Mbowe: Sikumtangaza Dr. Slaa mgombea urais 2015

...si nilisikia hili gazeti la mwananchi huwa linapelekewa habari na kiZito flani baada ya kuziandika mwenyewe....!!Nilisikia tu.
ninalofanyika na ccm hivi sasa ni kutafuta namna ya kuwagawa viongozi wa chadema sasa dawa ya sasa hivi kila watakacho sema kuhusu chadema sisi wana chadema tunajua ni uongo. sisi kazi yetu ni kufuata linalosemwa na viongozi wetu, ccm mnajisumbua.mbona amgusii meli iliyokamatwa na meno ya Tembo?.meli hiyo ni ya nani?
 
Calculator, 'love your enemy'. sihami post kirahisi sana. I deal with current issues. Tuko kwenye urais kwa sasa, ubunge baadae. Sina shida na mtu yeyote, ninachosema tuwe huru kutoa mawazo yetu kwa kuangalia uhalisia wa mambo. Tusiwe mandumilakuwili. Hoja hiyo hiyo akitoa Calculator jamii inamuandama, lakini the same issue akiitoa Computer, watu wanamshambulia kwa kashfa zisizokuwa na msingi. Tujadili hoja na sio mtu. CHADEMA kama taasisi inatakiwa kuwa makini kabla ya kutoa kauli kwenye vyombo vya habari.

Jipange vzr sana unapoingia kwenye mission ya kuchezea akili zetu.
 
Naona kauli ya Mwenyekiti Mbowe imewapa kupumua kidogo,maana mkisikia jina Dr.Slaa mnachanganyikiwa
mpaka wajukuu zenu. Hata Mbowe asipotangaza ukweli utabaki palepale kuwa chaguo la watanzani kwa urais
ni Dr.Peter Slaa. Kaeni mkao wa kunyolewa hii haina mjadala.

haa ha haa haa munanichekesha yaani mh Mbowe anakimbia kivuli chake BORA NIENDELEE NA HARAKATI ZA KUTAFUTA MDHAMANA WA SHEIKH PONDA
 
wewe unaelalamika ni chadema? sisi wanachadema Dr Slaa ni Nyerere wa tanzania,kwa hiyo wanachama wa chadema Slaa ndie tunamtaka agombee, wewe ccm unalalamika nini,?.kwa upande wenu mtu anaefaa kugombea urais ni Mwakyembe,maana ndie anaonekana mchapa kazi, lakinimkwa upande wetu sisi kama chadema hakuna kama Dr Silaa kwa sasa.
 
Jipange vzr sana unapoingia kwenye mission ya kuchezea akili zetu.

Its Freshthinking yaani fikra mpya sio kuchezea akili bali kunoa akili. Natamani ufikiri bila ushabiki. Lakini kukulazimisha siwezi.
Kuna wana demokrasia wa kweli Tanzania lakini platforms wanazotumia zinawaangusha kwa vile zilianzishwa kwa malengo binafsi badala ya jamii.
Inapotokea changamoto kama hizi za wasio waanzilishi kutaka kuleta mapinduzi/ mabadiliko ndipo unapogundua migongano na magomvi baina yao. Issue kubwa ni kuchumia tumbo yaani UBINAFSI. 'Love your enemy'
 
Wakuu,mi naona hapa kila mtu aliyeeleza kuhusu Dk Slaa kugombea Uraisi 2015 alikuwa anaongea kutokana na hisia zake na kusikiliza maoni ya wananchi kuhusu wanataka nani apeperushe bendera ya Chadema,ndo maana ukiangalia alichokizungumza Lema,Mzee Mtei na hata ukiwauliza wananchi wa humu mtandaoni na ambao hawapo mtandaoni utapata jibu hilohilo na ndio maana hata gazeti la mwananchi lilipopotosha habari ya Ndugu Mbowe kumtangaza Dr Slaa watu wengi walimuunga mkono kutokana na mapenzi yao kwa Dk. LAKINI CHA KUKUMBUKA NA KUSHIKA NI UAMUZI WA MWISHO WA CHAMA.
 
Anajikomba ili arudishwe TBCCM, walilete habari ya kichonganishi juu ya Nasari, Halima Mdee na Firikunjombe juu ya Zitto wakaambulia aibu sasa na hii wataambulia aibu maana mikutano ya chadema huwa wana chukua Video..
Mwananchi si lakuaminika tena Tido keshalirudisha Magambani Ccm hoyeeeeeeeeee
 
haa ha haa haa munanichekesha yaani mh Mbowe anakimbia kivuli chake BORA NIENDELEE NA HARAKATI ZA KUTAFUTA MDHAMANA WA SHEIKH PONDA
tatizo letu sisi waislamu ni kudhani kwamba ccm ni ya wislamu kwa kuwa rais wake ni mwislamu.hivi serikali ya kikwete amuoni inavyofanya.utapa wapi dhamana kwa ponda,ushangai dhamana anapewa Lulu muuaji ponda mwenye kuda tu, mali anashikiliwa rumande,lazima tukubali kwamba,Chadema wana dhamira ya kweli kuikomboa nchi hii. hivi ni kwa nini atulioni hili?
 
wewe unaelalamika ni chadema? sisi wanachadema Dr Slaa ni Nyerere wa tanzania,kwa hiyo wanachama wa chadema Slaa ndie tunamtaka agombee, wewe ccm unalalamika nini,?.kwa upande wenu mtu anaefaa kugombea urais ni Mwakyembe,maana ndie anaonekana mchapa kazi, lakinimkwa upande wetu sisi kama chadema hakuna kama Dr Silaa kwa sasa.
Huyu mnafiki mkubwa, alipe deni la Richmond kwanza au aendelee kusimamia msimomo wake wa juu ya swala la Richmond na siri alizozibakiza mpka zina muua taratibu aziseme...
 
Tanzania hata ukisema ukweli unalaumiwa, Nauliza kwa sasa nani kama Dr Slaa Tz hii? Hata kama mbowe alisema ndo awe mgombea kupitia CHADEMA, mimi naona yuko sahihi kabisa maana ndo uongozi huo, kuonesha njia sio kusubiri watu wanataka nini. Kumbuka Mkapa alisikiliza watu wanataka nini matokeo yake ni kutupa raisi feeeeki kabisa duniani.
 
Huyu mnafiki mkubwa, alipe deni la Richmond kwanza au aendelee kusimamia msimomo wake wa juu ya swala la Richmond na siri alizozibakiza mpka zina muua taratibu aziseme...
hiyo ndo tabu yenu ccm embu niambie ni nani wewe unaemuona anachapa kazi zaidi ya mwakyembe na makufuli,?
 
Mkuu, gazeti la mwanachi waliamua kupotosha hiyo habari kwa sababu zao.

Ndio maana wengi wetu hum Jf tulihoji utofauti wa hiyo habari kati ya mwananchi na Tanzania daima.
Mwananchi Mkurugenzi wake mkuu ni mtu makini sana (Mzee wetu alieyeondolewa TBC) na Wahariri wake ni makini sana maana mmoja wao ni katibu wa jukwaa la wahariri, sasa inakuwaje wanaacha habari hizi zipite bila kuakiki?
 
Back
Top Bottom