Mbunge akilamba posho ya bunge la sadc..ni dhambi??naomba msaada

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,722
21,775
Jamani naomba msaada kidogo kwa hili...najua kwenye bunge letu majuzi wameteua mwakilishi wa bunge la sadc baada ya kifo cha ndugu yetu mpendwa rich nyaulawa...naulzia je huyu ndugu akienda vikaoni analipwa hela za posho ya sadc je ana haki...nauliza kwa njia njema maana ni rafiki yangu alieteuliwa asije akalamba posho takukuru wakamngangania akiwa anarudi pale airport...naomba msada tutani
 
Wabunge wa SADC wanalipwa posho na Bunge la Tanzania. Alambe tu hakuna double payment hapo.
 
wabunge wa sadc wanalipwa posho na bunge la tanzania. Alambe tu hakuna double payment hapo.

thanks much zitto godbless u

vipi na kule tanesco ile ilikuwa ni double payment??embu nifungue kidogo br
 
Na vipi vikao vya sadc vinapogongana na vya kwetu huku...jamaa anaenda na posho hiyo hiyo ama analamba za huku anaelekeza mashambulizi na za sadc??
 
Jamani, habari za RICHMOND, AND KIWILA.

Nasema kwamba, suala la POSHO mbili liko hivi:

Kuna aina nyingi za POSHO lakini posho zinazosemwa TZ ni

1. Posho ya Kikao
2. Posho ya kujikimu

1. POSHO YA KIKAO

Posho ya kikao kwa Tafsiri ya Kanuni za Kudumu za Kudumu za Utumishi wa Umma ni kwamba, mtu anaweza kulipwa posho za kikao zaidi ya mara 10000 kwa siku kwa kuhudhuria vikao 10000. kwa sababu hii ni posho ya kuingia kwenye Kikao. Posho ya Kikao unaweza kulipwa hata kikao kikifanyika NDANI YA NYUMBA YAKO imlimradi umehudhuria KIKAO HICHO. Kosa la Posho hii ni kukuchukua wakati hujahudhuria kikao huo utakuwa ni WIZI.

2. POSHO YA KUJIKIMU

Posho ya kujikimu ni posho inayomuweza Mtumishi au Mtu yeyote kuishi kwa siku zile ambazo yupo Nje ya eneo lake la kazi au yupo mbali na nyumbani kwake au na sehemu aliyoajiiriwa. Posho hii huwezi kulipwa iwapo haujasafiri mbali ya eneo uliloajiriwa. Mfano Mbunge hawezi kulipwa Posho ya Kujikimu anapokwenda kuwaona wapiga kura wake au anapokuwa Nyumbani kwake alipoonyesha kwenye taarifa zake binafsi. Lakini anaposafiri kikazi nje ya Jimbo lake au sehemu ya Nyumbani kwake kama alivyoiainisha kwenye taarifa zake binafsi anatakiwa alipwe posho ya kujikumu ili imuwezeshe kulala na kula kwa siku ili au zile atakazokuwa amekaa huko au kule. kwa maana hiyo, siku huwa ni moja na huwezi kusema leo ni jumamosi asubuhi, leo ni jumamosi mchana au leo ni jumamosi jioni hivyo ulipwe posho ya kujikimi zaidi ya moja kwa siku moja.

Aidha, ukiwa umekwenda kikazi labda kuhudhuria Mkutano AICC Mjini Arusha kutoka Dodoma na wakati unaondoka Dodoma ulilipwa posho ya kujikimu kwa ajili ya kulala na kula ya siku 10, kule Arusha waandalizi wa Mkutano huo wa siku kumi hawatakiwa kukulipa posho ya kujikimu kwa siku hizo kumi ukilipwa posho hiyo na ukapokea UTAKUWA UMEFANYA WIZI. Isipokuwa Waandaaji wanaweza kukulipa posho ya kuhudhuria kikao kwa kila siku kwa hizo siku kumi. Na wakati mwingine posho ya kikao huwa kubwa kuliko posho ya kujikimu inategemea Mwongozo wa hiyo taasisi unasemaje kuhusu posho ya kikao.

Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anapoiwakilisha Nchi kwenye Mabunge ya Afrika Mashariki, SADCC, Jumuiya ta Madola huwa analipwa Posho ya kujikumu na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kulingana na Posho kama zilivyoainishwa kwenye mwongozo wa Mabunge hayo anayohudhuria. na Kule anapokwenda hatalipwa posho ya kujikimu badala yake atalipwa posho ya kuhudhuria kikao cha Bunge hilo husika.

Hapa hakuna utata wowote, hata kama vikao vya Bunge la Jamhuri ya Muungano vitagongana na Vikao vya Bunge la SADCC au Jumuiya ya Madola la Afrika Mashariki- Mbunge huyo atakuwa na uchaguzi. akiamua kwenye kwenye kikao cha Bunge la SADCC atalipwa na bunge la Tanzania Posho ya kujikimu kwenda kwenye Bunge hilo, ama akiamua kukaa kwenye Bunge la Tanzania atalipwa posho ya kujikimu kwa ajili ya Bunge la Jamhuri ya Muungano. Aidha, hata hapa Tanzania Wabunge wanalipwa Posho ya Kujikumu wanapokuwa Dodoma kuhudhuria Vikao vya Bunge hulipwa posho mbili.

1. Hulipwa posho ya kujikimu; na
2. Hulipwa posho ya kuhudhuria Vikao vya Bunge.

Mbunge kama hayupo Bungeni halipwa posho zote hizo mbili.

Aidha, hata wabunge wanapohudhuria Vikao vya Kamati za Bunge, huwa wanalipwa posho za Kujikumu na Bunge lakini Wizara husika huwa inawalipwa posho za kuhudhuria Vikao.
NA SIYO POSHO YA KUJIKIMU. iwapo wanalipwa posho ya kujiku na Bunge, na Wizara au Taasisi husika nayo inawalipwa Posho ya kujikimu kwa siku zile zile ambazo walisha lipwa na Bunge tena wanalipwa na Posho ya kikao. HUO NI WIZI.
 
Maelezo yako mazuri sana, maana watu walikuwa wanachanganya hizi posho mbili, ya kikao (ambayo wanaiita takrima) na ya kujikimu (per diem)!
 
Back
Top Bottom