Mbunge ala mamiloni! Awauzia TANESCO matairi 300 alipwa fedha ya matairi 600

Kwanini Hassan Ngwilizi asishitakiwa MAHAKAMANI kwa kulidanganya UMMA wa WATANZANIA?
Yaani pamoja na kula pesa za TUME BURE hakuona WIZI
?



CCM ikianguka hawa WOOTE wa CCM Waende JELA; Waanzishe RECONCILLIATION COURT

Kama ni kweli kamati ya Ngwilizi haikumtia Mbunge yeyote ambaye aliyesemekana ameshirikiana na Mhando kuihuju Tanesco hatiani, na kwa kuwa ilisemekana kwamba Kosa alilosimimishwa nalo Mhando ni kufanya biashara ambayo Wabunge hao walihusika na lingine ni kuwapa rushwa Wabunge hao, basi kuna sababu gani inayowazuia kumrudisha Mhando kazini mara moja maana tuhuma dhidi yake zitakuwa ni za Uongo automatically!
Au Wabunge wanaotajwa kumsababishia Mhando akafanya alichofanya hadi kumpelekea kusimamishwa ni Watu wa kufikirika? Kama ni hivyo basi na tuhuma dhidi ya Mhando ni za kufikirika!
Hakuna Nchi iliyokuwa na Amani kama Sieraleone- Jenerali Ulimwengu.
 
hawa watu wa intelegensia wanataka kutufunika kwa madogo wakati kuna makubwa zaidi ya haya .........
 
Umeona jinsi Balusconi alivyonyolewa bila maji? Ni kweli ipo siku iso na jina mambo yao yatajulikana na haki itatendeka.

Naingojea kwa hamu siku niwaone Ben, Ed, JK na wenzao wakiwa wamebeba makarai ya kokoto vichwani wakiwa wamevalia zile sare za rangi ya chungwa katika gereza la Maweni.
 
Hii itakuwa ni Zamu ya Prof. Muhongo kukaangwa bungeni. Kama ni mjuzi wa mambo ya kisiasa namshauri aanze kulichimbisha hili sakata sasa tena huku kwa raia walala hoi na sio bungeni.
 
Hii itakuwa ni Zamu ya Prof. Muhongo kukaangwa bungeni. Kama ni mjuzi wa mambo ya kisiasa namshauri aanze kulichimbisha hili sakata sasa tena huku kwa raia walala hoi na sio bungeni.

Nadhani wanapima kina cha maji kwa mguu au!
 
Nambari waniiiiiiiiiiiiiiiiiiiii eeeeeeeeeeeeehhhh, nambari wani ni CCM

kweli mkuu nambari wani.nasubiri siku komba akiimba wimbo wake huo wa nambari wani niuone uso wake utakuwaje,na aibu?na ujasiri?au uoga?Ila mtu akikosa uoga na aibu anachusha na hao ndio ccm
 
kuwa na akili wewe,una dola?una mahakama?una takukuru?au tuandamane kama uamsho?

wewe ndio huna akili hata moja dola, mahakama, takukuru waajiri wao ni nani? ni sisi wananchi wananchi tukiamua kwa umoja wetu leo hii rais ataikimbia ikulu na wala vifaru na mizinga na madege ya jeshi hayawezi kutuzuia, maana sisi ndio wenye nchi taasisi zipo kututumikia sio kutunyonya ila watu waoga kama wewe ndio unafikiri kuwa sisi hatna jeshi,mahakama n.k ondoa tongotongo kichwani amka tafuta haki yako
 
Nani aanzishe Reconciliation court kwa ajili ya wezi? dawa yao ni kuanzisha mahakama mfano wa ile ya kijeshi, court Marshall -baada ya hukumu tu, mtu anakula shaba.

Hiyo WATU watasema ni njia gani walizotumia kuiiibia NCHI; Na Wanataja Mali zilizofichwa UVUNGUNI; Na kweli itasaidia Ukimwambia JELA ni MIezi 6; lakini pesa alizookoa toka kwa WIZi wake ni MKUBWA

Kupelekana hizo Mahakama za KIJESHI kwa RAIA; ni Torcher and it is against International Crime Court...

