Mbowe, Slaa, Zitto, Mnyika na CHADEMA wote kwa Ujumla

Tatizo la kuzungumza bila kufanya utafiti, ndugu yangu vijana wengi sana wana vitambulisho na hili linatokana na wengi kugundua kuwa vitambulisho vile vinaweza kutumiwa katika shughuli nyingine kama benk, kuchukulia pesa tigopesa etc. Mnaposhindwa mkubali kushindwa sio kutafuta vijisababu visivyo na msingi.

Kuwa na kitambulisho na kuwa kwenye daftari la kupigia kura ni vitu viwili tofauti je hawa wapigaji kura wote uko Arumeru wanathibitishiwa vipi kuwa watatendewa haki yao ya kikatiba ya kumchagua mbunge wao wanaomwitaji? na hawa vijana wapya wenye moyo wa kujiandikisha na kupata haki yao ya msingi watafanyaje ingawa hawana vitambulisho?
 
uboreshwaji wa daftari la wapiga kura ni wajibu wa kila mtu kwa nafasi yake kama vile makanisa,vyombo vya habari,asasi zote za kiraia,mashirika na makampuni yote,makundi ya kijamii,vyama vyote vya siasa,vyuo na wanataaluma. Wote wapaze Sauti kuboreshwa hili daftari ili watu wenye sifa wapate nafasi ya kutumia haki yao ya kikatiba kupiga kura.
 
good je chadema wanamkakati gani kupinga hoja ya nec ya kutoboresha daftari la wapiga kura uko arumeru?
 
hapana tusilishwe propaganda za ccm vijana wengi wa Arusha kwa jumla wamejiandikisha ila hizi propaganda kuwa chadema ina wafuasi wengi hawajajiandikisha ni kuwaandaa watu kisaikolojia kupokea matokeo ya uchakachuaji bila kulalamika ni sawa na propaganda zile kuwa wapinzani wapo mijini tu ccm wanaiba kura vijijini watu wanakuwa kimya maana wameshaandaliwa kisaikolojia, Arumeru mashariki waliopiga kura 2010 ni 55,698 mnataka kusema hao ni wazee na wanawake?? hapa panaandaliwa mazingira ya kuhalalisha wizi wa kura!!
 
Mkuu,

Hapa nakubaliana na wewe, ila CCM wakiamua tume ya uchaguzi itangaze kuwa mgombea wao ndiye kashinda basi itakuwa hivyo na hakuna tutakachoweza kufanya; maana tume ni yao, Polisi ni yao, Jeshi ni lao....yaani is very complicated kusema kweli!

Kawaambie huo mchezo haupo tena! waliweza kufanya hivyo siku za nyuma..acha majeshi ya hapa hata waongeze na mamluki lazima watangaze matokeo halali..waambie wajaribu arumeru waone kitakachotokea!
 
Umesahau kuwasisitiza kutoacha kuendeleza mahusiano na KANISA, maana hii ndio ROHO ya uhai wa CHADEMA!

Shekh Yahya aliyekuwa anasaidia magamba kuwasilisha ujumbe kuwasafishia njia ya mauaji umemsahau? Au yeye ni mkristo?
 
ARUMERU MASHARIKI
Candidate
Political Party
Number of Votes
Percentage Votes
SUMARI JEREMIAH SOLOMON
CCM
34,66162.23
JOSHUA SAMWEL NASARI
CHADEMA
19,12334.33
JOHN YESAYA PALLANGYO
CUF
2650.48
LINDA PENIELI BANA
JAHAZI ASILIA
1760.32
FANUEL GABRIEL PALLANGYO
TLP
880.16
CHARLES MOSES MSUYA
UPDP
880.16
HII NDIO HALI HALISI YA 2010 PAMOJA NA UCHAKACHUAJI WA KUTISHA
SPOILT VOTES 1,297 2.33
TOTALS 55,698

mkuu nimependa majibu yako kwa kutoa takwimu halisi
 
Kaka tatizo sio Nec tatizo ni washabiki wa CDM na Viongozi wao angalia uitoke nje ya mada tafadhali tunataka kujua uboreshwaji wa dafatri la wapiga kura je NEC inaruhusu watu kwenda kujiandikisha kwasasa? ili nyie wapenda CDM vijana muweze kulikomboa jimbo la Arumeru? au ndio bla bla tuu viongozi tafadhali majibu

Kwa sasa na ilishawekwa clear kuwa NEC haitaandikisha wapiga kura wapya. Sheria zinongoza mchakato wa kuboresha daftrai na ni mara mbili tu baada ya kila uchaguzi.
 
ninachdhani ni cha msingi ni wizi wa kura, haya mengine yalishapitwa wakati, sas hivi hakuna anayeifikiria ccm, awe mzee, mama au baba achilia mbali vijana, na ndiyo maana chama icho kikongwe kilibwagwa maeneo ambayo hata hayakutegemewa, na huko wazee, akinamama na wizi ulitumika lakini hawakuambulia kitu.

cha masingi ni kuhamasisha watu kwenda kupiga kura siku ikifika, mabadiliko lazima
 
Kwa siku kazaa kumetokea majibishano concern Arumeru je mmeshafanyia hizi tafiti na mkajua mtashinda?

1. Kuboresha Daftari la wapiga kura
Ikumbukwe hili ndilo jambo la msingi kabla ya kuingia kwenye chaguzi ndogo Arumeru kwa kusema hivi ni kwamba tulio wengi hapa kila kukicha topic ni Arumeru CDM itashinda so, kivipi? au ndio ushabiki pasipo kujua takwimu halisi za mtaji wa kura zitakazopigwa jimboni hapo na walioandikishwa kwenye daftari la wapiga kura?

2. Vijana, tukubali CDM ndio mtaji mkubwa kwenu sasa mnatakwimu zozote zinazowaonyesha kuwa ni idadi ya vijana wangapi wamejiandikisha kwenye daftari la NEC? mkumbuke CCM pale inayo takwimu ya wanachama wake na inaitaji wangapi zaidi ili ishinde chaguzi je nyie vipi? au ndio mnalewa na umati wao pasipo kujua takwimu zao?

3. Je kwa wazee/ kina mama wote wa Arumeru na hapa ndio hasa CCM inategemea je nyie mmejiimarisha vipi kupata kura zao?

4. Mgombea wenu anakubalika? na anahistoria nzuri hapo Arumeru? kafanya nini or elimu yake ipo vipi na muonekano wake kwa jamii ikoje?

5. Mmejipanga vipi na wizi wa kura hili swala tusingependa tena ikawa ni sababu yenu ya kushindwa uchaguzi, tena tumelisikia mda mrefu na tunategemea mmeshapata majibu yake yakiwamo na kununuliwa kwa vitambulisho vya kupigia kura, vituo hewa, watu kupewa mlungula na vitisho vya wapiga kura nk?

JF and GT plse toa mchango wako wenye kuisaidia CDM ili ifanikishe malengo yake pia kina Slaa, Zito na Myika wapo humu tunaomba michango yao kuhusu Arumeru na mategemeo ya CDM kwa ujumla.

Gerald,

Asante kwa maoni yako; hata hivyo naomba nisijibu kwa kina maswali yote yaliyopo kwenye namba 2 mpaka 5, kuyajibu maswali hayo ni sawa na kuandika hadharani mikakati na mbinu ya ushindi. Lakini nikuhakikishie kwamba kiutendaji maoni mbalimbali yanazingatiwa na tunafuatilia kwa karibu mijadala mbalimbali mnayoifanya. Kazi Arumeru iliishaanza kwa mujibu wa ratiba ambayo tumeitangaza: Ratiba ya CHADEMA ya Uchukuaji Fomu na Uteuzi wa Mgombea wa jimbo la Arumeru Mashariki. Tunakaribisha maoni zaidi kwa kuwa pamoja na kuwa tayari kazi imeenza ngazi mbalimbali huko Arumeru, uteuzi wa mgombea, mikakati na bajeti vyote kwa ujumla wake vitadhibitishwa kwenye mkutano wa kamati kuu unaotarajiwa kufanyika Machi mwanzoni.

Suala no. 1 la uandikishaji wa wapiga kura wapiya ni la kisheria, lina kikwazo cha kisheria kwamba tume inafanya uboreshaji kwa vipindi na si kwa kufuata kila uchaguzi mdogo unaotangazwa; tumelitafakari suala hili faida na hasara zake (cost benefit analysis) na kuona kwamba tutalipa msukumo wa kisheria wa marekebisho ya sheria husika katika hatua za baadaye. Kwa kuwa suala hili ni la kisheria na kiutendaji, ili kuilazimisha tume kufanya uboreshaji inahitaji kwenda kuibadili sheria mchakato wake unachukua muda mrefu, katika kipindi hicho CCM ambayo tayari ilishaanza hujuma za aina mbalimbali ikiwemo kwa kutumia mamlaka zingine za kiserikali itapata muda mrefu wa kufanya hujuma husika. Mpaka ukifika kipindi cha kutangazwa kwa uchaguzi tayari watakuwa wameziba fursa ya hali mbaya waliyonayo hivi sasa na hitaji la mabadiliko waliloonyesha wananchi wa Arumeru kwa kutumia mbinu zingine haramu. Aidha, hata kama ukiibana tume kiutendaji, ikatumia nafasi hiyo kuboresha daftari kwa haraka; kwa muundo na mfumo wa tume na fungate lake na watendaji wa kiserikali ambao hupokea maagizo toka CCM, tutaingia katika kazi nyingine ya kudhibiti uchakachuaji wa daftari lenyewe. Hivyo, ni afadhali kuelekeza nguvu kwenye kuunganisha umma kwa kazi ambayo walishaianza vizuri mwaka 2010 kuhakikisha kwamba CHADEMA inashinda uchaguzi husika, ikumbukwe kwamba katika uchaguzi huo hata vijana ambao ndio inaelezwa kwamba wengi wahajajiandikisha walijitokeza kupiga kura. Kuandikisha wapiga kura wapya kungesaidia tu kusafisha daftari, kuingiza vijana wengine zaidi na kuwezesha wananchi kutimiza haki yao ya kikatiba na kiraia ya kupiga kura kwa ukamilifu. Haki hii tutaendelea kuisimamia kwa ajili ya chaguzi zinazofuata, lakini katika huu tunajipanga kuwashinda kwa hali iliyopo kama tulivyofanya kwenye uchaguzi mdogo wa Ubunge wa Tarime mwaka 2008; "kumchinja Kobe kunahitaji timing; strike the hammer while, the iron is hot"

JJ
 
Ukweli ni kwamba vijana wengi wamepata mwamko wa siasa wakati uchaguzi na baada ya uchaguzi wa 2010, lakini pia tumeweza kushinda majimbo mengi kwani tulishindaje? Arumeru tutapambana hadi mwisho, ccm haina sifa za kushinda uchaguzi wowote kwasasa!
 
Gerald asante kwa maswali ya uchokozi kwa uongozi wa CHADEMA.

Kimsingi majibu aliyotoa Mhe: Mnyika nayakubali ingawa....

Ila nimeipenda falsafa ya kushindana na CCM ktk uwanja wao, kwa kanuni zao na mechi ikichezeshwa na refa wao wenyewe na KUWASHINDA. Lazima kuonyesha uthubutu na uwezo kufanikisha hilo. It's a gung-ho approach!
 
Mkuu umenena sana, binafsi hakuna kitu kinaniumiza kichwa kwenye chaguzi ndogo zaidi ya WIZI WA KURA, uchakachuaji wa daftari la mpiga kura,na ununuaji wa shahada ili kulazimisha ushindi,tumeona kwenye chaguzi nyingi,ile ya igunga ndio usiseme ccm bila kutumia uharamia na ahadi za mawaziri wao kwa wananchi wa igunga jimbo lilisha ondoka,nakubaliana na wewe mkuu viongozi wa CDM ,wanachama na wapenzi wa CDM tunajifunza nini juu ya matatizo haya na jinsi ya kuyaondoa???yanawezekana kuyadhibiti hata kabla ya katiba mpya kwani katika uchaguzi wa 2010 ilishindaje kwenye majimbo yaliyokuwa ya ccm????ni kujipanga tu.
 
Kwa hiyo tuhesabu kuwa IMESHAKULA KWA CDM...maana waliopo kwenye daftari ni wazee - ambao ni wapigakura wa CCM.

Mara moja moja si mbaya ukachanganya na zako, yani kirahisi rahisi unakubaliana na ujinga huu kwamba arumeru mashariki hakuna vijana. Nani kakudanganya kwamba wazee hawaiungi mkono chadema?

Pamoja na ccm kuanza propaganda za kuwateka akili baadhi ya watu wasioweza kutafakari sawa sawa kwamba daftari lisipoboreshwa wao ndio watajinyakulia ushindi kwakuwa wapiga kura wengi ni wazee na akina mama, lakini watu wenye akili zao na wanazitumia vizuri kutafakari wanajua kwamba uchaguzi huu ni mgumnu sana kwa ccm kuliko chadema.
 
Gerald,

Asante kwa maoni yako; hata hivyo naomba nisijibu kwa kina maswali yote yaliyopo kwenye namba 2 mpaka 5, kuyajibu maswali hayo ni sawa na kuandika hadharani mikakati na mbinu ya ushindi. Lakini nikuhakikishie kwamba kiutendaji maoni mbalimbali yanazingatiwa na tunafuatilia kwa karibu mijadala mbalimbali mnayoifanya. Kazi Arumeru iliishaanza kwa mujibu wa ratiba ambayo tumeitangaza: Ratiba ya CHADEMA ya Uchukuaji Fomu na Uteuzi wa Mgombea wa jimbo la Arumeru Mashariki. Tunakaribisha maoni zaidi kwa kuwa pamoja na kuwa tayari kazi imeenza ngazi mbalimbali huko Arumeru, uteuzi wa mgombea, mikakati na bajeti vyote kwa ujumla wake vitadhibitishwa kwenye mkutano wa kamati kuu unaotarajiwa kufanyika Machi mwanzoni.

Suala no. 1 la uandikishaji wa wapiga kura wapiya ni la kisheria, lina kikwazo cha kisheria kwamba tume inafanya uboreshaji kwa vipindi na si kwa kufuata kila uchaguzi mdogo unaotangazwa; tumelitafakari suala hili faida na hasara zake (cost benefit analysis) na kuona kwamba tutalipa msukumo wa kisheria wa marekebisho ya sheria husika katika hatua za baadaye. Kwa kuwa suala hili ni la kisheria na kiutendaji, ili kuilazimisha tume kufanya uboreshaji inahitaji kwenda kuibadili sheria mchakato wake unachukua muda mrefu, katika kipindi hicho CCM ambayo tayari ilishaanza hujuma za aina mbalimbali ikiwemo kwa kutumia mamlaka zingine za kiserikali itapata muda mrefu wa kufanya hujuma husika. Mpaka ukifika kipindi cha kutangazwa kwa uchaguzi tayari watakuwa wameziba fursa ya hali mbaya waliyonayo hivi sasa na hitaji la mabadiliko waliloonyesha wananchi wa Arumeru kwa kutumia mbinu zingine haramu. Aidha, hata kama ukiibana tume kiutendaji, ikatumia nafasi hiyo kuboresha daftari kwa haraka; kwa muundo na mfumo wa tume na fungate lake na watendaji wa kiserikali ambao hupokea maagizo toka CCM, tutaingia katika kazi nyingine ya kudhibiti uchakachuaji wa daftari lenyewe. Hivyo, ni afadhali kuelekeza nguvu kwenye kuunganisha umma kwa kazi ambayo walishaianza vizuri mwaka 2010 kuhakikisha kwamba CHADEMA inashinda uchaguzi husika, ikumbukwe kwamba katika uchaguzi huo hata vijana ambao ndio inaelezwa kwamba wengi wahajajiandikisha walijitokeza kupiga kura. Kuandikisha wapiga kura wapya kungesaidia tu kusafisha daftari, kuingiza vijana wengine zaidi na kuwezesha wananchi kutimiza haki yao ya kikatiba na kiraia ya kupiga kura kwa ukamilifu. Haki hii tutaendelea kuisimamia kwa ajili ya chaguzi zinazofuata, lakini katika huu tunajipanga kuwashinda kwa hali iliyopo kama tulivyofanya kwenye uchaguzi mdogo wa Ubunge wa Tarime mwaka 2008; "kumchinja Kobe kunahitaji timing; strike the hammer while, the iron is hot"

JJ

Myika,
ahsante kwa majibu yako ila ni vizuri kama mmejizatiti vyema tusingependa kusikia tena hizi story za uchakachuaji,vituo hewa, nk na ndio maana nikasisitiza mmejiandaaje? Kwa mda sasa Igunga,Uzini na mwanzo wa chaguzi hizi kauli tumezisikia mno na kwa matumaini ya wapenzi wa CDM wasingependa kusikia the same story wakati mmeshasema mmejizatiti, kumbuka wapenzi wa cdm wanaitaji angalau kifuta machozi cha kushinda hilo jimbo ili propaganda zao ziweze kua hai vinginevyo mtawakatisha tamaa nawatakia kila la kheri na mungu awe juu yenu.
 
Back
Top Bottom