Mbowe: Tatizo la Mukama kaanza siasa uzeeni

Kwa masikitiko makubwa naomba niseme kuwa Yusuf Makamba alikuwa bora kuliko huyu Mukama. Mambo aliyoongea Mukama ni aibu tupu kwa CCM, Ikulu na Waziri Membe.

Mukama anasema makomando walipata mafunzo Libya 1990. Sijui kama anaugua ugonjwa wa kusahau lakini labda tumkumbushe huyu mzee kuwa vyama vingi vya siasa vilianza baada ya 1990 na hivyo kama kuna mafunzo ya makomando yaliyofanyika 1990 basi yatakuwa ya CCM maana kipindi hicho nchi ilikuwa chini ya chama kimoja (ccm). Na ufahamu wangu hadi 1990 uhusiano wa Tanzania na Libya haukuwa mzuri kihivyo. Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere bado alikuwa hai na asingeruhusu mahusiano ya karibu na Libya nchi iliyotupiga mabomu wakati wa vita ya Uganda. Mukama hajatulia!

Pili, madai kwamba CHADEMA wanaleta makomando toka nje ya nchi kama ni kweli basi CCM hawana sifa hata chembe ya kuongoza nchi hii tena. Nasema hivyo kwa sababu kwa serikali ya ccm kukaa kimya huku ikiwa na taarifa ya kuingia nchini watu wanaotishia usalama wa raia wake (Igunga na pengine popote nchini) ni usaliti wa hali ya juu. Na swali ambalo Mukama na serikali ya ccm wanatakiwa kujibu ni hili, usalama wetu sisi raia ukoje? Tayari tumeshakumbwa na milipuko ya mabomu, na pia ndege za kivita toka nchi nyingine (Qartar) zimekuwa zinatuwa kwenye viwanja vyetu vya ndege na kuchukuwa wanyama kupeleka kwao na serikali hii ya wakina Mukama ikikaa kimya! How safe are we under ccm government?

Juzi Mukama huyu huyu alitembelea nyumba wanayodai imechomwa moto na wafuasi wa CHADEMA huko Igunga. Kwa mshango nyumba imeungua isipokuwa karatasi linataja jina la CHADEMA! Narudia, nyumba imengua lakini karatasi yenye maneno 'CHADEMA si wanajidai wajanja' haikuungua. Pengine wanasayansi wanaweza kutuasaidia hapa kwamba inakuwaje karatasi hii haikuungua? Haya ndio mambo ya kitoto na ni fedheha kwa watanzania kuwa na viongozi wenye uwezo mdogo wa kufikiri kama huyu Mukama.

Mwisho, badala ya Mukama kuhuburi hizi siasa za mwaka 1947 ni vizuri atoe maelezo kwa nini tunafanya uchaguzi Igunga leo hii? Kwa nini Rostam Aziz aliachia nafasi yake ya ubunge kwa madai ya kuchoshwa na siasa uchwara? Na je Mukama kama mtendaji mkuu wa ccm ana mkakati gani wa kuiepeusha CCM na siasa uchwara? Hii mipasho ya mafunzo ya makomando amwachie Hadija Kopa na Kapteni Komba. Mukama asitupotezee air-time tena.

You can simply call mukama the hopless ccm secretary general.
 
Jambo lingine la kushangaza Mkama anadai eti Chadema walichoma banda la KUKU, mwenyenyumba pamoja na majirani walishindwa kuuzima moto huo uliokuwa unaunguza banda la kuku wakaenda kulala.[/QUOTE



HA HA HA HA HA HA HA HA nimecheka mbaka tumbo limeuma, very stupuid oldman
 
Mukama amesahau kapten komba alienda malawi kukampenia bakil muluzi mafunzo alichukulia wapi?
 
mi nilifikiri ni mambo ya siasa tu kumbe kweli? aisee kumbe box

''Alisema katika kipindi cha uchaguzi ni jambo la kawaida kwa chama chenye wapenzi wengi kama Chadema na CCM yenyewe kupokea mashabiki, makada na wapenzi kutoka nje ya eneo la uchaguzi. Mbowe alisema Chadema kina wapenzi na mashabiki kadhaa kutoka nje ya wilaya ya Igunga, lakini akaeleza kuwa siyo makomandoo kama anavyodai Mukama vinginevyo atoe ushahidi na kuwataja kwa majina''

Umeona eeeee!! hebu check hiyo statement hapo juu??? kuna kautata kuhusu hii habari, hebu ngoja tuvute subra.
 
Tuhuma zilizotolewa na Mukama si za kubeza kwani ndanimwe zimehusisha si tu Chadema bali pia hata Nchi walizochukua mafunzo hao makomandoo na kuonyesha vyombo vyenu vya ulinzi na usalama havifanyi kazi kwa umakini.

Ni vizuri akahojiwa na vyombo husika kuthibitisha kauli yake ili kuondoa khofu kwa wakaazi wa Igunga na wapiga kura wote.

Hapo kwenye red: (nchi) Mukama ametaja Afghanistan na Pakistan. Duniani kote inaeleweka nchi tajwa ni maarufu kwa kufunza magaidi na wahalifu wengine waliokubuhu kama maharamia na wauza mihadarati. Hilo neno "makomandoo" limeegeshwa na baada ya muda litabadilishwa ghafla kuwa "magaidi" lengo likiwa kujaribu kujenga taswira nyingine mbele ya jamii kwamba CHADEMA ni chama cha kigaidi na kiharamia.

Baada ya ukabila, ukanda, na hatimaye udini kuelekea kufifia linatafutwa lingine na usishangae magamba wote wakaanza kushabikia upuuzi huu. Kweli CCM mahututi.
 
Mwenyekiti wetu kasema kweli kabisa, mzee mkama kaanzia siasa uzeeni, tena akiwa amestaafu utumishi wa umma.

Na ndio maana watu wengi ambao hawakupitia mambo fulani enzi za ujana wao, wakishakuwa watu wazima na wakafanikiwa kupata vijisenti vya kubadilisha mboga, wanasumbua sana vibinti mitaani.

Sasa huyu mzee mukama naye anaumwa ugonjwa wa namna hiyo, hajawahi kushiriki siasa za ushindani hadi anastaafu utumishi wa umma then anakabidhiwa madaraka makubwa ndani ya chama, sasa anaishia kutunga propaganda za hovyp kabisa hata mzee makamba ana unafuu na tulikuwa tunamsamehe kutokana na kiwango chake cha elimu kuwa cha kawaida, sasa huyu mukama na shahada zake mbili ndiye anaongea utumbo kabisa.

vp na huyu kitibu mkuu wenu mchukua wake za wa2 uzeeni huenda hakuchukua vibinti vya washkaji zake ujanani?
 
Mtaaibika nyie mnaotumia nguvu nyingi kukanusha maelezo ya mukama.Unakumbuka yaliyowapata viongozi wa dini kuhusu madawa ya kulevya.Wabunge waliona live kabisa na wakapendekeza wanyongwe.LISEMWALO LIPO WANDUGU MUKAMA TUSIMDHIHAKI YAWEZA KUWA AMETONYWA NA TISS.
 
Police wapo wapi??? wamkamate na atoe ushahidi wa kuwepo magaidi Tanzania..Police wakikaa kimya sasa inaonyesha na wao magamba.Mbona hijabu watu wametiwa ndani? Mukama kusema watakaa kimya? Masaburi manene nyie....people for changes
 
Yani ccm wana boa kweli na siasa zao mchwara hayo mambo anayoyaongea huyo mzee hayana kichwa wala miguu, watu wameamka wanajua kuchambua mambo hivyo wanazidi kujishushia handi. Kifo cha ccm kimefika kama wenzao wa zambia wajiandae tuu.
 
Hapo Mheshimiwa Mbowe ameonyesha anavyoijua siasa. Ni kweli huyu Mzee amechoka sijui CCM walimpaje uongozi?! Big up mpaka kieleweke
 
Me nahisi wapenzi wa chadema wamelogwa na viongozi wao,tena uchawi wenyewe wa kinaigeria!! Hawaoni madudu ya chama chao!! YAANI MIJAMAA INAPELEKESHWA KAMA ZOMBIES FLANI HIVI!!! CHADEMA CANT BE TRUSTED,NEVER
 
Alidhani siasa ni sawa na kazi za ofisini za kuvaa tai na kula kiyoyozi, si ametoka Urusi juzi atazidi kuzeeka hadi wajukuu zake wamsahau.
...Na sharubu zake zile kama Vasco da Gama....Hana mvuto kabisa yule mzee sijui nini magamba kiliwafanya kumteua kuwa Katibu.
 
Hamkumwelewa Babu Mukama alivyosema Makomandoo alimaanisha wabunge wa CDM walioko Igunga kwenye Kampeni, maana kamapeni ya mbunge moja wa CDM ni sawa na wabunge 10 wa CCM. Kumbe bora hata ya Makamba huyu hovyo kabisa
 
me nahisi wapenzi wa chadema wamelogwa na viongozi wao,tena uchawi wenyewe wa kinaigeria!! Hawaoni madudu ya chama chao!! Yaani mijamaa inapelekeshwa kama zombies flani hivi!!! Chadema cant be trusted,never
ni heri ulogwe na chadema ambayo haijawahi kuiongoza nchi yetu kuliko kulogwa na mwizi,taahira,jambazi la mali ya uma,wanafiki,wachoyo,magaidi,wasema uongo na walafi ccm kwa miaka 50 hakuna kilichofanyika nchi yenye rasilimali kibao inakuwa ombaomba rais wa nchi anakuwa kiguu na njia wakati nchi ipo kwenye matatizo kibao yeye anakimbilia kupiga picha na 50 cent.
Umebadili id lakinihaikuasaidii wewe ni msaliti kwa sababu ya kamlo unachopatiwa na hao wezi ila nakuambia ole wako.
 
CCM mkae kushoto, mkajitazame upya, mrudi tena kwa watu muaangukie, labda 2025 mtachukua tena nchi
 
Kwa sababu ya akili yako ndogo ndio maana utakuwa umejiongezea matatizo na presha

rejao, yapange masaburi yako vyema...nadhani pilipili nyingi za kihindi zinakuzingua....sio lazima ujibu vingine unasoma unaacha...kwani nape anakulipa shilingi ngapi kwa contribution moja?
 
Back
Top Bottom