Mbunge asema sheria ya ndoa ibadilishwe ili watoto waolewe, Je ni mawazo yake au katumwa?

Angel Msoffe

JF-Expert Member
Jun 21, 2011
6,781
1,639
Nbunge/mwakilishi ktk Zanzibar amelalamika kuwa Waislam wa bara wananyanyaswa sana na sheria ya ndoa, kuwa inaruhusu kuozesha watoto wao kuanzia miaka 18, kinyume na sheria ya dini inayoruhusu mtoto kuolewa pale tu anapobalehe/kuvunja ungo.

Maswali yangu, Je kama mtoto kabalehe/kuvunja ungo na miaka 12 akiwa darasa la 5/6 atafaa kisheria kuacha shule na kuoa/kuolewa?
 
Ana Kichaa cha Kuku atawezaje kushabikia watoto wadogo waingie kenye mambo ya kunyanyswa kingono,mtoto mpaka awe na miaka 18 anaweza kuamua kama aolewe au lah lakini kulazimishwa kuolewa tuu kwa sababu kuna jitu zima lina taka ka kinda haiwezekani.

Mashirika yanayoshughulikia haki za watoto wanatakiwa kutoa tamko kuwakomesha wajinga kama huyo.
 
Mwanae akivunja sinia ana miaka 9 (maana ndo trend sikuizi sio kama zamani mika 12 hadi 14 bado) je atamwozesha?. au anatumia masaburi huyu.
 
Nimeandika kwenye ile thread nyingine naomba niandike tena hapa. Huyu mbunge ni muumini wa UBAKAJI wa watoto. Watoto siku hizi wanavunja ungo wakiwa na umri wa miaka 11, au 12.

Yeye anataka waolewe! tena anasema kama matakwa yake hayakufuatwa ataandamana. Huyu mbunge anawapa waislam reputation mbaya sana. Hawa watoto watasoma saa ngapi? child marriages ni illegal yeye anaona fahari kusimama bungeni kutoa huu upuuzi?

Lingine, Mh Kombani kasoma majina wajumbe wa tume ya kushughulia mahakama ya kadhi iliundwa na ofisi wa Waziri mkuu ikijumuisha watu toka ofisi ya mwanasheria mkuu na baraza la waislam.

Cha ajabu wajumbe wote toka baraza la waislam ni wanawake! hivi hakuna mwanamke mwislam anayejua sheria? Sitoshangaa wakileta huu upuuzi wa kuoza watoto wa darasa la tano.
 
Kweli siku hizi tuna wanawake na si wasichana, kama anabalehe ana miaka9 akija kufikisha umri wa mtu mzima 18 si anakuwa keshakuwa trench, amekongoroka? Ndo maana wanafanya umalaya wadogo kumbe na ukiviona navyo vinadai eti navyo vikubwa vyenzetu,kisa?

Tofauti na zamani 14-16.....humu ndani watu mnaongea kwa kutumia hisia hata bila kufikiria

Hvi mfano leo nikisema dini yangu inatambua ndoa ya mke/mme moja na si vingnevyo tatizo litakuwa ni langu ama ni dini yangu? Kama nanukuu biblia mie nina kosa gani?

Namaanisha tujifunze kujadili hoja badala ya kumuattack mleta hoja, hapa mbunge si hoja, hoja ni umri sahihi wa kuoa/kuolewa.
 
Kweli siku hzi tuna wanawake na si wasichana,kama anabarehe ana miaka9 akija kufikisha umri wa mtu mzima 18 si anakuwa keshakuwa trench,amekongoroka?Ndo maana wanafanya umalaya wadogo kumbe na ukiviona navyo vinadai eti navyo vikubwa vyenzetu,kisa?tofauti na zamani 14-16.....humu ndani watu mnaongea kwa kutumia hisia hata bila kufikiria

Hvi mfano leo nikisema dini yangu inatambua ndoa ya mke/mme moja na si vingnevyo tatzo litakuwa ni langu ama ni dini yangu?kama nanukuu biblia mie nina kosa gani?namaanisha tujifunze kujadili hoja badala ya kumuattack mleta hoja,hapa mbunge si hoja,hoja ni umri sahihi wa kuoa/kuolewa.

Rweye kuna madhara makubwa sana kiafya kwa mtoto mdogo kuanza ngono. Tanzania pamoja na kwamba hatufikia kutengeza rockets lakini nadhani tuna uelewa wa kutosha wa kujua kuwa kumuoza mtoto wa miaka 10 sio tu ni ukiakwaji wa haki zake kama mtoto bali pia tunahatarisha afya yake.

