Mbowe na tafakuri zake...

subiri Mnyika aamke asubuhi halafu aone hii topiki mbona utajua kama chai inawekwa sukari au ndimu!
 
Hili bado sijalielewa.. kwanini tunapenda kuwadiscuss watu binafsi... tuulize alilala na nani, wapi, alikunywa nini, na msalani alienda wapi.. why why why!!!
 
Nadhani mume munder estimate FREEMAN MBOWE kuwa anaweza akawa RAIS wa nchi na kama mwanasiasa ambaye atakuwa anawajibu wa kutuwakilisha nadhani ni vizuri tukamjua na yeye au chama chake ninaweza kujibu maswali haya bila kufanya mambo ya character assassination.

Huyu ni mwansiasa aliyepata KURA NYINGI sana na yuko kwenye public domain sasa kama LOWASSA au JK kila kukicha mnawachambua sasa why not FREEMAN? wanaJF mnataka kujua Mikataba wanayoingia wansiasa lakini hamtaki kujua wana elimu gani?

Kwani kuna ubaya gani wa kuuliza maswali hayo? Huyu ni mtu ambaye anapitisha au anapiga kura za kupitisha sheria zenye kuwahusisha Mama zetu, ndugu zetu na mpaka sisi wenyewe sasa why not kuuliza kuhusu maswali rahisi kama hayo?

What ever happened to OPEN DEMOCRACY ambayo mnaililia kila kukicha?
 
Duh,

Baadhi ya wajumbe wanashangaza kweli kweli.

DrWHO kishaanzisha threads kibao tu kuhoji maswali kuhusu watu mbali mbali maarufu. Nlizozipata kwa haraka haraka humu ni hizi:

RITA MLAKI
http://www.jamboforums.co.tz/showthread.php?t=2281

PIUS MSEKWA
http://www.jamboforums.co.tz/showthread.php?t=2289

Mama RWAKATARE na KAKOBE
http://www.jamboforums.co.tz/showthread.php?t=938

AHMED RAJAB
http://www.jamboforums.co.tz/showthread.php?t=1423

TIDO MHANDO
http://www.jamboforums.co.tz/showthread.php?t=581


Threads zooote hizo hakukuwa na kokoro wala nini. Leo kaguswa Mbowe imekuwa balaa.

Ikianzishwa thread 'Screw Muungwana', pamoja na kuwa matusi hayaruhusiwi humu, inaonekana ni OK.. inachangiwa na kushabikiwa. Ukihoji kuhusu Mbowe .. ishakuwa ni tatizo kubwa. Maswali hayajibiwi anaandamwa muulizaji.

Hehee, basi kaeni sawa .. maswali yanakuja mengi tu about huyu 'Rais'.
 
hata kama alihoji elimu ya "Nyerere", lakini je alihoji vilevile kama alivyowahoji wengine?
 
Kulikoni Umesahau ya CUF na Viongozi wao nao nilishawa-question lakini hili la MBOWE lishakuwa big deal.

Nashangaa mpaka Mwanakijiji of all people naye kaingiwa na wasiwasi.

Nakumbuka MBOWE aliingia humu kwa kusema kuwa THERE IS NOTHING TO FEAR BUT FEAR ITSELF

Sasa yako wapi?
 
hata kama alihoji elimu ya "Nyerere", lakini je alihoji vilevile kama alivyowahoji wengine?

Dr.WHO kaweka wazi kuwa hii ni kumpa nafasi huyu Rais au washabiki wake kuweka records clean. Sasa unless there is something to hide.. this is your chance to straighten things up!
 
Mbowe ni mwanasiasa kama wanasiasa wengine wanaoweza au kujitolea kwa umma kusaidia kile anacho weza kutoa wa umma, sijui kwanini iwe Mbowe mimi ni KADA mzuri wa chama tawala lakini ikizidi basi tunageuza shingo kuangalia upande wa pili,
upinzani ndiyo uliyo fikisha serekali ya awamu ya nne hapo ilipo kwa kujikosowa,
tupende upinzani kwa faida yetu.
 
