Mbowe: Sikumtangaza Dr. Slaa mgombea urais 2015

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by SEBM, Jan 3, 2013.

 1. S

  SEBM JF-Expert Member

  #1
  Jan 3, 2013
  Joined: Mar 7, 2012
  Messages: 495
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 18
  Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amenukuliwa akikanusha kutanganza kuwa Dkt. Slaa atakuwa mgombea wa Urais kupitia CHADEMA 2015. Alifafanua kuwa, alichokisema katika Mkutano wa hadhara Karatu mwishoni mwa wiki ni kuwa;

  1. CHADEMA haina Mgogoro bali ni mitazamo tofauti baina ya watu (hali ya kawaida panapokuwa na wengi)

  2. Hana nia ya kugombea urais 2015.

  3. Yeye na Dkt Slaa hawagombanii urais 2015. Dkt Slaa amefanya mengi katika Chama na hata uchaguzi wa 2010 alisaidia kupatikana kwa wabunge wengi.

  4. Akiwa Mwenyekiti wa Chama, atasimamia upatikanaji wa wagombea bora wa urais, ubunge na udiwani.

  Source: TANZANIA DAIMA 03/01/2013.

  MY TAKE

  1. Gazeti la Mwananchi limekuwa mstari wa mbele kuandika habari za upotoshaji kuhusu CHADEMA.
  2. Gazeti la Mwananchi huibua habari bila ya ku-balance mambo au kutupa mwendelezo(continuity).
  3. Nia ya Mwananchi si kuongeza tu readership/circulation, bali ni kupotosha kwa malengo wanayoyajua wao. Mfano Habari ya Mh. Arfi, Habari ya Lema. Habari ya Mh. Lema
   
 2. SINA JINA1

  SINA JINA1 JF-Expert Member

  #2
  Jan 3, 2013
  Joined: Feb 24, 2012
  Messages: 393
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  gazeti la mwananchi wameanza kulewa sifa sasa wanaharibu
   
 3. E

  ESAM JF-Expert Member

  #3
  Jan 3, 2013
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 957
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 18
  Mimi nilijua tu Mbowe na busara zake asingeweza kusema kama media zilivyoripoti. Sasi sana mwenye kiti kwa ufafanuzi
   
 4. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #4
  Jan 3, 2013
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,860
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 38
  Hili gazeti limeshanunuliwa na magamba!
   
 5. Nicole

  Nicole JF-Expert Member

  #5
  Jan 3, 2013
  Joined: Sep 7, 2012
  Messages: 4,284
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Litakuwa limeingia kwenye payrol ya nepi
   
 6. s

  sabas matata Senior Member

  #6
  Jan 3, 2013
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  waandishi makanjanja hao!
   
 7. MTENGETI

  MTENGETI JF-Expert Member

  #7
  Jan 3, 2013
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 2,227
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 38
  Hivi Mwananchi sisi si ndio tulioipandisha Chati baada ya Masumbuko Lamwai kuleta za kuleta na Majira yao. Mnaonaje kilichoitokea majira kirudi Mwananchi. KWA PAMOJA TUNAWEZA. dawa ni kulisusia tu kama inavyofanyika kwa majira, Uhuru, Mzalendo na mengine mengi ya Kidaku.
   
 8. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #8
  Jan 3, 2013
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,532
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 38
  Unapojibu habari unatengeneza habari. Ila kisiasa sio mbaya kila habari inatengenezwa kwa maana maalum.

  Nilijifunza hili mwaka 1998 mwezi August tarehe 28.

  Hivi vyama sijui vimelogwa?, Naibu katibu anabwabwaja, Mwenyekiti naye anabwabwaja, Angalau katibu!

  Nitaendelea kubakia bila chama kwa kweli
   
 9. Shardcole

  Shardcole JF-Expert Member

  #9
  Jan 3, 2013
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,308
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 38
  Hilo gazeti ni kipenzi chama kiongozi mmoja wa juu wa CDM.
   
 10. W. J. Malecela

  W. J. Malecela JF Tanzanite Member

  #10
  Jan 3, 2013
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 11,779
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 38
  - Nice sasa amesoma alama za nyakati na kujua kwamba alipotoka kuamua nani awe mgombea, all under Operation Chaos lakini the damage is done tayari!! too late!