Sijui kama wewe ni mzazi ndugu yangu Rweye lakini kweli ni sahihi kwa watu wazima kuongea mambo ya namna hii karne hii iliyoelimika? Kuna haraka gani hapa?

Na mara nyingi utakuta wanaume wanaooa hawa watoto wana umri kuzidi miaka 30! Taifa gani tunataka kujenga? Watasoma saa ngapi?
 
Ktk dunia ya leo bado anawaza kama yupo enzi za mawe.. Michango ya kipuuzi kama huo bungeni ndiyo maana akina Jairo na Luhanjo wanalidharau bunge. Kuna haja ktk katiba mpya kubadili mfumo kwa kuweka vigezo vipya jinsi ya kuwapata wabunge.

La sivyo tutaendelea kusikia pumba kama hizo. Alafu mtu kama huyo akikaa ktk vijiwe anadai dini fulani inapendelewa,kwasababu wamejaa ktk vyuo.
 
Source please na itakuwa vizuri ukiweka hansard yenyewe kwa sababu Miafrika kwa kuongezea maneno ndio yenyewe!
 
Source please na itakuwa vizuri ukiweka hansard yenyewe kwa sababu Miafrika kwa kuongezea maneno ndio yenyewe!

Mkandara ni kweli hii hoja imetolewa leo Bungeni na mbunge (sikumbuki jina lake) wakati anachangia bajeti ya wizara ya sheria. Msingi wa hoja yake ni kwamba kwa Tanzania kutoruhusu uwepo wa mahakama ya kadhi waislam wanakosa haki zao. Na akataja baadhi ya hizo haki:

1. Kwamba katiba ya Tanzania inatoa umri wa mtoto kuoa na kuolewa kinyume na miongozo ya kiislam kwamba kwao mtoto akivunja ungo basi yu tayari kuolewa (horror!). Hivyo anaona kutoruhusu mtoto wa kike aolewe mara akivunja ungo sio sahihi !

2. Talaka - mwanaume anaweza toa talaka tatu kwa mke wake lakini kwenye mahakama zetu lazima afuate taratibu ambazo kimsingi zinatoa maelekezo ya sababu na process ya kutoa talaka. Kwenye hoja yake ilionekana kabisa kwamba mwaume ndio anakuwa na nguvu (kwa sheria za mahakama ya kadhi) ku-issue divorce & not the other way round!

Kwa ujumla kaongea mambo ya kustua sana ni afadhali kabisa hukuona live. Na kama wewe ni mzazi ungeugua kiharusi. shocking!
 
Hata mimi leo hawa wabunge wa Zanzibar wameniacha hoi, kama kuna yule mbunge mmoja alikua akichangia kuhusiana na kiwango cha malipo kwa mahakimu pamoja na mawakili akasema eti ukiwaangalia majaji wamekondeana miguu eti miguu yao midoooogo halafu eti wamepinda mpaka wanavibiongo kwakuperuzi sheria! halafu akasema hata jaji haulipwa mshahara kidogo atashindwa hata kuoa mzungu! Aisee hawa ndugu zetu wanaviswahili vyaajabu.
 
..hivi mnafikiri kwenye sekondari za kata ni nini kinaendelea huko?

..mimi nashauri watoto wakimaliza sekondari za kata wapewe na vyeti vya ndoa kabisa.
 
wabunge wazenji wanafikilia kuvioa vitoto mbona kuna wanawake wakubwa hawajaolewa? Upuuzi wa mbunge huyu mi sikubaliani nae mbona atujawahi kusikia mtoto wa sheikh fulani ana miaka 12 kaolewa au mtoto wake kaolewa anataka hiyo sheria ili mtoto wa nani aolewe? Yani wametunyönya sasa wanataka kuoa vitoto vyetu . Walahi kama ningekua namjua ningeenda kumtolea posa bint yake wa miaka 12 tuone kama angekubali. Ms.$@nga nini
 
hawa wawakilish wa zanzibar ni bure kabisa wanawaza kuoa vibint vidogo na kutoa talaka wakielezwa mambo ya muhimu kuhusu katiba na muungano wanaishia kutukana.
 
Katoka mirembe juzijuzi, hajapona vizuri
<br />
<br />
Ametumwa na waislamu kusema maneno hayo? Au ni mawazo yake binafsi!? Yeye akamuozeshe mtoto wake. Mtoto wangu hata katiba ikisema aolewe na miaka 18 hataolewa! Ujinga mtupu!
 
Ana matatzo.
Walianza na hak sawa sasa wanataka muda wa kuolewa upunguzwe.
Akapimwe akili. Kaliona hlo n kpaumbele. Badala ya kusistza Elimu Kwanza, kuolewa baadae.
 
Back
Top Bottom