Elections 2010 Mbowe, Marando, Slaa, Zitto, Lissu, Mnyika

Kutoka kwenye ukumbi wa bunge haina maana, kutomtambua rais haina maana, kwa kuwa haimuondolei urais wake. Wananchi washamtambua hiyo imetoka.

Kumbuka CHADEMA wenyewe wanaelewa kuwa ushindi wa urais haukuwa wao, alichokuwa anakitaka PHd wa ukweli ni kura zake halali, ama awe ameshinda au lah, kwa sasa sie wananchi hatujaona base wanayosimamia ya kukataa matokeo maana hatuna comparizon ya uhakika kati ya matokeo ya tume na ya majimboni.

CHADEMA watajidanganya sana kama wadhani watanzania tuta support hiyo move ya kutoka nje ya bunge. wanachotakiwa kufanya ni kumtambua jambazi na kupambana nae kwa mtindo wowote anaokuja nao na sio kumkimbia. kumkimbia na kujifanya hawamtambui haitasaidia wala kutusaidia chochote sie tulio nyuma ya chama. Katika mpambano ukipingwa ngumi ukaanguka inuka uendelee na mpambano sio kumkimbia mpinzani wako.

Nawasihi sana wabunge wa chadema, wasimkimbie JK let fight them through available means. Imeshindikana kuwapiga via mhimili wa serikali basi tuwachapie huku kwenye Bunge.

No retreat no surender
 
Superman

Hujaonyesha kipengere kinacholazimisha mbunge kusikiliza hotuba ya ufunguzi.
Kuhusu kutoka induvidually au as a group sidhani kama hiyo ni issue mara ngapi bunge linakuwa tupu, half full or half empty.

Luteni;

Sina kumbukumbu kama Wabunge wa CUF waliposusia kule Zanzibar kama walisimamishwa au la. Kumbuka tu, Spika ana madaraka makubwa na kama taratibu zitakuwa zimekiukwa wanaweza kusimamishwa. Kama ikitokea itachukuliwaje?

Kumbuka bado Wabunge wa CCM wanaweza kuja na hoja binafsi ya kutaka wasimamishwe, then hili nalo limekaaje? mnakumbuka issue ya Zitto, ilikuwa kama mchezo lakini ilijaa ushabiki wa Kisiasa. hebu tuzitembelee kanuni tena:

SEHEMU YA SITA

AMANI NA UTULIVU BUNGENI
58.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya Kanuni ya 4(2), Spika, atawajibika kuhakikisha kuwa utaratibu bora unafuatwa Bungeni, na uamuzi wake kuhusu jambo lolote la utaratibu utakuwa ni wa mwisho.

(2) Mbunge yeyote atakayekiuka utaratibu au Kanuni za Bunge anaweza papo hapo kutakiwa na Spika, afuate utaratibu; na vile vile Mbunge mwingine yeyote aweza kusimama na kumfahamisha Spika kwamba kuna Mbunge anayekiuka utaratibu.
.
.
.

60.-(1) Endapo Mbunge yeyote ataonyesha kutojali mamlaka ya Spika, na kuendelea kuvuruga mwenendo bora wa shughuli za Bunge, basi Spika, aweza kumtaja Mbunge huyo kwamba amedharau mamlaka ya Spika. Papo hapo Mbunge mwingine yeyote aweza kutoa taarifa ya mdomo kwa kutumia Kanuni ya 51 (1), kwamba anakusudia katoa hoja baadaye, ya kumsimamisha kazi Mbunge huyo aliyetajwa. Mbunge aliyetoa taarifa hiyo atapewa nafasi ya kutoa hoja yake mara baada ya hoja iliyokuwa ikijadiliwa kuamuliwa, na hoja hiyo itajadiliwa na kuamuliwa kama hoja nyingine yoyote. Kama kosa limetendeka, katika Kamati ya Bunge Zima, basi papo hapo Mwenyekiti atasimamisha shughuli za Kamati hiyo, Bunge litarudia na Mwenyekiti atatoa taarifa kwa Bunge kuhusu mwenendo wa Mbunge mhusika. Baada ya hapo utaratibu utakuwa kama ilivyokwisha kuelezwa katika fasili hii.

