Mbunge azuiwa kufanya ziara jimboni kwake!

tumpale

JF-Expert Member
Nov 20, 2010
200
35
Katika hali inayoshangaza mkuu wa wilaya ya mbarali amempiga marufuku mbunge wa jimbo la mbarali (ccm) kufanya ziara jimboni mwake, kisa amekuwa akiwatetea wananchi walioporwa ardhi na mwekezaji. Pia ccm mkoa wanapanga kumnyang'anya kadi yake ya uanachama. swali la kujiuliza mbona ni ngumu sana kuwaondoa mafisadi katika chama lakini ni rahisi sana kuwasulubu wanaojaribu kupigania maslahi ya watanzania?
 
Mkuu naomba utupatie source ya taarifa hizo. Lakini kama hizo habari ni za kweri basi jibu lakeni hili:

Ukiwa kondoo usikubali kuajiliwa na fisi, kazi ya kuuza nyama (Butcher). Akishikwa na njaa atakuja kula bila kulipa, maana yeye hajali swala la faida katika biashara hiyo, ila njaa yake tu. Ukijaribu kumshauli au kumzuia asile, basi lazima utafukuzwa. Hivi ni busara kuondoka, tena kwa kukimbia mapema, vinginevyo utaishia kuwa kitoweo pia.
 
hahaaaa CCM hivi mna chama au kijiwe cha wacheza draft.....hivi hiki chama kina mwenyekiti kweli hiki
 
Katika hali inayoshangaza mkuu wa wilaya ya mbarali amempiga marufuku mbunge wa jimbo la mbarali (ccm) kufanya ziara jimboni mwake, kisa amekuwa akiwatetea wananchi walioporwa ardhi na mwekezaji. Pia ccm mkoa wanapanga kumnyang'anya kadi yake ya uanachama. swali la kujiuliza mbona ni ngumu sana kuwaondoa mafisadi katika chama lakini ni rahisi sana kuwasulubu wanaojaribu kupigania maslahi ya watanzania?

Waache wawaondoe ili waje kwetu tuanhitaji watu kama hao na ccm si mahala pao.
Bila kujijua wanatusafishia njia ya 2015
 
kuna timu moja (SIO SIGARA) ilivuma sana kwa kuokoteza wachezaji waliokuwa maarufu kutoka timu nyingine....ilikuja itwa TANZANIA STARS na baadaye almaarufu KAJUMULO
Naifananisha na chama kimoja cha siasa
 
Kuwa kichaa si lazima uvute bangi
kuna timu moja (SIO SIGARA) ilivuma sana kwa kuokoteza wachezaji waliokuwa maarufu kutoka timu nyingine....ilikuja itwa TANZANIA STARS na baadaye almaarufu KAJUMULO
Naifananisha na chama kimoja cha siasa
 
Katika hali inayoshangaza mkuu wa wilaya ya mbarali amempiga marufuku mbunge wa jimbo la mbarali (ccm) kufanya ziara jimboni mwake, kisa amekuwa akiwatetea wananchi walioporwa ardhi na mwekezaji. Pia ccm mkoa wanapanga kumnyang'anya kadi yake ya uanachama. swali la kujiuliza mbona ni ngumu sana kuwaondoa mafisadi katika chama lakini ni rahisi sana kuwasulubu wanaojaribu kupigania maslahi ya watanzania?

Swala la source ni muhimu please!
 
Mbunge we una watu huko huko wilayani, DC ana rais na tena anakaa angani unashindwa ninin kutumia watu wako ili mlete maendeleo? Mbona karagwe dc alishawahi kuzuia mikutano ,mbunge akauitisha saa nane usiku na kuhutubia vijiji viwili? USIOGOPE jipe moyo.
 
Hiki ndicho chama tawala kinachotetea mafisadi tu lkn nbunge kuungana na wananchi wake anaambiwa ye ni mpinzani kwa ina maana hii nchi ni ya wageni na wawekezaji tu na si watz? Maana ukiwatetea watz basi we ni mchochezi haya ila ipo siku mamabo yatakuwa hadharani.
 
Mbunge we una watu huko huko wilayani, DC ana rais na tena anakaa angani unashindwa ninin kutumia watu wako ili mlete maendeleo? Mbona karagwe dc alishawahi kuzuia mikutano ,mbunge akauitisha saa nane usiku na kuhutubia vijiji viwili? USIOGOPE jipe moyo.

Una uhakika na unachokisema? Ni mbuge yupi, DC alikuwa nani na huyo mbunge alifanyisha mkutano katika vijiji viwili katika kata ipi na mwaka gani?
 
hivi mkuu wa wilaya ni bosi wa mbunge?
Sasa kwa nini sisi wananchi tusichague wakuu wa wilaya basi? Kuliko wabunge wasio na nguvu
 
Kimfumo, DC ni mwakilishi wa Rais (Head of State & Government) ngazi ya Wilaya. Anapeperusha bendera ya nchi. Kiutendaji, ana uwezo wa kumweka ndani kwa masaa kadhaaa mtu yeyote pamoja na wanaochaguliwa na wananchi, mfano Diwani na Mbunge. Mimi sijui kama ni boss kwa Diwani au Mbunge, lakini ninachojua DC na RC wana mamlaka makubwa kwa muundo wa Serikali yetu. The DCs and RCs are very powerful, but usually they don't exercise the powers vested in them.
 
Huyu anatakiwa kufukuzwa kwenye chama kwasababu anatekeleza sera za chama kingine sio kile kilicho mweka madarakani. Yeye atee wananchi , CCM watetee mafisadi wao tuone nani atashinda
 
kweli kabisa unayoyasem, maana hao wote si wateuliwa wa 'Bwana Mkubwa'? kwahiyo hawawezi kwenda kinyume na direction ya kiongozi wao. ulishaona kiongozi wao anafanya hayo wanayoyapinga?CHANGES MUST COME FROM OUTSIDE THE SYSTEM AND NOT FROM WITHIN
 
Back
Top Bottom