Mbunge asema sheria ya ndoa ibadilishwe ili watoto waolewe, Je ni mawazo yake au katumwa?

Kweli siku hizi tuna wanawake na si wasichana, kama anabalehe ana miaka9 akija kufikisha umri wa mtu mzima 18 si anakuwa keshakuwa trench, amekongoroka? Ndo maana wanafanya umalaya wadogo kumbe na ukiviona navyo vinadai eti navyo vikubwa vyenzetu,kisa?

Tofauti na zamani 14-16.....humu ndani watu mnaongea kwa kutumia hisia hata bila kufikiria

Hvi mfano leo nikisema dini yangu inatambua ndoa ya mke/mme moja na si vingnevyo tatizo litakuwa ni langu ama ni dini yangu? Kama nanukuu biblia mie nina kosa gani?

Namaanisha tujifunze kujadili hoja badala ya kumuattack mleta hoja, hapa mbunge si hoja, hoja ni umri sahihi wa kuoa/kuolewa.
With all due respects Sir....would you please make or even force me to understand you on this thing.....?
Please I beg you...
 
Mkandara ni kweli hii hoja imetolewa leo Bungeni na mbunge (sikumbuki jina lake) wakati anachangia bajeti ya wizara ya sheria. Msingi wa hoja yake ni kwamba kwa Tanzania kutoruhusu uwepo wa mahakama ya kadhi waislam wanakosa haki zao. Na akataja baadhi ya hizo haki:

1. Kwamba katiba ya Tanzania inatoa umri wa mtoto kuoa na kuolewa kinyume na miongozo ya kiislam kwamba kwao mtoto akivunja ungo basi yu tayari kuolewa (horror!). Hivyo anaona kutoruhusu mtoto wa kike aolewe mara akivunja ungo sio sahihi !

2. Talaka - mwanaume anaweza toa talaka tatu kwa mke wake lakini kwenye mahakama zetu lazima afuate taratibu ambazo kimsingi zinatoa maelekezo ya sababu na process ya kutoa talaka. Kwenye hoja yake ilionekana kabisa kwamba mwaume ndio anakuwa na nguvu (kwa sheria za mahakama ya kadhi) ku-issue divorce & not the other way round!

Kwa ujumla kaongea mambo ya kustua sana ni afadhali kabisa hukuona live. Na kama wewe ni mzazi ungeugua kiharusi. shocking!
Hiyo yaweza kuwa kweli sio kweli bado ni hearsay! Hoja uangu naomba hansard tuone kasema nini?...Aliposema Waislaam Wa bara wanaonewa una maana Waislaam wa Zanzibar wanaruhusiwa?.. hadi hapa ni hearsay nataka nimsome mimi mwenyewe kasema nini huyo mbunge..

Besides, yawezekana kasema - mtoto akisha barehe anaweza kuolewa!..Kwa maana ya kwamba kipimo cha mtoto wa kike kuolewa kiwe kuvunja Ungo badala ya kutumia miaka. Kisha usipende sana kutazama sheria za wazungu ukaziweka zitumike kwetu kwa sababu wazungu wamesema... Kati ya watoto millioni mbili hadi tatu wanaojiunga na shule za msingi ni asilimia chini ya 30 humaliza masomo ya darasa la saba na asilimia zaidi ya 50 hushindwa kuendelea hadi sekondari..Kifupi, kielimu nchini ni asilimia ndogo sana hupata kuendelea na masomo na kibaya zaidi waathirika zaidi ni watoto wa kike. Sasa kama tunashindwa kutazama jinsi tunavyoshindwa kuwaendeleza watoto hao lakini wepesi wa sheria kuzuia ndio hayo yaliyopelekea Watu wa nyanda za juu kuwakeketa na kuwashona watoto wao wa kike wa miaka 3 hadi 4 wakifikiri ndio wanawalinda wasianze haya maswala mapema...

Ni muhimu sana kukatafuta njia bora ya kuwasaidia badala ya kufiiria tu kwamba miaka 9 na 14 wanatakiwa kuwa shule wakati hizo shule haziwezi kuchukua asilimia kubwa ya watoto haohao tunaowataka waende shule. It's very Okay kwa mswahili kwenda Corner bar na kutembea na mtoto wa miaka 14 lakini aibu kwa mtoto huyo huyo kuolewa! Huu ndio unafiki naozungumzia. Yes, hatuwezi kuweka sheria ya ndoa kwa watoto wakike wa miaka 9, 14 au 18 as a fact hatutakiwi kuweka sheria yoyote kuhusiana na umri wa ndoa kwa sababu hata miaka 18 au 20 inaweza kutokuwa sawa vile vile inategemea na case ya mwanamke na mwenyewe..

Katika mazingira tulokuwa nayo, ukuaji wa population, Inflation na umaskini unavyopelekea hali mbaya ya maisha ktk jamii nzima ya Kitanzania hasa kwa watoto wetu wa kike INATISHA tunaelekea wapi! sidhani kama hili mumewahi kulitazama kwa makini zaidi ya kusoma maandishi ya wazungu kuhusiana na mazingira yao..Muhimu kwetu ni kujiuliza tutafanya nini kuwasaidia waotot wa kike ambao maisha yanawalazimisha kufanya mambo mazito kuliko umri wao.. Tunaelekea kuwa Thailand ya Afrika na wala sii aibu tena kumwona mzungu miaka 50 au 60 akitembea na mtoto wa miaka 18 hadi 20 ati wapenzi.. Hakuna kitu hii Ulaya wala Amerika!

Majuzi nilivyokuwa Bongo nilishuhudia watoto wa shule wakikataliwa kuingia ktk Daladala, wenmgine wakiomba ride barabarani kwa watu wasiowajua, watoto wengine sidhani kama walifika shule...Maajabu ya Mungu basi ktk kila gari niloliona likipita almost all cars has one person driving tunashindwa hata kuwasaidia watoto hawa, tumeshindwa kuweka mabus ya shule na tunashindwa leo tunataka kuzungumzia sheria ya mambo ambayo hatuna kabisa uwezo nayo!!.

Kwa hiyo naomba tena hiyo hansard kwa sababu hapa JF watu wanaandika vitu kwa sababu wanajisikia tu kuuchukia Uislaam na sijui ndio fashion iloingia Bongo kuchukia Uislaam na kuulani ndoa zake wakati baba zenu wenyewe wana wake zaidi ya mmoja, mama zenu waliolewa wakiwa na umri wa miaka 15 au 16 na pia baba zenu wamezaa nje ya ndoa lakini husikii wakisema ndio Ukristu!.
 
Ndugu MKANDARA ukibaini kw haya maneno yoote ni kweli yamenenywa na yalitoka kwenye kinywa cha (mwislam)mwakilishi tk zanzibar utachukua hatua gani?
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Ndugu MKANDARA ukibaini kw haya maneno yoote ni kweli yamenenywa na yalitoka kwenye kinywa cha (mwislam)mwakilishi tk zanzibar utachukua hatua gani?
Swala sio mimi nitachukua hatua gani, bali nataka nimsome huyu mbunge kasema nini!.. Sitaki maelezo yako kwa sababu ulichosema hapo juu ndio kinanipa wasiwasi na hasa lengo lako kuanzisha mada hii?.
 
Kwa hiyo naomba tena hiyo hansard kwa sababu hapa JF watu wanaandika vitu kwa sababu wanajisikia tu kuuchukia Uislaam na sijui ndio fashion iloingia Bongo kuchukia Uislaam na kuulani ndoa zake wakati baba zenu wenyewe wana wake zaidi ya mmoja, mama zenu waliolewa wakiwa na umri wa miaka 15 au 16 na pia baba zenu wamezaa nje ya ndoa lakini husikii wakisema ndio Ukristu!.

Ndugu MKANDARA! Uovu ni uovu bila kujali kautenda nani na wapi! Uovu ni uovu bila kujali uliwahi kutendwa bila kuhojiwa! Endapo mama zetu walizaa wakiwa chini ya 15, haiondoi haki ya kulindwa kwa hao makinda na wajibu wa jamii kuwalinda.Suala hapa si uislam wala ukristo...baaadhi ya jamii zetu zinahalarisha kuoa watoto wadogo. Hizi zote lazima kupingwa kwa nguvu zote. Kwa bahati mbaya anayetoa mtizamo wa aina hii ni kiongozi mwenye dhamana ya kutetea wananchi pamoja na hao under 18! Jambo la kujiuliza hapa, vipi kama angekuwa binti yako ungemkimbiza kumpeleka kwa bwana au unampeleka shule? Nijuavyo mimi, kwa bahati mbaya sana jamii zote (waislam, wakristo na makabila mbali mbali), ukimkuta mtu anashabikia binti yake mwenye 9-14kuolewa, angalia hali ya kipato chao! Angalia kiwango cha uelewa wao! NAKWAMBIA HUYO MBUNGE ATAKUPELEKA MAHAKAMANI AKIKUKUTA UMESIMAMA NA KABINTI KAKE KWENYE KONA YA GIZA, SEUZE KUPROPOSE KUOA? TUACHE UNAFIKI, TUWALINDE WATOTO WA KIKE, NA HASA WANAOTOKA JAMII MASIKINI,VINGINEVYO KWA USHABIKI HUU TUNAENDELEZA UBAGUZI...WA KIUCHUMI TUKIWADIDIMIZA WALE AMBAO TAYARI MAISHA YAMEWAPIGA TAYARI
 
Hata mimi leo hawa wabunge wa Zanzibar wameniacha hoi, kama kuna yule mbunge mmoja alikua akichangia kuhusiana na kiwango cha malipo kwa mahakimu pamoja na mawakili akasema eti ukiwaangalia majaji wamekondeana miguu eti miguu yao midoooogo halafu eti wamepinda mpaka wanavibiongo kwakuperuzi sheria! halafu akasema hata jaji haulipwa mshahara kidogo atashindwa hata kuoa mzungu! Aisee hawa ndugu zetu wanaviswahili vyaajabu.
<br />
<br />
Mkuu me pale nilijiuliza kwa zile kauli zake,alikuwa anawatetea au alikuwa anawatukana?eti miguu imekondeana halafu vinumbu vimeshuka chini.
 
Ndugu zangu waislam huwa wanalalamika kuwa wakristo wanapendelewa katika masuala ya maendeleo, mfano shule, ajira n.k.! Hivi kwa hii hoja ya huyu mbunge (sijui ni wa chama gani) kuna mtoto wa kike wa kiislamu anayeweza kufanya maendeleo yoyote? Mbona tunataka kurudishana nyuma jamani?
 
Hivi ndivyo dini yake inavyomtaka au ni mawazo yake?

lakini pia unajua hili linchi halina dini, huo mchango wa huyo mama ni utumbo wa kuku.
 
Swala sio mimi nitachukua hatua gani, bali nataka nimsome huyu mbunge kasema nini!.. Sitaki maelezo yako kwa sababu ulichosema hapo juu ndio kinanipa wasiwasi na hasa lengo lako kuanzisha mada hii?.
<br /> <br / nakutoa wasiwasi kw ni kweli kbs kw mbunge hy anataka sheria ya ndoa ibadilishwe ili mtoto akipevuka aruhusiwe kuoa/kuokewa na lengo langu la kuanzisha mada hii ni kutaka kujua mawazo ya wana jf kuhusu mbunge hy kw ametumwa awanenee waislamu wa bara? Na je kauli yk ni sahihi? NAKUOMBA WEKA UDINI PEMBENI TUJADILI HOJA YA MSINGI IWE RUKSA MTOTO KUOA/KUOLEWA PUNDE TU ANAPOPEVUKA?
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Huyo mbunge inabidi akapimwe masaburi yake, siyo kichwa maana anafikiri kutaka kwenye hayo masaburi ukipima kichwa anaweza kuwa fit lakini tatizo litakuwa kwenye hayo makalio anayotumia kufikiri
 
[/COLOR]Ndugu MKANDARA! Uovu ni uovu bila kujali kautenda nani na wapi! Uovu ni uovu bila kujali uliwahi kutendwa bila kuhojiwa! Endapo mama zetu walizaa wakiwa chini ya 15, haiondoi haki ya kulindwa kwa hao makinda na wajibu wa jamii kuwalinda.Suala hapa si uislam wala ukristo...baaadhi ya jamii zetu zinahalarisha kuoa watoto wadogo. Hizi zote lazima kupingwa kwa nguvu zote. Kwa bahati mbaya anayetoa mtizamo wa aina hii ni kiongozi mwenye dhamana ya kutetea wananchi pamoja na hao under 18! Jambo la kujiuliza hapa, vipi kama angekuwa binti yako ungemkimbiza kumpeleka kwa bwana au unampeleka shule? Nijuavyo mimi, kwa bahati mbaya sana jamii zote (waislam, wakristo na makabila mbali mbali), ukimkuta mtu anashabikia binti yake mwenye 9-14kuolewa, angalia hali ya kipato chao! Angalia kiwango cha uelewa wao! NAKWAMBIA HUYO MBUNGE ATAKUPELEKA MAHAKAMANI AKIKUKUTA UMESIMAMA NA KABINTI KAKE KWENYE KONA YA GIZA, SEUZE KUPROPOSE KUOA? TUACHE UNAFIKI, TUWALINDE WATOTO WA KIKE, NA HASA WANAOTOKA JAMII MASIKINI,VINGINEVYO KWA USHABIKI HUU TUNAENDELEZA UBAGUZI...WA KIUCHUMI TUKIWADIDIMIZA WALE AMBAO TAYARI MAISHA YAMEWAPIGA TAYARI[/B]
Nakubaliana na wewe ktk mtazamo wako lakini mweka mada hii namjua ni mdini kupita maelezo..Hachangii kitu isipokuwa kwa rangi na ushabiki wa Kidini..

Lakini lazima ifahamike kwamba Bungeni wabunge wanakuja wakilisha waanchi wa jimbo lake sii kwa sababu ya dini zaoi bali maslahi ya wahusika..Na huwezi kusema UOVU ni UOVU ili hali watu tunakwenda vitani kupigana vita wakati dini inatukataza kuua, hapa sijui Uovu ni upi na Uhalali ni Upi..

Mimi nimezungumza hili kwa ujumla wake kwamba tunapozungumzia habari za ndoa ni maswala ya tamaduni za wahusika na hatuwezi kuiga sheria za Ulaya ili kuhalalisha kitu au kikifanya haramu isipokuwa sheria zetu zitawalinda watu kutokana na athari zitokanazo..Ulaya leo hii sii lazima watu wa jinsia moja kufunga ndoa hivyo huwezi kulazimisha tamaduni hiyo ktk jamii yetu kwa sababu tu Ulaya wameona uhalali wa jambo hilo..

Na ndio nikasema kwamba sioni makosa ya mbunge au mtu yeyote atakayesema wanawake waruhusiwe kuolewa wakisha vunja ungo pamoja na kwamba ni umri unaotakiwa mtoto awe shuleni... Na sababu kubwa ilonifanya niseme hivyo ni kwamba asilimi zaidi ya 50 ya watoto wetu wa kike leo hii hawapo shuleni kutokana na uwezo mdogo wa shule, walimu, fedha na kadhalika. Hivyo kuwalazimu pasipo hiari yao kuingia ktk Umalaya au kuzaa hovyo nje ya ndoa kwa sababu wanatafuta rikizi kwa njia nyinginezo..

La muhimu kwetu ni kutazama uwezo wetu kwa asili zaetu jinsi ya kuwasaidia hawa watoto wa kike ambao tumewaruhusu kurudi shule baada ya kuzaa lakini matokeo yake leo hii asilimia kubwa ya watoto miaka 16 wanashika mimba wakijua wataweza kurudi darasani.. Hapa tumewasaidia wao watoto wa miaka 16 lakini tumewasahau watoto waliozaliwa ambao ktk makuzi yao watakosa huduma ya mama.. tatizo ni kwamba tutnatazama upnade mmoja tu wa shilingi, na kibaya zaidi ni sheria zinazotungwa na Mwanamme...

Mwisho kama huna jibu la hoja ilowekwa ubaoni ni bora kaa kimya kuliko kuchangia mada ili hali unachotafuta ni kulaumu dini au mtoa hoja wakati wewe mwenyewe huna jibu wala suluhisho..Sasa unaposema tuwalinde hawa watoto wadogo unawalinda vipi kwa kuweka sheria hali huna suluhu ya umaskini wao! Kuna mlinzi mkubwa zaidi ya Mungu ambaye yeye mwenyewe kamtoa stage moja kuingia nyingine?...Haya sawa leo watoto hawaolewi chini ya miaka 18 lakini mbona malaya wengi mjini ni hao hao tulowalinda jana kwa sheria lakini hukuboresha maisha yao?. Tufikirie zaidi kuboresha maisha ya watoto wetu hili swala la ndoa litajirekebisha lenyewe. Ulaya siku hizi wanawake hawataki hata kuolewa kabisaaa, wengine wanaolewa wakiwa na umri wa miaka 30 kwa sababu wamewezeshwa kupata elimu, ajira na uwezo wa kijitegemea na sii hadithi tupu..Ni asilimia chini ya 10 ya watoto wao wa KIKE hushindwa kuendelea na masomo kwa hali hiyo huwezi kulinganisha na asilimia 70 ya watoto wetu wa KIKE wanaoshindwa kuendelea na masomo..
 
