Mbowe na tafakuri zake...

Great! but, this is not what your title stands for. You are talking of deconstructing Mbowe rather than his ideas or his literary work. I don't need to read Jacques Derrida to understand this simple English word. Remember you are not writing to philolosophers in this forum. We are people of different intellectual backgrounds and not all of us are interested with Jacques Derrida philosophical works! Good writing requires simplicity and straightforwardness. If "deconstruction" is an English word, then it is clear that you cannot apply it to a person. Simply put, you cannot deconstruct a person, because it is a physical entity. Deconstructing a person will amount to destroying that person all together, and that is why I was staggered by your title. You can only deconstruct a socially constructed idea or concept. For example, gender is a socially constructed concept and it can therefore be socially deconstructed

My friend,

I agree with only 10% of what you had to say. But, my response will necessitate a lengthy discourse on Derrida which, as you aptly noted, may not be appropriate here. So, I will refrain.

Anyway, if Derrida is a tough nut, I reckon Woody Allen - "Deconstructing Harry" - should be okay.
 
Mogongo Mugongo

Don't make this language difficult, is this the reason you mentioned earlier?

I’m still waiting for my request.
 
I was laughing reading all the emotional responses to my article. This is how it works: Mbowe writes, everybody cheers. Mbowe criticised, everybody jeers. My simple advice: if you continue to intellectually coddle Mr. Mbowe, something he is used to in his entire life, you will make him a continual dependant of the Ansbert Ngurumo types for his writings. If Mr. Mbowe's views are not put to interrogation, and if this whole JF enterprise becomes a CHADEMA cheerleading fest, you will be nurturing mtindio wa tafakuri on the party's leadership and supporters. Basically, nawaweka kundi moja na wale makada wa CCM kule Bongo ambao kazi yao ni kuimba na kusifia tu.

What is worrisome here is that you are not interogating Mbowe's views; you are actually trying to malign his personality. For example, when you say "... a spoiled kid, who failed at school, failed entrepreneur...", what sort of ideas are you interogating here? And then when you say that all JF members are coddling Mbowe, what do you want us to reply back. This is provocation and I don't see anything intellectually engaging in this kind of argument!
 
My friend,

I agree with only 10% of what you had to say. But, my response will necessitate a lengthy discourse on Derrida which, as you aptly noted, may not be appropriate here. So, I will refrain.

Anyway, if Derrida is a tough nut, I reckon Woody Allen - "Deconstructing Harry" - should be okay.


Be careful in pulling other people's titles loosely! Harry there was used symbolically, to represent ideas. There is nothing in your post to show that Mbowe stands as a symbol of ideas. You categorically stated that Mbowe "ana mapungufu ya tafakuri". So, how then can you say you used him in the title as a symbol of ideas. Big hypocrisy heee!
 
My point has been made. You get the last word, my friend. You may take it as "winning" the argument. :)

Unfortunately, there is no competition in all this. There are only alternative view points! Instead of saying you have made your point, I would prefer to say 'you have done your work' quite well! Have a good day.
 
Tatizo kubwa la siasa Tanzania ni watu wenye - AMBITION!
Hapa ndio ngoma kubwa sana!
I have problem with motivated person with goal in mind - to become a President! - JK mmoja wapo, as to a person who is motivated with desire and willingness to lead people to a better place.
Hii ndio tofauti kubwa kati ya mitume na viongozi wetu, kiasi kwamba mitume walikuwa wakifuatwa na kuaminiwa kwa sababu waliweza ku-deliver hali viongozi wetu wengi kama wanavyosema waungawana na Ung'eng'e.
It is for them alone to point out what we ought to do, as well as to determine what we shall do - PRESIDENT..

Mkandara,
sidhani kama kuwa na ambition ni kitu kibaya. Ni kitu kizuri sana. Tatizo ninaloliona mimi ni mtu mwenye ambition ambae ajenda yake ni madaraka tu na wala sio nini atafanya na hayo madaraka. Hili ndio tatizo la wanasiasa wengi wa Tanzania. Tukitoka hapo, watu wakiwa wanajua nini wanataka kufanya na wakashawashi jamii basi tutakuwa na viongozi wazuri sana.

Mimi pia niunge mkono wale wote waliomshukia mugongo na hasa mwanasiasa. Nadhani ameelewa na hatarudia "deconstructing" somebody. Au decomposition?
 
Ndabita,

Nadhani hukuisoma vizuri hoja yangu..
Ambition haiwezi kuwa na uzuri wowote ktk kutafuta kiti cha urais - IKULU!
Ndio maana nikaweka mfano wa JK, jinsi alivyowakanyaga kanyaga wote waliokuwa mbele yake utadhani Idd amin alipokubali kushindana na bodyguard wake kuogelea!..
Tafauti na Ambition ya kutaka kuwaongoza wananchi ili wafike sehemu fulani salama - KUOKOA. Hii haimlazimu mtu kuwa - lazima awe rais!.. hizi ndizo ambition tulizo ziona toka kwa kina Abdoul Wahid Sykes, Bomani, Fundikira, Mwapachu na wengine wengi ambao walikubali kukaa mbele ya mtumbwi wakipiga kasia na kumwacha nyuma Nyerere akiongoza mashua.

Now, hapa sijasema Mbowe ni mmoja kati yao hao wenye ambition ya kiti IKULU, ila inakuwa vigumu sana kwa mtu kuelewa tofauti kati ya lamb na wolf kwa yule aliyezoea kuona sheep. KUELEWA kitu ni bora kuliko KUONA kwa macho maanake wolf akivaa ngozi ya lamb huwezi kumshitukia na mara nyingi huwa too late!
Ndabita,
I know Freeman, huyu ni sawa kabisa na wale wanaonifahamu mimi maanake wengi hawaamini kuwa Mkandara yule wanaemfahamu ktk madisco ndiye huyu anayeandika hapa..Vipaji, hekima na busara hazina mhuni wa mtaani wala msomi mwenye Phd!...
Point kubwa ya mgongo mgongo ambayo mimi kidogo imeniacha na fikra mpya ni pale aliposema Mbowe kenda shule wakati wananchi wanamhitaji sana kuliko wakati wowote!...
Yes, shule muhimu sana lakini umuhimu wake unashinda kujitoa mhanga!.. na je, kenda shule ili apate credit kwa wadanganyika kuwa Mbowe ana uwezo wa kukalia kiti cha urais IKULU?..

Sisi binadamu hatuishi kufikiri, kuweka dhana na pengine yawezekana kuwa tunachotakiwa kuhofia zaidi (FEAR) ni hofu yenyewe (FEAR).
 
Huyu Mugongo ni shwain tu. Katika viposti vyake kiduchu hakuna hata moja inayokosoa na kutoa mapendekezo kwa serikali na CCM yake.

Kwa jinsi alivyoilalia macho Chadema and Mbowe tu, inaonyesha kabisa chuki na si kitu kingine chochote.

Kiongozi wa CCM asingeweza kuandika vizuri zaidi against Mbowe kama huyu monkey boy. Tuseme yeye si Sisiemu(anavyodai), lakini amefanya kazi nzuri ya kuisadia Sisiem katika juhudi za kubomoa upinzani, Chadema ikiwa real threat kwa chama tawala. Swali ni kwa nini afanye kazi ya kusaidia Sisiem ikae madarakani na kuifilisi nchi hii, kama yeye hana anachopata huko?

Wengi wetu humu tuko genuine na kilio chetu kwamba Sisiem na serikali yake ni jeuri. Huyu shwain anaona upande mwingine.
 
mkutano wa hazara na Bw. mugongo mugongo CCM Oyeeeeee

zidumu fikira za mugongo ,kwanza wewe unamatatizo tuna jua wewe ni CCM 100% sasa ushabiki wako wa kisiasa siyo wakwako wewe umetumwa siumwambaye katibu mkuu wa ccm aje humu ajibu hoja za wapigakura wake CCM Oyeeeeee


kuwa hapa tunakufamu sana pia aliye kutuma tuna mjua hiyo siyo akili yako, ninaomba kuuliza swali kwanini serikali ya awamu ya nne ina wapambe wengi sana CCM Oyeeeeee



hawana idadi sasa bw. mugongo upambe wako ndiyo ulio kupa kazi wewe endelea unatabia ya kuongea mambo ya watu binafsi sasa tukiweka yako hapa na picha yako hapa tutakuumbua CCM Oyeeeeee



sasa ili ni onyo au mwambie JM kazi aliyo kutuma huiwezi sisi tunataka kujenga taifa letu, siyo ushabiki wa vyama hapa au upambe kwa kiongozi fulani ,

angalia tutakuanika humu akuna rangi utawacha kuona bro.

kidumu chama cha mapinduzi, na zibumu fikira za mwemyekiti wa ccm atakama hazifai..........kweli tuna hasara
 
Zanaki,

Wewe unajiondoa kwenye list YETU? Nilikuweka kwenye kundi letu. Kwa sasa tupo zaidi ya 700. Naamini kufikia mwezi ujao tutafikia Elfu Moja!

Kama ni Management bado haijawa set up. Napendekeza jina lako mkuu!

Just kidding but probably u fit... Nshasema zaidi ya mara 5... JamboForums.com si yangu, si yake na wala si yao! Ni yetu sote.

Need I say more?
__________________

Maybe i was misunderstood,what i meant was,watu wenye jina la INVISIBLE mko wa ngapi?Maana naona kama kuna characters mbili tofauti.

Mimi ntafurahi sana kama niko kwendi kundi lenu
 
Zanaki kwa kukusaidia kuna Invisible ambaye ni Admin na kunamwingine Invicible ambaye ni member, hapa tofauti ni s na c

Admin toa ufafanuzi huyu Invicible hata mimi ananichanganya
 
Admin toa ufafanuzi huyu Invicible hata mimi ananichanganya

Mara zote pale ninapotakiwa kutoa ufafanuzi sisiti kufanya hivo.

Kwakuwa wawili mmechanganywa basi kuna wengi hawatutofautishi. I believe after this no more quiz.

This' not a better thread to explain but let's use it once anf for all:

Invisible (mimi):
-Unseen
-Imperceptible
-Undetectable
-Hidden
etc

Invincible (member):
-Unbeatable
-Unshakable
-Indomitable
-Impregnable
-Indestructible
etc

Hope the above meanings will never confuse you.

Thanks and regards
 
Vyama vingi; kinga ya ufisadi wa watawala

Freeman Mbowe




WIKI iliyopita, niliandika na kuahidi kuendelea kuandika hadi kieleweke! Nimepata salamu nyingi. Nawashukuru wale wote ambao wamenipongeza na kunitia moyo. Nawasihi wasiishie kwenye pongezi, ila wajiunge nami tuendeleze harakati kwa faida ya taifa letu na vizazi vijavyo.


Kama nilivyotegemea, wako walioingiwa hofu. Kadhaa kwa maneno tofauti yenye hitimisho moja walisema: “…Mheshimiwa, kuwa mwangalifu, …hata kama uko Ulaya... hawa jamaa ni hatari sana! ...Mafia hawa… wanaua kwa siri!!”


Hawa nao walinipa kazi ya kutafakari kifo, harakati, hofu na woga!


Nilijiuliza:


Mosi; hivi kweli hofu hii ya kuuawa kwa siri ipo? Au viongozi wetu wanasingiziwa? Tumekuwa kwenye mfumo wa vyama vingi vya siasa kwa mwaka wa 15 sasa! Ni wangapi na kina nani wameuawa kwa siri na serikali au CCM?


Pili; hofu hii ya kuuawa kwa siri, ambayo nikiri imeenea sana miongoni mwa Watanzania (pamoja na kuwa wengi wao hawathubutu kutamka hadharani), imeasisiwa na nani na kwa malengo gani? Sijui kama viongozi wetu wanajua kuwa wanahusishwa na hisia za utayari wa kuua!


Tatu; inanikumbusha marehemu wanaharakati Che Guavara wa Cuba na shabiki wake mkubwa Prof. Sethi Chachage katika imani yao kuwa, “…ni heri kufa umesimama kuliko kuishi umepiga magoti...” Mungu azilaze roho zao mahali pema peponi. Msemo huu unatufundisha nini Watanzania?


Ndiyo, wako Watanzania wamepoteza maisha yao wakitetea taifa hili. Wote tunakumbuka mauaji ya Pemba na Unguja ya Januari 26 na 27, 2001 kufuatia uchaguzi uliokuwa wa kiini macho. Serikali ya CCM iliua. Ilikana, ikashindikana! Ukweli ulijulikana. Hayakuwa mauaji ya siri yale. Damu ya Watanzania wale ni ukombozi wa Watanzania na haikupotea bure. Familia zao zimepotelewa, lakini harakati za kutafuta haki zilirutubishwa. Leo, maandamano ruksa! Ni hatua.


Katika maisha haya, kila jambo lina heri yake. Kila siku tunazika wapenzi wetu. Wengi wanakufa kwa vifo vya uzembe na udhaifu wa wengine.


Harakati zinazoogopa kifo si harakati, ni usanii. Usanii ni mchezo. Harakati ni kazi na hazihitaji masihara. Haki hupatikana tu pale pande zote mbili, yaani watawala na watawaliwa, zitakapokubali kuwa salama iko kwenye kweli na haki.


Leo, watawala na wapambe wao hawana hofu kwani wanajua salama iko upande wao na si kwenye haki na kweli. Watawaliwa nasi tumekubali kunyang’anywa haki, na wengi tumeishia kunung’unika. Tumegeuzwa “misukule,” tumekuwa mateka!


Naam! Hofu imejengwa makusudi kwa kutumia propaganda na imejengeka! Taifa limeingia woga na sasa wananchi wanajiwekea gavana wenyewe (self censorship). Watawala nao wanachekelea ubwete huu. Wanamudu kulala usingizi katikati ya vilio!


Wananchi sasa hawaheshimiwi. Utawala umekuwa usanii. Ufisadi unafanywa mchana kweupe bila hata kupepesa macho. Hofu ya Watanzania sasa ni ngao ya watawala. Wanapenda sana kuhubiri amani na utulivu kumbe ni mkakati mahsusi wa kuendelea kujenga hofu!!


Hebu tuchukue mifano michache mibichi! Hivi karibuni, vyombo vya habari vimetoa taarifa za kina kuhusu baadhi ya mikataba yenye utata ambapo mabilioni ya fedha za mifuko ya hifadhi za jamii, NSSF na PSPF zilifujwa katika mazingira ya kutatanisha.


Ni shutuma nzito, lakini vyama vya wafanyakazi ambavyo wanachama wake ndiyo wachangiaji wa mifuko hii, vimeshona midomo! Serikali nayo kimya! Wabunge wa CCM wamekuwa mabubu!


Viongozi ambao tulitegemea wachukue hatua, wanamgeuzia kibao Reginald Mengi na vyombo vyake vya habari vilivyoshikia kidedea kashfa hizo! Eti ana ugomvi wa kibiashara na mhusika mkuu, mfanyabiashara Yusuf Manji! Mambo ya usanii, aibu na fedheha. Serikali, Bunge na mamlaka zake nyingine, zinageuzwa sasa wapiga debe wa Manji! Jeuri ya fedha hizo hizo tunazotaka maelezo yake!!


Sawa, inawezekana Mengi ana ugomvi na Manji! Lakini, je, hii inaondoa ukweli wa taarifa hizo? Wabunge wa upinzani tu ndio wanaosema, lakini watawala wameweka pamba masikioni. Wana uhakika wa usalama wao.


Kabla hili halijatulia, linaibuka sakata la Kampuni ya Richmond na kisha Dowans Holdings! Hawa ni watoto wa baba mmoja mama mbalimbali. Tatizo si nani mmiliki wa mkataba, tatizo ni mkataba wenyewe! Tukumbuke kuwa, mkataba huu unatekelezwa chini ya Serikali ya Awamu ya Nne ambayo imeahidi Watanzania kupitia mikataba yote yenye utata ya awamu iliyotangulia! Usanii mtupu. Hawa ni wamoja!


Hili halijatulia, linarejeshwa suala la wizi wa kutisha katika mkataba wa ununuzi wa rada. Ukweli unaanikwa hadharani kwa Watanzania. Watawala wetu wanalijua hili vizuri sana! Ni pesa nyingi za kutisha! Wanajifanya hamnazo!


Viongozi wa upinzani wanaitisha maandamano ya wananchi kulaani ufisadi huu. Idadi ya wananchi wanaojitokeza inakatisha tamaa. Ni wananchi hawa hawa wanaolalamikia ugumu wa maisha, lakini hawako tayari kwa harakati za kukomesha uharamia huu. Kwa mtaji huu, watawala lazima wawe na jeuri! Wana uhakika na usalama wao!


Katika nchi za wenye uchungu na nchi zao, watu wasingelala usingizi. Hapa hakuna cha itikadi au lolote! Watu wangeandamana hadi kieleweke – na kueleweka ni watu kufukuzwa kazi, watu kupelekwa mahakamani, watu kujiuzulu nk. Kwetu aah! Kafsha nzito zimegeuzwa mazungumzo ya vijiweni, kwenye baa nk.
 
NCHI YETU INA LAANA YA NANI?

Kila mahali utasikia CCM wabaya bwana! CCM hatari sana, CCM mafia! Yaani leo tunaiogopa CCM kuliko maisha yetu na vizazi vyetu! Hebu fikiria: Huyu CCM tunayemwogopa ni nani hasa?


Mambo haya na mengine mengi yananifanya nifikirie upande wa pili wa shilingi. Najiuliza, mfumo wa vyama vingi vya siasa umeisaidia nchi hii au umeiingiza kwenye matatizo zaidi? Hii ndiyo tafakuri yangu ya leo!


Yako mawazo yatakayokinzana kuhusu hoja hii. Wako watakaosema kuwa vyama vingi ni tunda la fikra za Mwalimu Nyerere kwani alikuwa wa kwanza kutamka hadharani umuhimu wa CCM kuona ulazima wa kuukubali mfumo huu. Hii ilikuwa mwaka 1991.


Wengine watadai ni zao la mabadiliko ya mifumo ya kisiasa duniani kufuatia kumalizika kwa vita baridi (cold war). Vita baridi ilikuwa mvutano wa kiitikadi na kisera duniani. Mataifa ya Magharibi yakiongozwa na Marekani, yalisimamia itikadi za kibepari na sera za uchumi wa soko. Zile za Mashariki zikiongozwa na Urusi, zilisimamia itikadi za kijamaa/kikomunisti na sera za uchumi hodhi.


Mataifa mengi duniani yaliamua kuwa upande mmojawapo wa mvutano huu. Yapo yaliyodai kuwa "hayafungamani na upande wowote" (Tanzania ikiwemo), lakini dhana hii iliishia zaidi kuwa ya kinadharia kuliko vitendo. Ukweli Tanzania ilifungamana zaidi na nchi za Mashariki.


Wengine watadai vyama vingi ni zao la shinikizo la nchi za Magharibi kwa nchi za dunia ya tatu, kufuatia ushindi wao katika vita baridi. Utawala wa demokrasia ya vyama vingi, sambamba na mabadiliko kadhaa ya kisera sasa, yalitumiwa kama chambo ili kuwezesha nchi hizi za dunia ya tatu (zilizokuwa hoi kiuchumi), Tanzania ikiwamo, kupata misaada mbalimbali.


Vyovyote iwavyo, vyama vingi tunavyo. Sasa hebu tuangalie historia inatueleza nini kuhusu chimbuko la ufisadi wa kutisha baada ya mfumo huu kuanza.


Wakati wa utawala wa awamu ya kwanza, hasa baada ya Azimio la Arusha, nchi hii ilikuwa na itikadi iliyoeleweka. Ilikuwa ya Ujamaa na Kujitegemea, chini ya mfumo wa chama kimoja. Kiongozi Mkuu, Mwalimu Nyerere, aliweza kutoa dira iliyotokana na sera na falsafa alizoziasisi na kuziamini. Kama sera na falsafa hii ilikuwa sahihi, si shabaha ya tafakuri yangu leo.


Pengine kwa sababu ya uadilifu wa Mwalimu, awamu hii haikufanya masihara na mafisadi. Watu walichapwa viboko hadharani. Viongozi waandamizi na wafanyabiashara hawakupewa fursa ya kuwa mawakala wa kiongozi mkuu, yaani rais. Tukiacha mambo ya nje, agenda za vikao zilikuwa ni wananchi na mustakabali wa taifa. Hakuna historia ya ufisadi.


Awamu ya pili chini ya Rais mstaafu, Mzee Ali Hassan Mwinyi, ilikuwa awamu ya mpito na hapa nchi ilianza kupoteza dira kiitikadi, kisera na hivyo kimwelekeo. CCM ilizika kimya kimya itikadi na sera za kijamaa na kukumbatia sera za kibepari na uchumi wa soko. Unafiki wa kisiasa hapa sasa uliota mizizi.


Itikadi na sera za ujamaa, zilionekana kupendwa zaidi na wananchi, lakini zilipigwa vita na wafadhili. CCM iliegemea upande wa wafadhili, ikazika itikadi ya ujamaa na kuanza kubadilisha sera zake za kiuchumi kuwa za soko. Wananchi hawakushirikishwa. CCM ikaendelea kudanganya mpaka leo kupitia katiba ya nchi kuwa, nchi hii ni ya Ujamaa na Kujitegemea. Hata ndani ya chama chenyewe, wanachama wameendelea hadi leo kudanganywa chama chao kina itikadi ya Ujamaa na Kujitegemea – eti kwa mtindo wa kisasa!


Viongozi wakuu ghafla wakaanza kuwa na washirika wa karibu. Ikulu ikavamiwa na wapambe ambao wanabadilishana viti kila serikali ikibadilika. Uswahiba na watawala vikawa sera isiyo rasmi hadi leo. Wako wengi wametajirikia Ikulu na jamii kamwe haiwajui hawa. Madalali hawa wa nchi wapo na wamebana kimya. Muda utasema. Wametumika kama kinga kwa viongozi wakuu.


Awamu hii ilisimamia uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi. Wananchi wengi hawakuwa na hofu bado. Ilikuwa almanusra CCM iende na maji. Wamshukuru Mwalimu Nyerere.


Awamu ya tatu ya Benjamin Mkapa iliingia madarakani kwa nguvu ya ziada. Michubuko ya uchaguzi wa vyama vingi ilimtesa kwa kipindi chote cha utawala wake.


Aliweka misingi mibaya ya uhasama wa kisiasa. Alibariki vyombo vya serikali katika azma ya kuzima kukua kwa demokrasia ya vyama vingi. Alitumia vyombo vya dola hasa usalama wa taifa na Jeshi la Polisi kudhibiti wapinzani ambao sasa walionekana adui wa serikali na chama chake na si wadau muhimu katika mustakabali wa kusimamia haki na ustawi wa nchi. Wapinzani walichukiwa na kutengwa. Hapa ndipo hofu ilipojengwa kwa nguvu zote.


Awamu hii iliwajenga madalali wa nchi kwa nguvu zote. Wengine Ikulu haikuwatosha, wakajipenyeza na kwenye chama tawala, CCM. Hawa wameshiriki vilivyo katika kuuza nchi, huku wakikinga biashara chafu za viongozi wakuu tuliowapa dhamana ya kutuongoza.


Mikakati ya makusudi ya kiharamia ilifanywa kudhibiti na kudhalilisha wapinzani. Dola ilitumika kunyima upinzani rasilimali watu na rasilimali mali. Wafanyabiashara waliounga mkono vyama vya upinzani, walishughulikiwa na kufilisiwa. Wenye roho nyepesi (ambao ni wengi) walilazimishwa kimazingira kuvikimbia vyama hivyo. Wasomi nao hali kadhalika. Mapambano ya kisiasa sasa yakawa mapambano ya kitabaka.


Matajiri wafanyabiashara wa ndani na nje wakaiteka CCM. Wasomi nao kwa mfumo huu tegemezi wakatangaziwa kuwa vyeo na kinga ya ajira viko CCM. Wakatimka. Yeyote aliyependa fadhila, utajiri na cheo, akaingia CCM. Yeyote aliye na cha kuficha akapata kinga CCM. Nchi ikageuzwa "shamba la babu" ambamo kila mwenye nguvu anachuma kadiri ya uwezo wake na babu hana uwezo wa kuzuia.


Fedha ikawa itikadi ya CCM. Nchi ikakosa mwelekeo wa kisera. Fedha, ya wafadhili wa nje au wa ndani ndiyo ikawa sera na mhimili wa taifa na maendeleo yake.


Awamu ya Mkapa, iliendeleza sera za uhuru wa soko - fikra na dira zikitoka kwa wafadhili. Uchumi sasa ukashikwa rasmi na wageni. Wazawa wakatelekezwa na kurushiwa "mapanki." Akatokea "mwenzao" Iddi Simba akatetea wazawa! We! Cha moto alikiona!


Utandawazi ukachukua nafasi kubwa katika agenda za kiongozi mkuu. Wizi (wa viongozi na wafanyabiashara wa ndani na nje) ukashamiri kwa mgongo wa ubinafsishaji na uwekezaji. Wenye kuitetea nchi wakaonekana si mali kitu! Wengine hata uraia ukawa matatani. Siasa ndani ya CCM sasa ikawa biashara chafu. Fedha ni fedha, iwe ya dawa za kulevya, iwe ya rushwa nk haijalishi. Hapendwi mtu wala nchi hapa – ‘fweza tu!!'


Bunge nalo halikuachwa nyuma. Huko nyuma nililiita mchezo wa kuigiza. Nikafunguliwa mashitaka. Nikajitetea kwani sikubali kuwa kondoo. Niliamini nilichokisema. Narudia leo: ‘Bunge limegeuzwa kitanzi cha haki na sasa limekuwa kisagio cha kodi za wananchi na baraza la kuhalalisha ufisadi.' Wapinzani wanasema, lakini serikali sasa inatumia wingi wa wabunge wa CCM kuhalalisha uharamia. Watanzania "wanafaidi" matunda ya ushindi wa tsunami.


Sasa tuna awamu ya nne ya Jakaya Kikwete. Haina jipya. Itikadi hakuna. Sera mpya hakuna. Fikra mpya hakuna! Ni awamu mahiri kwenye mambo ya sanaa na mahusiano - mbwembwe, ndoa na vyombo vya habari, mashairi, sherehe, vibwagizo na kaulimbiu tamu tamu, ziara, ahadi, nk.


Nikiri, walikuwa makini katika kampeni! Walikuwa hawana "mswalie mtume" – kuanzia wenyewe kwa wenyewe hadi wapinzani. Umahiri wao wa sanaa ulionekana tangu hapa. Fikra zao ziliishia siku ya kuingia Ikulu. Wamefanikiwa! Watanzania bado wanajipa matumaini kuwa ari, kasi na nguvu mpya ni sera!! Ya wapi… Muda utahukumu.


Rais Kikwete kakiri, hana jipya na viatu vya Mkapa ni vikubwa kwake!! Ataendeleza yale yote mazuri ya Mkapa?! Hajatuambia mabaya ni yapi na atayafanyaje! Sasa tutegemee nini? Mkuu keshakata tamaa?


Chama kinachotuongoza kiko vipande vipande! Kinajua bila dola hakipo. Bila mikwara, hofu haitaendelezwa. Kimepata wapiga zumari wasioweza kueleza itikadi yao, kwani hawana. Wana agenda moja: NYONGA UPINZANI LAKINI USIUE. Ukiua, misaada ya kimataifa hakuna. Ukiua, kinga ya ndani ya ufisadi wao haipo! Hii ndiyo dhana ya upinzani kufanywa kinga ya ufisadi wa watawala!


Wote wako kwenye utando wa buibui, hawana jinsi, lazima walindane. Kinachowaunganisha hawa si itikadi, kwani haipo, ila ni kuwa kila mmoja ana kapu na yuko tayari kuvuna ndani ya "shamba la babu."


Tuonane wiki ijayo!

Source:http://www.freemedia.co.tz/daima/2007/1/31/makala3.php
 
Kumekuwa na trends za kumkashifu Bwana Mbowe humu karibu kwenye kila topiki inayohusiana na UPINZANI TANZANIA.

Sasa nadhani hii iwe semehu ya eyeye Kuja kuweka RECORDS CLEAN na maana aliwahi kuja humu kisha akapotea lakini ni nafasi nzuri kuweka records clean then hii thread tutaisevu for FUTURE REFERENCE itakapotokea maswali. Na si kwa sababu huyu FREEMAN anaweza akaja kuwa RAIS WANGU in the future then naamini nastahili kujua hizi habari na kama kuna mwenye maswali zaidi ayaweke hadharani.


freeman_mbowe




Nilikuwa naamini kuwa kuna watu wanania ya KUKUCHAFULIA JINA Bwana Mbowe lakini maswali naona yanazidi kuwa mengi na kukaa kimya siyo dawa!

The usual questions kuhusu mbowe ni hivi:

1. JE, NI KWELI FREEMAN MBOWE ANASOMA VYUO 3 TOFAUTI NCHI 3 TOFAUUTI? KAMA NI KWELI NI VYUO VIPI?

2. JE, KATIKA VYUO HIVYO ANASOMEA KOZI ZIPI? MASOMO HAYO YANACHUKUA MUDA GANI?

3. YUKO KWENYE KIWANGO (Level) GANI?

4. JE, ANAUHUSIANO GANI NA NDESAMBURO?

5. JE, ANAUHUSIANO GANI NA LUCY OWENYA?

6. JE, ANAUHUSIANO GANI NA GRACE KIHWELU?

8. JE, MAJOR DONORS (WAFADHAILI) WAKE NI AKINA NANI?
 
Nimekuwa nina soma kabla sijaanza kuchangia Mbowe amekuwa akiingizwa katika majaribu mengi sana ya kumchafua yeye na familia yake na chama chake mimi ninaona jinsi watanzania walivyo walemavu wa akili, sijui wamerithi kwa nani.

Watanzania wana tabia ambayo haitawatoa kwenye umasikini tanzania ni nchi yeye utajiri wa kurithi visivyo rithiwa na watu wenye akili timamu.

Wamekuwa na kasumba ya kuamini wanacho kiamini walichoambiwa na mtu wanao amini ni changuo la Mungu.

Dr.WHO iweke hapa basi historia ya JK ili tulinganishe na ya Mbowe kama hazifanani au zimezidiana.

Sisi tunawajua sana JK amezaliwa kwenye siasa Mbowe anamiaka 15 kwenye siasa lakini angalia power aliyo nayo.

Mbowe ameumia sana roho anavyoona jinsi watanzania wanavyopata shida ni mtoto wa kwanza wa tajiri kuona huruma kwa familia za masikini, wangapi wamezaliwa katika familia za utajiri kazi yao kutunyanyasa na utajiri wa wazazi wao au nafasi za wazazi wao.

Wao wanafaida gani na sisi au watoto wetu kwa maisha ya baadaye, kama siyo wataishia gerezani baba yake asipo kuwepo.

Sijui ni kwanini Mbowe tu inaonyesha uoga CCM iliyonayo kuhusu Mbowe. Hii ndiyo njia ya kumpa Mbowe jina kubwa na umaarufu.

Mimi siyo Chadema.
 
Nakiri kuwa mie ni CCM,

Maendeleo hayaletwi na CCM pekee, although wamekuwa kwenye power miaka yote hiyo lakini still hakuna lolote, kwani unadhani wapinzani wapo kwa ajili ya nani ? Ndio pia wanajali maslahi yao, lakini kwa imani yangu ni kwa sababu tunahitaji mawazo tofauti, unlike in this scenario wapinzani wanapuuzwa sana nyumbani tz na chama tawala.

WanaJF wengine, naombeni tuangalie sana kuwapakazia chuki viongozi wetu kwani sio vizuri.

By the way, mie sio Chadema na wala sio Mnyika, maana msije mkaanza kusema mie Mnyika, mie Mbowe, mie huyu na yule. Mie ni Kada tena Mpinzani.
 
Back
Top Bottom