Mbowe: Mbunge mmoja wa Chadema sawa na 30 wa CCM

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,268
33,040
Mbowe(41).jpg

Mwenyekiti wa Chama cha demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe



Mwenyekiti wa Chama cha demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amesema mbunge mmoja wa chama chake ni sawa na wabunge 30 wa Chama Cha Mapinduzi, (CCM).

Alisema hayo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Chadema iliyofanyika juzi Usa River, wilayani Arumeru.
Katika uzinduzi huo, Chadema kilikuwa kina mnadi mgombea wake Joshua Nassari anayewania kuwa mbunge wa Jimbo

la Arumeru Mashariki kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Jeremia Sumari aliyefariki dunia hivi karibuni.
“Ninaomba wananchi wa Arumeru, mnipatie Nassari kuwa mbunge , nadhani mmeona kazi za wabunge wa Chadema

wakiwa bungeni, akisimama kutoa hoja utawaona wale wa chama cha magamba wanavyopata shida…mbunge mmoja wa Chadema ni sawa na wabunge 30 wa chama cha magamba,” alisema huku akishangiliwa.

Alisema wabunge wa Chadema pamoja na uchache wao bungeni, lakini wamekuwa wakiwameza wabunge wa chama tawala wapatao 257.

“Alisema endapo Nassari ataingia bungeni, atakuwa ameiongezea nguvu Chadema kwa uwingi wabunge ambapo nguvu yake itakuwa sawa na wabunge magamba wa CCM 30,” alisema na kuongeza kuwa endapo mgombea wake

atachaguliwa chama chake kitakuwa na uwakilishi wa wabunge 49 bungeni.
Mbowe alisema wabunge wa chama chake ni machachari na wamekwenda bungeni kufanya kazi moja tu ya kutetea maslahi ya Watanzania.




CHANZO: NIPASHE
 
''Chagueni mtu ambaye atasikilizwa na Serikali na mtakayeshirikiana naye kutatua matatizo na sio mtu ambaye anasema kwa ukali ambaye anapotosha jamii." haya ni maneno ya mbunge wa CCM Mwigulu,akimaanisha kuwa CDM huwa hawasikilizwi na serikali, sasa huyu ni ukucha tu Tundu Lissu ambao ukirefuka kidogo unakatwa
 
ccm =wengi kwa namba ila wachache kwa uelewa,ujenzi wa hoja na mzigo kwa walipa kodi.

cdm = wachache kwa namba ila wengi kwa uelewa,ujenzi wa hoja na kielelezo cha taifa.
 
Mheshimiwa Mbowe umesema kweli,wabunge wa Magamba si lolote si chochote kazi yao ni kusinzia,kupiga makofi na kuzomea ila kazi ya wabunge wa CHADEMA ni kutetea wanyonge.
 
uwo niukweli usiopingika. nyie amuwaonaga jinsi wanavyo lala tuu na kusubiri waambie NDIO AU SIO.

CCM ni janga la kitaifa.
 
Kama ni kweli MBUNGE 1 CDM = WABUNGE 30 wa CCM. Tunaomba MDAHALO LIVE kati ya Nassari V Sioyi kabla ya April fool! WARNING hakuna kuingia mitini kwa kisingizio chochote kile.
 
Bange Mbaya! hivi Kwa nini viongozi wengi wa CDM wanapenda hii kitu?
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom