Mbowe: Tutawasha moto Bunge la bajeti

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
na Edward Kinabo



MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, amesema chama chake kitahakikisha kinalitumia Bunge lijalo la bajeti kuishinikiza serikali kupunguza kodi zinazotozwa kwenye bidhaa na huduma muhimu ili maisha ya wananchi yawe nafuu.

Mbowe alitoa msimamo huo jana wakati akihutubia maelfu ya wakazi wa mji wa Makambako katika mfululizo wa ziara ya maandamano na mikutano ya hadhara ya chama hicho inayoendelea kwenye mikoa ya nyanda za juu kusini.
Alisema ikiwa wabunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM) watatumia wingi wao vibaya kupinga ajenda ya kupunguzwa kwa kodi, CHADEMA itarudi kwa wananchi kutumia nguvu ya umma mpaka kieleweke.

Alisema hali ngumu ya maisha inayowakabili Watanzania hivi sasa inasababishwa na kodi kubwa ya ongezeko la thamani (VAT) iliyowekwa katika bidhaa na huduma mbalimbali hivyo kufanya bei za mahitaji mbalimbali ya kimaisha kuwa juu.
Alisema CHADEMA haipingi serikali kutoza kodi lakini inapinga kodi kuwa kubwa katika bidhaa na huduma mbalimbali bila kujali uwezo wa mdogo wa kipato walio nao wananchi.

“Watanzania wanataabika kwa sababu ya kodi zinazotozwa. Laiti Watanzania wangejua serikali inachukua kodi kiasi gani, laiti Watanzania wangejua. Tutapiga mzigo ndani na nje ya nchi mpaka kieleweke, tunakwenda kuwasha moto kwenye bunge la bajeti,” alisema Mbowe.

Mbowe alitoa mfano wa bei ya sukari akisema katika kilo moja inayonunuliwa mwananchi hukatwa kodi ya sh 750.

Pia alitoa mfano wa soda ambazo alibainisha kuwa bei yake kiwandani haizidi sh 150 lakini kwa sababu ya kodi ya takriban sh 300 iliyowekwa, gharama za usafiri na faida ya muuzaji, soda moja huuzwa kwa sh 500 hadi 600.

“Mfuko mmoja wa simenti unapoununua unakatwa kodi ya sh 8,000, ukinunua bia unakatwa kodi ya sh 750…kila kitu unachonunua ni kodi kodi kodi. Ukilipia umeme kodi..kama kodi hizi zingepunguzwa maisha yenu yangekuwa nafuu sana. Tutawasha moto katika Bunge la bajeti, wakiutumia vibaya wingi wao tutarudi kwa wananchi nchi nzima, tutatumia nguvu ya umma mpaka kieleweke,” alisema Mbowe na kushangiliwa.

Alisema serikali ya CCM licha ya kukusanya kodi kubwa kwa mwezi ya sh bilioni 27 wakati wa Rais Ali Hassan Mwinyi, bilioni 295 wakati wa Rais Benjamin Mkapa na bilioni 430 kwa mwezi ya hivi sasa chini ya Rais Jakaya Kikwete, bado maisha ya Watanzania yamezidi kuwa magumu kwa sababu ya pesa hizo kuibwa na kutumiwa vibaya.

Alitoa mfano wa matumizi mabaya ya kodi ya wananchi yaliyowahi kufanywa na serikali kuwa ni kudai imenunua ndege ya Rais kwa takribani sh bilioni 40 wakati ndege hiyo ikiwa na thamani ya takribani sh bilioni 20.

Mifano mingine ya matumizi mabaya ya kodi ya wananchi aliyoitoa Mbowe katika mkoa huo, ni viongozi kutumia pesa nyingi kujilipa mishahara, posho na kugharamia matibabu yao nje ya nchi.
Katika mkutano huo Mbowe alipokea wanachama wapya kutoka kwenye vyama mbalimbali vya siasa akiwemo aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Makambako, Edson Msigwa.

Msigwa alisema ameamua kuachana na CUF baada ya kuona chama hicho kinashirikiana na CCM kutumia vibaya raslimali za taifa. “Nimeamua kuachana na CUF kwa sababu imefunga ndoa na CCM, sasa CHADEMA ndio chama pekee cha upinzani cha kutumainiwa katika kupigania haki na maslahi ya Watanzania,” alisema Msigwa.
 
Kenya walifanya hvyo bungeni na kikaeleweka,ila msisahau pia kujipanga kuhusu katiba,nina wasiwasi ccm ikaitoa mada ya katiba kwa kisingizio cha mda kuwa mfinyu kwa hyo suala la katiba kuondolewa na kuegemea bajeti
 
Safi,timizeni wajibu wenu makamanda. Msiwe Kama wale washangiliaji kila hoja ya serikali na kuzomea kila kisemwacho kuipinga serikali
 
Mheshimiwa Mnyika................, chairman kalonga na sisi msituangushe.
Support yako ni: Lisu, Mdee, Zitto, Regia etc
 
I like Mbowe he puts things in perspective for a layman. Chadema mkiendelea na ufafanuzi wa namna hii kuhusu dhuruma ya kodi basi watu wataelewa na itakuwa rahisi kuwasha huo moto baada ya bunge la budget.
Hivi vipi pia swala la PAYE mbona imekaa vibaya. Tunaofanyakazi kwenye makampuni ya private tunakaangwa sana na PAYE sijui kama watumishi wa umma hili shoka linawapitia pia. Mfanyakazi analipa PAYE na bado analipia kodi zote za bidhaa.
Nikianagliaga PAYE huwa nalengwalengwa na machozi maana ni kama nafanyia kazi serikali na tumbo.
 
Mradi wasiuze mashirika ya umma.....kodi siyo sababu,faida ndiyo sababu
 
Kuwasha moto haisaidii kama budget itapita

Sasa ninaamini kwanini CDM wanafanya wanaenda kwa wananchi kuwaeleza yale viwavi wachumia tumbo wa magamba waliyotumia wingi uliopatikana kifisadi/wizi wa kura kupinga.
Ninaunga na nitaunga mkono maandamano. leteni hoja zenu kwetu tutazifanyia kazi. Msiogope wingi. Wapitishe uchafu wao sisi tunaelewa. Tunao uwezo wa kupunguza miaka mitano ya ofisini hadi miwili. Sisi ni WAAJIRI WAO TUU.
 
Uh! Watanzania tunatabia yakushabikia matukio badala ya matokeo, thread imekaa vizuri lkn vilaza wa ccm watakubali.
 
yani tunasubiri kwa hamu wasishushe ili tuandamane na ikiwezekana tuwaondoe kabla ya 2015.
 
Back
Top Bottom