lifeofmshaba
JF-Expert Member
- Feb 19, 2011
- 867
- 219
MAAJABU YA DUNIA MBUNGE WA WADI MWANYANYA KUINGIA BUNGENI KWA 19%?
CCM wanatamba kwa ushindi kama huo
Ni sawa na asilimia ya 19% ya wapigakura (walipaswa kupiga kura watu 4,059 na yeye kapata kura 807 ni kura kidogo kuliko baadhi ya madiwani.
Watu kutopiga kura ni ujumbe tosha kwa mbunge mteule kutokuwa na mvuto kwa jamii anayoiwakilisha,
Kwa wenye hekima huyu ni mshindi aliyeshindwa ( ni wakati sasa katiba kuwakataa wabunge kama hawa wasiokubalika wanakotoka)
Sekreterieti mpya ya ccm ilikwenda Zanzibar kutafuta kura 807, hii ni aibu kwa ccm kutokana na nguvu waliyotumia kwenye huo uchaguzi mdogo
CCM wanadhani wamepata kura 807 kwa sababu wamevua gamba ya kwamba sasa wanakubalika na wananchi kwa kupata kura 807 katika ya kura 4059 za wanaositahili kupiga kura.
Watanzania kama tusipo amka na kujua umuhimu wa kura zetu basi tutaendelea kupata wabunge kama HAMZA KHAMIS JUMA, hiyo 19% ni ya watu
waliojiandikisha kupiga kura kama tukifanya utafiti zaidi unaweza kubaini kwamba huyo mbunge kachaguliwa na watu chini ya asilimia 10, kwa maana nyingine ruhusa yake kuwakisha hiyi jamii ni kama haipo kabisa.
Hapa ndio naona KATIBA inatakiwa kuweka kikwazo cha asilimia za ushindi wa wabunge kwa kuzingatia watu wanaopaswa kupiga kura na kura alizopata mbunge, yawezeka kabisa watu kutopiga kura ni aina ya kuwakataa wagombe wote waliopo katika mchakato, Katiba inatakiwa kuwatema wabunge walipata mwitikio mdogo kwenye majimbo yao wakati wa
uchaguzi ili kuongeza nguvu ya umma katika uwakilishi kwenye hilo jengo la kutunga sheria.
Kwa misingi hiyo wagombea wataamasishwa watu kwenda kupiga kura badala ya kununua kadi zao ili wasipige kura, hii itawakomesha ujanja wa wachache wanaofikilia kupunguza idadi ya wapiga kura kwa vitisho na hira ndio njia ya kushinda uchaguzi.
Mimi nina hakika kama kila mtu hatapewa nafasi ya kusimama mbele ya sandukula la kura pale sirini hawezi kuiuza nafasi yake,
Watanzania huu ni wakati wa kwenda kupiga kura, serikali haiwezi kuwaamasisha kupiga kura maana hiyo ni moja ya mikakati yake kuendelea kubaki madarakani, nchi zote zenye maendeleo ni kwa sababu wanaheshimu na kuthamini sana kura zao, kura ni kila kitu, ni huduma zote za jamii na maendeleo ya nchi. kura ina thamini kuliko hiyo kazi unayofanya, maana kama bunge na serikali wakiingia watu wenye uchu kama ilivyo sasa watakula mali zote unazozalisha kila siku na ulizozalisha kwa muda mrefu.
SOURCE: lifeofmshaba.com