&lt;br /&gt; &lt;br / nakutoa wasiwasi kw ni kweli kbs kw mbunge hy anataka sheria ya ndoa ibadilishwe ili mtoto akipevuka aruhusiwe kuoa/kuokewa na lengo langu la kuanzisha mada hii ni kutaka kujua mawazo ya wana jf kuhusu mbunge hy kw ametumwa awanenee waislamu wa bara? Na je kauli yk ni sahihi? NAKUOMBA WEKA UDINI PEMBENI TUJADILI HOJA YA MSINGI IWE RUKSA MTOTO KUOA/KUOLEWA PUNDE TU ANAPOPEVUKA?
<br />
<br />
mi naona tupinge na kuchukia ndoa za watoto kama tunavyopinga na kuuchukia ushoga! maana vyote ni sawa tena heri ushoga mtu anafanya kwa kujitambua na si watoto wa watu ambao hata akili zao hazujapevuka
 
@Mkandara, with all due respect, I have to say majibu yako ni total nonsense & irresponsible!

Watu wanasoma ili watumie elimu kuboresha maisha yao. Yes, wapo ambao kwa sababu mbalimbali hawakupata/hawatapata elimu either ya msingi na hata elimu ya juu. Lakini kwa vizuri (kama si wajibu wa binadamu) kwa wale waliopata elimu wakaitumia elimu hiyo kusaidia na wengine including those ambao hawakupata elimu.

Inawezekana hoja yako kuhusu kuolewa wewe unachukulia kama mambo ya umri ni 'kuletwa na wazungu etc. Kwa hivyo unaona sahihi mtoto wa miaka 10 ambaye kwa bahati mbaya haendi shule aolewe? Soma vizuri hapo kwenye red uone ulichoandika maana inaonekana unataka kuonesha kuwa wewe you are so very passionate about Africa coming up with an original idea maybe?

Ni hivi majuzi nimetoka kutembelea wamama wanafanyiwa upasuaji kwa sababu ya FESTULA. Hivi unajuwa madhara ya kiafya kwa mtoto kama wa miaka 10 kuingiliwa na mtu wa miaka 30! unajuwa au unaongea? Na wengi wa watoto wanaokumbwa na mikasa kama hii ya early marriages hawana sautu maskini ya mungu. Kwa nini kwa mtu kama wewe uliyesoma utumie elimu yako kusaidia watoto wasiingizwe kwenye mikasa kama hii? Kuna haraka gani? Tunaposema kuwa hatuko kwenye zama za ujima ni kwa sababu tumeelika na kuboresha maisha tofauti na enzi hizo. So hoja kwamba wazazi wetu walituzaa wakiwa na miaka 15 haina maana kuwa tuendelee na huo utamuduni mbovu. Unataka kuturudisha huko kwa sababu kuna report inasema 50% ya watoto wanashindwa kuendelea na sekondari?

Pia hoja kwamba kuna watu wazima wanatembea na watoto wadogo - definately hilo ni kosa na ndio maana wengi wanafanya kwa kujificha. Lakini kuhalalisha haramu hii ndio kosa kubwa zaidi maana itawaondelea watoto wasio na sauti haki yao. I just hope siku ukiwa na mtoto wa kike (kama bado hauna) hautamwoza mara akivunja ungo.

Kuhusu kuwa unataka Hansard ili uamini, kwanza hulazimishwi kuamini walichoandika watu hapa. na kama unataka sana hiyo Hansard just GOOGLE Bunge and ask them to sort you out. Siku zote umekuwa unachangia kwa hoja tena nyingi tu bila kudai Hansard, why today?

Hiyo yaweza kuwa kweli sio kweli bado ni hearsay! Hoja uangu naomba hansard tuone kasema nini?...Aliposema Waislaam Wa bara wanaonewa una maana Waislaam wa Zanzibar wanaruhusiwa?.. hadi hapa ni hearsay nataka nimsome mimi mwenyewe kasema nini huyo mbunge..

