Mbowe - Magufuli anatekeleza ahadi za CHADEMA

AKILI TATU

JF-Expert Member
Feb 10, 2016
2,658
2,804
Wakuu,

Nimekuwa nikijiuliza sana juu ya jambo hili na sipati majibu ya kina hii ni kutokana na miezi ya mwanzoni ya utawala wa Ndugu Rais Magufuli wakati huo alipokuwa anatumbua majipu mfululizo na safari za ghafla ghafla.

Mwenyekiti wa CHADEMA taifa Ndugu Freman Mbowe alinukuliwa akisema kuwa Bwana Magufuli anatekeleza ilani ya CHADEMA kwa kuwa imebainisha hayo mambo aliyokuwa akiyafanya na ilifika hatua CHADEMA wakawa wanawabeza CCM wakisema kuwa wamemchagua mtu mwenye mwili wa CCM ila roho ya CHADEMA.



Kadri siku zilivyozidi kwenda mbele naona CHADEMA nao wamembadilikia Ndugu JPM kwa kusema ati hafuati kanuni na misingi ya uongozi, inawezekana hata ile Ilani pia.

Sasa naomba kufafanulia hapa Rais Magufuli anaongoza kwa kupitia ilani ipi?
 
Back
Top Bottom