Mbowe, Slaa, Zitto kulipua bomu Mwanza

leseiyo

Senior Member
Oct 25, 2007
116
3
Na Reuben Kagaruki
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kesho kutwa kinatarajia kufanya mkutano mkubwa wa hadhara mkoani Mwanza kutoa tathmini ya mapambano ya vita dhidi ya mafisadi.

Mkutano huo unaotarajiwa kuhutubiwa na Mwenyekiti wake, Bw. Freeman Mbowe, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya mwaka mmoja tangu CHADEMA itangaze orodha ya mafisadi 11 katika mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Mwembeyanga, Dar es Salaam, Septemba 15, mwaka jana.

Akizungumza na gazeti hili Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa CHADEMA, Bw. David Kapalila, alisema mkutano huo pia utahudhuriwa na viongozi wengine wa kitaifa wa chama hicho.

"Katika mkutano huo viongozi wa CHADEMA wataeleza mwelekeo wa vita dhidi ya ufisadi na jinsi CCM ilivyoshindwa kupambana nayo,"alisema Bw. Kapalila.

Alisema kutokana na CCM kushindwa kupambana na vitendo hivyo, chama chake kitatumia mkutano huo kutangaza mkakati maalumu wa kupambana na mafisadi ili kutokomeza vitendo hivyo.

Mbali na Bw. Mbowe, alitaja viongozi wengine watakaohutubia mkutano huo kuwa ni pamoja na Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Wilbroad Slaa, naibu wake, Bw. Zitto Kabwe na Mwanasheria wa chama hicho, Bw. Tundu Lisu

Bw. Kapalila alisema mkutano huo ni sehemu ya utekelezaji wa maazimio ya kikao cha Kamati Kuu kilichokutana hivi karibuni jijini Dar es Salaam.

Katika mkutano uliofanyika viwanja vya Mwembeyanga, mwaka jana Dkt. Slaa akisaidiwa na Bw. Lisu walitaja orodha ya vigogo 11 waliodaiwa kuhusika na vitendo vya kifisadi.

Baadhi ya viongozi hao ni aliyekuwa Waziri wa Miundombinu, Bw. Andrew Chenge, aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Bw. Nazir Karamagi, Katibu Mkuu Hazina, Bw. Gray Mgonja na aliyekuwa Waziri Mkuu, Bw. Edward Lowassa.

Baadhi ya vigogo waliotajwa kwenye orodha hiyo walitishia kumburuta Dkt. Slaa mahakamani, lakini hadi leo hakuna aliyethubutu kuchukua hatua hiyo.
 
Kama ni kurudia yale yale ambayo kila mtu anayajua hakuna hata haja ya mkutano, ishu ingekuwa kutumia nguvu, shinikizo na msaada wa nchi zinazosaidia katika bajeti kuhakikisha kuwa mafisadi wote wamechukuliwa hatua, short than that ni kumpigia mbuzi gitaa.
 
Kama ni kurudia yale yale ambayo kila mtu anayajua hakuna hata haja ya mkutano, ishu ingekuwa kutumia nguvu, shinikizo na msaada wa nchi zinazosaidia katika bajeti kuhakikisha kuwa mafisadi wote wamechukuliwa hatua, short than that ni kumpigia mbuzi gitaa.

Itawezekana pale tu utakapothubutu kuongeza nguvu kwao na kupunguza nguvu kwenye ngome kuu ya ufisadi......

Tanzanianjema
 
habari imeandikwa tangu juzi usiku itakuwaje BREAKING NEWS au ndio unazi wa CHADEMA umekujaaa tuu?

Hivi hawa bado wanazo politics za kulipua mabomu? washamsahau huyu mwenzao?

j6.jpg
 
nao waachane na maneno, wamtume Tundu Lissu aandae mashitaka dhidi ya mafisadi waende mahakamani
 
habari imeandikwa tangu juzi usiku itakuwaje BREAKING NEWS au ndio unazi wa CHADEMA umekujaaa tuu?