Besides, yawezekana kasema - mtoto akisha barehe anaweza kuolewa!..Kwa maana ya kwamba kipimo cha mtoto wa kike kuolewa kiwe kuvunja Ungo badala ya kutumia miaka. Kisha usipende sana kutazama sheria za wazungu ukaziweka zitumike kwetu kwa sababu wazungu wamesema... Kati ya watoto millioni mbili hadi tatu wanaojiunga na shule za msingi ni asilimia chini ya 30 humaliza masomo ya darasa la saba na asilimia zaidi ya 50 hushindwa kuendelea hadi sekondari..Kifupi, kielimu nchini ni asilimia ndogo sana hupata kuendelea na masomo na kibaya zaidi waathirika zaidi ni watoto wa kike. Sasa kama tunashindwa kutazama jinsi tunavyoshindwa kuwaendeleza watoto hao lakini wepesi wa sheria kuzuia ndio hayo yaliyopelekea Watu wa nyanda za juu kuwakeketa na kuwashona watoto wao wa kike wa miaka 3 hadi 4 wakifikiri ndio wanawalinda wasianze haya maswala mapema...

Ni muhimu sana kukatafuta njia bora ya kuwasaidia badala ya kufiiria tu kwamba miaka 9 na 14 wanatakiwa kuwa shule wakati hizo shule haziwezi kuchukua asilimia kubwa ya watoto haohao tunaowataka waende shule. It's very Okay kwa mswahili kwenda Corner bar na kutembea na mtoto wa miaka 14 lakini aibu kwa mtoto huyo huyo kuolewa! Huu ndio unafiki naozungumzia. Yes, hatuwezi kuweka sheria ya ndoa kwa watoto wakike wa miaka 9, 14 au 18 as a fact hatutakiwi kuweka sheria yoyote kuhusiana na umri wa ndoa kwa sababu hata miaka 18 au 20 inaweza kutokuwa sawa vile vile inategemea na case ya mwanamke na mwenyewe..

Katika mazingira tulokuwa nayo, ukuaji wa population, Inflation na umaskini unavyopelekea hali mbaya ya maisha ktk jamii nzima ya Kitanzania hasa kwa watoto wetu wa kike INATISHA tunaelekea wapi! sidhani kama hili mumewahi kulitazama kwa makini zaidi ya kusoma maandishi ya wazungu kuhusiana na mazingira yao..Muhimu kwetu ni kujiuliza tutafanya nini kuwasaidia waotot wa kike ambao maisha yanawalazimisha kufanya mambo mazito kuliko umri wao.. Tunaelekea kuwa Thailand ya Afrika na wala sii aibu tena kumwona mzungu miaka 50 au 60 akitembea na mtoto wa miaka 18 hadi 20 ati wapenzi.. Hakuna kitu hii Ulaya wala Amerika!

Majuzi nilivyokuwa Bongo nilishuhudia watoto wa shule wakikataliwa kuingia ktk Daladala, wenmgine wakiomba ride barabarani kwa watu wasiowajua, watoto wengine sidhani kama walifika shule...Maajabu ya Mungu basi ktk kila gari niloliona likipita almost all cars has one person driving tunashindwa hata kuwasaidia watoto hawa, tumeshindwa kuweka mabus ya shule na tunashindwa leo tunataka kuzungumzia sheria ya mambo ambayo hatuna kabisa uwezo nayo!!.

Kwa hiyo naomba tena hiyo hansard kwa sababu hapa JF watu wanaandika vitu kwa sababu wanajisikia tu kuuchukia Uislaam na sijui ndio fashion iloingia Bongo kuchukia Uislaam na kuulani ndoa zake wakati baba zenu wenyewe wana wake zaidi ya mmoja, mama zenu waliolewa wakiwa na umri wa miaka 15 au 16 na pia baba zenu wamezaa nje ya ndoa lakini husikii wakisema ndio Ukristu!.
 
mkandara nakuona umeelemea kwenye udini zaidi na kwa kukusaidia 2 ni kuwa huwezi kuijadili hoja hii bila kueleza aliyenena maneno hayo ni nani, na aliwanenea akina nani? Aliyenena maneno haya ni mwakilishi(muislamu) tk zenji na alinena kwa kuwajumlisha waislamu wote. Ndo mana nikauliza je alitumwa awanenee hayo au aliamua kuwanenea bila kutumwa? na wala kwenye swala hl uislamc wakujadiliwa sn cha kujadiliwa ni huo umri wa watoto kuolewa/kuoa je ni sahihi? mm ni muislam swafii lkn kamwe siwez unga mkono upuuzi km huu kwani sitapenda kuona mtoto akiolewa.
 
Nbunge/mwakilishi ktk Zanzibar amelalamika kuwa Waislam wa bara wananyanyaswa ....
Haya ndio Tundu Lissu kayasema jana kuhusu kuingiliwa na Wazanzibar.

Wewe Mbunge wa Zanzibar, ndoa sio suala la Muungano, yanakuhusu nini haya? Kazi kuchokoa ya wengine kwani mwachokoa pweza hapa? Unataka kuoa vitoto vya Bara, huko kwenu vimeisha? Maana mtu mmoja anaruhusiwa kuoa up to vitoto vinne, mmevimaliza huko visiwani sasa mwataka na vya Bara? Ndio hizi faida za Muungano, kuoa na kuoleana vitoto vya shule?

I am sick to my stomach with this Zanzibar business, disappear to the middle of the Indian Ocean like Nyerere wished. Please!
 
@Mkandara, with all due respect, I have to say majibu yako ni total nonsense & irresponsible!

Watu wanasoma ili watumie elimu kuboresha maisha yao. Yes, wapo ambao kwa sababu mbalimbali hawakupata/hawatapata elimu either ya msingi na hata elimu ya juu. Lakini kwa vizuri (kama si wajibu wa binadamu) kwa wale waliopata elimu wakaitumia elimu hiyo kusaidia na wengine including those ambao hawakupata elimu.

Inawezekana hoja yako kuhusu kuolewa wewe unachukulia kama mambo ya umri ni 'kuletwa na wazungu etc. Kwa hivyo unaona sahihi mtoto wa miaka 10 ambaye kwa bahati mbaya haendi shule aolewe? Soma vizuri hapo kwenye red uone ulichoandika maana inaonekana unataka kuonesha kuwa wewe you are so very passionate about Africa coming up with an original idea maybe?

Ni hivi majuzi nimetoka kutembelea wamama wanafanyiwa upasuaji kwa sababu ya FESTULA. Hivi unajuwa madhara ya kiafya kwa mtoto kama wa miaka 10 kuingiliwa na mtu wa miaka 30! unajuwa au unaongea? Na wengi wa watoto wanaokumbwa na mikasa kama hii ya early marriages hawana sautu maskini ya mungu. Kwa nini kwa mtu kama wewe uliyesoma utumie elimu yako kusaidia watoto wasiingizwe kwenye mikasa kama hii? Kuna haraka gani? Tunaposema kuwa hatuko kwenye zama za ujima ni kwa sababu tumeelika na kuboresha maisha tofauti na enzi hizo. So hoja kwamba wazazi wetu walituzaa wakiwa na miaka 15 haina maana kuwa tuendelee na huo utamuduni mbovu. Unataka kuturudisha huko kwa sababu kuna report inasema 50% ya watoto wanashindwa kuendelea na sekondari?

Pia hoja kwamba kuna watu wazima wanatembea na watoto wadogo - definately hilo ni kosa na ndio maana wengi wanafanya kwa kujificha. Lakini kuhalalisha haramu hii ndio kosa kubwa zaidi maana itawaondelea watoto wasio na sauti haki yao. I just hope siku ukiwa na mtoto wa kike (kama bado hauna) hautamwoza mara akivunja ungo.

Kuhusu kuwa unataka Hansard ili uamini, kwanza hulazimishwi kuamini walichoandika watu hapa. na kama unataka sana hiyo Hansard just GOOGLE Bunge and ask them to sort you out. Siku zote umekuwa unachangia kwa hoja tena nyingi tu bila kudai Hansard, why today?
Sawa umeona majibu yangu ni total nonsense & irresponsible! - Umetumia kipimo gani kama sii cha elimu ya wazungu ulofundishwa?..

Soma nilichoandika kwa makini sana, kisha pima halafu elezea hoja inayopingana na hoja zangu sii kukurupuka na kunipa case isiyonihusu. Halafu wewe unazungumzia maswala ya kujamihiana na sii swala la ndoa kwa sababu sioni sababu ya mtoto wa miaka 10 KUINGILIWA na mtu wa miaka 30 inaingia vipi ktk mada hii kama sii fikra za kijinga kuhusiana na mnavyofundishwa kuhusu Uislaam.

Mada nzima inazungumzia mtoto wa kike kuolewa anapovunja ungo hakuna mahala miaka imekuwa issue isipokuwa mloichagua nyie ndio mmekuja na haya ya watoto miaka 10 ati siku hizi watoto huvunja ungo kwa hiyo walindwe wasiolewe lakini sioni mahala mnawalinda wasitembee kupata mimba au kufanya Umalaya! Licha ya hivyo mtoto wa kike akishavunja ungo huitwa MSICHANA hili la utoto tuliache pembeni..Je, anaweza kuolewa?...

