Kwenye msiba wa Bob Makani Katibu Mkuu wa CCM aliteleza na Mbowe akanyosha maneno kwa kutoa historia fupi.
Ndani ya historia kuna mahali alitaja washiriki wa kikao naye mwenyewe akiwepo kama kiongozi wa vijana.
Inawezekana kabadilika lakini kwa nini awe kibaraka wa CCM sasa ambapo CDM imeanza kupata mafanikio?
Tujadiliane kwa amani.
Tatizo la Mbowe siyo kuhisiwa kua kibaraka , bali Mbowe ni mfaidikaji mzuri sana wa historia na mfumo wa CCM, mtu wa namna hii huwezi kumuamini kama atakuja kubadilisha mifumo ya uongozi na ufanisi wa serikali akipewa nchi achilia mbali kurudisha mali zetu zilizoibiwa na kuwafunga hawa wezi...Mbowe ni mtu wa tabaka la juu la wanufaika wa uhuru wa Tz, hawezi kuwaangalia machoni na kuwaumiza na kuwazika wanatabaka wenzake hata siku moja hamna mwanajamii hata siku moja anapingana kiukweli na tabaka lake na kutetea tabaka asilokuepo. Mbowe mjanja tu anataka ubwana mkubwa basi na siyo ukombozi wa wanyonge wa Tanganyika.
Nawasikitikia wale wanyonge wanaompa matumaini makubwa huyu bwana