Hivi hawa bado wanazo politics za kulipua mabomu? washamsahau huyu mwenzao?

j6.jpg

Huyu ndiyo wa kupewa nchi...Mimi nitampigia kampeni huyu...Huyu ni mkombozi na mzalendo...HUYU NDIYE SHUJAA.....Hata akifa leo jina lake tutapigana liwekwe kwenye historia...SAHAMANI..UNAFIKI NAWEKA KANDO.
 
Haya mabomu mwisho yatawalipukia wenyewe ,si mumeona kwenye gazeti la leo yule jamaa aliemlenga ngedele kumbe amejilenga mwenyewe na kufwa papo hapo baada ya kufyatua gobole.
 
CCM wadaiwa kuhusika wizi wa EPA kuendeshea kampeni 2005

Na Salim Said
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Wilbrod Slaa ameendelea kuibana serikali na sasa ameibuka na jipya kuwa fedha zilizoibwa kwenye Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), zilitumiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuendeshea kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka 2005.

Dk Slaa alitoa tuhuma hizo jana akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam.

Alisema fedha hizo bado hazijarejeshwa ndio sababu serikali imeshindwa kuwataja waliozirejesha au kuwachukulia hatua za kisheria.

Dk Slaa alisema fedha hizo za EPA hususan za Kampuni ya Kagoda na Deep Green Finance zilitumiwa na CCM kuendeshea uchaguzi mkuu wa 2005 uliomuweka madarakani Rais Jakaya Kikwete.

"Hatujawahi kusema maneno haya lakini leo tunatangaza rasmi kwamba fedha za EPA hususan za Kagoda na Deep Green Finance zilitumiwa na CCM kwenye kampeni za uchaguzi mkuu wa 2005 ulioiweka madarakani serikali hii ndio maana inashindwa kuwachukulia hatua za kisheria wahusika," alsema Dk Slaa.

Alisema kauli za kurejeshwa kwa fedha hizo ni za kujikanganya na kwamba hazijarejeshwa, jambo ambalo limeifanya serikali kushindwa kueleza kiasi kilichorejeshwa na wahusika waliozirejesha.

"Hazijarejeshwa kwani hata Rais hakuwa tayari kusema ziko wapi alipotoa hotuba yake bungeni, Akaunti maalum za serikali zipo sita na hakuna hata moja kati ya hizo ambayo imeingiza fedha za EPA au Rais atuambie ni ipi kati ya hizo iliyotumika kurejesha fedha hizo," alisema.

Alisema Kamati Kuu ya Chadema imesisitiza kuwa uamuzi wa Rais Jakaya Kikwete kushindwa kuwafikisha mahakamani wezi wa EPA ni mfano mbaya wa utawala.

Alifafanua wezi wote wa EPA wanakabiliwa na kosa la wizi na sio deni na hivyo kuwataka warejeshe fedha hizo ni sawa na kuvunja sheria kwa kubadilisha kesi ya jinai na kuwa kesi ya madai.

Hata hivyo CCM kwa nyakati tofauti iliwahi kukana tuhuma za kuhusika kwake na kueleza kuwa wananchi wasubiri uchunguzi wa timu ya Rais ambayo hata hivyo haikuwekwa hadharani.

Kuhusu wajibu wa Chadema kupambana na ufisadi, Dk Slaa alisema Kamati Kuu ya chama hicho, imeagiza kuwa kazi hiyo iendelee mpaka hapo serikali itakapoamua ama kuondoka madarakani au kuwachukulia hatua mafisadi.

''Ili kupanua wigo wa mapambano dhidi ya ufisadi nchini, Kamati Kuu imeazimia kuwa viongozi wote wa chama kuanzia ngazi ya tawi wanapaswa kuchukua hatua za kupambana na vitendo vyote vya kifisadi vinavyofanywa na serikali katika maeneo yao na kuwasilisha taarifa hizo katika uongozi wa juu wa Chama,'' alieleza Dk Slaa.

Aidha Dk. Slaa alisema Chadema inaendelea na mashtaka dhidi ya watu na vyombo vyote vya habari vilivyohusika katika kuwachafua viongozi wa chama hicho kwa kuandika habari zilizolenga kuharibu sifa ya chama na viongozi wake mara baada ya kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Tarime Chacha Wangwe.

