Mbowe: Nitajiuzulu siasa tusipochukua jimbo la Masasi

MHE: Wasira siku ya jana kasema kauli mbiu ya M4C sio mpya na kwamba hii ni mwendelezo wa kushindwa kuwa na falsafa moja ya kuwashawishi watanzania kuiamini kuwa CHADEMA ni Chama mbadala, Pia Chama hicho kina makundi makubwa yasiyojionyesha lakini yafukuta kama moto wa Tanuru. AKAONGEZA" Chadema imezidi Majigambo kuwahadaa wananchi kuamini kuwa watachukua nchi 2015 bila kujua kuwa siasa na uchaguzi huendana na matukio!" CCM bado IMARA katika kukabili mawimbi mazito zaidi ya haya yanayoendelea leo.-DAKIKA 45 ITV JANA.

Mkuu unatuletea nukuu toka Gombe, hizo ni muflisi hazikubaliki.
 
MWENYEKITI wa Chadema, Freeman Mbowe amesema moto uliowashwa na chama hicho katika Operesheni Sangara utaendelea nchi nzima, lengo likiwa ni kuiondoa CCM madarakani na iwapo itasalimika mwaka 2015, atajiuzulu siasa.

Mbowe alitoa kauli hiyo juzi alipohutubia mamia ya wakazi wa Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara wakati chama hicho kilipofanya mkutano mkubwa kwenye uwanja wa mpira wilayani humo.

Alisema CCM kimepoteza mwelekeo wa kuongoza taifa na ndiyo sababu maisha ya Watanzania yamezidi kuwa mgumu kadri miaka inavyozidi kusonga mbele.

“Wajibu wa Serikali kokote duniani ni moja tu, kuwezesha watu wake kutoka katika hali ngumu za maisha na kuwapeleka kwenye heri, leo CCM wameligawa Taifa katika vipande, wanauza rasilimali za nchi na kuwadidimiza watu wa kipato cha chini wengi wao wakiwa ni wakulima,” alisema Mbowe na kuongeza:

“Ndugu zangu ngojeni niwaulize swali, wakati wa utawala wa Mwinyi na Mkapa (marais wastaafu, Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa), ni kipindi gani maisha yalikuwa mazuri?” Wananchi wakajibu (kipindi cha Mwinyi). Miaka 10 ya uongozi wa Mkapa na miaka saba ya Kikwete, ni kipindi gani maisha yamekuwa magumu zaidi?" Wakajibu (Kikwete); Je, 2015 wanakuja tena kutuomba kura huyo atakayekuja si ndiyo itakuwa mbaya zaidi, Chadema hatuwezi kukubali na moto huu tuliowasha utaendelea nchi nzima hadi Uchaguzi Mkuu wa 2015 na kama CCM itasalimika nitajiuzulu siasa.”

Mbowe alikishambulia CCM akidai kimepoteza mwelekeo uliowekwa na waasisi wake, chini ya uongozi wa Mwalimu Julius Nyerere wa kuzingatia usawa, udugu huku kikijikita katika msingi wa kutetea wakulima wanyonge na wafanyakazi lakini sasa kimewagawa wananchi katika matabaka ya walio nacho na wasio nacho.

“CCM ya Mwalimu Nyerere ilijali wakulima na wafanyakazi wa kipato cha chini, ilijenga mshikamano baina ya Watanzania wote bila kujali ukabila. Tanzania ina makabila zaidi ya 120, lakini tunaishi kama mtu na ndugu yake, leo taifa limegawanyika vipande huku maadili ya uongozi yakiporomoka,” alisema Mbowe.

Katika mkutano huo uliokutanisha viongozi wote wa kitaifa wa chama hicho, Mbowe alisema kwa sasa CCM kimevuruga hata mitalaa ya elimu huku akituhumu watunga sera kuwa wanafanya hivyo makusudi kwa kuwa watoto wao hawasomi katika shule hizo.

“Mwalimu alijenga CCM iliyozingatia usawa, watoto wote walisoma shule moja, mimi nilisoma na watoto wa Mwalimu Nyerere, mawaziri na wakulima katika shule hiyo, leo watoto wa mkulima wanasoma shule za kata ambazo hazina walimu, vitabu, maabara wala library (maktaba), wakati watoto wa vigogo wakisoma nchi nje na wale wa wakuu wa wilaya wakisoma shule za (academy),” alisema Mbowe.

Aliwataka wakazi wa mikoa ya kusini, Lindi na Mtwara kuunganisha nguvu kwa lengo la kukiondoa CCM madarakani katika chaguzi zote ukiwamo mkuu wa 2015.

“Ndugu zangu wa Masasi, mimi Mbowe ninatimiza miaka 21 nikiongoza siasa za upinzani zenye lengo la kuleta ukombozi wa kweli kwa Taifa hili, nimefunguliwa kesi za uchochezi tisa hadi leo, lakini sitaacha harakati hata wakinifunga, bado nitaendelea na harakati za ukombozi hadi Watanzania watakapofikia kwenye uhuru wa kweli,” alisema Mbowe.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willibrod Slaa alieleza kusikitishwa kwake na umaskini unaoukabili Mkoa wa Mtwara licha ya kuwapo rasilimali nyingi zinazouzunguka ikiwamo gesi na korosho.

Alisema kumekuwa na ufisadi mkubwa unaofanywa katika ununuzi wa korosho na licha ya wananchi kukatwa Sh30 katika kila kilo wanayouza, bado mikoa hiyo ya kusini inakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa maji, huduma muhimu za kijamii kama zahanati na shule.

“Taifa linaweza kuendelea ikiwa rasilimali za nchi ambazo zinatoka kwa wananchi zitawarudia na kutumika katika kuendeleza miradi ya maendeleo. Leo mnakatwa Sh30 katika kila kilo moja ya korosho mnayouza, tumetafuta ni kiasi gani cha korosho kimepatikana kwa mwaka hapa nchini lakini taarifa hizo hatuzipati.”

“Lakini taarifa tulizopata Ulaya zinasema Tanzania imeuza tani 157,000 kwenye soko la dunia, haya mabilioni ya fedha mnazokatwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo zinatumika wapi?” alihoji na kuongeza kuwa fedha hizo zinastahili kudaiwa.

Source:
Mwananchi

My concern

Huu msimamo naungojea kwa hamu kuuona kama utafanikiwa na kutimia
TUmeshawazoea wakishindwa watasema wameibiwa kura.
Hiyo mimi naiita PUBLIC STUNT
 
MWENYEKITI wa Chadema, Freeman Mbowe amesema moto uliowashwa na chama hicho katika Operesheni Sangara utaendelea nchi nzima, lengo likiwa ni kuiondoa CCM madarakani na iwapo itasalimika mwaka 2015, atajiuzulu siasa.Mbowe alitoa kauli hiyo juzi alipohutubia mamia ya wakazi wa Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara wakati chama hicho kilipofanya mkutano mkubwa kwenye uwanja wa mpira wilayani humo.Alisema CCM kimepoteza mwelekeo wa kuongoza taifa na ndiyo sababu maisha ya Watanzania yamezidi kuwa mgumu kadri miaka inavyozidi kusonga mbele.“Wajibu wa Serikali kokote duniani ni moja tu, kuwezesha watu wake kutoka katika hali ngumu za maisha na kuwapeleka kwenye heri, leo CCM wameligawa Taifa katika vipande, wanauza rasilimali za nchi na kuwadidimiza watu wa kipato cha chini wengi wao wakiwa ni wakulima,” alisema Mbowe na kuongeza:“Ndugu zangu ngojeni niwaulize swali, wakati wa utawala wa Mwinyi na Mkapa (marais wastaafu, Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa), ni kipindi gani maisha yalikuwa mazuri?” Wananchi wakajibu (kipindi cha Mwinyi). Miaka 10 ya uongozi wa Mkapa na miaka saba ya Kikwete, ni kipindi gani maisha yamekuwa magumu zaidi?" Wakajibu (Kikwete); Je, 2015 wanakuja tena kutuomba kura huyo atakayekuja si ndiyo itakuwa mbaya zaidi, Chadema hatuwezi kukubali na moto huu tuliowasha utaendelea nchi nzima hadi Uchaguzi Mkuu wa 2015 na kama CCM itasalimika nitajiuzulu siasa.”Mbowe alikishambulia CCM akidai kimepoteza mwelekeo uliowekwa na waasisi wake, chini ya uongozi wa Mwalimu Julius Nyerere wa kuzingatia usawa, udugu huku kikijikita katika msingi wa kutetea wakulima wanyonge na wafanyakazi lakini sasa kimewagawa wananchi katika matabaka ya walio nacho na wasio nacho.“CCM ya Mwalimu Nyerere ilijali wakulima na wafanyakazi wa kipato cha chini, ilijenga mshikamano baina ya Watanzania wote bila kujali ukabila. Tanzania ina makabila zaidi ya 120, lakini tunaishi kama mtu na ndugu yake, leo taifa limegawanyika vipande huku maadili ya uongozi yakiporomoka,” alisema Mbowe.Katika mkutano huo uliokutanisha viongozi wote wa kitaifa wa chama hicho, Mbowe alisema kwa sasa CCM kimevuruga hata mitalaa ya elimu huku akituhumu watunga sera kuwa wanafanya hivyo makusudi kwa kuwa watoto wao hawasomi katika shule hizo.“Mwalimu alijenga CCM iliyozingatia usawa, watoto wote walisoma shule moja, mimi nilisoma na watoto wa Mwalimu Nyerere, mawaziri na wakulima katika shule hiyo, leo watoto wa mkulima wanasoma shule za kata ambazo hazina walimu, vitabu, maabara wala library (maktaba), wakati watoto wa vigogo wakisoma nchi nje na wale wa wakuu wa wilaya wakisoma shule za (academy),” alisema Mbowe.Aliwataka wakazi wa mikoa ya kusini, Lindi na Mtwara kuunganisha nguvu kwa lengo la kukiondoa CCM madarakani katika chaguzi zote ukiwamo mkuu wa 2015.“Ndugu zangu wa Masasi, mimi Mbowe ninatimiza miaka 21 nikiongoza siasa za upinzani zenye lengo la kuleta ukombozi wa kweli kwa Taifa hili, nimefunguliwa kesi za uchochezi tisa hadi leo, lakini sitaacha harakati hata wakinifunga, bado nitaendelea na harakati za ukombozi hadi Watanzania watakapofikia kwenye uhuru wa kweli,” alisema Mbowe.Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willibrod Slaa alieleza kusikitishwa kwake na umaskini unaoukabili Mkoa wa Mtwara licha ya kuwapo rasilimali nyingi zinazouzunguka ikiwamo gesi na korosho.Alisema kumekuwa na ufisadi mkubwa unaofanywa katika ununuzi wa korosho na licha ya wananchi kukatwa Sh30 katika kila kilo wanayouza, bado mikoa hiyo ya kusini inakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa maji, huduma muhimu za kijamii kama zahanati na shule.“Taifa linaweza kuendelea ikiwa rasilimali za nchi ambazo zinatoka kwa wananchi zitawarudia na kutumika katika kuendeleza miradi ya maendeleo. Leo mnakatwa Sh30 katika kila kilo moja ya korosho mnayouza, tumetafuta ni kiasi gani cha korosho kimepatikana kwa mwaka hapa nchini lakini taarifa hizo hatuzipati.”“Lakini taarifa tulizopata Ulaya zinasema Tanzania imeuza tani 157,000 kwenye soko la dunia, haya mabilioni ya fedha mnazokatwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo zinatumika wapi?” alihoji na kuongeza kuwa fedha hizo zinastahili kudaiwa.Source: Mwananchi My concernHuu msimamo naungojea kwa hamu kuuona kama utafanikiwa na kutimia
tANI 157,000 = KILO 157,000,000. WAKIWAKATA SH 30, INA MAANA WALIPATA JUMLA YA SH 4,710,000,000 WOW! ITS IS GOOD BUSINESS RELY..! (BILION 4 NA MILIONI MIA SABA NA KUMI..!!) WANA ZIPELEKA WAPI?. HIYO NI KOROSHO PEKE YAKE , ... AISEE WANALAMBA, LAKINI ITAWATOKEA PUANI. TIME WILL TELL,
 
Kama hali ilikuwa mbaya wakati wa maraisi wa nyuma yeye aliwezaje kujilimbikizia?
Au sasa mizizi yake imekatwa? Dunia nzima inalia uchumi mbaya sembuse TZ!.

Sikuzote nasema bado hatuna viongozi wenye moyo hapa TZ. Bora hili zimwi...(ccm)
kisa gani kujitoa kisiasa kama mambo hayatakuwa? Utakuwa umelisaidiaje Taifa?
 
Ana uhakika atafika hiyo 2015, maana Mungu hafanyiwi kejeli.
 
ritz Anza na Zitto Kabwe kwanza ndio alitangaza hatogombea Ubunge mwaka 2010 ili arudi kufanya kazi zake za Taaluma aliyosomea.

Hata wachezaji mpira wapo wanaoahidi asipofunga goli mechi fulani basi atajiuzulu, hizi ni dhamira anazopaswa kuwa nazo mtu Jasiri na dume la mbegu, na hata JK alipaswa kuahidi hivi kwamba asipotimiza ahadi ya kununuwa meli mpya kama ya Mv Bukoma basi tusichaguwe tena CCM.

All in all haya ni mambo ya kawaida na ni muhimu katika kuwapa watu hamasa kwani siasa nayo kuna wakati inahitaji burudani zake.

Mkuu Matola hilo la meli hebu liache kwanza watu wasije wakakumbuka !
 
Mbowe andaa barua mapema ya kujiuzulu maana kushindwa ni lazima unadanganyika kuona watu wamejaa unafikiri wote wanaiunga mkono CDM.jiandae kupata heart attack.
 
Hili wala sio jambo geni kwa wanasiasa, wakishindwa atasema ni katika kuhamasisha.

Kwani kuna viongozi wangapi walioapa kutogombea tena kisha tukaambiwa wazee wamewashauri waendelee hivyo wanasikiliza wito.
 
Ingekuwa vyema kama ungeweka dhamira yako wazi ya kupindisha heading.

Pamoja na kwamba ume-copy from Mwananchi Web site na ku-paste hapa bado ulidhamiria kupindisha heading....maana hakuna sehemu ambayo aidha Mwananchi au Mbowe ame-specify jimbo na Masasi. Kwa mtazamo wangu wa haraka ulikuwa na lengo la kupotosha wanajamii tu.
 
Wewe Gamba la kobe peleka ushauri wako Magambani

Molemo,
Tumia busara yako uliyojaliwa na Muumba wako kusoma nia za hawa wanasiasa wetu.

Sio kila anayepanda jukwaani kuiimba mageuzi ana nia njema na nchi. Wapo wengi wenye nia binafsi 90% na nchi only 10%. Kupiga kwako makofi bila kudadisi hakutaisaidia nchi.
 
Molemo,
Tumia busara yako uliyojaliwa na Muumba wako kusoma nia za hawa wanasiasa wetu. Sio kila anayepanda jukwaani kuiimba mageuzi ana nia njema na nchi. Wapo wengi wenye nia binafsi 90% na nchi only 10%. Kupiga kwako makofi bila kudadisi hakutaisaidia nchi.
Molemo siku zote hana busara
 
Back
Top Bottom