(2) Kama hoja yoyote chini ya fasili hii itapitishwa na Mbunge kusimamishwa kazi, basi ikiwa ni kosa lake la kwanza ataendelea kuwa ameendelea kusimamishwa hadi kikao cha tano, kama kosa la pili hadi kikao cha ishirini, lakini kama kosa ni la tatu au zaidi basi Mbunge huyo ataendelea kuwa amesimamishwa kazi hadi hapo Bunge litakapoamua kwamba kusimamishwa huko kwa Mbunge kukome.
(3) Bila kujali masharti ya fasili zilizotangulia za Kanuni hii, Bunge laweza kumchukulia hatua nyinginezo za kinidhamu Mbunge yeyote aliyetenda kosa chini ya Kanuni hizi, kwa kumpitishia azimio ambalo litataja hatua hizo zinazokusudiwa kuchukuliwa, pamoja na sababu zake.

Ushauri wangu kwa CHADEMA, inawabidi waliangalie kwa makini sana swala hili na madhara yake. Kumbuka CCM wako wengi na mchezo wa kisiasa unaweza kuchezwa. unless kama CHADEMA watakuwa na hoja yoyote ya nguvu zaidi.
 
Mi nadhani hapa inabidi utafutwe utaratibu mzuri, bila kuathiri wabunge wa CHADEMA
 
Nawasihi wabunge wa CHADEMA wahudhurie hotuba ya rais maana wameshaapa na kuitetea katiba iliyopo.

Pia hata wakitoka nje na wakati wakishiriki kumpgia kura waziri mkuu ambaye atateuliwa na rais wasiyemtambua haina maana. Rais ataunda baraza la mawaziri ambalo wabunge wa CHADEMA watakuwa wakiwauliza maswali na kupata na pia kutunga sheria ambayo watashiriki kupitisha kama mswada na kusainiwa na rais wasiyemtambua itakuwa na maana gani.

Nashauri wasikilize hotuba ya rais
 
Luteni;

Sina kumbukumbu kama Wabunge wa CUF waliposusia kule Zanzibar kama walisimamishwa au la. Kumbuka tu, Spika ana madaraka makubwa na kama taratibu zitakuwa zimekiukwa wanaweza kusimamishwa. Kama ikitokea itachukuliwaje?

Kumbuka bado Wabunge wa CCM wanaweza kuja na hoja binafsi ya kutaka wasimamishwe, then hili nalo limekaaje? mnakumbuka issue ya Zitto, ilikuwa kama mchezo lakini ilijaa ushabiki wa Kisiasa. hebu tuzitembelee kanuni tena:

SEHEMU YA SITA

AMANI NA UTULIVU BUNGENI
58.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya Kanuni ya 4(2), Spika, atawajibika kuhakikisha kuwa utaratibu bora unafuatwa Bungeni, na uamuzi wake kuhusu jambo lolote la utaratibu utakuwa ni wa mwisho.

(2) Mbunge yeyote atakayekiuka utaratibu au Kanuni za Bunge anaweza papo hapo kutakiwa na Spika, afuate utaratibu; na vile vile Mbunge mwingine yeyote aweza kusimama na kumfahamisha Spika kwamba kuna Mbunge anayekiuka utaratibu.
.
.
.

60.-(1) Endapo Mbunge yeyote ataonyesha kutojali mamlaka ya Spika, na kuendelea kuvuruga mwenendo bora wa shughuli za Bunge, basi Spika, aweza kumtaja Mbunge huyo kwamba amedharau mamlaka ya Spika. Papo hapo Mbunge mwingine yeyote aweza kutoa taarifa ya mdomo kwa kutumia Kanuni ya 51 (1), kwamba anakusudia katoa hoja baadaye, ya kumsimamisha kazi Mbunge huyo aliyetajwa. Mbunge aliyetoa taarifa hiyo atapewa nafasi ya kutoa hoja yake mara baada ya hoja iliyokuwa ikijadiliwa kuamuliwa, na hoja hiyo itajadiliwa na kuamuliwa kama hoja nyingine yoyote. Kama kosa limetendeka, katika Kamati ya Bunge Zima, basi papo hapo Mwenyekiti atasimamisha shughuli za Kamati hiyo, Bunge litarudia na Mwenyekiti atatoa taarifa kwa Bunge kuhusu mwenendo wa Mbunge mhusika. Baada ya hapo utaratibu utakuwa kama ilivyokwisha kuelezwa katika fasili hii.