''Kamati Kuu imeiagiza Secketarieti kuwasiliana na jeshi la polisi kutoa ufafanuzi iwapo kwenye upelelezi wao kuhusu kifo cha Wangwe kuna sababu nyingine zaidi ya ajali iliyosababisha kifo hicho na kama ipo Kamati Kuu itaomba uchunguzi kufanyika," alisema Dk Slaa.

Alisema Kamati Kuu ya Chadema imeunda kamati ndogo ikiongozwa na Muasisi wa chama hicho,Bob Makani kufanya uchunguzi dhidi ya viongozi na wanachama wanaotuhumiwa kukihujumu chama katika ngazi mbalimbali.

Alifafanuwa kuwa taarifa ya kamati hiyo itawasilishwa kwenye kikao kijacho kwa ajili ya hatua zaidi kuchukuliwa kwa wote watakaobainika kuhusika.

Akizungumzia kuhusu matumizi ya ruzuku, Dk Slaa alisema kutokana na hisia kuwa fedha za ruzuku zinaishia Makao Makuu, Kamati Kuu inamtaka Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Fedha za Serikali (CAG), kuiweka hadharani taarifa yake ya ukaguzi wa fedha za vyama vya siasa ambavyo vinapata ruzuku ya serikali kuanzia 2005 hadi mwaka huu.

Kuhusu shutuma za ubaguzi na ukabila ndani ya chama, alisema ni mkakati wa dhahiri uliolenga kukichafua chama unaofanywa na wapinzani wao na kutokana na hali hiyo wametoa orodha ya viongozi wakuu, wakurugenzi na maafisa waandamizi wa chama makao makuu kwa majina na maeneo wanayotoka.

''Tunafahamu kuwa uongo ukiachwa utamalaki Watanzania wanaweza kuamini uongo huo kuwa ndio ukweli, mfano kati ya viongozi watano wa ngazi ya taifa ni mmoja tu anatoka Kilimanjaro (Mchaga), na kati ya wakurugenzi 10 walioteuliwa na kamati kuu ni watatu tu wenye asili ya Mkoa wa Kilimanjaro (Wachaga) huku kati ya Maofisa waandamizi 12 ni mmoja tu Mchaga" alisema Dk. Slaa.

 
Nimeshasema hapa ukumbini kwetu mwanana kwamba ufisadi hautakwisha Tanzania mpaka CCM wafundishwe adabu na wapiga kura kwa kuondolewa madarakani, vinginevyo hakutakuwa na la maana lolote kuhusiana na mapambano ya mafisadi.

Sasa ni karibu mwaka mmoja hakuna aliyekamatwa, majina ya waliorudisha hizo pesa ambazo hakuna anayejua zimewekwa wapi bado ni siri. Mafisadi bado wanaendelea kupeta na mabilioni yao haramu ndani na nje ya nchi. Hata Waziri Mkuu Pinda, Mwanasheria Mkuu Mwanyika na Mkuu wa polisi walithubutu kutamka hadharani kwamba mafisadi ni matajiri wakubwa hivyo kuwakamata kutasababisha nchi iwake moto! Kwa maana nyingine serikali yenye jeshi lilimtoa nduli na "kuikomboa Comoro", polisi, FFU, na wananchi 40 millioni wanaounga mkono mapambano dhidi ya ufisadi linaogopa kikundi cha mafisadi kisichokuwa na watu hata 1,000! Only in Tanzania!
:(:(:(
 
Kwa hiyo Rais wa Jamhuri ya Tanzania Mh Jakaya Mrisho Kikwete alilidanganya Bunge la jamhuri na amevunja sheria kwa kubadili kosa la uhalifu kuwa la madai. Kesi ifunguliwe sasa
 
Sasa hivi imeanza kusikika kwamba Tayari wameanza kukusanya pesa za uchaguzi kwa kuchota kasma za seikali.

Yaonekana kuchota BOT itakuwa ngumu na kelele zitasikika tena. Sasa Wizara zinakata mafungu kukipa chama ili kufikia 2010 wawe na kitita cha kutosha.

Waulize walioko maofisini, utaambiwa hakuna hata karatasi za kuandikia ingawa baadhi ya Wizara zina nyongeza ya bajeti kuliko miaka ya nyuma.

Naona makatibu wakuu bado ni Makada wa Chama.
 
...zimewekwa katika bank ipi na ni kiasi gani maana mnatoa namba ambazo zinapingana mara shilingi bilioni 53, mara shilingi bilioni 60. Hebu twambie ukweli pesa hizi ziko wapi na ni kiasi gani?

CHADEMA: Fedha za EPA hazijarudi

na Salehe Mohamed
Tanzania Daima~Sauti ya watu

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema fedha zilizoibwa katika akaunti ya malipo ya madeni ya nje (EPA) hazijarejeshwa na serikali inaogopa kuwachukulia watuhumiwa hatua kwa sababu fedha hizo zilisaidia kuipa ushindi CCM mwaka 2005.

Kauli hiyo imetolewa jana jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, baada ya kumalizika kwa kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho kilichofanyika Septemba 6, mwaka huu.

Alisema fedha za EPA, hazijarejeshwa kama serikali inavyotaka Watanzania waamini, kwani kama kweli zimerejeshwa wangeweza kuwataja waliozirejesha na kuwafikisha mahakamani na hiyo inaonyesha wazi udhaifu wa utawala wa Rais Kikwete.

Alisema wezi walioiba fedha hizo hawakutakiwa kulipa peke yake, kwani hilo halikuwa deni bali walipaswa kufikishwa mahakamani kwa kosa la jinai na wala si kubadilisha kesi hiyo kuwa ya madai.

Aliongeza kuwa hata taarifa za kiasi cha fedha kilichorejeshwa mpaka hivi sasa zimekuwa za kujikanganya kutokana na serikali hasa ya CCM kujua chimbuko la fedha hizo na matumizi yake.

"Udhaifu wa utawala wa Rais Kikwete hasa katika kupambana na ufisadi umebainika wazi hasa baada ya kushindwa kuwafikisha mahakamani wezi wa EPA, fedha hizo hazijarejeshwa," alisema Slaa.

Alisema dola limeyumba kutokana na udhaifu ulioshindwa kusimamia mali na rasilimali za taifa dhidi ya genge dogo la mafisadi ambao sasa wanaamua mwelekeo wa Serikali ya Rais Jakaya Kikwete.

Aidha, alisema CHADEMA, itaendelea kusimamia vita dhidi ya ufisadi mpaka hapo serikali iliyopo madarakani itakapoamua kuachia ngazi na kuachana na majibu ya ujanja ujanja kwa masuala yanayohusu upotevu wa fedha za wananchi maskini.

Alibainisha kuwa hivi sasa kuna mkakati wa kuhujumu taswira nzuri ya CHADEMA hasa kwa kumuhusisha Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe, na kifo cha aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wake marehemu Chacha Wangwe.

Alisema vyombo vya habari, baadhi ya wanasiasa wa kambi ya upinzani na CCM wamekuwa wakitumia msiba wa marehemu Chacha Wangwe, kujijenga, jambo ambalo ni kinyume na utamaduni wa Mtanzania.

"Vyama vya siasa vinapaswa kujikita katika ajenda za siasa na wala si kutumia misiba ya watu au kuchafuana, jambo hilo ni hatari kwa maendeleo ya taifa," alisema Slaa.

Aliongeza kuwa Kamati Kuu, imepokea taarifa ya awali ya jopo la wanasheria wake na kulielekeza jopo la wanasheria wa chama kuendelea na mashitaka dhidi ya watu na vyombo vya habari vinavyohusika katika kuwachafua viongozi wa chama.

Alisema hivi sasa kuna mkakati wa kuuaminisha umma kuwa CHADEMA imekuwa ikifuja ruzuku inayopata kwa ajili ya ofisi kuu, jambo ambalo si sahihi bali linafanywa ili kuidhoofisha dhidi ya mapambano yake ya ufisadi.

