Mbowe, Slaa wala pilau ya Iddi na wananchi Morogoro

armanisankara

JF-Expert Member
Jul 15, 2011
283
49
katuni%20jaki...2.jpg

Viongozi wakuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wakiwa na baadhi ya viongozi wa chama hicho wanaoshiriki Operesheni Sangara wakila chakula na wananchi kusherehekea Idd El Fitri mjini Morogoro juzi. Kutoka kushoto ni Arcado Ntagazwa, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa, Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Zanzibar, Said Issa Mohamed na Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe.


Viongozi wa wakuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wakiongozwa na Mwenyekiti wa Taifa, Freeman Mbowe, juzi walilazimika kusimamisha ziara za vuvugu la mabadiliko (M4C) katika Operesheni Sangara wilayani Mvomero ili kushiriki na wananchi chakula cha sikukuu ya Eid El Fitri.

Aidha, Mbowe alitumia muda huo kuwaaga viongozi wenzake pamoja na makamanda wanaoshiriki operesheni hiyo mkoani Morogoro huku akieleza kuwa anatarajia kwenda Florida, Marekani wiki hii kwa shughuli za kuimarisha chama.

Mbowe aliambatana na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Zanzibar, Said Issa Mohamed, Katibu Mkuu, Dk. Willibrod Slaa, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Yusuph Mohamed, viongozi na makamanda wa chama hicho walioko Morogoro kwa shughuli za operesheni ya vuguvugu la mabadiliko.

Wote walishiriki chakula hicho katika mtaa wa Konga Manispaa ya Morogoro.

Akizungumza na wananchi baada ya chakula hicho, Mbowe aliwashukuru makamanda wa chama hicho kwa kushiriki vema katika kampeni za M4C mkoani humu na kueleza kuwa shughuli za ukombozi zinahitaji watu wenye moyo na kujituma.

"Nawapongeza sana makamanda kwa kazi mnayoifanya hapa Morogoro napenda kuwaongezea chachu katika harakati za ukombozi wa mkoa wa Morogoro ambao umeangukia mikononi mwa Chama Cha Mapinduzi,” alisema.

Alisema baada ya kumalizika kwa sikukuu ya Eid, wabunge wa Chadema wataungana na operesheni hiyo kwa awamu na kwamba kwa sasa wabunge hao wamerejea majimboni kwao kwa muda baada ya Bunge la Bajeti kumalizika.

Alisema baadhi ya wabunge sita wataungana na operesheni ya M4C mkoani Morogoro na wengine wataungana na timu ya operesheni mkoani Iringa ikiwa ni pamoja na yeye mwenyewe.

Mbowe, ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani bungeni na Mbunge wa Hai, alisema chama chake kimejipanga kufanya mkutano mkubwa katika Jimbo la Morogoro na viongozi wote wa chama hicho watashiriki.

Aliwataka wakazi wa mkoa wa Morogoro kutoa ushirikiano kwa timu ya operesheni chini ya mkuu wa operesheni hiyo, Benson Kigaila, ili kuwezesha dhamira ya chama hicho ya kuwawezesha wananchi wa mkoa huu kubadilika na hatimaye kuona umuhimu wa kukichagua chama hicho katika uchaguzi ujao.








CHANZO: NIPASHE

 
Nawaambieni ya kwamba janga letu kubwa la Taifa letu ccm tu!

Hakika sisi sote ni wa ndg moja kama alivyosema member mwenzangu na hata Mi nakoleza!

ccm yao ngumu hakika!
M4c tu pamoja A to Z na hakika ni mpaka kieleweke!

2015 naona ni mbali lakini tutafika tu kwani hakika tuna MUNGU aliye hai!
 
Aiseee baba yangu magamba walidai hiki chama ni cha kidini sasa wanafanyaje hapa

ngoja nikate mbege
 
Hongereni viongozi kwa kuonyesha mshikamano,adui yetu ni ccm,sisi sote ni ndugu moja.

Wewe kila siku huwa unasema una chama leo vipi tena unasema adui yenu ni CCM yaani viongozi wa Chadema kula pilau ndio kuonyesha ushikamano...
 
hao walio vaa nguo nyekundu unawafahamu? unajua kazi zao?. Muulize aliyekuwa mkuu wa wilaya Igunga mh.Fatuma. mia
 
Wameonesha mshikamano na rushwa. Picha hizi Ritz zitatumika wakati wake ukifika.
Rushwa gani acha kuchachawaa kwani kushiriki na wananchi kula ni rushwa ??? viongozi wa CDM wanaonyesha mshikamano na wananchi. Hakuna jambo baya kula na wananchi ni upendo. CCM wamezoa kutoa rushwa za chakula ndio maana wanachanganyikiwa

Tanzania ni nchi ya amani mitazamo na tofauti za kivyama sio itufanye tuwe maadui..vyama vya siasa vinapita tu utaifa wetu upo milele.....

Tupendane
 
Tanzania ni nchi ya amani mitazamo na tofauti za kivyama sio itufanye tuwe maadui.Vyama vya siasa vinapita tu utaifa wetu upo milele.
wewe unaota ndoto,yaani mie nataabika na maisha wewe unaponda mali bila kutoa jasho unadai eti niwe rafiki yako wakati unaniibia huku nakuona.hiyo amani unayo wewe na sio watanzania kama unavyodai.amani ya maneno siifagilii,angalia watu wanavyoteseka na umasikini,unyanyasaji wa kikatili na serikali ya magamba.mnawakandamiza,kula mlo mmoja wenyewe kwa shida,hawana uhakika na afya zao,mbaya zaidi elimu mnaizika kila kukicha,natamai uwe ritz tu na usiwe riz.one.
 
Dr si ana kisukari? au alikuwa anagonga mweupe na mboga mboga kwa wingiiiii!
 
Back
Top Bottom