Elections 2010 Mbowe, Marando, Slaa, Zitto, Lissu, Mnyika

kama posho si issue kubwa kwa chadema, tunaomba ile ahadi ya elimu bure ianze sasa kwa michango ya wabunge wenu kusomesha angalau watoto mayatima ktk majimbo yao ndipo kauli ya posho sio issue iwe ni kweli!!!
Dawa ya huyu kilaza ni kutomjibu lolote! Yuko jukwaa ambalo hajui anafanya nini!
 
Mimi naunga mkono jambo hili. Lazima kifanyike kitu, call it kituko, if you will. Kitu ambacho kitaufanya ulimwengu wote utambue uhaini uliofanwa na CCm ktk uchaguzi. Hata hivyo ni vizuri kulifanya hilo within the bounds of bunge by-laws and the constitution. Nina uhakika kuwa viongozi wa upinzani ndani ya CHADEMA na vyama vingine watazingatia kanuni na sheria.
 
Hayo yote mnayoyasema ni kweli, lakini bila ya kuwapa wafuasi wake moyo uenda wakamkimbia kwa kukata tamaa. Aina budi ieleweke kukitoa chama kilichoko madarakani siyo reremama hasa kwa nchi kama zetu ambapo viongozi wengi wanahofia hali yao ya baadaye ikiwa watatoka madarakani na kukabidhi serikali kwa mahasimu wao. Tusidanganyane katika hali ya sasa ambapo Dr. Slaa amekuwa akitishia kuwa akiingia madarakani atawafikisha mafisadi papa wote mahakamani, haitatokea wakamwachia madaraka hivi hivi.
 
Najua Dr. Slaa ni Mwanasaikolojia na najua anajua wafuasi wake wanvyoteseka ingawa mafisadi wanateseka zaidi.

Lakini ni vema aje aseme tutarajie nini na lini (timeframe)
 
Mkuu hilo umenena. hata miye nimekuwa naumiza sana kichwa kutafuta majibu sipati. Je ukimya huu unatokana na nini hasa? Je kuna vitisho labda au kulikoni hata sijajua. Tunaomba kweli Dr. utupatie msimamo wako maana sie bado tuko pamoja nawewe. Tamko lako tunalisubiri na hatujakata tamaa maana kukata tamaa ni dhambi kubwa.
Ahsante nawasilisha
Mnajua sometimes huwa nawaita wavivu wa kusoma michango mingi ya JF la sivyo husingeweka post yako hii hapa kwa tamko alilotoa Dr. Chomoa hapa kuona updates: https://www.jamiiforums.com/uchaguz...-mbowe-marando-slaa-zitto-lissu-mnyika-2.html
 
Kama Wabunge wa CHADEMA watatoka as individuals sina tatizo na hili. lakini kama watatoka wote as CHADEMA ina maana nafasi yao kama opposition katika kikao hich haitakuwepo.
Kwa mujibu wa kanuni nadhani wanaweza kupewa BAN. Then, where will we be heading?
Basi watoke mmoja mmoja kama enzi zile akifundisha mwalimu ambaye wanafunzi wamemkataa. waondoke mmoja mmoja mpaka wabaki sisi em A na B
 
Hata hivyo katika mambo mazito kama haya, ambayo Tamko lolote linaweza kulifikisha nchi katika hatua ambayo haikutarajiwa, ni lazima Busara kubwa itumike, uvumilivu mkubwa na subira wakati Tafakuri ya kina inafanyika. Ndiyo hicho kinachofanyika Luteni.
Niseme tu subiri na Taifa lisubiri for a big surprise punde. Chadema ni chama kinachokwenda kwa mahesabu na hakikurupuki na wala hatakurupuka kamwe.
Jamani, haya maneno kweli yanatoka ktk kichwa chenye mvi!
Nimekukubali hapo Dr. Waiting for suprise :cool:
 
Namuunga mkono Lasikoki kutoka nje ya ukumbi haitasaidia kitu kama kweli wangekuwa serious na issue nzima wamgeretariate from the begining ila sasa is too late. Hii itakuwa sawa na kumkimbia adui wakati unatakiwa upambane hadi kufa. Kuzila , kususa ni tabia za kizamani bora kubakia na kumsoma adui anaudhaifu gani kisha kuponda kichwa km cha nyoka.
 
Ningekuwa mimi ninge march out bse kumsikiliza ni sawa na kukubaliana nae wakati leo wametoa tamko kuwa hawamtambui
 
ni muhimu kwa DR W P SLAA kusubiri hadi apate taarifa zote muhimu ndipo atoe statement. Kuhusu wabunge kususia kikao au hotuba y rais huko ni kupot6ka kabisa. Tena nina wasiwasi wanaotoa wazo hilo wametumwa na CCM. Plz CHADEMA msifanye hivy6 kamwe
 
Hata mimi nawategemea wafanye kama walivyofanya wajumbe wa baraza la wawakilishi kupitia CUF mwaka 2005, Karume alipoingia kuhutubia, wenyewe wali match out kuonyesha ulimwengu kuwa aliiba kura na si raisi halali. Wakifanya vinginevyo na ukimya uliopo sasa sisi wananchi tuliowaamini na kuwashabikia hatutawaelewa.

It has to happen
 
ni muhimu kwa DR W P SLAA kusubiri hadi apate taarifa zote muhimu ndipo atoe statement. Kuhusu wabunge kususia kikao au hotuba y rais huko ni kupot6ka kabisa. Tena nina wasiwasi wanaotoa wazo hilo wametumwa na CCM. Plz CHADEMA msifanye hivy6 kamwe

Please give your justification as well as the implication of doing so. So that they either attend or not attend. this will make them make informed decision.
 
Ni vizuri Dr. Slaa angeatoa vielelezo vinavyoonesha uchakachuaji kabla ya hotuba, ili hata wakikacha kikao ionekane kuna 'supportive document' kuliko kutoka kama 'mbayuwayu'
 
Luteni,
Thanks a lot. Napenda kukushukuru sana. Napenda tu nikuhakikishie kuwa Chadema is not just waiting for something to happen. i) Tulitangaza kutotambua matokeo na kutomtambua Rais aliyepatikana kwa kura kuchakachuliwa. ii) Chadema hatukuhudhuria Kutangazwa kwa matokeo na wala kwenye sherehe ya kuapishwa kwa Rais. Maana yake tulikuwa tunapeleka ujumbe mzito kwa Rais aliyepatikana kwa mchakato usio halali na kwa Tume ya Taifa ya uchaguzi iliyokiri hadharani kuwa "ilifanya makosa mathalan waliponipa kura 3,789 iliyotangazwa na Judge Lewis Makame badala ya 22,021 iliyotangazwa na RO Geita. (Hatimaye walirekebisha). Maeneo mengi yalitangazwa kwa sura hiyo, japo hayakurekebishwa. Hali hii ni dhahiri iliashiria kuwa jumla ya kura za Dr. Slaa zilizokuwakitangazwa na Tume,ilikuwa au inabadilika au haifanani na Kura zilizotangazwa na RO katika Wilaya husika. Kasoro hizi baadhi zilirekebishwa wakati wa kujumlisha matokeo ya jumla, hivyo kasoro hii isiporekebishwa sura ya kura halisi ya nchi hii haiwezi kuwa sawa.iii) Tulilalamikia kubadilika badilika kwa idadi ya Waliojiandikisha kupiga kura mathalan kabla ya uchaguzi Tume ilitangaza idadi ya Wapiga kura 19,670,631 na siku ya matokeo ilitangaza idadi ya waliojiandikisha kuwa 20,137,303. Tumehoji tofauti hii hadharani. iv) Tumehoji idadi ndogo sana ya Wapiga kura 8,626,283 kati ya au 19 Millioni + au 20Millioni +) na kusababisha kiongozi wa nchi yenye watu zaidi ya 43 Millioni kuchaguliwa na idadi ndogo tu ya wapiga kura 5,276,822 kati ya wapiga kura halisi 8,398,394 tu. Hali hii inaashiria nini katika Governance? Hivyo kwa hoja hizi Chadema haikusubiri tu ...jambo literemke from heaven.
Hata hivyo katika mambo mazito kama haya, ambayo Tamko lolote linaweza kulifikisha nchi katika hatua ambayo haikutarajiwa, ni lazima Busara kubwa itumike, uvumilivu mkubwa na subira wakati Tafakuri ya kina inafanyika. Ndiyo hicho kinachofanyika Luteni.
Niseme tu subiri na Taifa lisubiri for a big surprise punde. Chadema ni chama kinachokwenda kwa mahesabu na hakikurupuki na wala hatakurupuka kamwe.

Dr. W. Slaa ninaku-salute, walipokuengua kuwawakilisha wananchi wa karatu wakati huo, walijidanganya ya kuwa walikumaliza,
kumbe walikupa nafasi ya kuwaumbua mbele ya macho ya watanzania,
wameiba kura za kukuunga mkono, wanadhani wamefaulu, anguko lao ni kuu, tena laja upesi.
wananchi "wapiga kura" tunasema sisi em wanatapatapa bali kuondoka madarakani hawana hiyari. muda utawaduwaza!!!

THE STONE THAT THE BUILDER REFUSED, SHALL BE THE HEAD CORNER STONE,
 
Swala hili ni zito sana na linahitaji busara kubwa kulichukulia uamuzi. Ingependeza sana kama tamko rasmi la CHADEMA lingetangulia kabla ya hiyo siku ya hiyo hotuba. Lakini lazima pia tukumbuke kuwa kumshinikiza kiongozi ambaye amevuna heshima kwa wananchi wa Taifa hili kwa uchapa kazi wake, umakini na ujasiri mkubwa kama ule wa kuthubutu kuwaumbua mafisadi, ni kukosa kumtendea haki. Hakika wananchi wapenda maendeleo na mabadiliko nao wamefanya kazi kubwa sana. Nina hakika kabisa atafanya kama baadhi tunavyofikiri, kwenda kuwashukuru. Lakini hilo linaweza kungoja kidogo wakati haya mambo yanawekwa sawa. Ninakubaliana 100% na wazo kwamba ni lazima ishara iwepo ya kupeleka ujumbe kwa chama tawala kuwa ukiritimba na ubabe wake unaelekea ukingoni. Na kama walivyotangulia watoa hoja, ili na mataifa jirani na rafiki wa nchi yetu wawe wamepata ujumbe huo. Hiyo mishara kama ni ya wabunge wa CHADEMA kutoka bungeni au kujifunika nyuso kwa karatasi/gazeti wakati wote wa hiyo hotuba mimi sijui kama ni lipi linakubalika kwa taratibu za bunge letu. Lakini ninataka kuamini kuwa Bunge ni lazima liwe pahala pa kufikishia hisia za wananchi wote bila woga. Ninahakika CHADEMA wanafahamu hilo jukumu la kuziwasilisha hisia za wananchi siku hiyo wakiwa makini kabisa. Hii ni changa moto! Labda JK ampe Dr. Slaa U-PM na mawaziri watatu tu kutoka CHADEMA hapo kitaeleweka. (ukiyataka sana mabadiliko unaweza kuota ota ndoto za mchana).
 
Mimi naona wabunge wanaweza kusikiliza kama sheria inawabana kam haiwabani watoke ila napendekeza Dr. Slaa aandae evidence zake ziwe tayari mara tu baada ya hotuba yake na yeye usiku huo huo awaeleze watanzania wayforward, kupitia Chombo cha habari (TV) au waandishi wa habari ili magazeti yaamke na habari ndo hiyooooo. Timing here is very crucial
 
Congrats Chadema kwa kususia hafla ya kuapishwa kwa waziri mkuu kama mlivyoahidi tunasubiri tukio lile kuu la kutoka nje wakati wa hotuba ya Kikwete najua mtaendeleza msimamo wenu tuko pamoja.
 
Mimi ninaimani they will walkout kuonyesha kuwa anayeongea si chaguo la watanzania na msg itakuwa imetumwa kwa wafadhili kabla ya Dr. Slaa kuongea
 
Back
Top Bottom