Mbowe: Lowassa ni dhaifu, ni bubu

Status
Not open for further replies.
Kwa mujibu wa wandani wa siasa za chama kipindi hicho walikuwa tayari kuwakilishwa na hata jiwe kugombea ili mradi 'mfumo' ung'oke. Hivyo msishangae 'koment' hizi.
 
Mh.Mbowe amenukuliwa na Tanzania Daima akimchana Mh.Lowasa kuwa ni mgombea dhaifu na bubu wa kukemea ufisadi.

Amesema UKAWA hawawezi kuwa nae,hivyo asiwatishe CCM kuwa ana nafasi UKAWA.

Source:Tanzania Daima page no.5
Ikawaje tena wakamchukua?
 
Mbowe alikuwa sahihi kwa alichokisema. Ububu na udhaifu wa Lowassa katika kukemea ufisadi umewaambukiza Chadema.

Leo hii nao Chadema wameacha kukemea ufisadi wamekuwa wadhaifu na mabubu.
 
xana ndio nini? Ndio maana nasema nyie vijana hamjielewi zaidi ya ushabiki wa kijinga.yani ni bendera fuata upepo ukiulizwa unachompendea Lowasa ninini hujuwi.any way we dogo hata kura unaweza usipige ngoja nikuache uendelee kukomaa kiakili.
Sasa hivi uko radhi kula kimba la lowassa....bei yenu chee sana.
 
Kwa Tanzania yote haya yanawezekana! Akili zetu zinaruhusu kuambiwa hata usile ukila utakufa mtu kweli anaamua asile ili asife kwa kula chakula, halafu anakufa kwa njaa!
 
Jamani hebu tuweni wakweli tuwache ushabiki mandazi, Mbowe kwa Lowassa ni sawa kufananisha mlima Kilimanjaro na mlima Tegeta.

Kwanza elimu za hawa watu ni kipimo tosha.

Dr.Slaa mwenyewe akimfikilia Lowassa presha inapanda ndani ya Chadema kwenyewe kuna mapandikizi ya Lowassa.

Duh Maandikizi ya Lowasa kumbe yalikuwa Mbowe, Lema, Tundu Lisu na Msigwa!
 
Mh.Mbowe amenukuliwa na Tanzania Daima akimchana Mh.Lowasa kuwa ni mgombea dhaifu na bubu wa kukemea ufisadi.

Amesema UKAWA hawawezi kuwa nae,hivyo asiwatishe CCM kuwa ana nafasi UKAWA.

Source:Tanzania Daima page no.5
Watu ni wanafiki na wasaliti kwa kiwango cha mwendo haraka.
 
lowasa ni vizuri akapumzika na kuendelea kupata pension yake ya uwaziri mkuu mstaafu japo hakustahili. watanzania masikini wa fedha lakini matajiri wa fikra hawako tayari kuona ikulu yao inamilikiwa na mapacha watatu kamwe. lowasa sio bubu tu bali hafai kwenye taasisi nyeti kama ya urais..
Nakunukuu.
 
OKW BOBAN SUNZU

Lowassa ni mdhalimu sana. Aliwahadaa wana jimbo lake kuwa atawawekea lami kwenye barabara zote za "mitaani" za miji mikubwa Jimboni kwake. Alichokifanya akachukua hela za mfuko wa Jimbo, akazitumia kuweka Lami barabara za hapo Monduli Mjini hadi kwake tu.

Udhalimu huu ulifanywa na Mwandosya kwa kubadilisha matumizi ya hela za ujenzi wa Uwanja wa Mwanza, akazipeleka kwenye ujenzi wa Uwanja wa Songwe; kadhalika Magufuli alivyo-diverge ujenzi wa barabara ya Busisi - Bukoba; ikanyooka kupitia kwake Chato, then Biharamulo, Muleba, Bukoba badala ya kukunjia pale Bwanga ikatokee Biharamulo, Muleba, Bukoba kama ilivyokuwa kwa mpango wa awali.
Upo JF?
 
Mkuu hii ni kuchochea kuni tu na si vinginevyo, Hapa Mbowe anajaribu kuwaambia ccm kuwa Wamfukuze au wamzuie tu Lowassa kugombea kupitia Ccm, na hili likitokea ni Mende kudondoka juu ya Marumaru akiwa miguu juu mgongo chini kwa ccm.

Mbowe na upinzani mzima wanachochoa kuni kwenye tanuri..!!

Ccm wakimpitisha Lowassa....nchale, Wasipompitisha...... nchale!!!!! Unajua kwanini?

Wakimpitisha Lowassa ndipo watakumbana na maswali magumu toka kwa wananchi, Je lile walilokuwa wakidai kuwa ni Gamba, lini imepata kuvuliwa na kubaki ngozi nyororo..? Hapa wataanguka asubuhi saa tatu kwenye uchaguzi..!!!

Wasipompitisha Lowassa, ndiposa Lowassa atatangaza hadharani kwamba ule ufisadi wa Richmond ulikuwaje? Nani muhusika na alihusika vipi..!! Lowassa anasiri nyingi za ccm maufisadi yote iwe ni Tangilod, EPA, Escrow na ufisadi wote mwingine unaoujua..!!! Unapopambana na Lowassa unapambana na Chenge, unapambana na Rostam, Unapambana na makundi yote makuu ya ufiaadi ndani ya ccm..!! Haya ndiyo yaliyoapa Lowassa lazima awe mgombea ndani ya ccm. Lengo lao kuu ni kulipa kisasi kwa yaliyowapata kisiasa ndani ya utawala huu.

Kama wao walipata ajali ya kisiasa basi lazima watu fulani wapate kifo cha kisiasa...!!!

Hiviq unakumbuka namna Rostam Azizi alivyojiuzulu nyadhifa zake zote ikiwemo Ubunge na Ujumbe wa NEC?? Unadhani aliondoka kwa Amani??

Mwaka hui tutaona mengi we subiri

BACK TANGANYIKA
Huonekani JF siku hizi mkuu
 
Hawana Uhuru wa kuhoji mambo kwenye chama lakini wamekazana kusema Magufuri ana minya demokrasia.
 
Kama kawaida ya watanzania kila kunapotokea jambo nilalotulazimu kujikumbusha wosia wa mpenwa wetu Nyerere hatuna budi kujikumbusha baadhi ya maneno yake ya busara kwa sababu ni kiongozi wa kitaifa anayeheshimika hapa Tanzania.

Pia kwa sasa hatuna budi kujikumbusha wosia wa Ndugu Mbowe kwa watanzania ili kuchagua kiongozi mzuri kwa maana ya utendaji, maadili na mwadilifu

Quotes;


"Wanajidanganya, Lowassa ni dhaifu sana. Amekaa serikalini zaidi ya miaka 30 na hakuna maendeleo yanayoonekana ndani ya serikali zaidi ya kila siku wizi na ubadhirifu kuongezeka," Freeman Mbowe.


"Hao wanaomtaka Lowassa ni wale wanaojua kuwa watanufaika binafsi akipita kwenye urais lakini kimsingi huyu jamaa ni dhaifu sana na hafai kuongoza Tanzania ya sasa yenye changamoto lukuki. Wapambe wake wanasema si msemaji bali mtendaji, hivi nani atakubali porojo hizo wakati tunajua akiwa Waziri Mkuu hakufanya lolote kukemea wizi, ubadhirifu na ufisadi? Richmond ilikuja akiwa wapi?," Mbowe.

"Sina ugomvi wala simchukii Lowassa binafsi, lakini ni vema hawa wanaosema ni mtu wa maamuzi magumu wakaueleza umma wakati watendaji wa serikali wakitafuna mabilioni ya fedha, CCM wakipitisha Katiba inayopendekezwa ya hovyo pale Dodoma wakitetea kwa wizi...yeye alisema au kufanya nini?," Mbowe.

"Huyu mtu yumo ndani ya mfumo wa ufisadi ulioiharibu nchi kwa takriban miaka 50 halafu mnataka kutuaminisha ni mchapakazi, tuwe serious jamani, nchi inahitaji mabadiliko ambayo yanapatikana UKAWA," Mbowe.

"Msipate shida, UKAWA ni kiboko ya Lowassa na CCM yake, ikifika Oktoba wananchi watuchague tuwakwamue kutoka hapa tulipo, haiwezekani miaka 50 sisi tungali maskini wa kutupwa ilhali tuna rasilimali lukuki," Mbowe.

"Sasa tutapambana na CCM jino kwa jino mpaka kieleweke, wao walikuwa wakishinda kirahisi kwa sababu walikuwa na wenyeviti wa vijiji, lakini sasa wataonja nguvu yetu,"
Nimemuelewa sana
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom