Mbunge akutwa akifanya Mapenzi kwenye Gari

Bajabiri

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
9,730
1,201
Mbunge wa Misri ajifedhehesha

21 Julai, 2012

Mbunge wa Misri wa chama cha Kiislamu chenye msimamo mkali, amekutikana na makosa ya kuvunja adabu ya kijamii, kuhusu tukio ambapo amekutikana anafanya mapenzi ndani ya gari lake.

120710101942_egytp_304x171_afp.jpg

Kesi hiyo imewatia aibu Waislamu wanaoitwa Salafi - ambao wanadai kuwa wanaume watengwe kabisa na wanawake.

Mbunge huyo, Ali Wanis, alipewa hukumu ya kifungo cha mwaka mmoja na nusu, kwa kufanya mapenzi na mwanafunzi, na kwa kumshambulia askari polisi
Mbunge huyo ni wa chama cha Nour, kwenye bunge la mwanzo kuundwa baada ya utawala wa Rais Mubarak - bunge ambalo lilifutwa mwezi uliopita baada ya mahakama kuamua kuwa bunge hilo siyo halali.

SOSI: BBC

Najiuliza hivi wabunge wana akili zinazofanana?juzi hapa kuna mtu ameripot kuwa kuna mbunge wa Kondoa alikutwa akifanya mapenzi kwenye gari na kabinti huko ARUSHA
 
Ungesema "aliyekuwa" mbunge maana huyo kisha hukumiwa ina maana na ubunge hanao tena. Natamani sheria kama hizi za uzinzi zingefika hapa kwetu.
 
Tujadili mambo ya msingi yatakayotusaidia kama watanzania.mbona juzi tuu hapa wazir wa serikali hii kafumaniwa na mke wa mtu?
 
Msimamo mkali?
wanaweka sheria kali kwa wengine
wao haziwahusu kabisa,
Wanataka wengine wasifanye,
wakati wao wanaiwaza kila dakika,

Kinachosaidia kuficha maovu,
siyo ukali wa sheria walizoweka,
bali ni usiri unaotawaliwa na,
kibano unachopewa na jamii,
ukijifana kutoa siri.
 
Wabunge ni watu tu kama wengine, with 'feelings' and 'frailities" as well. Na ujue, haya mambo yanafanyika na watu wengi sana, sema kwa kuwa habari ikiwa inagusa mtu anaye enjoy high public profile, inakuwa rahisi kufahamika nk. Tendo la ngono, achana nalo bwana. Hakuna hero pale.
 
Mbunge wa Misri ajifedhehesha

21 Julai, 2012

Mbunge wa Misri wa chama cha Kiislamu chenye msimamo mkali, amekutikana na makosa ya kuvunja adabu ya kijamii, kuhusu tukio ambapo amekutikana anafanya mapenzi ndani ya gari lake.

120710101942_egytp_304x171_afp.jpg

Kesi hiyo imewatia aibu Waislamu wanaoitwa Salafi - ambao wanadai kuwa wanaume watengwe kabisa na wanawake.

Mbunge huyo, Ali Wanis, alipewa hukumu ya kifungo cha mwaka mmoja na nusu, kwa kufanya mapenzi na mwanafunzi, na kwa kumshambulia askari polisi
Mbunge huyo ni wa chama cha Nour, kwenye bunge la mwanzo kuundwa baada ya utawala wa Rais Mubarak - bunge ambalo lilifutwa mwezi uliopita baada ya mahakama kuamua kuwa bunge hilo siyo halali.

SOSI: BBC

Najiuliza hivi wabunge wana akili zinazofanana?juzi hapa kuna mtu ameripot kuwa kuna mbunge wa Kondoa alikutwa akifanya mapenzi kwenye gari na kabinti huko ARUSHA

Juma nkamia au nani?
 
Nimekurupuka nikadhani ni pale Chako ni Chako ama kwenye viunga vya CBE kumbe Misri! Pelekeni jukwaa la kimataifa.
 
Ama kweli dini ya mtu haiko kwenye Kanzu na Kibarakashia anachovaa, na wala haiko kwenye Joho wala msalaba ambao mtu anavaa. Pia haiko kwenye jina alilobeba kama vile "Mwisilamu wa sala tano" au "Mlokole". Bali dini ya mtu inadhihirishwa na moyo wake. Kama huyu mujahidina anafumaniwa akizini, itakuwaje kwa wale waislamu wa kawaida? Unafiki ni kitu kibaya sana. Huyu hana tofauti na kafiri tena ni mbaya kuliko kafiri kwababu ya unafiki. Ni heri kafiri maana yeye amekubali kujulikana jinsi alivyo.
 
ungesema "aliyekuwa" mbunge maana huyo kisha hukumiwa ina maana na ubunge hanao tena. Natamani sheria kama hizi za uzinzi zingefika hapa kwetu.
atabaki mtu pale,,,,,,hata katibu wa bunge habaki
 
Back
Top Bottom