(2) Kama hoja yoyote chini ya fasili hii itapitishwa na Mbunge kusimamishwa kazi, basi ikiwa ni kosa lake la kwanza ataendelea kuwa ameendelea kusimamishwa hadi kikao cha tano, kama kosa la pili hadi kikao cha ishirini, lakini kama kosa ni la tatu au zaidi basi Mbunge huyo ataendelea kuwa amesimamishwa kazi hadi hapo Bunge litakapoamua kwamba kusimamishwa huko kwa Mbunge kukome.
(3) Bila kujali masharti ya fasili zilizotangulia za Kanuni hii, Bunge laweza kumchukulia hatua nyinginezo za kinidhamu Mbunge yeyote aliyetenda kosa chini ya Kanuni hizi, kwa kumpitishia azimio ambalo litataja hatua hizo zinazokusudiwa kuchukuliwa, pamoja na sababu zake.

Ushauri wangu kwa CHADEMA, inawabidi waliangalie kwa makini sana swala hili na madhara yake. Kumbuka CCM wako wengi na mchezo wa kisiasa unaweza kuchezwa. unless kama CHADEMA watakuwa na hoja yoyote ya nguvu zaidi.

Asante Superman

naona unaleta vifungu vya jumla jumla kitu ambacho hakitatusaidia, mbunge anahesabika mtoro baada ya kutohudhuria kwa siku ngapi consecutively hapa sijaongelea kutoka bungeni kwa masaa mawili au matatu.
 
Kutoka kwenye ukumbi wa bunge haina maana, kutomtambua rais haina maana, kwa kuwa haimuondolei urais wake. Wananchi washamtambua hiyo imetoka.
You missed my point hatuhitaji kumuondolea Kikwete urais wake tunachotaka ni kuuonyesha umma na dunia uharamia alioufanya, njia mojawapo kama ulivyoshauri Chadema watafute ni pamoja na ku boycott hotuba yake, utajisikiaje kama mtoto wako utamtuma na kupuuza maagizo yako.
 
wow,what a thought man,nakubaliana nawe asilimia zote,for sure hii itakua moja kati ya salamu nzuri sana kwake jk
 
Asante Superman

naona unaleta vifungu vya jumla jumla kitu ambacho hakitatusaidia, mbunge anahesabika mtoro baada ya kutohudhuria kwa siku ngapi consecutively hapa sijaongelea kutoka bungeni kwa masaa mawili au matatu.

Kamnda Luteni;

Amini sisi si Wabunge na hatuko conversant na kanuni zote. lakini amini Zitto alisimamishwa na hoja ilikubalika. Amini pia CUF nadhani nao CUF walisimamishwa kwa muda. Mamlaka ya Spika yako wazi na hatakiwi kudharaulika kama atatumia lungu lake baada ya maelekezo yake kukataliwa. Pia bado kuna hoja binafsi ambazo mimi na wewe hatuwezi zitakuja vipi.

Ndiyo maana nasema CHADEMA inabidi wafanye analysis ya pro and cons na kama kususia kwao kutakuwa na tija yoyote.

Naambatanisha na Kanuni za Bunge for reference.
 
Attachments

  • StandingOrders_1977.pdf
    1.9 MB · Views: 80
Watu, unafahamu chochote katika Bunge letu kanuni inasemaje acha ya wenzetu?

Superman?

Bila kuona ya wenzetu ulimwengunu hata huo uchaguzi ungekuwepo?

Tungebaki na chama kimoja bila magazeti wala tv tukiendele kusimuliwa yanayotokea duniani na warithi wa Nyerere

Inawezekana kabisa kanuni zetu hazina hili la kutoka kwani wakizitunga hawakujua litakuja tokea hili

Now ndio hivyo imetokea Chadema watoke tu.

Unadahni hata hao wachachuaji hawajui madhara ya kuto kuwa na bunge lenye wapinzani?
 
Asante Watu. Nakusoma na tuko pamoja.

Nimeambatanisha kanuni toleo la 2004, tunaweza kupitia machache.
 
Luteni,
Baada ya Tume ya Taifa kumtangaza JK kuwa ndiye mshindi, JK ndiye rais wa nchi, ukubali matokeo, usikubali matokeo, JK ndiye Rais wa nchi. Umtambue, usimtambue, haibadilishi kitu, JK bado ndie rais halali hata kama ameshinda kwenye uchaguzi ambao sio huru na wa haki, mshindi akishatangazwa ndio mshindi na wengine wote mnabwaga manyanga chini, mnasalimu amri na kuanza kujipanga upya kwa 2015.

Kitendo cha kukosa kusema chochote siku ya kutangazwa matokeo, was a mistake na missed opportunity kutoa duku duku lao la moyoni, sasa unanaka wakose na another opporturnity ya kutoa kauli yao kama kiongozi wa upinzani bungeni.

Usiwachuuze Chadema, afterall kususa ni tabia za kike, za kiume ni kupambana!.
 
..Nakubaliana kabisa na namna yeyote ya kuprotest, hata hiyo ya kutoka nje ..LAKINI;
Iwe proven beyond any reasonasble doubt kuwa haitaweza kuwa twested against CHADEMA na .. ANNE MAKINDA et al..wakipatia mwanya hawataicha CHADEMA... na huu uangalifu utiliwe maanani kwa mika 5 ijayo.

Nasema lazima kuwa waangalifu kupindukia...

Hadi sasa ..hakuna any evedence ya usalama wa CHADEMA kutoka..

So they should totaly and completely attend the session!!

Kama kuna mtu ana ushahidi kupitia sheria za bunge..aulete .. lakini so far hakuna so..hakuna kuchezea shilingi ******!

We simply want objective justfication for the move...kama hakuna ...then hakuna mtu kutoka ..wote wahudhurie..!
 
You missed my point hatuhitaji kumuondolea Kikwete urais wake tunachotaka ni kuuonyesha umma na dunia uharamia alioufanya, njia mojawapo kama ulivyoshauri Chadema watafute ni pamoja na ku boycott hotuba yake, utajisikiaje kama mtoto wako utamtuma na kupuuza maagizo yako.

CHADEMA hadi sasa wapo kimya, hawajaweza kuuthibitishia UMMA kuwa wameidhulumiwa na kwa kiwango gani. Dr kasema bado wanakusanya ushahidi. Mpaka hapo CHADEMA watakapothibisha ki ukweli kuwa wamedhulumiwa ndipo tuangalie reaction agaist dhuluma. Hadi hivi sasa JK ataendelea kuwa halali hadi hapo CHADEMA watakapotoa report yao na ikakubalika kuwa kweli walidhulumiwa. na kwa jinsi wanavyochelewa kuitoa hiyo report na ndivyo inazidi kupoteza thamani yake. CHADEMA has to speedup kutoa hiyo repoti yao kabla joto hili la uchaguzi halijaisha.

Wabunge na uongozi wa chadema please msiwape CCM nafasi nyingine ya kuwaangusha kwa kususia Bunge. Kwa nchi hizi duni kususa kuwa hakusaidii. Mfano mzuri tunao ni CUF. Walisusa weeeeeeeeeeee mwisho wa siku hao wamenunuliwa now they are CCM B.

Mpambanaji wa ukweli huwa hategemei huruma wala silaha alokwisha poteza, hutumia kile alichonacho. CHADEMA tumia wabunge wenu na madiwani vizuri. watanzania tupo pamoja nanyi
 
Mm,nafikiri itapendeza sana kama tutaujulisha uongozi wa chadema,ili wao wakutane na kujadili lipi bora,na je kufanya hivyo kunavunja sheria,kisha wafanye maamuzi sahihi.hii itakuwa kwa faida ya chama na taifa kwa ujumla
 
Kamnda Luteni;

Amini sisi si Wabunge na hatuko conversant na kanuni zote. lakini amini Zitto alisimamishwa na hoja ilikubalika. Amini pia CUF nadhani nao CUF walisimamishwa kwa muda. Mamlaka ya Spika yako wazi na hatakiwi kudharaulika kama atatumia lungu lake baada ya maelekezo yake kukataliwa. Pia bado kuna hoja binafsi ambazo mimi na wewe hatuwezi zitakuja vipi.

Ndiyo maana nasema CHADEMA inabidi wafanye analysis ya pro and cons na kama kususia kwao kutakuwa na tija yoyote.

Naambatanisha na Kanuni za Bunge for reference.
Asante nimejaribu kuzipitia lakini hakuna sehemu inayomlazimisha mbunge kukaa ndani ya ukumbi wa bunge kwa kutwa nzima bila kutoka ila nimepata hiki kipengere
SEHEMU YA KUMI NA SITA
MENGINEYO
117. Kuhudhuria vikao vya bunge ni wajibu wa kwanza wa kila mbunge. Mbunge yeyote atakayeshindwa kuhudhuria Mikutano ya bunge mitatu mfululizo, bila ruhusa ya Spika iliyotolewa kwa maandishi atapoteza ubunge wake
Hii haimnyimi mbunge haki ya kutoka ndani ya bunge wakati wowote anaotaka wakati shughuli za bunge zikiendelea.
Ninachojua serikali na hata JK anaombea jambo hili lisitokee maana litakuwa embarrassment ya hali ya juu kwake binafsi na kwa mataifa rafiki.
 