Nimesema ya kwamba njooni na solution ya kuwasaidia hawa watoto sio kupinga tu ili mradi unapinga ati Uovu ni uovu ili hali ni nyie wanaume mnaotembea na hao watoto wadogo kuwatia mimba na wengine kuwalazimu kuuza miili yao na mnawaita MALAYA. Sasa wewe usiyesema nonsense unamsaidia nini msichana wa miaka hiyo 10 na kesha kavunja ungo, unamyima hata elimu ili kujiandaa na maisha ya baadaye unamrahisishia kitu gani?.

Nichokisema mimi ni hali halisi ambayo huwezi kuikana kutokana na kwamba umaskini wetu unatuwazimisha watoto wa kike kwa malaki if not millions each year hawafiki kidato cha kwanza kutokana ana sababu mbali mbali.. Na hatuna kabisa mikakati yoyote ya kuwasaidia hawa mnaowaita watoto isipokuwa kuwatumia kama malaya na udanganyifu wa kiume..Kwa sababu hizo, hili ni swala la dharura ktk jamii yetu na hatuwezi kuchukua maamuzi kama ya Wasomali kukeketa watoto au kuwashona kama ndio njia ya kuzuia umalaya au kuwazuia kutoolewa kama kinga kwao wakati maamuzi yote haya hayawasaidii chochote ktk maisha yao. Kama umewahi kunisoma vizuri, utagundua kwamba siku zote mimi hupinga maamuzi ya kumuadhibu victim ukifikiria unawalinda kwa maamuzi mepesi ili hali hujawaondolea tatizo.
 
mkandara nakuona umeelemea kwenye udini zaidi na kwa kukusaidia 2 ni kuwa huwezi kuijadili hoja hii bila kueleza aliyenena maneno hayo ni nani, na aliwanenea akina nani? Aliyenena maneno haya ni mwakilishi(muislamu) tk zenji na alinena kwa kuwajumlisha waislamu wote. Ndo mana nikauliza je alitumwa awanenee hayo au aliamua kuwanenea bila kutumwa? na wala kwenye swala hl uislamc wakujadiliwa sn cha kujadiliwa ni huo umri wa watoto kuolewa/kuoa je ni sahihi? mm ni muislam swafii lkn kamwe siwez unga mkono upuuzi km huu kwani sitapenda kuona mtoto akiolewa.
Wewe usiyekuwa mdini umejuaje kama ni Muislaam na kwa nini uandike Muislaam ktk hoja ilosemwa na Mbunge kwani kutaja jina lake pekee kingepungua kitu gani?.
Leo hii mimi niandike kwenye gazeti lolote kuhusu Regia Mtema (mkristu) kasema - YESU ambaye ni Mungu hufanya pia makosa! nitakuwa na lengo gani kama sii kuanzisha ubishi wa kidini uhusiana na YESU kuwa Mungu mwenye kutenda makosa!...tena unapojua mimi Muislaam ndio inakupa mashaka zaidi hata kama Regia kasema kweli. Kwa nini lazima muwa lebel watu na dini zao ktk kila hoja! lakini akisemwa Dr.Slaa padre na mktistu mnachukia!
 
Simshangai sana MP kwa sababu aliyeleta sharia alimchumbia kabinti cha miaka 6 (aisha) akachukua jumla alivyofika miaka 9 kaoa mzee(khadija) mwenye miaka 42 wake 9 kwa wakati mmoja hapo utaona kwamba tatizo sio mbunge bali mfumo wao (sharia) auendani na scientific facts na socially realits
 
Hata mimi leo hawa wabunge wa Zanzibar wameniacha hoi, kama kuna yule mbunge mmoja alikua akichangia kuhusiana na kiwango cha malipo kwa mahakimu pamoja na mawakili akasema eti ukiwaangalia majaji wamekondeana miguu eti miguu yao midoooogo halafu eti wamepinda mpaka wanavibiongo kwakuperuzi sheria! halafu akasema hata jaji haulipwa mshahara kidogo atashindwa hata kuoa mzungu! Aisee hawa ndugu zetu wanaviswahili vyaajabu.
<br /> <br / si kw wanaviswahili vya ajabu lugha laini kbs ni hawa wa2 ni wapumbavu
 
Back
Top Bottom