Mbunge awaangukia mafisadi

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,006
Nani anayewateua wabunge kama huyu wagombee ubunge? :confused:
Badala ya kutoa ushauri hao mafisadi wakamatwe na pesa zao zote zirudishwe hazina, yeye anawataka watumie pesa walizopata kiharamu kuwekeza!...ukistaajabu ya Mussa...

Mbunge awaangukia mafisadi

na Salehe Mohamed, Dodoma
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

MBUNGE wa Busega, Raphael Chegeni, amewataka watu wanaotuhumiwa kwa ufisadi wasifiche fedha walizo nazo nje ya nchi bali wazitumie kuwekeza katika miradi ya umeme ili kujinufaisha wao na wananchi wa Tanzania kwa ujumla.

Aidha, alisema inakadiriwa zaidi ya sh bilioni 900 zimeibwa na watu wenye kujali masilahi binafsi na kuziweka nje ya nchi au kuzitumia katika matumizi mbalimbali ambayo kwa kiasi kikubwa hayana manufaa kwa taifa.

Chegeni alitoa kauli hiyo alipokuwa akichangia muswada wa umeme wa mwaka 2007 uliowasilishwa juzi bungeni na Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja.

Alisema umeme ni muhimu kwa taifa la Tanzania ili liweze kupiga hatua za maendeleo hasa katika maeneo ya vijijini ambayo yana tatizo kubwa la ukosefu wa nishati hiyo.

“Naomba hawa wanaoficha fedha nje ya nchi wasifanye hivyo, waje hapa nchini kuwekeza katika miradi ya umeme ili nchi iweze kuendelea na wao waendelee pia,” alisema Chegeni.

Alisema hii ni nafasi kwa Watanzania kufanya mabadiliko ili waweze kujikwamua katika lindi la umaskini ambalo katika siku za hivi karibuni limeonekana kushamiri.

Mbunge huyo alisema imekuwa kama desturi kwa Tanzania kukopa fedha au kutegemea wahisani wakati kuna Watanzania wenye uwezo wa kuwekeza katika miradi hiyo, lakini wanaficha fedha zao nje ya nchi kwa sababu wanazozijua wenyewe.

Alisema kwa muda mrefu serikali imekuwa ikijitahidi kupeleka umeme vijijini bila mafanikio na hata wawekezaji waliokuja katika sekta hiyo nao inaonekana hawaoni umuhimu wa kupeleka miradi yao maeneo ya vijijini.

Chegeni alitumia fursa hiyo kuiponda Serikali kwa kuchangia kuliua Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (Tanesco) kwa kutolipa madeni inayodaiwa na shirika hilo.

Alisema serikali ndiyo iliyoingia mikataba mibovu ambayo inaifanya Tanesco kutumia fedha nyingi katika kulipa gharama za huduma kwa kampuni binafsi zinazozalisha umeme.

Kwamba kama Tanesco inatumia zaidi ya asilimia 90 ya mapato yake kuzilipa kampuni zinazozalisha umeme, itawezaje kujiendesha kwa faida na kufikia malengo yake?

“Tuwe wazi jamani, hivi ni nani ambaye ameifikisha Tanesco hapo ilipo kama si serikali na watu wake ambao walikuwa hawalipi umeme na wakati mwingine walikuwa wakitoa maamuzi ya kuliumiza shirika hilo?” alisema Chegeni.

Alisema viongozi wa serikali ni watu wa kushangaza, kwani utawala wa shirika hilo ulipokuwa wa Waswahili walikuwa hawalipi madeni yao lakini ulipokuja utawala wa Wazungu kutoka Afrika Kusini walianza kulipa baada ya kukatiwa umeme katika ofisi za serikali.

Aliitaka serikali kuwa makini na wawekezaji watakaokuja kuwekeza katika sekta ya umeme kwa vile kuna wawekezaji wa mikoba ya mkononi (briefcase) ambao wanakuja bila kitu lakini wanaondoka na faida nono kwa kufanya utapeli wakishirikiana na baadhi ya Watanzania.

Akichangia muswada huo, Mbunge wa Tunduru, Mtutura Abdala Mtutura (CCM), alisema muundo mbovu wa Tenesco, ndio uliolifikisha shirika hilo hapo lilipo, kwani lina wakurugenzi wengi kuliko inavyotakiwa.

Alifafanua kuwa shirika hilo lina uwezo wa kuzalisha umeme wa megawati 600 na lina wakurugenzi 21 wakati Shirika la umeme la Zambia (Zesco) lina uwezo wa kuzalisha umeme wa megawati zaidi ya 1,200 lakini lina wakurugenzi saba.

Aidha, Mtutura alisema shirika hilo linapoteza sh milioni 183 kwa mwezi kwa sababu ya wafanyakazi wake ambao ni zaidi ya 4,000, wanaolipia umeme senti 20 kwa uniti moja wakati wananchi wa kawaida wanalipa sh 165 kwa uniti moja.
 
kazi kwelikweli akinaziro 0% bado wapo; tena wabunge!! hiyo ndo Tz yetu na hao ndo wabunge wetu.
 
CCM , CCM, CCM .
Hivi hawa wanaitwa Chama Cha Mapinduzi , walifanya mapinduzi yapi ? Ama ndiyi haya ya kuweka pesa nje ?
 
yale yale ya kurudisha pesa za epa kimya kimya!

karibu tutaambiwa na kodi wasamehewe.
 
Hizo ni taktiki za kuanzia kuyanyamazisha mambo ,hivi hamuielewi CCM ,huyo jamaa ameweka cross au kona kiki ,sasa subirini hekaheka za jamaa kutaka kufunga goli.
 
"Alifafanua kuwa shirika hilo lina uwezo wa kuzalisha umeme wa megawati 600 na lina wakurugenzi 21 wakati Shirika la umeme la Zambia (Zesco) lina uwezo wa kuzalisha umeme wa megawati zaidi ya 1,200 lakini lina wakurugenzi saba"
 
Back
Top Bottom