Luteni,
Baada ya Tume ya Taifa kumtangaza JK kuwa ndiye mshindi, JK ndiye rais wa nchi, ukubali matokeo, usikubali matokeo, JK ndiye Rais wa nchi. Umtambue, usimtambue, haibadilishi kitu, JK bado ndie rais halali hata kama ameshinda kwenye uchaguzi ambao sio huru na wa haki, mshindi akishatangazwa ndio mshindi na wengine wote mnabwaga manyanga chini, mnasalimu amri na kuanza kujipanga upya kwa 2015.

Kitendo cha kukosa kusema chochote siku ya kutangazwa matokeo, was a mistake na missed opportunity kutoa duku duku lao la moyoni, sasa unanaka wakose na another opporturnity ya kutoa kauli yao kama kiongozi wa upinzani bungeni.

Usiwachuuze Chadema, afterall kususa ni tabia za kike, za kiume ni kupambana!.
You also missed my point.
 
Mengi yamejadiliwa kwa marefu na mapana yake....ninacho amini ni kuwa hata mataifa rafiki yameshapata ujumbe wa kilichotendeka Tz...mara ngapi nimekuwa nikisoma ktk vyombo vya habari kuwa mabalozi wa Mataifa mbalimbali wamemtembelea Slaa??? Waliongea nini?? Hakuna ajuaye, walimshauri nini bado ni Dr. wa ukweli ndo ajuae....

Ku-boycot kwa wabunge wa CHADEMA si lazima watoke nje ya ukumbi.....Humo ndo zinapojadiliwa mada zote zinzohusu taifa hili.....waboycot humo....they shudnt run away......But further more CHADEMA have got people wanaijua sheria mo than i do......Am sure they will come up with a +ve move......A move that will have no harm to the paty and party memberz..........
 
Luteni,
Thanks a lot. Napenda kukushukuru sana. Napenda tu nikuhakikishie kuwa Chadema is not just waiting for something to happen. i) Tulitangaza kutotambua matokeo na kutomtambua Rais aliyepatikana kwa kura kuchakachuliwa. ii) Chadema hatukuhudhuria Kutangazwa kwa matokeo na wala kwenye sherehe ya kuapishwa kwa Rais. Maana yake tulikuwa tunapeleka ujumbe mzito kwa Rais aliyepatikana kwa mchakato usio halali na kwa Tume ya Taifa ya uchaguzi iliyokiri hadharani kuwa "ilifanya makosa mathalan waliponipa kura 3,789 iliyotangazwa na Judge Lewis Makame badala ya 22,021 iliyotangazwa na RO Geita. (Hatimaye walirekebisha). Maeneo mengi yalitangazwa kwa sura hiyo, japo hayakurekebishwa. Hali hii ni dhahiri iliashiria kuwa jumla ya kura za Dr. Slaa zilizokuwakitangazwa na Tume,ilikuwa au inabadilika au haifanani na Kura zilizotangazwa na RO katika Wilaya husika. Kasoro hizi baadhi zilirekebishwa wakati wa kujumlisha matokeo ya jumla, hivyo kasoro hii isiporekebishwa sura ya kura halisi ya nchi hii haiwezi kuwa sawa.iii) Tulilalamikia kubadilika badilika kwa idadi ya Waliojiandikisha kupiga kura mathalan kabla ya uchaguzi Tume ilitangaza idadi ya Wapiga kura 19,670,631 na siku ya matokeo ilitangaza idadi ya waliojiandikisha kuwa 20,137,303. Tumehoji tofauti hii hadharani. iv) Tumehoji idadi ndogo sana ya Wapiga kura 8,626,283 kati ya au 19 Millioni + au 20Millioni +) na kusababisha kiongozi wa nchi yenye watu zaidi ya 43 Millioni kuchaguliwa na idadi ndogo tu ya wapiga kura 5,276,822 kati ya wapiga kura halisi 8,398,394 tu. Hali hii inaashiria nini katika Governance? Hivyo kwa hoja hizi Chadema haikusubiri tu ...jambo literemke from heaven.
Hata hivyo katika mambo mazito kama haya, ambayo Tamko lolote linaweza kulifikisha nchi katika hatua ambayo haikutarajiwa, ni lazima Busara kubwa itumike, uvumilivu mkubwa na subira wakati Tafakuri ya kina inafanyika. Ndiyo hicho kinachofanyika Luteni.
Niseme tu subiri na Taifa lisubiri for a big surprise punde. Chadema ni chama kinachokwenda kwa mahesabu na hakikurupuki na wala hatakurupuka kamwe.

Nimeamua kuwataja nyie kwa vile naelewa mnaweza kunifikishia ujumbe wangu kwa viongozi na wana Chadema wote.

Kwanza nianze kwa kuwapongeza na kuwashukuru kwa kazi nzito mnayoifanya, pili ujumbe wangu ni mfupi tu kwa leo naomba kwa niaba ya kura zaidi ya milioni mbili za watanzania tulizowapa na zingine zikaibiwa muwe na msimamo wa pamoja.

Aliyekuwa mgombea urais Dr.Slaa(PhD) ameyakataa matokeo, nadhani wakati anaamua hivyo alikuwa na baraka zote za chama. Kama alikuwa na baraka za chama, pia chama kilikuwa na mikakati yake ya baadaye(plan-B). Sitaki kuamini kuwa mkakati wenu ulikuwa kutoyatambua matokeo tu basi baada ya hapo mkae kimya waiting for something to happen from heaven.

What I know you are still collecting data for evidence but whilst doing that please, DO NOT ATTEND THE INAUGRATION OF THE PRESIDENT'S SPEECH THIS WEEK. But if you decide otherwise you will have disappointed me and many of your supporters who voted you and Chadema on 31October 2010.

It is my plea.
 
Luteni,
Thanks a lot. Napenda kukushukuru sana. Napenda tu nikuhakikishie kuwa Chadema is not just waiting for something to happen. i) Tulitangaza kutotambua matokeo na kutomtambua Rais aliyepatikana kwa kura kuchakachuliwa. ii) Chadema hatukuhudhuria Kutangazwa kwa matokeo na wala kwenye sherehe ya kuapishwa kwa Rais. Maana yake tulikuwa tunapeleka ujumbe mzito kwa Rais aliyepatikana kwa mchakato usio halali na kwa Tume ya Taifa ya uchaguzi iliyokiri hadharani kuwa "ilifanya makosa mathalan waliponipa kura 3,789 iliyotangazwa na Judge Lewis Makame badala ya 22,021 iliyotangazwa na RO Geita. (Hatimaye walirekebisha). Maeneo mengi yalitangazwa kwa sura hiyo, japo hayakurekebishwa. Hali hii ni dhahiri iliashiria kuwa jumla ya kura za Dr. Slaa zilizokuwakitangazwa na Tume,ilikuwa au inabadilika au haifanani na Kura zilizotangazwa na RO katika Wilaya husika. Kasoro hizi baadhi zilirekebishwa wakati wa kujumlisha matokeo ya jumla, hivyo kasoro hii isiporekebishwa sura ya kura halisi ya nchi hii haiwezi kuwa sawa.iii) Tulilalamikia kubadilika badilika kwa idadi ya Waliojiandikisha kupiga kura mathalan kabla ya uchaguzi Tume ilitangaza idadi ya Wapiga kura 19,670,631 na siku ya matokeo ilitangaza idadi ya waliojiandikisha kuwa 20,137,303. Tumehoji tofauti hii hadharani. iv) Tumehoji idadi ndogo sana ya Wapiga kura 8,626,283 kati ya au 19 Millioni + au 20Millioni +) na kusababisha kiongozi wa nchi yenye watu zaidi ya 43 Millioni kuchaguliwa na idadi ndogo tu ya wapiga kura 5,276,822 kati ya wapiga kura halisi 8,398,394 tu. Hali hii inaashiria nini katika Governance? Hivyo kwa hoja hizi Chadema haikusubiri tu ...jambo literemke from heaven.
Hata hivyo katika mambo mazito kama haya, ambayo Tamko lolote linaweza kulifikisha nchi katika hatua ambayo haikutarajiwa, ni lazima Busara kubwa itumike, uvumilivu mkubwa na subira wakati Tafakuri ya kina inafanyika. Ndiyo hicho kinachofanyika Luteni.
Niseme tu subiri na Taifa lisubiri for a big surprise punde. Chadema ni chama kinachokwenda kwa mahesabu na hakikurupuki na wala hatakurupuka kamwe.

Dr nakushukuru kwa kuyatolea maelezo mambo muhimu na hasa kupitia jamvi hili.
 
Back
Top Bottom