"Mbunge Analipwa Mshahara Mdogo Kuliko Mkuu wa Wilaya" by Sita aka SS

SITA anagombea URAIS?
Sisi tunataka MDAHALO baina ya wagombea wa kiti cha URAIS.

Samahani SS haujafikia level ya Dr. Slaa.

Level yako ukafanye mdahalo na Halima Mdee
[/
QUOTE]


:becky::becky::becky::becky::becky: hii imetulia
 
Mimi sikuzote sikuwahi kuwaamini kina sita na kina Kilango wale ni wanafiki tu hakuna kitu

Kula kumi mzee!!!
Huo ndio ukweli unafiki mtupi, waliivamia hoja ya kupambana na mafisadi ili iwaweke pazuri tu.. hakuna kingine!!!
 
Sikonge Thanks.

Hili Gazeti la RAI linamilikiwa na Rostam Aziz(RA) kwa lugha nyingine ni la Mbunge wa Chama cha Majambazi(CCM).

Kwa hiyo habari hizi si uzushi wala longolongo. Ni habari za ukweli na uhakika. Ambaye hataki kuzikubali au kuziamini akajinyonge.
Hizo ndizo pesa wanazokula Wabunge wa Bunge la Wadanganyika. Hata RA anajua hivyo na ndiyo maana zilipoandikwa na gazeti lake hakuzikataa ndo maana akaruhusu Gazeti liingie sokoni ili kuwahabarisha Wadanganyika.

Hapa ndipo Watanzania wenye kuipenda nchi hii wanatakiwa kupiga kura za NO kwa CCM kwasababu wanatufanya sisi Watanzania kuwa ni mazezeta na hatujui lolote kuhusu raslimali na utajiri ilio nao nchi yetu hii.

  • Kama mtu anajilipa mshahara wa 6.9m na mwisho wa Bunge anaondoka na 45m-60m kwanini asihonge ili arudi Bungeni?????Kwa hesabu za haraka haraka Mbunge anaweza kuajiri Wafanyakazi wa KCC 51 na kuwalipa mshahara kwa Mwezi(KCC Basic salary ni 135,000/=).
  • Tuwaulize wana CCM walitumia kigezo/vigezo gani kujipa mishahara/marpurupu haya ikiwa wanatuambia kuwa hali ya uchumi ni mbaya na ndiyo maana JK akawatangazia Wafanyakazi kuwa hataweza kuwalipa Mshahara wa Tshs.315,000/= kwasababu haulipiki!!!!!!!Hata wakidai kwa miaka 8 ijayo hawatalipwa!!!!!!!!!Je,ni kweli HAIWEZEKANI???Huo ni uongo wa mchana kweupe.
  • Tuwaulize tena kama wao Wabunge wanaweza kujilipa Mishahara/Marupurupu haya inakuwaje HAWATAKI KUWALIPA WAFANYAKAZI KIMA CHA CHINI CHA TSHS.315,000/=
  • CCM wanatufanya Watanzania hatuna akili,hatukusoma wala hatuwezi kufanya simple mathematics kama hizi za mishahara(kutoa,kujumlisha,kuzidisha na kugawa)!!!!!
Lakini still bado utashangaa kuwa siku ya KUPIGA KURA JITU ZIMA AU ZEE NA MVI ZAKE LINAENDA KUWAPA CCM KURA ILI LIENDELEE KUKANDAMIZWA,KUNYONYWA NA KUTAWALIWA KIFIKRA,KIUCHUMI NA KIITIKADI HII NI HATARI SANA.

Yawezekana kabisa kuwa nchi yetu hii imelaaniwa kwasababu mambo yanayofanyika hapa Tanzania kwa nchi za wenzetu hayapo na hayakubaliki. Haiwezekani Kiongozi wa nchi kwa maana ya JK asimame mbele ya vombo vya habari halafu awadanganye watu wazima na akili zao tena wasomi kuliko hata yeye halafu watu wananyamaza kimya kana kwamba alichoongea ni nukuu za kutoka msahafu call it a Bible or Quran na kuwa hakuna mtu wa kuhoji. HII NI NINI KAMA SIYO UNAFIKI? HALAFU WATU WANAKAA VIJIWENI WANAAANZA KUJADILI SPEECH MBOVU KAMA HIYO NA WANAISHANGILIA HUKU VOMBO VYA HABARI VIKIPIGIA CHAPUA.