  Le Mutuz!
   
 11. MTENGETI

  MTENGETI JF-Expert Member

  #11
  Jan 3, 2013
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 2,227
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 38
  Au Tiddo anataka kurudi TBC?
   
 12. M

  Mzee wa fund JF-Expert Member

  #12
  Jan 3, 2013
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 520
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Chezea propaganda za magamba ninyi?Eee!!!
   
 13. Mohamedi Mtoi

  Mohamedi Mtoi R I P

  #13
  Jan 3, 2013
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,326
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 0
  Kina TUNTEMEKE Ritz na TandaleOne wana mkanda walio mrekodi Mbowe ngoja waje watusikilizishe.

  Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. Shardcole

  Shardcole JF-Expert Member

  #14
  Jan 3, 2013
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,308
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 38
  ngoma ni ile ile 2015 Dkt.Slaa for presidency mpaka mkae.
   
 15. MD25

  MD25 JF-Expert Member

  #15
  Jan 3, 2013
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 3,112
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 38
  Inanikera sana pale mtu mzima wa miaka 45+ anapokua anategemea "ugali wa kengere".... yeye anachofanya ni u-PIMP TU...
   
 16. Shardcole

  Shardcole JF-Expert Member

  #16
  Jan 3, 2013
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,308
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 38
  Mkuu huyo TUNTEMEKE sijui huwa ni chama gani kwani kazi yake yeye ni kupotosha tu.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 17. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #17
  Jan 3, 2013
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 39,337
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 83
  Hivi na wewe uwa Chadema? Haya siyo maneno yangu namnukuu Molemo,

  "Familia imeishaamua Dr Slaa ndiyo mgombea urais 2015 kupitia Chadema. Dr Slaa atosha" Molemo wa JF.

  Wewe na Mtei nani mwenye chama?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. Shoo Gap

  Shoo Gap JF-Expert Member

  #18
  Jan 3, 2013
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 225
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 18
  MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, amesema baadhi ya vyombo vya habari vimemlisha maneno, na hivyo kupotosha kauli yake aliyoitoa katika mkutano wa hadhara jimboni Karatu hivi karibuni.

  Alisema kuwa upotoshaji huo umeibua mjadala kwa baadhi ya wanasiasa na vyombo kadhaa vya habari wakijaribu kupotosha kuwa ndani ya chama hakuna demokrasia.

  Mbowe alifafanua kauli yake jana wakati akizungumza na Tanzania Daima na kueleza kile alichokisema katika mkutano wake huo ili kuondoa upotoshaji unaoendelea.

  Alisema kuwa chimbuko la kauli yake lilikuwa ni baada ya kusikia watu wakisema kuwa kuna makundi ndani ya chama ambayo yanawaunga mkono yeye, Katibu Mkuu, Dk. Willibrod Slaa na Naibu Katibu Mkuu (Bara), Zitto Kabwe yakiwataka wagombee urais 2015.

  “Nilichokisema ni kwamba hakuna makundi katika chama, ila kuna mitazamo tofauti katika mambo mbalimbali jambo ambalo ni la kawaida sana,” alisema.

  Mbowe alifafanua kuwa, aliwaambia wananchi kuwa hawana makundi, bali wana utofauti wa mtazamo na kwamba hakuna ugomvi kati yake na Dk. Slaa kwa sababu ya urais 2015.

  “Nilisema sigombei, hivyo hatugombanii vyeo, tunaheshimiana na tunaelewana. Niliongeza kuwa 2010 sikugombea, tulimtuma Dk. Slaa na alitosha katika nafasi ile na hakuna anayebisha kuwa hakutosha maana alitupatia wabunge wengi.

  “Niliwaambia kuwa mimi ni mwenyekiti, nitasimamia kanuni na taratibu za kuwapata wagombea wazuri, tangu rais, wabunge na madiwani, na nikasema ni vema tukawatambua wagombea mapema kwani hatutakubali wale wanaojiunga mwishoni kutoka CCM kwani tumegundua ni mamuluki.

  “Hao wananilisha maneno kwa kunitolea kauli tofauti na niliyoisema kulingana na malengo yao,” alisema.

  Mbowe alisema kuwa anaomba Watanzania waelewe kuwa yeye ni mwenyekiti wa chama na anaelewa umuhimu wa vikao na kuheshimu uamuzi wa vikao hivyo.

  “CHADEMA si mali ya Mbowe, ni mali ya wanachama, hivyo siwezi kupinga suala la uamuzi wa pamoja ambao mimi mwenyewe ndio nawashauri wengine,” alisema.

  Alisema kuwa yeye ni mmojawapo wa waasisi, na amekuwa mjumbe wa Kamati Kuu zaidi ya miaka 20 sasa, na kwamba anajua maana na umuhimu wa kufanya kazi kama timu, lakini akaomba kuwa tafsiri za watu binafsi au baadhi ya vyombo vya habari zisipotoshe alichokisema.


  Chanzo: Tanzania Daima
   
 19. Mingoi

  Mingoi JF-Expert Member

  #19
  Jan 3, 2013
  Joined: Jul 21, 2012
  Messages: 8,581
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 48
  Too late azma yao imeshajulikana mgombea wa CHADEMA lazima atoke kaskazini.
   
 20. Babkey

  Babkey JF-Expert Member

  #20
  Jan 3, 2013
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 2,654
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 38
  ...si nilisikia hili gazeti la mwananchi huwa linapelekewa habari na kiZito flani baada ya kuziandika mwenyewe....!!Nilisikia tu.
   
 21. Mingoi

  Mingoi JF-Expert Member

  #21
  Jan 3, 2013
  Joined: Jul 21, 2012
  Messages: 8,581
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 48
  Mbowe katika kuizima kashfa ya ufisadi wa mradi wa maji akaona awapoze wana Karatu kwa kuwaambia Babu atakuwa raisi ajaye 2015.
   
 22. l

  lufungulo k JF-Expert Member

  #22
  Jan 3, 2013
  Joined: Apr 19, 2012
  Messages: 643
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  MSIJARIBU kulikwepa hili, wachangiaji wengi humu jf, hasa wale wenye mrengo wa CDM bila kufikiri kwa kina WALIGEUKA na kuwa sawasawa na gazeti hilo La MWANANCHI. kwa kuandika wakipongeza maamuzi hayo yakupotoshwa ya MH mbowe, TUJIFUNZE tuwe wa kwanza kukataa, kile ambacho tunaamini ni kinyume cha taratibu maana leo hii tungekuwa tunapongezana kwa kile tulichokosoa. heri yangu nilipinga .
   
 23. T2015CCM

  T2015CCM JF-Expert Member

  #23
  Jan 3, 2013
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 7,540
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  SIKU moja baada ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kumtangaza Dk Willibrod Slaa kuwa ndiye mgombea wa urais mwaka 2015 kwa tiketi ya chama hicho, makada wa chama hicho wamegawanyika baadhi wakimponda na wengine kumuunga mkono.

  Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana, baadhi ya makada wa chama hicho walisema mwenyekiti wao amekosea kumtangaza mgombea kabla ya wakati, huku wanaomuunga mkono wakisema hajakosea kwa sababu hatua hiyo itasaidia kuondoa makundi ndani ya chama hicho.

  Juzi, Mbowe akihutubia mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Karatu mkoani Arusha, alisema Katibu Mkuu wa Chadema Dk Willibrod Slaa atapewa fursa ya kuwania tena urais kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2015, huku mwenyewe akijiweka kando kuwania nafasi hiyo.

  Hata hivyo, Dk Slaa alipoulizwa iwapo ana nia ya kuwania nafasi hiyo alihoji: “Kwani mwaka 2010 nilijitangaza mwenyewe,? Iwapo wanachama wa Chadema watanipendekeza nitafikiria kufanya hivyo.” Mwasisi wa chama hicho Edwin Mtei, Wajumbe wa Kamati Kuu; Profesa Mwesiga Baregu na Dk Kitila Mkumbo, Naibu Katibu Mkuu Zitto Kabwe, Mwenyekiti wa Bavicha John Heche na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema walitoa maoni yanayopingana kuhusu kauli hiyo ya Mbowe.

  Wanaounga mkono

  Mtei alisema anaunga mkono kauli ya Mbowe akisema kiongozi huyo hajakosea kumtangaza Dk Slaa kuwania urais mwaka 2015.

  “Ninaunga mkono Dk Slaa kuwania tena nafasi ya urais mwaka 2015. Mwenyekiti amemtangaza baada ya kupata baraka ya vikao vya chama,” alisema Mtei.

  Ingawa Mtei hakuwa tayari kusema ni kikao gani kilichopitisha jina la Dk Slaa kuwania nafasi hiyo, alisisitiza: “Kuna vikao vya Kamati Kuu vimefanyika hivi karibuni, vinaweza kuwa vimefanya uamuzi huo. Mwenyekiti hawezi kuzungumza jambo bila baraka za vikao vya chama.”

  Hata hivyo, kauli hiyo ya Mtei inapingana na ile aliyoitoa Oktoba 6, mwaka huu baada ya Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini kutangaza kutogombea tena ubunge badala yake kusema anataka kugombea urais katika uchaguzi wa mwaka 2015.

  Mtei alisema hatua ya Zitto kutangaza kuwania urais mapema kungesababisha mzozo na mpasuko ndani ya chama hicho.

  Mtei alisema amekuwa akimshauri Zitto mara kwa mara kuhusu hatua yake hiyo akimtaka kuwaunganisha wana Chadema na siyo kuwagawa au kuwavuruga.

  “Hakuna shida kuonyesha hisia, lakini unatengeneza mzozo mkubwa sana ukitangaza sasa. Mimi nimeshamshauri sana Zitto, ahakikishe anakiunganisha chama na siyo kukigawa wala kukivuruga.”

  Alisema mbunge huyo kutangaza kutogombea tena ubunge na badala yake kujipanga kuwania urais mwaka 2015 kumekuja mapema mno na kuonya kuwa itaibua mzozo ndani ya Chadema.

  Mtei ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Fedha na Gavana wa Benki Kuu enzi za utawala wa Mwalimu Julius Nyerere, alisema kwamba wakati mwafaka ukiwadia, Chadema kitaamua ni nani mwenye sifa za kugombea urais huku akisema kina utaratibu wake wa kuwapata wagombea mbalimbali wa uongozi.

  Hata hivyo, Zitto jana alikataa kuzungumzia suala hilo akisema: “Nimesikia hata mimi kwenye vyombo vya habari ila sina cha kuzungumza kuhusu hilo.”

  Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha), John Heche alisema kauli hiyo Mbowe siyo yake binafsi, bali ni ya wananchi.

  “Ni kauli na maoni ya Watanzania wanaomwamini Dk Slaa kuwa anaweza kumudu kuliongoza taifa hili kama walivyoonyesha kwa kumpigia kura nyingi kuliko mgombea yeyote wa upinzani katika nafasi ya urais (mwaka 2010),” alisema Heche.

  Heche alisema ingawa ndani ya Chadema kuna viongozi wengi wenye uwezo wa kuliongoza taifa, nyota ya Dk Slaa bado inang’ara.

  Msimamo wa Heche uliungwa mkono na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema ambaye alisema ni sahihi Dk Slaa kugombea urais mwaka 2015.

  Lema alisema katika historia ya chaguzi za vyama vingi nchini, hakuna mgombea wa upinzani aliyewahi kupata kura nyingi kama Dk Slaa mwaka 2010 akadai kwamba ndiyo maana hivi sasa CCM kinafanya kila njama kumdhoofisha.

  Lema alisema hatua ya kumtangaza Dk Slaa kuwa mgombea wa urais mwaka 2015, itaondoa harakati za chinichini zilizokuwa zikifanywa na watu ndani na nje ya Chadema kuwagombanisha viongozi wakuu wa chama hicho, hasa Mbowe na Dk Slaa.

  Wanaopinga

  Wakati Mtei akieleza kuwa Mbowe amepata Baraka za chama, Profesa Baregu alisema kutangazwa kwa jina la Dk Slaa kuwania urais ni maoni binafsi ya mwenyekiti huyo.

  “Hayo ni maoni yake, lakini vikao vya chama ndivyo vyenye uamuzi wa mwisho kuteua jina la mgombea urais na havijakaa,” alisema Profesa Baregu.