Mzee Kada,

Hapa ni mawe tu, hatujali kiongozi ni nani.

Look at this now, huoni hata aibu? Dr. Who kum-question Mheshimiwa Membe Waziri Wa Mambo ya Nchi za Nje na mbunge wa CCM, ni sawa sawa ila akiuliziwa mwenyekiti wa Chadema?

Heshima katika forum hupatikana kwa kazi nzito ya kukata ishuz, sio kuandika ya upande mmoja tu. Sasa hii changamoto ya Dr.Who ndio msema ukweli kuwa mjadala wa siku hizi unatakiwa uwe against CCM tu na Muuugwana na serikali yake, ndio kinachotuweka pembeni.

Lakini wakati wowote utakapokuwa tayari ku-debate bila matusi na wala kuwasumbua wananchi hapa wanaotaka kuelimika nifahamishe, siko mbali na ninatumia at least masaa manne kwenye mtandao, lakini only utakapokuwa tayari kwa mjadala wa kweli sio kama ulivyoanza na huu.

Maswali yaliyoulizwa hapo ni valid na ni fair, huna majibu kaa pembeni muachie Freeman au wengine wajibu, wapo kina Mnyika wanaweza kumjibia; kuna wanaosoma naye hapa kina Mwanasiasa, Lunyungu na wengineo wanaweza kumjibia. Mbona mnapotukana CCM hakuna anyewatisha au kuwatukana?

I mean hamuoni hata aibu?

Kama mtu huna hoja kaa pembeni waachie wenye nazo, na for the Dr. Who's sake itabidi tumsaidie, ninasema kama huna hoja waachie wenye nazo, lakini usilete kejeli.

Thank You Sir na siko mbali, na wala sijafungasha, Dr. Who na wapenda maendeleo huu mjadala uendelee, this is good for siasa na demokrasia ya kweli, na bravo Mzee Kulikoni kwa siku zote kujaribu kuweka some balance.

Hoja hujibiwa kwa hoja, kama huna kaaa pembeni!
 
MBOWE anachukua pesa nyingi tu toka kwa wananchi ambao walimpigia kura awawakilishe na sijui marupu rupu yake ni kiasi gani lakini ninajua kuwa ni KODI ZA WANANCHI sasa kuna ubaya gani wananchi wakam-question both PUBLIC an PRIVATE life yake?

After all huyu mtu ni POTENTIAL PRESIDENT wa UNITED REPUBLIC OF TANZANIA kwani in politics anything can happen


Mzee ES:

Nashangaa imekuwaje ule msemo wa HOJA HUJIBIWA KWA HOJA?

Tazama siku zingine tunavyo iandama IKULU tazama LOWASSA asivyopewa Muda akapumua sasa leo hiii imekuwa nongwa KUULIZA Mbowe anasomea nini ili hali bado anavuta pesa za walipa kodi?

Aliyenishangaza zaidi ni huyo MWANAKIJIJI naye kubandwagon tu bila kuuliza maswali ya msingi... ndie anategemewa kuwa ni alternative wa redio za nyumbani

This is a joke!
 
Safi sana hata nami nasubiri kwa hamu record zisafishwe. Lakini kabla ya hiyo mleta hoja atumwagie jamvini jinsi RECORD ILIVYOCHAFUKA. Mfano aeleze taarifa alizonazo kuwa Mbowe anasoma vyuo gani na kozi gani zisizofaa au zisizowezekana au amefikia level gani isiyokubalika kwa sasa na kwamba yeye aliona au alisikia kuwa Mbowe ana mahusiano gani na Ndesaburo, Lucy na Grace zaidi ya kuwa Mtanzania mwenzao.
Plz throo hiya thoz polutanti rekodis b4 I spredi my profetiki klining wevu.
 
duh, wanaJF -Kada na Mzee ES punguzeni/ondosheni munkari (pressure) hii ni sehemu ya kujielimisha wala sio kulumbana. Kama kuna member kakosea basi aeleweshwe kwa lugha nzuri, tutumie hekima wajameni.