Tukajiweka kwenye Matatizo badala ya kuyatatua
 
Mimi nitamlaumu raisi wetu tu mpaka mwisho. Yeye anacheka na kufanya mzaha kila kitu. Sitta aliwahi kusema nanukuu ''mweshimiwa rais naomba uonyeshe kaukali kidogo'' mwisho wa kunukuu. Hii ilikuwa bungeni.
 
ukweli inauma sana na wakati mwingine inaudhi sana maana ni kama nchi haina wakuiongoza wala wakuisaidia yaani ni ujinga. Kila kukicha tutafika kweli kwenye ukweli wa maendeleo?
 
Kwanini Hassan Ngwilizi asishitakiwa MAHAKAMANI kwa kulidanganya UMMA wa WATANZANIA?
Yaani pamoja na kula pesa za TUME BURE hakuona WIZI
?


CCM ikianguka hawa WOOTE wa CCM Waende JELA; Waanzishe RECONCILLIATION COURT

Upuuzi ni hapo juu, NGWILIZI kumchuza Mhandao ni sawa na Ngwilizi kumchunguza Mbowa yaani bosi wake wa zamani, sio kweli kwamba Mwenyekiti wa BODI ya TANESCO General Mboma hakunufaika au kufumbia macho uchafu wa Mhando, na wala sio natural Ngwilizi kuwa kwenye hiyo kamati. Bunge (SPIKA) na serikali wanajua uchafu uliokuwepo hapo TANESCO wanachojaribu ni kufunika hii kesi ya ufisadi hapo ndani ya TANESCO
 
Mungu eepushe balaa isije ikawa hata hayo Matairi 300 Ni ya babaji.:angry::angry::angry::angry::angry:
 
Hayo mambo yanakuja pole pole ndugu yangu,Hawa watu watakuja kusimama Mahakamani kwa huu udhalimu wanaofanya wakiwa madarakani.Si umesikia huko Italia leo Waziri Mkuu wa zamani Silvio Belascuoni (76),amehukumiwa kifungo cha miaka 4 jela kwa kudanganya/kukwepa taxes kwenye Biashara zake za Media,kwenye kipindi alichokuwa Waziri Mkuu.Pia bado kuna kesi nyingine ipo pending nayo pia itatajwa tena ya kufanya ufuska na mtoto mdogo mwenye umri wa miaka 17 (wakati huo)

Mkuu nilipo sikia taarifa kuhusu Silvio Belascuoni kitu cha kwanza nilicho fikilia ni TAIFA letu - hivi nchi hizi za dunia ya tatu tunaweza kuwa na ujasiri wa kuwafungulia mashtaka viongozi walio tangulia, kama waliwahi kujihusisha na kashfa za aina fulani.

Oh, that reminds me mwanamme wa shoka, the late Mwanawasa (Raisi wa Zambia). Jamaa huyu alikuwa jasiri sana, alimfugulia mashtaka ya ufisadi na wizi Chiluba; nasikia Chiluba hakuamini kilicho msibu - akawa analalama kwamba Mwanawasa hana shukurani bila Chiluba bwana Mwanawasa asingeweza kupata urais wa Zambia - na kweli Chiluba ndiye alihusika sana katika kumpigia debe Mwanawasa na wote walikuwa wanatoka chama kimoja; Mwanawasa alipo fanikiwa kuukwaa Urais kamgeuzia kibao Chiluba na kumfungulia mashtaka bila kujari fadhila za Chiluba wakati wa utawala wake.

Sijawahi kusikia tena ujasiri mwingine barani Africa kama wa the late Mwanawasa, no wonder Bara hili limebaki nyuma miaka nenda rudi; watu wangekuwa wanakwenda makanisani/misikitini kwa nia thabiti ya kusikiliza vizuri maagizo ya Mola wao sina shaka mambo ya ufisadi/wizi/kutojali binadamu wenzao and what have you - vices zote hizo wangekuwa wana zikimbia kama ukoma.
 
Umeona jinsi Balusconi alivyonyolewa bila maji? Ni kweli ipo siku iso na jina mambo yao yatajulikana na haki itatendeka.

Sasa kaka kazi ni wewe na mie tufanye kweli tuwatoe hawa Ccm magamba tuwaweke Chadema maake kwa hapa kwetu ndio chama pekee ambacho kimeonyesha nia ya kututoa kwenye uoza huu wa ufisadi hakuna Chama chengine ambacho kitaweza kuwaburuta hawa kina Chenge na wenziwe zaidi ya Chadema so we have to do something na mwisho wa siku tuwaone kina Kikwete,Mkapa na mawaziri kibao pale Mahakamani Kisuti ndani ya kijumba kileeee the later watakuwa kama Belusconi tu hii kitu inawezekana sana tu.Let us do man tunaweza kabisa kura yako ya ndugu yako mkeo/girlfriend/mama yako na wengine kwa familia yako tuwape Chadema kura zote 2015 Mungu atusaidie Itafahamika tu,Peoples Power
 
Taarifa za karibuni zaidi zinaonyesha kwamba mmoja wa wajumbe wa Kamati hiyo, Sarah Msafiri, alikuwa na uhusiano na Kampuni ya M/S Sharrif’s Services & General Supply iliyokuwa ikifanya biashara na TANESCO na yeye kusimamia malipo yenye utata kutoka shirika hilo ambalo mbunge huyo analisimamia.


Tayari katika uchunguzi wa Mhando na wenzake zimebainika kasoro lukuki kuhusu mwenendo wao kama viongozi wa TANESCO. Hali pia si swari kwa upande wa Bodi ya TANESCO inayoongozwa na Jenerali (mstaafu) Robert Mboma, ikielezwa kuwa bodi hiyo kwa namna fulani ni sehemu ya uozo uliokuwa ukiendelea TANESCO ikiwa ni pamoja na kulea kile kinachoelezwa kuwa mgawo wa umeme wa kutengeneza ‘mezani.’

Huyo Sara Msafiri akisafishwa bunge loote litakuwa halina maana. Kazi ya huyu mdada iko wazi alishirikiana na Mhando na Mboma akisapotiwa na ZZK kuihujumu TANESCO. Wako karibu sana na kijana Zito na ndio maana kijana huyo kaona aibu sana kawa kama Bundi arukaye mchana na kuzomewa na ndege wengine. Subirini Bunge lianze muone Zitto akiongea tu kuhusu rushwa, au ufisadi wabunge wengine wote hata wahudumu wa Bunge wanaangalia pembeni kwa kusikia kichefuchefu. Anayebisha asubiri aangalie kwa makini hizo body language mtaniambia. Hii ni kwa sababu Kijana aliyekuwa mpiganaji sasa amekuwa kigeugeu, double dealer (CCM & CHADEMA) na ni wa kutumiwa na mafisadi na sisi tumemfuatilia na kuona haya matatizo. Kwa nini Zitto awe karibu na watu mbofumbofu kama hawa akina Sara, Mboma au na Gosbert Blandes mtu asiye aminika kabisa hata huko Karagwe? Je umeona Silaa au Mnyika au Lissu akishirikiana na kuwa karibu na mafisadi?

Na huyo mstaafu Mboma ndiye janga kubwa maana ni kweli alikuwa anamlinda sana Mhando kwa biashara walizokuwa wanafanya pamoja. Lakini kila lenye mwanzo halikosi kuwa na mwisho!

Sisi tutamuunga mkono Maswi kwa ushujaa wake akisaidiana na Mawaziri wake wote maana wanajua wanachokifanya katika kuliokoa shirika la TANESCO ambalo lilikuwa limefanywa kuwa pango la mafisadi kwa kutotengeneza miundo mbinu na pia kuliendesha shirika kwa gharama kubwa za kifisadi kwa ajili ya watu wachache. Watanzania wote tuko macho tunasubiri tu mgeuze kibao eti mafisadi ndio waombwe msamaha muone matokeo yake!!




 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom