinachoitwa --------kikristo kwa serikali ya kikwete. kwa hiyo kwwangu hiyo si habari kabisa. someni gazeti la mwananchi may 27, 2010, mchungaji mtikila alisema nini.
 
Kigwangala wiv tu unao msumbua

JK ni rais wa nchi na ni m/kiti wa chama tawala wanachama wote anawajua vizuri uwezo wao ndiyo maana anawateua na chama kinamuani vingivyo kingepitisha sheria ya wateule hao kuthitishwa kwanza ndipo waanze kazi

Hata JK hajaanza leo kuteua watendaji na yeye si wa kwanza wote walio mtangulia waliteua au imekuwa nongwa kwa JK tu sometime tuwe wakweli
Pengine kidogo enzi ya mzee Mwinyi kuliluwa na upendeleo fulani wa kidini lakini sio enzi ya Nyerere wala Mkapa; wao uteuzi wao haukuwa unalalamikiwa kwani hawakuwapa watu vyeo kwa sababu ya uswahiba au imani zao bali uwezo wao!! Mkweree kwa upande wake ametoa agizo kwa wasaidizi wake ambao wengi wao ni wa dini yake kuwa nafasi zipatikanapo katika serikali na mashirika ya umma waisilamu wapewe priority!!This speaks for itself I don't have to substantiate.
 
Huyu JK ndiyo zake kwa kuteua viongozi kwa kufuata uswahiba ni bingwa! tuvumilie tu jamani amalize muda wake ili atupishe,other wise nchi iko kwenye janga.
 
Kama hakuahidiwa, atakuwa amefanya lobbying ili ateuliwe kuwa balozi, sasa imekuwa kinyume na matarajio yake ndipo ameamua kusema yaliyo moyoni mwake.
Ama favour aliyopata wakati anawania ubunge imemlevya hata amesahau kwamba njia aliyopita hadi kufika hapo alipo ndio hiyo hiyo wanayopitishwa akina marmo, kamala na batilda.

Nyani haoni dudu lake.
 
Back
Top Bottom