  Alipoulizwa maoni yake kuhusu sababu za Mbowe kumtangaza mgombea urais sasa kabla ya wakati, Profesa Baregu alisema: “Mbowe atakuwa amefanya hivyo kwa sababu watu wengi walikuwa wanadhani kwamba yeye pia anawania nafasi hiyo ya urais.”

  “Hivyo ili kuweka mambo sawa ameamua kutangaza mapema kuwa hatawania urais na kwamba Dk Slaa ndiye anayefaa kuwania nafasi hiyo,” alisema.

  Profesa Baregu alisema haoni tatizo kwa wanachama wa Chadema kutangaza nia mapema kwa sababu hiyo ni haki yao kwa mujibu wa katiba... “Hata kama watu wengi watatangaza nia ya kuwania urais, siyo jambo baya katika ujenzi wa demokrasia, lakini uamuzi wa mwisho ni wa vikao vya chama.”

  Kauli ya Profesa Baregu kuhusu vikao iliungwa mkono na Dk Mkumbo ambaye alisema kwamba anachojua vikao vya chama ndivyo vyenye uamuzi wa mwisho kuhusu uteuzi wa wagombea wa ngazi ya urais.

  Dk Mkumbo alionyesha shaka kama kweli Mbowe alimtaja Dk Slaa kuwa ndiye atakayewania nafasi hiyo akisisitiza: “Ninachofahamu ni kwamba yeye ametangaza kuwa hatagombea nafasi hiyo.”
   
 24. mdeki

  mdeki JF-Expert Member

  #24
  Jan 3, 2013
  Joined: Mar 28, 2011
  Messages: 3,240
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 38
  Aaaaah siasa,sihasa
   
 25. Tumaini Makene

  Tumaini Makene Verified User

  #25
  Jan 3, 2013
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 2,576
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 38
  Hujui unenalo. Huwezi kufanya japo utafiti kidogo tu, kabla hujaamua kubisha, achilia mbali kujenga hoja kinzani dhidi ya hoja nyingine au mtu mwingine usiyekubaliana naye!
   
 26. Mingoi

  Mingoi JF-Expert Member

  #26
  Jan 3, 2013
  Joined: Jul 21, 2012
  Messages: 8,581
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 48
  Makene viongozi wako hawana dhamana utawatetea sana lakini haisaidii kitu.Suala hapa si kujenga hoja au utafiti tatizo ni matamko na jazda za jukwaani za viongozi wako wakilenga kuiteka hadhira mwisho wake wanajikuta wameharibu.
   
 27. Shoo Gap

  Shoo Gap JF-Expert Member

  #27
  Jan 3, 2013
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 225
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 18
  Tunapaswa kuwa makini sana na magazeti yetu, yanaandika kile kitakachouza magazeti yao hata kama ni UONGO bila kuwaza athari mbaya zitakazotokea. Shetani ana tabia hiyo hiyo ya kusema ukweli 99% na kuchomeka uongo 1% ambayo ita-distort content & context ya habari yote. TUNAPASWA KUWA MAKINI SANA. Nadhani CDM wanapaswa kuwaandikia magazeti yaliyopotosha habari hii na kuwapa onyo na iwapo watarudia kufanya yanayofanana na haya watangaze kuwa haya magazeti sio adilifu ili wananchi tuyakwepe.
   
 28. Petro E. Mselewa

  Petro E. Mselewa Verified User

  #28
  Jan 3, 2013
  Joined: Dec 27, 2012
  Messages: 4,308
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 48
  Kumbe?!
   
 29. SaidSabke

  SaidSabke JF-Expert Member

  #29
  Jan 3, 2013
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 1,312
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 38
  Ina maana aliongea kichaga au kiswahili kama ni kiswahili aliyasema hayo anayoshutumiwa nayo
   
 30. Mingoi

  Mingoi JF-Expert Member

  #30
  Jan 3, 2013
  Joined: Jul 21, 2012
  Messages: 8,581
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 48
  Mkuu lufungulo,asante kwa udadavuzi leo wanakana walichokinena wao wenyewe.Tatizo la pro CDM ni kuunga mkono kila linalosemwa na viongozi wao hata kama ni la kipuuzi .
   

Share This Page