Mbowe kutumia gari la serikali kwenye kampeni ni sawa?

Sio mbowe tu. maalim seif alipo kwenda tuliani mvomelo amepelekwa na gari tano za serikali hivyo wakongwe hawa tuwaulize haya sio matumizi mabaya ya fedha za umma.
 
Nimemuona Freeman Mbowe mwenyekiti wa Chadema taifa akitumia gari la serkali (KUB) kwenye kampeni za udiwani maeneo mengi nchini, nikajiuliza sheria inasemaje wadau.......

Tunathamini mchango wa freeman Mbowe na Dr Slaa katika kuifikisha chadema hapo ilipo lakini nafikiri katika uchaguzi ujao wa chama Ndugu hawa wawili wapumzike na chama kipate viongozi wapya sababu kuendelea kwa kuwa viongozi kutakigharimu chama hasa kwa kuwa wapinzani wao wameshapata maeneo ya kuwasemea kama mapungufu
 
Mada inahusu wagombea au matumizi ya magari ya serikali kwa shughuli za chama?
 
Tunathamini mchango wa freeman Mbowe na Dr Slaa katika kuifikisha chadema hapo ilipo lakini nafikiri katika uchaguzi ujao wa chama Ndugu hawa wawili wapumzike na chama kipate viongozi wapya sababu kuendelea kwa kuwa viongozi kutakigharimu chama hasa kwa kuwa wapinzani wao wameshapata maeneo ya kuwasemea kama mapungufu
Kwa kifupi unachosema ni kwamba Mbowe na Slaa sasa hivi hawafai kuongoza Chadema. Siyo?
 
Nawapenda sana Pro chadema hapa jukwaani,kwa matusi na kejeli zao,wanazidi kukijenga chama chao na matokeo tumeona walivyoshinda kwa kishindo viti vya udiwani,na 2015 itakuwa hivi hivi tu,
 
acha unafiki ndugu unakua kama sio mzalendo tumia wewe basi kama unaona mbowe anafaidi
wewe usiruke mkoa wakilimanjaro tutaondoka nashingo yako
na nikwanini usimpige picha kama sio umbeya >?

He! kumbe CDM ni ya watu wa Kilimanjaro! ngoja nisiiseme vibaya nikajakukatwa shingo bure! maana Kule Kilimanajaro ndio nakoishi.
 
hata kama katumia kwani ni vibaya mbona watu wa sisiem hutumia sana magari hayo kwani nayo ni sawa? mbowe ni mtanzania wacha atumie mali ya taifa.
 
Wakuu, mbona hua mnamini vitu haraka hivi? Kwani Mbowe anaongoza serikali gani? kivuli au? mleta hoja labda kama amechanganya sura ya mtu mmoja wa magamba na Mbowe au kama vipi, weka na picha but sio photo shop hapa tutajua namna ya kutofautisha!
 
Nimemuona Freeman Mbowe mwenyekiti wa Chadema taifa akitumia gari la serkali (KUB) kwenye kampeni za udiwani maeneo mengi nchini, nikajiuliza sheria inasemaje wadau.......
Serikali ya CCM ni DHAIFU inashindwa kusimamia mali zake. Kamuuluze mwenyekiti wa CCM Taifa kuhusu sheria zinasemaje? CCM imeshika hatamu na tunafuata Dira za chama.
 
Waliikwapua thread yangu sasa ningewekaje na hata ningeiweka wasingekawiya kusema photoshop.Vipi kamanda wako mbona wamemwondosha M4C au hili dogo kwako ha ha ha ha.

........
Picha za kicgapo cha Lema uliweka nirudi kuangalia?
 
Mkuu BHULULU sijajichanganya mimi ni ngongo na nitabakia kuwa ngongo Mingoi anaweza kuja hapa kukuthibitishia na ukitaka unaweza kuomba msaaada wa Mods.

Hoja hapa ni Mheshimiwa Mbowe kutumia gari la serekali kwenye kampeni za chama chake ?.Badala ya kujibu hoja mnakimbilia kutukana wadadisi kwakuwa mkosaji hapa anatoka upande unaoushabikia ?.

Jamaa amejichanganya kweli na mi-ID yake hiyo mara@Mingoi,mara@Ngongo, kazi kweli kweli
 
Last edited by a moderator:
Mkuu BHULULU sijajichanganya mimi ni ngongo na nitabakia kuwa ngongo Mingoi anaweza kuja hapa kukuthibitishia na ukitaka unaweza kuomba msaaada wa Mods.

Hoja hapa ni Mheshimiwa Mbowe kutumia gari la serekali kwenye kampeni za chama chake ?.Badala ya kujibu hoja mnakimbilia kutukana wadadisi kwakuwa mkosaji hapa anatoka upande unaoushabikia ?.
Sina uhusiano wa kindugu,kijumuiya wala kiitikadi na Ngongo.Nimejiunga jf baada ya kuwa viewer kwa takribani miaka 3 sijawahi kuwa shabiki,mfuasi wala mkereketwa wa maoni na mtazamo wa Ngongo.Simfahamu huyo mtu kwa njia yeyote zaidi ya mwanaJF mwenzangu.
 
Hebu sikilizeni wenzangu, Mh Mbowe si kiongozi wa Serikali, bali anaongoza upinzani, kwa hiyo hata kama amepewa gari na serikali, hakupewa kwa ajili ya shughuli za serikali bali kwa shughuli zake za upinzani (izingatiwe kuwa shughuli kuu ya upinzani ni harakati za kukiondoa Chama kinachotawala madarakani) kwa hiyo akilitumia kwenye kampeni za kuiondoa CCM madarakani ni sahihi kabisa, si ndio kazi yake!
 
Back
Top Bottom