Mbowe vs Ndugai live on TBC1

Kumbe kanuni haijabadilishwa au usanii tu.

Mkuu kanuni haijabadilishwa wala kinachogombewa si uongozi wa kuwa viongozi wa kambi ya upinzani wala si uwaziri vivuli,
kinachopigiwa kelele ni kuongeza tafsiri ya neno kambi rasmi ya upinzani inyomaanisha sasa wenyeviti wa kamati nyeti zinazoongozwa na upinzani sasa zitagombewa na wapinzani wote na si cdm pekee.
Kwa mujibu wa ndugai kambi rasmi ni ile kambi ya jumla ya wapinzani wote wakifikisha asilimia 12 ya wabunge wote ndio itakuwa rasmi na si chama kimoja kuwa ndio kambi rasmi,
Kwa mantiki hiyo kifungu husika kinasema wwenyeviti wa kamati hizo watatoka ktk kambi rasmi ya upinzani ambayo kwa tafsiri iliyopo ni vyama vyote vya upinzani ndio kambi rasmi as long as wamefikisha asilimia 12 kwa umojawao.
Mkuu samahani nimekariri lakini sijakariri vifungu
 
Hili swala la muungano wa vyama vya upinzani linapelekwa ki propaganda sana na ajenda nyuma yake si maslahi ya taifa,ni kuidhoofisha cdm tu ingawa yatazungumzwa mengiiii! na kuna baadhi ya wana cuf wanafata mkumbo ki propaganda bila kujua malengo ya haya na hata nafasi yao baadae.vyama vingine sababu zipo wazi hasa TLP,UDP na NCCR lakini CCM wanajua faida ya varangati hili na mwisho wake ni "superdupa profit" kwao.wadau kazi ipo nchi hii,mfumo uliopo unaitaji neema ya Mungu kuvuka salama kisiasa.
 
hebu nielezeni kidogo hapa! !sasa chadema walitoka bungeni kwa hoja ipi kama leo inasemwa ni ruksa kwako kuunda kambi ya upinzani Bungeni??

hoja hapa mkuu ni kwamba wametafsiri kanuni kwamba kambi rasmi bungeni ni wapinzani wote hivyo kuwazesha wapinzani kugombea uenyekiti wa kamati muhimu tatu zinazotakiwa kuongozwa na upinzania bila kupitia kwa kiongozi rasmi wa upinzani bungeni. Kwa kuwa CUF,NCCR,UDP na TLP ni vibara wa CCM watachaguliwa wao wakati wa kura kwa kuwa CCM ni wengi bungeni hivyo kuipunguzia CHADEMA udhibiti wa serikali.
 
hebu nielezeni kidogo hapa! !sasa chadema walitoka bungeni kwa hoja ipi kama leo inasemwa ni ruksa kwako kuunda kambi ya upinzani Bungeni??
Hoja ni kwamba kanuni iliyobadilishwa inawafanya wabunge wengine wa upinzani kuwemo katika kambi ya upinzani(hata CUF ambao wana ndoa na CCM)Na kwa kuwa katika kamati za bunge ambazo zinatakiwa wenyeviti wawe kutoka kambi ya upinzani ambao CHADEMA ndio walitaka waziongoze,suala hilo halitakuwepo tena kwa kuwa ndani ya kamati hizo wabunge wa CCM ni wengi na watawapigia kura wagombea wa nafasi hizo wanachama wa vyama vingine si CHADEMA.
Hapo ndio tatizo lilipo.
 
nafikiri chadema ni wachanga katika kuelewa vifungu vya bunge

Unajua kama kuna jambo hulielewi ni busara kukaa kimya,ukasubiri usome hoja za watu wanaojua. Kanuni mojawapo ya bunge ni kwamba wenyeviti wa kamati 3 muhimu za bunge watatokana miongoni mwa wabunge wa kambi rasmi ya upinzani ambayo kwa kanuni zilizopo ni Chadema. Lakini CCM jana wamebadili tafsiri ya kanuni ili kambi rasmi ya upinzani ijumuishe na vibaraka wa CUF,TLP Mrema na UDP cheyo ambao hawafanani na upinzani labda wanaweza kuwa timu B ya CCM. Kwa kufanya hivyo kamati zile nyeti zinagombewa na akina Cheyos na Kafulilas na watu kama Hamad rashid na kwa namna ilivyo katika upigaji kura kutokana na wajumbe wengi wa kamati kuwa wa CCM watahakikisha hawa wapinzani uchwara yaani CUF,TLP na UDP wanaongoza kamati zile na hivyo kamati kutokuwa na nguvu ya kuichachafya serikali maana hao ni kama CCM. Wanaogopa kivuli cha Chadema kwahiyo wanajaribu kuidhoofisha kwa makusudi.