Heshima ni kitu cha bure hupaswi kulipa chochote ili upate heshima, hapa kwenye JF sote ni watu wazima kwa nini watu wazima wenye elimu nzuri tu wanabehave si kama wahuni wa kijiweni. Hapa tunataka watu wajibu hoja sio matusi na dharau hazitufikishi pahali.

Naamini hii forum watu wengi wanasoma tena wenye heshima zao. So long kuwa tunatumia majina ya kubuni isiwe sababu ya kutufanya tuandike tunachotaka - tuwe wastaarabu jamani

Peace peace peace ....... Amani iwe juu yenu
 
Mzee ES,

Achana na Kada Mpinzani. Tumia muda kujibu hoja za msingi.

Maswali ya Dr Who stay. Hoja za kada na wenzake OVERRULLED.

Tunangoja maswali yajibiwe...............

FD
 
Mzee Kada,

Sio tabia yangu kukimbia malumbano isipokuwa huna hoja, ninasema mimi ni CCM kwenye damu, wananchi wameamua chama chako kiwe msaidizi wa kuiamusha CCM isilale, ndio hata yaliyokuwa maneno ya baba wa taifa akiwa hai, sasa kama matatizo ya CCM yanaweza kuongelewa basi na ya Chadema yaongelewe.

CCM ina wazee kina Malecela na Kingunge, hiyo ni fact so is Chadema Ndesamburo sio American Idol contestant, CCM ina upendeleo so is Chadema uongozi wake una-base na kaskazini na upendeleo kwa kina mama pia, kama kuna viongozi wa CCM hawana elimu ya kutosha hata Chadema wapo, we can go on and on and on!

Ndugu yangu siasa ni pande zote sio upande mmoja tu.

Tuendelee kukata ishu, mimi nipo hapa mtandaoni bro!

Ahsante! Na ninakuomba tusiuharibu huu mjadla ambao ni makini sana hongera DR.WHo tupo pembeni!
 
Mzee MKJJ

Huwa una chombo cha kutusaidia sana. Haya maswali naamini mtu open kama Mbowe anaweza kujibu bila ya ku-spin a single word. Tumia muda mfupi sana this week ongea na Mbowe na maswali ya hawa wananchi hapa ni vyema yakajibiwa na yeye mwenyewe kwa sauti yake. Linawezakana na it is very possible baada ya hapo kuna mahasimu wake hapa watakuwa hawana la zaidi ila kutafuta mengine.

Mbowe anachukua pesa wapi dakta huu? Mbowe ni Kiongozi wa Upinzani yaani ndani Chadema na si Mbunge. Ukisema watu kupewa madaraka kwa undugu hapa tutaleta a very long list ili kuuliza ni sahihi?

Kwa sasa nadhani Mbowe ahojiwe ajibu hii Tuhuma.
 
Kumradhi watanzania,

Nimelazimika ku-edit posts zenu KARIBIA ZOTE ili kuweza kuendelea na topic kwa kadiri ninavyodhani itapendeza kuendelea kuongeleka. Aidha nadhani tuendelee kujibu HOJA kwa HOJA ili iwe rahisi kupata contents. Inakuwa kazi ngumu ku-edit lugha kalikali jama!

Inshallah, tutafika! Mjadala mwema
 
Mzee Es:

Nimeamka!

Naona mnanichokoa kusema. Nimenyamaza kwa miezi mingi kuzungumzia watu!

Iliwahi kusemwa-watu wenye akili/hekima kidogo huzungumzia watu, watu wenye akili/hekima za kawaida huzungumzia matukio, lakini watu wenye akili/hekima nyingi huzungumzia masuala. Na ndio maana wakati wote naepa kuzungumzia watu.

Lakini wewe umekwenda mbali-umeibua hoja za kumhusu Mbowe(mtu) lakini umezihusisha na Masuala(Ukweli vz Uwongo, Uongozi Vs Kuwa safi/coming clean, Kuweka kumbukumbu sahihi vs Kuchafulia jina).

