Mbunge apasuliwa kichwa

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,316
33,125
MBUNGE wa Ruangwa mkoani Lindi, Sigfrid Ng’itu (CCM), amefanyiwa operesheni ya kichwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam.

Mbunge huyo amelazwa katika Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili (MOI) hospitalini hapo, hali yake imezidi kuwa mbaya.

Mmoja wa wanafamilia alisema jana kuwa, Ng'itu alifanyiwa operesheni hiyo usiku wa kuamkia jana.

Mwanafamilia huyo hakutaja jina lake, lakini alisema, Mbunge huyo alipasuliwa kichwa kwa kuwa hali yake haikuwa nzuri na kwamba amelazwa wodi ya uangalizi maalum (ICU).

Mkurugenzi wa MOI, Profesa Laurent Museru jana alithibitisha kuwa, Daktari Bingwa wa Upasuaji , Profesa Joseph Kahamba, ndiye aliyemfanyia operesheni hiyo.

Prof Museru alipoulizwa kuhusu hali ya mgonjwa alisema,pamoja na upasuaji aliyofanyiwa, bado hata Rais atakapofika hataweza kuzungumza nae kwa kuwa ana mang’amung’amu kutokana na operesheni hiyo.

Hata hivyo hakufafanua zaidi sehemu ya kichwa alikopasuliwa na kumtaka mwandishi wa habari hizi amtafute Prof Kahamba.

Profesa huyo hakupatikana kwa kuwa madaktari jana walikuwa na ujio wa Rais Jakaya Kikwete hospitalini hapo aliyetarajiwa kufika jana jioni kumjulia hali mgonjwa huyo.

Hiyo ni mara ya pili kwa Rais Kikwete kufika hospitalini hapo kumsalimia Ng’itu ambapo mara ya kwanza alifika Jumanne wiki hii.

Ng’itu alilazwa hospitali ya Muhimbili Jumatatu wiki hii kwa ugonjwa wa kiharusi akitokea Hospitali ya Masana, Mbezi, Dar es Salaam, alipata na mshtuko wa kichwa Jumapili.

Kabla ya kufanyiwa upasuaji huo MOI, Ng’itu alikuwa amelazwa katika wodi ya Mwaisela namba 313 katika Hospitali ya Muhimbili, hali yake ilibadilika ghalfa na kusababisha kupooza upande mmoja wa mwili.

http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?n=3643&cat=kitaifa
 
Back
Top Bottom