Mbowe: Muungano lazima ujadiliwe

EasyFit

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
1,269
1,082
Akifungua kikao cha Baraza Kuu la Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe amesema wananchi watajadili Katiba kadiri wanavyotaka na siyo kama anavyotaka Rais Jakaya Kikwete na kwamba hata suala la Muungano litajadiliwa kwa vile ni haki yao.

Source: Tanzania Daima.
 
Akifungua kikao cha Baraza Kuu la Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe amesema wananchi watajadili Katiba kadiri wanavyotaka na siyo kama anavyotaka Rais Jakaya Kikwete na kwamba hata suala la Muungano litajadiliwa kwa vile ni haki yao.

Source: Tanzania Daima.
Ivi ssi watanganyika tunapata nni ndani ya huu muungano?
 
...Kila kitu kilichokuwemo ndani ya katiba ya sasa na vile ambavyo havimo lakini vinahusu nchi zote mbili lazima vijadiliwe. Kama Watanganyika tutaamua kuwepo kwa Serikali tatu ya Tanganyika, Zenj na Muungano basi iwe hivyo ila kwa maoni yangu kutakuwa na gharama kubwa sana za uendeshaji. Serikali moja tu inatosha ila Wazenj hatakubali Serikali yao imezwe ndani ya Serikali moja ya Tanzania.
 
Kila kitu kiwekwe wazi hata hiyo hati ya Muungano iwekwe wazi tuisome tuelewe nini kilikubaliwa wakati huo, sababu huo muungano ni wa nchi mbili zenye wananchi, au km vipi basi uwe muungano wa CCM na Zenji basi, si wanaficha hati ya muungano!
 
Mheshimiwa nampa mkono wa hongera 100%. Mambo hayo lazima yajadiliwe na wanachi maana matatizo makubwa yamo kwenye suala tete la muungano. Mh. Mbowe kura yangu nimekupa tayari.
 
Kamanda Mbowe haitoshi kusema tu tunataka kwa vitendo sasa kwa kuitishwa kura ya maoni hatuoni haja ya huu muungano wa magamba.

Kuna fungu kubwa la pesa linaibiwa na mafisadi kwa kisingizio kuwa ni la Zanzibar lakini ukweli ni kwamba huko Zenji haliwafikii linaishia kwa mafisadi wa magamba, kamanda lifanyie uchunguzi hili!!
 
Wazanzibari hasa wapemba wanaufaidi muungano kuliko Watanganyika.
Wazanzibari hao hao wanataka kuuvunja muungano kwa sababu ya mafuta.
Muungano wenyewe umekaa kimtindo mtindo. Zanzibar wana Bendera yao Tanganyika hawana, Zanzibar wana serikali yao Tanganyika hawana, Zanzibar wana katiba yao Tanganyika hawana.
Muungano wa kisanii
 
Back
Top Bottom