Angalieni wenzetu kule Sauz(SA) kwa Mzee Madiba. Jacob Zuma imebidi akubali yaishe!!! Wafanyakazi wameweka Tools down. Hakuna kazi na halkuna wa kupiga Bomu wala nyau gani. Hakunaaaaaaa!!!

Lakini siyo Tanzania nchi ya watu ambao Bongo zao ni kama zina mgando wa aina fulani. Mwana siasa anakutisha kuwa ukigoma utapigwa mabomu na utaota ngeo kwa mkong'oto kwa hiyo ni bora usigome. Huyu anayekwambia usigome kwasababu serikali haina pesa yeye anajilipa 7M kwa mwezi na halip KODI. Yuko TAX HOLIDAY. Wewe na kimshahara chako kiduchu kila mwezi kinafyekwa kodi.

Usawa uko wapi Watanzania????Please tell me! Maana ninapowazia mambo haya natamani kuingia msituni to wage a war against these CCM thugs! NCHI HII MUNGU AMETUJALIA KUWA NA UTAJIRI WA ASILI;MADINI YA KILA AINA,MBUGA ZA WANYAMA,MLIMA KILIMANJARO n.k. LAKINI SISI TUNAZIDI KUWA MASKINI KILA KUKICHA! WHY KWANINI?

  • JK kaingia madarakani mwaka 2005 kilo ya sukari ikiwa TSHS 500/= LEO HII SUKARI KILO MOJA NI TSHS.1600 ongezeko la asilimia 320%.
  • Dollar moja ya Marekani ilikuwa Tshs za Kitanzania 800/= LEO DOLA MOJA NI TSHS. 1400/=!
  • Halafu unapanda kwenye majukwaa unatuambia MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA na HUKU HUTAKI KUONGEZA MSHAHARA????Hakika HUU NI UWENDAWAZIMU WA CCM.
JAMANI EEH NAWAOMBENI TAREHE 31-OKTOBA-2010 TUWANYIMENI KURA CCM HAWANA ADABU. NAFIKIRI WAKIKAA PEMBENI KWA MIAKA 5 WATATIA ADABU ILI WAKIRUDI TENA WAWE WAMEJIREWKEBISHA.
 
Sita asituletee za kuleta,alishindwa kuendesha bunge kwa viwango kama alivyosema,mpaka wananchi walivyooanza kuwazomea alivyomfukuza Kabwe ndio akajua namana ya kuendesha bunge kidogo,hana adabu kwelikweli kutufanya sisi wote wajinga kutuaminisha kwamba mkuu wa wilaya anamshahara mkubwa kuliko mbunge mkuu wa wilaya maskini ni mtu anayeishi katika mazingira magumu akisubiri rehema za mkurugenzi wa halmashauri na wakuu wa vitengo,akabiliane na hoja lakini sio kubisha tuu wakati ukweli watanzania wengi wanaujua
 
Huyu SS anajaribu kujiweka karibu na kundi la JK, EL na RA ili aweze kupigiwa tena chapuo awe SPIKA, wakati anajua fika Dr. ni Mashine ya Nguvu.

Ama kweli siasa ni unafiki wa hali ya juu. Hivi kweli leo SS eti anajidai yuko against Dr. Slaa!!! wakati yeye mwenyewe amekuwa akimuunga mkono kwenye hoja zake nyingi tu! Asitegemee safari hii pamoja na unafiki wake eti kina RA na EL watamuhurumia na kumuona mwenzao!!! Hivi huyu ndo yule aliyekuwa akijidai ni Spika wa viwango? Shame TO you SS.

Sheria zetu hazijakaa vizuri, Jaribuni kufikiria kama Katiba ingesema Waziri Mkuu akitoka Chama "A" basi Spika wa Bunge atoke Chama Kikubwa cha Upinzani nadhani maendeleo yangeonekana na spika angesimamia Serikali ifanya mambo kwa haki pasipo longolongo nyingine.
 
Nimerudi tena kwenye mada hii ya Mishahara ya Wabunge na Vigogo wa nji hii.

Nauliza tu kuwa hawa Jamaa wanajilipa Posho ya Mafuta TSHS,2,500/= kwa lita ya PETROL AU DIESEL. Je, hii bei ni ya mji gani hapa Tanzania???Maana najua kabisa kuwa wakti ule Bei ilipanda sana ilifikia TSHS.2000 tena kwa baadhi ya miji iliyoko pembeni sana mwa nchi hii.

Hawa wanatakiwa washtakiwe kwa kuiibia SERIKALI kwa kudanganya bei halali ya Mafuta kulingana na BEI ELEKEZI YA WATU WA EWURA. Kujilippa Tshs.2.500 kwa lita ni sawa na kughushi kwa kusema bei ya uongo amabyo haipo hata kwenye soko.

Kwanini tusiwalaumu hawa Wabunge kwa kuchochea kupanda kwa bei ya Mafuta???Maana kama yeye analipwa 2,500/=wakati bei halali ni 1600/= mpaka 1800/=atajuaje ughali na ugumu wa maisha??? Na ndo maana WAUZA MAFUTA WANANWEZA KUPANDISHA MAFUTA WANAVYOTAKA KWA KIGEZO KUWA WABUNGE NA MAWAZIRI WANAPATA POSHO KUBWA YA MAFUTA.!!!!!

Na hizi ndizo mbinu za MAFISADI popote pale. WENGI WAO WANA VISIMA VYA MAFUTA(Petrol stations) kwa hiyo hela wanayopewa na Serikali inarudi kwenye mifuko yao kwa maana ya Vitega uchumi vyao.

Je,ni saa ngapi majitu haya yatakaa chini yafikirie habari ya ugumu wa maisha ya Mtanzania wa chini kama siyo danganya toto??????
 
Aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samweli Sita amenukuliwa na Gazeti la Mwananchi akisema kwamba Mbunge wa Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania analipwa mshahara mdogo kuliko Mkuu wa Wilaya; Nukuu;

"Alisema mbunge anapata mshahara mdogo kuliko hata mkuu wa wilaya ambaye yuko daraja la LSS6 na "sijui kama anafanya utafiti, lakini alipaswa kuzikataa fedha za mshahara; mbona alikuwa anapokea? Alianza kujenga hoja hii baada ya kuona anataka kugombea urais, Slaa aache ghilba". aliyasema hayo akipinga hoja ya Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CHADEMA, Dr. W. Slaa. Habari zaidi bofya hapa chini:

Sitta ajitwika zigo la CCM

Kuna ukweli gani juu ya hoja ya Sita?

Allaaaa kumbeeee! Kama mshahara wa Mkuu wa Wilaya ni mkubwa kuliko wa Mbunge basi na Wakuu wa Wilaya wapunguziwe mishahara yao!

Eti "Dk. Slaa alipaswa kuzikataa fedha za mshahara!" Sitta ana majibu ya kitoto tena ule utoto wa kindergarten ya "kama ile pipi uliyopewa na mama ulikuwa huitaki mbona uliila"! This comment is really absurd coming from a leader - the Speaker of Parliament.

Tumuulize Sitta ambaye naye bila shaka ana mawazo ya kuwa rais wa nchi hii. Atawaambia nini wananchi juu ya matabaka ya walionacho na wasionacho nchini; matabaka yanayotokana na mgawanyo mbovu wa keki ya taifa? Sitta yuko radhi Mtanzania mwenziwe apate kima cha chini cha laki moja na ushei wakati yeye anaogelea kwenye mamilioni ya pesa kwa kisingizio tu kwamba yeye ni Mbunge?

Eti hawa ndio waliokuwa wasaidizi wa Mwalimu Nyerere aliyekuwa anajali sana maslahi ya wananchi wote na zaidi wanyonge! Nyerere aliyetuasa juu ya hatari ya kuwa na matabaka yanayojengwa kwa makusudi kwa kuwakandamiza wanyonge. Iko siku wanyonge watachoka na watataka kuwanyang'anya kwa nguvu akina Sitta matonge mdomoni hapo ndipo watakapogundua kwamba wananchi wamechoka kuonewa! Sitta na familia yake wanakula wanashiba na kusaza kwa mshahara wa Ubunge na marupurupu yake wakati katika jimbo analowakilisha wapo wananchi ambao hawali wakashiba na hata hawapati elimu na matibabu wanayostahili kwa kuwa yeye Sitta anatetea mishahara minono kwa Wabunge!

Shame on him!!
 
Samuel Sitta amekwisha soma alama za nyakati kuwa ule uspika aliosema anauhakika kuupata safari hii umekwisha ota mbawa kwani Malecela aliyemuahidi kumpigia debe ndio huyo kaanguka chali hatakuwemo mjengoni na mafisadi wameapakuwa Sitta hatavaa joho lile tena!! Sasa jinsi ya kujihami anaona afadhali ajikombe kwa kuleta za kuleta dhidi ya DR; hapo ajue ndio anazidi kujipaka matope na mwisho asipoangalia hayo matope yanaweza kugeuka najisi!! Mtu mzima huchezi gololi bwana!
 
Sitta kama anataka mdahalo, tuomba ashiriki mchakato majimbo ya TBC;
 
SITA anagombea URAIS?
Sisi tunataka MDAHALO baina ya wagombea wa kiti cha URAIS.

Samahani SS haujafikia level ya Dr. Slaa.

Level yako ukafanye mdahalo na Halima Mdee

Buahahahahahahahaha kaka umeuaaa. Tatizo anajifanya anajiamini kupita kiasi wakati ni mchemshaji na mnafiki mkubwa. Shame on him na CCM yake ambayo ni uozo mtupuuuuu
 
- Kama Sitta amedanganya, dawa ni sisi kuweka facts hapa kwa namba zinazoonyesha mshahara wa DC na mshahara wa Mbunge, ama sivyo wenye akiili nyingi watashindwa kutofautisha nani anasema ukweli nani anasema uongo, tutafute nambas kwanza ndio tumjibu Sitta kama alivyosema Chairman Mao " No research, no right to speak" JF we should know better mambo ya kuongea bila FACTS, mpaka tutakapo-prove with numbers maneno haya ya Sitta yanasimama as A FACT!

Respect & Kwaherini Ya Kuonana Tena!


WAZEE WA SAUTI YA UMEME!
Mkuu wangu tuwe na ushahidi gani zaidi ya mbunge mwenyewe?.. Dr.Slaa (mbunge) katueleza wazi Mshahara wa Wabunge akiwa yeye ni mmoja kati yao, na Sitta (Spika) amekataa bila kutueleza wazi..Na hakuna mbunge hata mmoja alowahi kuja kusema ukweli au kupinga hoja ya Dr.Slaa wakati bunge likiwa wazi. Pengine yawezekana yeye kuwa ni Spika hajui Mbunge anapokea kiasi gani maana panga lake ni kubwa zaidi yao..

Sasa kama Dr.Slaa alishapokea hizo fedha, kiasi cha kulalamika hadi bungeni kuhusiana na malipo hayo makubwa na wakamkwaza hoja yake, sisi wananchi tuamini nani zaidi?
 
Mkuu wangu tuwe na ushahidi gani zaidi ya mbunge mwenyewe?.. Dr.Slaa (mbunge) katueleza wazi Mshahara wa Wabunge akiwa yeye ni mmoja kati yao, na Sitta (Spika) amekataa bila kutueleza wazi..Na hakuna mbunge hata mmoja alowahi kuja kusema ukweli au kupinga hoja ya Dr.Slaa wakati bunge likiwa wazi. Pengine yawezekana yeye kuwa ni Spika hajui Mbunge anapokea kiasi gani maana panga lake ni kubwa zaidi yao..

Sasa kama Dr.Slaa alishapokea hizo fedha, kiasi cha kulalamika hadi bungeni kuhusiana na malipo hayo makubwa na wakamkwaza hoja yake, sisi wananchi tuamini nani zaidi?

Mkuu thanks na kwa kuongezea kuna gazeti la rai hapo limekokotoa watufahamishe inakuwaje!!!
 
Nchi ingelikuwa inaendeshwa kwa mujibu wa sheria, kama alivyojisemea Sofia Simba basi Sita ingelimlazimu kushitakiwa kwa kugushi nyaraka kwa maslahi binafsi. Fikiri Tsh 900 inayozidi kwenye litre mara 1000kwa mwezi mara 320 idadi ya wabunge mara 12 kwa mwaka mara 5 miaka ya ubunge.
Ni kiasi gani cha pesa serikali inapoteza kwa huu wizi?
UMASIKINI WA KUDUMU WA WATANZANIA UMECHANGIWA NA IDADI KUBWA YA WABUNGE WA CCM BUNGENI. INAWEZEKANA KUBADILI MFUMO HUU, NA WAKATI WA KUFANYA HIVYO NI SASA!
 
Na mimi nasema mwalimu analipwa mshahara mdogo kuliko wote hao. Sitta alipaswa kutazama mantiki ya hoja yenyewe kabla ya kuleta ulinganisho wa mshahara na ule wa mkuu wa wilaya.
 
attachment.php

kwa mapato hayo no wonder hata viungo vya binadamu hutumika kuutafuta ubunge!
 
Back
Top Bottom