Mbunge amwaga simu kwa wapiga kura

Kibongoto

JF-Expert Member
Aug 5, 2009
227
5
MBUNGE wa Jimbo la Biharamulo Magharibi mkoani Kagera Bw. Oscar Mukasa ametoa simu 74 za mezani zitakazotumiwa na wapiga kura wake katika kuwasiliana naye.

Bw. Mukasa alikabidhi simu hizo wiki iliyopita katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Biharamulo ambapo kila kijiji jimboni humo kitapata simu moja.

Alisema uamuzi wa kutoa simu hizo ameufikia baada ya kuona wapiga kura wake wakipata ugumu katika kuwasiliana naye hivyo akawataka kuzitumia kueleza matatizo na ushauri utakaohitajika kupatiwa ufumbuzi ndani ya jimbo hilo.

“Ndugu zangu simu hizi zitusaidia katika mawasiliano ya mara kwa mara nanyi na zina uwezo wa kutumiwa na watu wapatao 15 mpaka 20 kwa wakati mmoja hivyo tunaweza kuendesha majadiliano kupitia simu hizi badala ya kulazimika kuonana ana kwa ana," alisema Bw. Mukasa.

Mbali na simu hizo, Mbunge huyo alisema anatarajia kuweka mwakilishi wake katika kila kata ili kurahisisha mawasiliano au utatuzi wa kero mbalimbali zinazojitokeza.

Aliwataka wananchi hao kutumia
fursa mbalimbali zinazoibuliwa wilayani humo ikiwemo mikopo ya pembejeo za
kilimo ili kutimiza kauli mbiu ya Kilimo kwanza. Source: http://majira.co.tz/index.php?optio...mu-kwa-wapiga-kura&catid=36:mikoani&Itemid=59
 
Wananchi wa biharamulo magharibi hawahitaji sana simu kwani ni wengi wana simu za mkononi, wao wanahitaji maji safi, umeme wa uhakika, huduma za afya, elimu n.k.

Huyo mkasa badala afikirie kuanzisha mfuko wa kusomesha watoto yatima jimboni kwake, anawapelekea simu ambazo hawana hata pesa ya kuziendesha, Mkasa huna jipya.
 
Kama watu wa Biharamulo wanahitaji simu basi ndio hizo lakini Watu wa huko sio muhimu kuwa na simu wakati hali za watu ni Duni sana
 
Back
Top Bottom