Mimi nawaombeni hapa niyajadili haya masuala. Nawaomba kabisa nisijadili watu wala mtu. Na najua naweza kupata lawama toka kwa chama changu kutokana na michango ninayoitoa humu. Lakini naamini hatma ya siku ukweli utatufanya huru.

Nitachangia kiasi kuhusu Swali Na. 1 mpaka 3. Swali namba 4 mpaka 7(imeandikwa 8), nitayaacha kwa sababu mbili-mosi mjadala wa family business nimesema nitachangia siku za baadae lakini pili- mtoa hoja na hata wachangiaji wengine bado hawajasema bayana nini ni nini kinachotakiwa kutolewa ufafanuzi. Kwa hiyo kama mnataka ufafanuzi sema ni masuala yapi hayo. Na kama nilivyosema nitazungumzia masuala! Sio mtu. Na kama mnataka nizungumzie mtu au watu,basi niambieni kabisa niache kuendelea kuchangia.

Suala la Elimu ya Mbowe lilisemwa humu sana kwenye thread nyingine. Sikuchangia wakati huo nikijua hoja zilizotolewa na watu mbalimbali zilijitokeza. Lakini naona linaendelea kuibuliwa tena na tena , kwenye mijadala tofauti tofauti. Sijui ni kwa nia gani. Kila tukijadili masuala nyeti ya kitaifa Mbowe anaingizwa katikati. Inaleta hisia kwamba ni mkakati wa kuhamisha mjadala.

Suala hili limeshika chati wiki hii kutokana na hoja za Kulikoni. Nadhani hata Mzee Es ameamua kulichukua kuanzia hapo.

Sasa kwa nia ya kuchagiza mjadala na kuweka kumbukumbu sahihi nirudie hoja za Kulikoni:

1. Kwamba Mbowe anasoma Shahada tatu
2. Kwamba Mbowe anasoma Shahada hizo zote kwa miezi 18
(kulikoni aliyasema maneno hayo katika thread hii http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=2032&page=10)


Nikamwambia Kulikoni kuwa Mbowe anasoma shahada mbili: moja Hull na nyingine kwa distance Learning. http://www.jamboforums.com/showthread.php?p=25927#post25927

Na nikamuomba Kulikoni alete ushahidi wa maneno yake kwamba Mbowe anasoma Shahada tatu kwa miezi 18 ama walau atuambie ni wapi Mbowe amesema meneno hayo:

Kulikoni akaleta ushahidi wa chanzo chake cha habari kuwa ni http://www.habaritanzania.com/articles/1609/1/Mbowe-amua-kunoa-ubongo-Ulaya

Ukisoma chanzo cha Kulikoni chenyewe utaona amemua kudanganya(natumia neno hili badala ya neno kukosea kwasababu amerudia maneno haya mara kadhaa pamoja na kuona wazi kabisa kuwa chanzo kinasema tofauti na pamoja na kuelezwa ukweli):

Mosi: Chanzo kinasema Mbowe anasoma programu mbili. (kwa maana ya shahada mbili) ila kwa nchi tatu tofauti.) . Kwa hiyo kulikoni kusema Mbowe anasoma Shahada tatu amemua kwa dhati kabisa kupotosha. Hii inaleta hisia ya kwamba alilenga katika suala la kumchafulia Mbowe jina lake kwa kumfanya uonekane ni mdanganyifu. Sasa Kati ya Kulikoni na Mbowe nani ni mdanganyifu? Kwa bahati mbaya kwako Mbowe anasoma Hull, anasoma distance learning na kama sehemu ya digrii yake ya Hull atakwenda Japan-hii ni special arrangement ambayo amepanga kuifanya kwa ajili ya kupata exposure ya masuala ya middle East)

Pili: Chanzo kimesema Mbowe atasoma kwa miaka mitatu. Kulikoni amesema Mbowe atasoma kwa miezi 18. Kwa hiyo Kulikoni ameamua kudanganya. Kwa motive gani? Ama unataka ijengeke picha kuwa Mbowe anasoma digrii ya uzushi ama ya kununua kama zile za Udaktari wa Mawaziri kadhaa wa Serikali ya CCM ya awamu ya nne ya Kikwete? Kwa bahati mbaya kwako ukweli unajulikana wazi kuwa Mbowe yuko Hull ambacho ni moja ya vyuo vinavyoheshimika.

Nimeandika kwa kifupi. Nimeepuka kuandika kwa kina- na siwezi kuandika kwa kina kwa kuwa sipendi kujiingiza katika mjadala wa kujadili watu, sitaki kila sentensi niandike Mbowe, Mbowe, Mbowe, Mbowe. Nataka nipate wasaa wa kujadili masuala ya nchi.

Mimi nami ni kiongozi wa kisiasa. Na watu wanaamini maisha ya kiongozi wa kisiasa ni maisha ya umma. Kila kitu lazima kifahamike kwa umma. Lakini kumbuka hata mwanasiasa ni binadamu na anayo maisha yake binafsi. Yanakuwa tu yakujadiliwa kama yana uhusiano na masuala ya umma. Binafsi huwa naweka mambo wazi lakini si kila kitu. Uanike kila njia unayotaka kupita ili wapinzani wako wakuwekee vikwazo? Kama CCM waliweza kutuma mtu kwenda Kenya kufanya Booking ya Helikopta katika kampuni ambayo CHADEMA ilipanga kukodi Helikopta inashindwaje leo nikisema naenda kusoma chuo fulani mkaanza kuweka kauzibe? Ndio maana hata Mbowe alitangaza kuwa anakwenda Hull baada ya kufanikisha kila kitu ikiwemo visa ya kwenda masomoni. Kama Besigye anaminywa kutoka Uganda, kama Tvangirai ananyimwa kutoka Zimbabwe, wanasiasa wa upinzani waamini vipi hii Comrades Club ya CCM, ZANU PF, Movement nk? Kwa hiyo msitegee kuchokonoa tutoe kila taarifa hapa. Mambo mengine tutawaambie-UKWELI ni huu, kwa taarifa zaidi subirini miaka mitatu ijayo wakati mambo yote yamekamilika.

Kwa herini kwa leo…tutaonana panapo majaliwa………ngoja nielekee kwenye mkutano wa hadhara katika kata mojawapo Hapa Ubungo…..Hakuna Kulala, Mpaka Kieleweke.

JJ


(Mzaha)Ps: Mkimaliza kuuliza maswali haya kwa Mbowe muulize maswali kama hayo kwa Kikwete, Lowasa, Mwinyi etc…duh kwa kwa heli orodha ni ndefu na muulize maswali hayo-nani ana elimu gani, ana uhusiano gani na nani, anapata wapi pesa zake na anazitumiaje!. Lakini msiwajadili maisha yao binafsi mjadili masuala UKWELI VS UWONGO, UONGOZI Vs MASLAHI YA TAIFA etc teh teh teh, its like hide and seek(Joke)


“Mabadiliko ya Kweli, hayawezi Kuletwa na Mafisadi wale wale, wa chama kile kile, chenye uoza ule ule, wakiendeleza yale yale, eti kwa Ari, Nguvu na Kasi mpya…kwa falsafa ya Chukua Chako Mapema……Tanzania yenye neema haiwezekani”.
 
Dr.WHO,

Really?

But sijatoa maana na dhamira ya thread husika. Au ulifungua thread ili iwe kama ilivyokuwa inaelekea? I did not notice that it's your intention to where we were redirecting ourselves. Kama dhamira yako ilikuwa hiyo basi mzee kumradhi nisingeruhusu watu waparane na kuhama hoja. I had to do my best to bring people back to the topic. Meanwhile; nisingependa kuchangia kwenye thread zaidi.

Am out

NB: Thanks JJ kwa hoja na naomba wengine tuendeleze HOJA
 
Mpaka sasa sijaona hoja ya msingi ambayo wenzangu wana JFtumeshindwa kuelewana, mimi kama mpinzani bado sioni kosa kwa kuhojiwa Mheshimiwa Mbowe, tatizo liko wapi?
Nafikiri tuache malumbano tuwapishe wenye kuweza kujibu maswali watusaidie.
 
Back
Top Bottom