Alisema ili kuuthibitishia umma jambo hilo si kweli, inamtaka Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuiweka hadharani taarifa yake ya ukaguzi wa fedha kwa vyama vya siasa ambavyo vinapata ruzuku ya serikali kuanzia mwaka 2005.

Kuhusu kuwapo kwa ukabila katika CHADEMA alisema hizo ni hoja za kikabila zinazoenezwa kwa makusudi na tayari walishazitolea ufafanuzi.

CHADEMA imetangaza kuwa Septemba 15 kila mwaka itakuwa ni kumbukumbu ya vita dhidi ya ufisadi nchini, na mwaka huu kitaifa itaadhimishwa jijini Mwanza chini ya ujumbe wa ‘Chukia Ufisadi, Tetea Rasilimali.'
 
Sijui mpaka Mungu ashuke ndiyo wajue kuwa si tu ni kosa bali ni dhambi?
 
Mabomu ni muhimu hasa kwa SISEMU kwani huwafanya wasiwe standby tena na ufisadi na kushughulikia kujisafisha NA KUTAFUTA MCHAWI si unajua. Hapo then BOT panakuwa shwari kwani wanakosa muda wa kupiga misele BOT.

Hivyo kabla wamalize kujisafisha tunapiga bomu jingine kwa kosa jingine kwani wana makosa idadi sawa na fedha zilizoibwa BOT. Hivyo ni mkakati wa ki-inteligensia haswa kwa wanaoweza kufikiri what I want to bring or make it home.

Mbinu ni hiyo hiyo tu hamna nyingine ili kuwapotezea mood ma appetite ya kuiba pesa kwa sababu inaelekea wakiwa idle wanakuwa na ample time nyingi ya kutupiga mabao makavu kama walivyofanya ya BOT na kwenye mikataba na miradi mbalimbali. Now tunawaweka busy ikiwa hawataki kutushughulikia wananchi na wana muda wa ufisadi we see that they are damn idle ndo mana wanakwiba. Wevi kabisa hawa wanachama na viongozi wa SISIEMU. Au vipi invicible

Mabomu huwaweka busy na ku-alert them on their f**kin behaviour
 
Kiasi kwani wameishiwa na sasa sera zao ni kulipua mabomu, bahati mbaya hayalipuka yanbaki ardhini na accidentally yanakuja walipukia wenyewe!
 
Kiasi kwani wameishiwa na sasa sera zao ni kulipua mabomu, bahati mbaya hayalipuka yanbaki ardhini na accidentally yanakuja walipukia wenyewe!

Ndio kama la Chacha Wange ,si unaliona linavyofuka moshi ,nasikia Mtikila amekamata utambi ?
 
Hiyo ni kweli ila ukihoji utaaambiwa lete ushahidi ama futa kauli. Udikteta katka demokrasia.

Tanzania bado ila tunaelekea anyway hata mwalimu angekuwa hai nchi ilpofika asingeweza elewa ni nini kinatokea angehisi labda hata kuna jamaa wako msituni siku yeyote watatokeza. Inatisha watu wamechoka na kila siku nyimbo zile zile hata tune haibadiliki!
 
Sasa mnategemea nani amkamate nani wakati ni wao kwa wao ? Jeshini wamo ,Polisini wamo,usalama wa Taifa wamo,kwenye upinzani wamo wamechomekwa ,Serikalini ndio wamejaa ,hivi hamkufahamu maana ya Chama kushika hatamu ? CCM wamekamata mpini na anaetokeza pua tu atakiona kilichomfanya Mbuni asiruke japo ni ndege mwenye mbawa kubwa tu.
 
Kutoa tathmini sio kitu kibaya. Nini kimefanyika toka oradha ya aibu itajwe. Wananchi walipokeaje hizo taarifa, na wamezifanyia kazi vipi? Tunawasubiri waheshimiwa mtuletee mengine zaidi.

Ni muhimu kukomaa na mafisadi na vibaraka wao...na wengine tunao humu humu kwenye jamvi. Msianze kupiga ramli. Ebo!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom