Mbowe: Muungano lazima ujadiliwe

Akifungua kikao cha Baraza Kuu la Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe amesema wananchi watajadili Katiba kadiri wanavyotaka na siyo kama anavyotaka Rais Jakaya Kikwete na kwamba hata suala la Muungano litajadiliwa kwa vile ni haki yao.

Source: Tanzania Daima.

Mie huyu jamaa huwa simsikilizagi kabisa tangia alipofanya ule ufisadi wa magari mabovu yake kuiuzia CDM, na magari hayo sasa yako juu ya mawe. Tangia hapo kila anachosema namuona ni kwa kujitafutia umaarufu. Hiyo Tume iliyoundwa haina haki yakujadili muungano , kwani sheria iliyowateua wao wenyewe inawazuia.
 
Kama wewe huutaki unaujadili nini sasa? si unasusa tu, au umesahau kuwa kuna kususa?

Kusema si kujadili. Naona hujui maana ya mjadala.
Ribosome lipi bora kwako kwa watu wasiotaka muungano kususa ama kujadili, unajua kuwa implications za kususa ni mbaya zaidi ya kujadili. Iwapo kwa mfano wazanzibari wakisusa au wakijitoa kwenye mjadala wa katiba unafikiri wanaotaka muungano uendelee watakuwa wameshinda? NO, You have to think in both ways.

Umesema 'kusema si kujadili' mimi nasema 'kusema ni kujadili'.
 
Ngoja wafuasi wake wa ione hii watakushukia mi nakimbia.Ushauri vaa helmet usijepata brain concusion.
Mie huyu jamaa huwa simsikilizagi kabisa tangia alipofanya ule ufisadi wa magari mabovu yake kuiuzia CDM, na magari hayo sasa yako juu ya mawe. Tangia hapo kila anachosema namuona ni kwa kujitafutia umaarufu. Hiyo Tume iliyoundwa haina haki yakujadili muungano , kwani sheria iliyowateua wao wenyewe inawazuia.
 
Mbowe vitu kama hivi ambavyo ni muhimu katika mustakabali wa taifa letu ni muhimu ungekuwa unasemea bungeni kwa nafasi yako...sasa unakwenda kusemea kwenye vikao vya chama chako.
 
nini cha kujadili kwenye muungano??

Muungano huu amba Tanzania Visiwani wanautaka wa kuwa na haki sawa kati ya Zanzibar na Tanzania Bara haupo, Angalia Idadi ya watu, angalia eneo la ardhi, mahitaji n,k. Tanzania Visiwani wakati miaka ya 70s tulikuwa tunajua ni mikoa miwili ya Tanzania. Leo wanakuwa wakali kuambiwa mikoa wanataka iwe nchi. HAWATAFIKA.:smile-big:
 
Mbowe vitu kama hivi ambavyo ni muhimu katika mustakabali wa taifa letu ni muhimu ungekuwa unasemea bungeni kwa nafasi yako...sasa unakwenda kusemea kwenye vikao vya chama chako.
Bungeni kuna taratibu zake huwezi kusema chochote wakati wowote hata kama ni kizuri namna gani. Kwenye mada hii tunachotakiwa tukiangalie ni hoja yake je ina mantiki na siyo wapi kasemea.
 
Wazanzibari hasa wapemba wanaufaidi muungano kuliko Watanganyika.
Wazanzibari hao hao wanataka kuuvunja muungano kwa sababu ya mafuta.
Muungano wenyewe umekaa kimtindo mtindo. Zanzibar wana Bendera yao Tanganyika hawana, Zanzibar wana serikali yao Tanganyika hawana, Zanzibar wana katiba yao Tanganyika hawana.
Muungano wa kisanii

Mkuu, hapo kwenye red ndo pamekuwa pakinitatiza sana. Enzi za nyuma, kwenda Zanzibar ilikuwa lazima uwe na pasipot lakini wao kuja hakuna pasipot.

Nakumbuka pia ishu ya mtikila wakati anatafuta wathamini ili chama chake kiweze kupewa usajili wa kudumu,mwanzoni alikataa kwenda zanzibar kwa madai sio sehemu ya Tanzania (yaani sio nchi moja) kwa sababu ingekuwa nchi moja kusingekuwa na umuhimu wa pasipoti.
 
Mbowe vitu kama hivi ambavyo ni muhimu katika mustakabali wa taifa letu ni muhimu ungekuwa unasemea bungeni kwa nafasi yako...sasa unakwenda kusemea kwenye vikao vya chama chako.

Kama baba mwanaasha alipoenda kuomba kibali ccm cha kuvunja baraza la mawaziri sio?
 
nashangaa viongozi wa cccm wanaogopa kujadili swala la muungano-hata wakilikwepa kwa mtindo gani-lazima mwisho wa siku lijadiliwe tu-kukwepa swala la muungano ni woga wa kuface realities na kufanya hivyo hakusaidii muungano ila kunazid kuchochoea moto-
LAZIMA LIJADILIWE NA KAMA HAKUNA FAIDA ZA KUUNGANA-HUO MUUNGANO NI BORA UFE-MAANA NI AIBU KIONGOZI ANATOA FAIDA ZA MUUNGANO KWA KUSEMA ETI "TUMEOANA,WA HUKU WAMEOA+KUOLEWA KULE,LIKEWISE WA KULE"HIO KWA PRUDENT MAN SI FAIDA
 
Kama mlimuelewa Raisi Kikwete hakusema tusiujadili muungano! Amesema tusijadili kuvunja muungano bali tuujadili jinsi gani tunaweza kuuboresha
 
la kujadili ni muundo wa muungano kama ubaki kama ulivyo au ubadilishwe na kama ubadilishwe uwe wa serikali ngapi? moja,tatu au ubaki kuwa mbili kama ulivyo
 
Suala hili la muungano linaweka hadharini picha halisi ya waafrika kwa nini tuko hapa tulipo maskini wa kutupwa.kikubwa kinacho tusukuma katika mijadala ni roho mbaya na fikra finyu.Karne ya 21 bado kuna watu wanafikiri maendeleo yao yataletwa kwa kupewa misaada na nchi nyingine,na wengine wanadhani wana mali nyingi na hawako tayari kushirikiana na ndugu zao.Hivi watu hajiulizi kwa nini Marekani,Ujerumani,Uingereza,Canada,Uswisi zina mafanikio makubwa kiuchumi? Zote hizi ni muungano wa states mbalimbali ambazo zimeungana kujenga nchi imara.Tuige mifano hii kama kweli tunataka kupata maendeleo ya kweli.Matatizo yapo mengi tu tena pande zote mbili lakini busara si kugawana mbao kila mtu abaki na umaskini wake,bali ni kuzichanganya tupate mtumbwi mkubwa tuvue samaki wengi.
 
Kwa sasa suala la Muungano waliache kama lilivyo maana hawana nguvu ya kulisukuma. wanachotakiwa kufanya ni kujiongezea nguvu kwanza za idadi ya wabunge huku bara then from there wanaweza wanashurutisha lolote na likafanikiwa.

Unless bungeni CMD wawe 47% or above hakuna sheria ya nchi wataweza kuibadili, sana sana CCM wanaweza ku respond kwa namna ya kuwa favor wao CCM. Mfano mzuri ni mabadiliko ya hii katiba. CCM wamekubali kupooza tu pressure lakini haiwezi kubadilika vile upinzani na watanzania walio waelewa wangependa iwe.
 
Mkuu sidhani kama hujui hili swala haliamuliwi na wabunge linapelekwa kwa wananchi, hata hivyo kama ni idadi bungeni ni masuala mangapi yaliyoanzishwa na CDM yamefanikiwa wakiwa na idadi ileile likiwemo la muswada wa kuanzisha katiba na hili la juzi la mawaziri kujiuzulu.
 
Kwa sasa suala la Muungano waliache kama lilivyo maana hawana nguvu ya kulisukuma. wanachotakiwa kufanya ni kujiongezea nguvu kwanza za idadi ya wabunge huku bara then from there wanaweza wanashurutisha lolote na likafanikiwa.

Unless bungeni CMD wawe 47% or above hakuna sheria ya nchi wataweza kuibadili, sana sana CCM wanaweza ku respond kwa namna ya kuwa favor wao CCM. Mfano mzuri ni mabadiliko ya hii katiba. CCM wamekubali kupooza tu pressure lakini haiwezi kubadilika vile upinzani na watanzania walio waelewa wangependa iwe.

ukiamua unaweza kubadili katiba iwe kama wananchi tunavyotaka sasa kama wewe mwenyewe unakaa pembeni halafu mbeleni uje ulalamike amka usingizini wewe.SHITUKA BADO ASUBUHI
 
Back
Top Bottom