Mbunge amwaga chozi hadharani

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
MBUNGE wa Nyamagana, Ezekia Wenje (Chadema), ameangua kilio mbele ya wapiga kura wake baada ya kuelezea changamoto anazopelekewa na wapiga kura hao ofisini kwake.

Wenje, ambaye alikuwa anashukuru wakazi wa Nyamagana kwa kumchagua kwa wingi kuwa mbunge, alisema katika kipindi kifupi alichokaa ofisini kwake, amekutana na wananchi hasa wanyonge, wakiwa na changamoto nzito na nyingi zikiwa ni za kuuziwa viwanja mara mbili.

“Ndugu wananchi, juzi alikuja mzee ofisini kwangu akinionesha makaratasi ambayo yanathibitisha yeye kuuziwa kiwanja na kuwa mmiliki halali wa eneo lake.

“Lakini siku moja alishangaa kuona watu wakienda kwenye kiwanja hicho na kumwaga mawe, kumbe yale makaratasi yalikuwa ni batili, hivi huyu sasa atakwenda wapi, na kibaya zaidi badala ya kulipwa fidia ya Sh milioni moja, aliambiwa alipwe Sh 600,000 tu, hivi kweli hii ni haki?” alihoji Wenje huku akibubujikwa na machozi.

Alisema yeye kama mtoto wa mama ntilie, dhamira yake kubwa mara baada ya kuchaguliwa kuwa mbunge, ni kuhakikisha anapambana kufa au kupona na changamoto zinazowakabili wananchi wa Nyamagana kwa haki na usawa bila upendeleo.

“Kuna watu ambao hawanitakii mema, pale wanapoona naitaja hadharani mikakati ya
kupambana na wala rushwa, hawasiti kuniita mchochezi na hili la ardhi ninasema waniite sasa mimi mchochezi.

“Mimi mwili wangu hauna thamani ya fedha za dunia, bali ninachoamini ni kuona watu wanaowanyanyasa wananchi katika maeneo yao kwa kuwapokonya haki zao za msingi, wanachukuliwa hatua mara moja na katika jiji letu la Mwanza tunaanza na tatizo sugu la ardhi,” aliongeza.

Wenje, ambaye alimtambulisha rasmi Meya wa Jiji la Mwanza, Josephat Manyerere, aliyechaguliwa hivi karibuni kwa tiketi ya Chadema, ambaye pia alikuwa kivutio kwa wananchi mara baada ya kuingia kwenye mkutano huo.

“Yeye ni mcha Mungu na si mjanja mjanja katika kushughulikia matatizo yenu, ofisi yake itakuwa wazi kama ofisi yangu saa 24, mwoneni mnapokuwa na matatizo yenu,” alisema.
 
safi sana mikakati mizuri na utekelezaji ndiyo kujitengenezea njia ya kuicjukua inchi
 
Kama analia hao wananchi wenye matatizo wafanye nini sasa, waanze kumbembeleza au nao wapinge wangi?

Wenje has to grow up, kama kazi ngumu sema.
 
Back
Top Bottom