Labda niseme tu CCM wanakosea sana na hizi strategy zao,wananchi wengi wanazidi kuwa discredit kwa huu uhuni wanaoufanya.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika
 
Hoja ni kwamba kanuni iliyobadilishwa inawafanya wabunge wengine wa upinzani kuwemo katika kambi ya upinzani(hata CUF ambao wana ndoa na CCM)Na kwa kuwa katika kamati za bunge ambazo zinatakiwa wenyeviti wawe kutoka kambi ya upinzani ambao CHADEMA ndio walitaka waziongoze,suala hilo halitakuwepo tena kwa kuwa ndani ya kamati hizo wabunge wa CCM ni wengi na watawapigia kura wagombea wa nafasi hizo wanachama wa vyama vingine si CHADEMA.
Hapo ndio tatizo lilipo.

mkuu..kanuni haijabadilishwa..imefanyiwa tafsiri tu.... na CDM wameunda peke yao kambi rasmi ya upinzani...tatizo ni kama ulivyo elezea kuhusu upataikanaji wa wenyeviti wa kamati nyeti tatu za bunge
 
Kimsingi hoja inayopiganiwa hapa ni kumnyima mandate mkuu wa upinzani bungeni na genge lake kuteua au kupitisha wenyeviti wanaowaamini ktk kuongoza kamati nyeti za bunge.
 
Tumewachagua wakatetee maendeleo ya wananchi wao wanahaha kubadili/kufasiri kanuni ili wapate vyeo...shame on them....sisiemu wanajitahidi kubrainwash watu ili wasahau ajenda ya ufisadi...hatujalala. Badilini kanuni tafsirini mnavyotaka mwisho wa siku ni watanzania watakaotoa hukumu...there is more wisdom in keeping silent...lets wait and see
 
duuu!kweli ccm wamebanwa pabaya,hakuna kukubali hilo litokee kamwe.

Sijui Kama ni CCM kubanwa; ispokuwa kwa mtu makini atajiuliza maswali yafuatayo.

1. Siku zote Bunge husema kwamba linaheshimu mihimili mingine ya dola ikiwemo mahakama na hata hoja ya Dowans imetupiliwa mbali kwa sababu kesi iko mahakamani. Kazi ya mahakama ni kutafisri sheria zilizotungwa au zitakazotungwa na bunge baada ya miswaada/ bills kutoka serikalini kupelekwa huko kujadiliwa.
Swali: Tangu lini Bunge likawa ni sehemu ya kutunga sheria, kanuni na taratibu na pia likawa ni sehemu ya kuzitafsiri sheria hizo, kanuni hizo, na taratibu hizo... ? Mbona hapa linaingilia kazi ya kutafsiri wakati kazi hii ni kazi ya mahakama...?

2. Nani aliwaambia wabunge wa CCM kwamba CDM inahitaji msaada wa kulahisisha utafisilishaji wa kanuni hiyo iliyofanyiwa marekebisho?

3. Ni nini maana ya kuwa na serikali kivuri/opposition government kama sio wao wapinzani wenyewe kujiamulia mambo kwa mujibu wa kanuni zilizowekwa na zilizokuwa zinajulikana kabla hata ya bunge hili la 10?

4. Kuna haja gani kanuni hiyo kuhitaji tafisili mpya tofauti na ile iliyokubalika ktk mabunge likiwemo lile la 9 kama sio mbinu chafu za kuudhofisha upinzani hasa unaounda serikali kivuli? Hii pia inaonesha kwamba wabunge wa ccm hawana uwezo wa kupambanua mambo ndo maana wanakimbilia matusi na utani ambao watu kama vijana na watoto hawategemi kuoneshwa na waheshimiwa

5. Ni kwa nini tafsiri hiyo mpya isiwe effective katika bunge la 11 na na iwe effective sasa?

6. Wabunge hao wanaozomeazomea CDM watajisikia vipi kama na wao siku moja wakiwa kwenye receiving end kama mambo haya hayatarekebishwa?

7. Na hao Zomea zomea wanataka kutoa taswira gani ya nchi yetu, wapiga kura wao na heshima yao wanayopewa kwa kuitwa waheshimwa kama hawana tofauti na watu wa vijiweni? na hao wanasema kwamba watu watwangane makonde...? hivi siku hizi tumekuwa kuku au jogoo wa kupigana bila mpango?

8. Ushauri: CDM endeleeni kue-exercise democracy with inteligence and intergrity nasi tutawasaidia kueleza ndugu zetu jinsi CCM inavyotaka kuwabuluzeni NA CCM NYIE endelezeni Ukihiyo wane kwa zomeazomea hata bila kujua ni nini kinacholalamikiwa...ipo siku mambo yatawageukia na kulamba matapishi yenu...
 
je kanuni za mabunge ya jumuiya ya madola haijavunjwa wadau? wanaofahamu wanisaidie hili
 
Chadema wanajua nini tunataka watanzania.. Ila ccm hawajui..

Sasa tunachowapa ni hali halisi ya watanzania kwamba ccm tumeichoka..

Mbowe ni kiongozi makini hatuna shaka naye hata chembe.. Na hata wakibadilisha nini bungeni.. Sauti ya umma itashinda tu kama siyo leo basi hata kesho..
 
hebu nielezeni kidogo hapa! !sasa chadema walitoka bungeni kwa hoja ipi kama leo inasemwa ni ruksa kwako kuunda kambi ya upinzani Bungeni??

kilichopo ni kua, baada ya marekebisho ya jana, mbunge yeyote kutoka chama chochote cha upinzani anaweza kugombea uwenyekiti wa zile kamati tatu nyeti za kusimamia matumizi ya fedha za serikali bila kua na ulazima wa kupitishwa na uongozi wa kambi rasmi ya upinzani.sasa ukizingatia uhusiano uliopo kati ya ccm na chadema its obvious akisimama mgombea toka CUF au UDP au TLP kuchuana na mgombea toka chadema lazima wa chadema atashindwa kwa sababu wabunge wa ccm kwa vyovyote watakua against wagombea wa chadema.
 
kuna mambo yanaendelea ndani ya Taifa letu yanatoa kiashiria kuwa ccm ipo kwenye coma, kufa ni lazima.
 
nafikiri chadema ni wachanga katika kuelewa vifungu vya bunge

1.Vifungu gani hivyo unavyodai CDM hawavielewi?
2. Jeumekwisha wauliza wakakili kwamba hawavielewi ?

3. Hiyo conclusion yako kwamba hawavielewi umeitoa wapi? una evidence? UVCCM Walisha sema NO research no right to speak na kwa ku-apply msemo huo KWAKO kama hujawapa CDM benefit of the doubt kukiri kwamba ni kweli CDM ni Vihiyo wa Kanuni hizo unazozisema basi you have no right to write and post upupu wako humu JF maana jukwaa hili limejaa watu makini: TAFADHARI SANA with capitals...
 
Mkuu kanuni haijabadilishwa wala kinachogombewa si uongozi wa kuwa viongozi wa kambi ya upinzani wala si uwaziri vivuli,
kinachopigiwa kelele ni kuongeza tafsiri ya neno kambi rasmi ya upinzani inyomaanisha sasa wenyeviti wa kamati nyeti zinazoongozwa na upinzani sasa zitagombewa na wapinzani wote na si cdm pekee.
Kwa mujibu wa ndugai kambi rasmi ni ile kambi ya jumla ya wapinzani wote wakifikisha asilimia 12 ya wabunge wote ndio itakuwa rasmi na si chama kimoja kuwa ndio kambi rasmi,
Kwa mantiki hiyo kifungu husika kinasema wwenyeviti wa kamati hizo watatoka ktk kambi rasmi ya upinzani ambayo kwa tafsiri iliyopo ni vyama vyote vya upinzani ndio kambi rasmi as long as wamefikisha asilimia 12 kwa umojawao.
Mkuu samahani nimekariri lakini sijakariri vifungu

huu ndio upupu waliolalamikia chadema..wanachotaka ccm labda kwa msaada maana nimesoma mada nyuma nkajua umeelewa wanataka cuf nao wagombee na ktkt kwenye kura unakuta cuf watupu wamejaa ambao ni CCM -B
HAKI YA WATANZANIA ITALINDWA NA WATANZANIA WENYEWE .......CCM HATA WAFANYE NINI MBOWE NJOO DAR TUINGIE MTAANI HII NDI SOLN YA KUTOA UPUMBAVU WA SOKWEMJINGA-CCM
 
Tatizo ni nafasi za uongozi katika kamati hizo, yaani nakumbuka Makinda alitoa ufafanuzi kabla ya bunge kuanza kuwa CDM wana haki ya kuunda kambi rasmi ya upinzani na hakutakuwa na kambi mbili bungeni sasa imeonekana kuwa CDM wakichukua kamati zote balaa linaweza kutokea kwa siri nyingi kuleak na kuiondolea serikali imani zaidi kwa wananchi.
 
huu ndio upupu waliolalamikia chadema..wanachotaka ccm labda kwa msaada maana nimesoma mada nyuma nkajua umeelewa wanataka cuf nao wagombee na ktkt kwenye kura unakuta cuf watupu wamejaa ambao ni CCM -B
HAKI YA WATANZANIA ITALINDWA NA WATANZANIA WENYEWE .......CCM HATA WAFANYE NINI MBOWE NJOO DAR TUINGIE MTAANI HII NDI SOLN YA KUTOA UPUMBAVU WA SOKWEMJINGA-CCM

Mkuu tupo pamoja,
issue ipo hivi, kwa mujibu wa tafsiri mpya sasa itabidi vyama vyote vya upinzani vipeleke jina moja moja kwaajiliya uchaguzi wa kamati hizo,
mfano kamati ya mahesabu ya serikali cuf mnyaa, cdm zitto, udp cheyo, hapo sasa inabidi kura zipigwe na wajumbe wa kamati hiyo ya mahesabu ya serikali ambayo kiidadi inawajumbe zaidi ya nusu wa ccm.
Ukiangalia hapo juu utaona kwamba wajumbe wa kamati ni lazima watampa wa cuf au udp sababu wao ni weng na hawaipendi cdma
 
Hili swala la muungano wa vyama vya upinzani linapelekwa ki propaganda sana na ajenda nyuma yake si maslahi ya taifa,ni kuidhoofisha cdm tu ingawa yatazungumzwa mengiiii! na kuna baadhi ya wana cuf wanafata mkumbo ki propaganda bila kujua malengo ya haya na hata nafasi yao baadae.vyama vingine sababu zipo wazi hasa TLP,UDP na NCCR lakini CCM wanajua faida ya varangati hili na mwisho wake ni "superdupa profit" kwao.wadau kazi ipo nchi hii,mfumo uliopo unaitaji neema ya Mungu kuvuka salama kisiasa.
Hawa jamaa wameisha vuruga mambo mengi kwa kipindi cha siku moja tu wakitumia wingi wao bungeni. Wanakejeli, wanatukana, wanatuona Watanzania wote ni vilaza hatuwezi kutafasili maana ya wanayo yafanya. Uzuri wake wajumbe wetu ingawa ni wachache watazidi kutoa changa moto bila kukubali uozo unaofanywa na hao mafisadi. Hili bunge inaonyesha litakuwa ruber stamp ya SISIEM pomoja na spika wao.
 
mkuu..kanuni haijabadilishwa..imefanyiwa tafsiri tu.... na CDM wameunda peke yao kambi rasmi ya upinzani...tatizo ni kama ulivyo elezea kuhusu upataikanaji wa wenyeviti wa kamati nyeti tatu za bunge

Jamani Kubadili tafsiri kisheria ni mabadiliko makubwa kwani tafsi moja inaweza kuwa imebadili maana nzima ya neno husika.

Hiki ndicho kilichofanyika na kwa maana hiyo hakuna tena neno Kambi Rasmi ya upinzani. Na kwa sababu neno hilo limebatilishwa kwa kutoa taafsiri tofauti na iliyokuwapo hawali ndiyo maana tunasema Kanuni imebadilika.

Si hivyo tu fanyeni utafiti katika mabunge ambayo tunafuata utamaduni wao kunakuwa na pande mbili tu chama kinachounda serikali na Chama kinachofuata kinakuwa ni kile chenye wabunge wengi ,na ndicho kinachounda Official opposition not otherwise.huwa kunakuwapo vyama vingine vyenye wabunge wachache bila kuungana.

katika mjadala wajana watu waliochangia positive hawakutaka kutueleza sababu zilizopelekea muungano wa kambi 2005-2010.CUF as cuf hawakufika record ya 12.5 percent as they where 2000.Turudi nyuma mwaka 2000 CUF walikuwa na wingi huo na waliform upinzani peke yao.

what happen this year is the same Chadema peke yao wamefika more 12.5 percent ,na kama alivyoeleza kiongozi wangu Mbowe mazingira ya 2010 hayafanani na miaka iliyopita kwa maana hiyo hakuna ulazimu wa kuunganisha nguvu.Jambo ambalo wenye uwelewa watakubaliana na mimi kuwa TLP,UDP,NCCR,CUF zimepita katika mchakato ambao tumepoteza imani nao.

Ndugu zangu kama kweli watu hawa walikuwa na nia ya dhati ya kufanya muungano au kama walilijua hili la umoja uleta mshikamano mbona tulipowaomba wakati wa Campaign kila mtu alitokomea kivyake?

Ndugu zangu inawezekana wengi hatujui kutafsiri sheria au kanuni mbalimbali sababu ya mazingira husika,lakini kwa kila mwenye uchungu na nchi hii atajua hila hii.

Dunia nzima kamati nyeti kama POC husimamiwa na upinzani ili kudhibiti hali ya ubadhilifu na kuweka wazi maovu ya serikali tawala.Kamati zingine kamati zingine 2 zipo tanzania tu.

Tukumbuke fedha nyingi za serikali zinaliwa kupitiwa Halmashahuri zetu na mashirika ya umma,na wote ni mashahidi wa hili.
 
Back
Top Bottom