Mbowe, Kunahitajika mkakati wa haraka Bungeni

FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
31,635
37,840
Wakuu,

Naona kila dalili kwamba wabunge wa CHADEMA na wale wa NCCR - Mageuzi wapo pamoja na naona ushirikiano wao ni mzuri sana bungeni. Kinacholeta tatizo ni huyu mwenyekiti wa NCCR - Mageuzi ndugu Mbatia ambaye bado ana donge la kushidwa ubunge wa kawe na Mh. Halima Mdee kiasi kwamba hata kesi aliyofungua dhidi yake amegoma kuifuta.

Ukimwondoa Mbatia katika NCCR - Mageuzi wanaobaki ni wapiganaji na wanatetea maslahi ya watanzania kama walivyo CHADEMA. Naomba ushirikiano huu uendelee hata huko Igunga ambako tunajiandaa kuchukua Jimbo basi tuite " CHADEMA & NCCR MAGEUZI OPERATION CHUKUA JIMBO". Pongezi zangu ziende kwa wabunge wote wa NCCR - Mageuzi kweli nyie ni wapiganaji wenzetu. Sisi wananchi wanyonge tunafarijika sana tukiona mnakuwa kitu kimoja.

ref: Hotuba ya Mbuge kijana wa NCCR (jina limenitoka) alivyoguswa kwa kutolewa bungeni kiuonevu kwa Mh. Wenje jana.

Tatizo la nccr ni mbatia. Lkn kule mjengoni mambo sasa yanaenda sawa, Mbatia alitaka kuwachanganya hasa pale mwanzoni alipotaka wabunge wa nccr waungane na ccm wakati wa uchaguzi wa uspika.

Wakuu,

Naona kila dalili kwamba wabunge wa CHADEMA na wale wa NSSR - Mageuzi wapo pamoja na naona ushirikiano wao ni mzuri sana bungeni. Kinacholeta tatizo ni huyu mwenyekiti wa NCCR - Mageuzi ndugu Mbatia ambaye bado ana donge la kushidwa ubunge wa kawe na Mh. Halima Mdee kaisi kwamba hata kesi bado hataki kuifuta.

Ukimwondoa Mbatia - NCCR - Mageuzi waliobakia ni wapiganaji na wanatetea maslahi ya watanzania kama walivyo CHADEMA. Naomba ushirikiano huu uendelee hata huko Igunga ambako tunajiandaa kuchukua Jimbo basi tuite " CHADEMA & NCCR MAGEUZI OPERATION CHUKUA JIMBO". Pongezi zangu ziende kwa wabunge wote wa NCCR - Mageuzi kweli nyie ni wapiganaji wenzetu. Sisi wananchi wanyonge tunafarijika sana tukiona mnakuwa kitu kimoja.

ref: Hotuba ya Mbuge kijana wa NCCR (jina limenitoka) alivyoguswa kwa kutolewa bungeni kiuonevu kwa Mh. Wenje jana.

Naunga mkono hoja. Nadhani ulimaanisha NCCR-MAGEUZI na sio NSSR-MAGEUZI

Wakuu,

Naona kila dalili kwamba wabunge wa CHADEMA na wale wa NSSR - Mageuzi wapo pamoja na naona ushirikiano wao ni mzuri sana bungeni. Kinacholeta tatizo ni huyu mwenyekiti wa NCCR - Mageuzi ndugu Mbatia ambaye bado ana donge la kushidwa ubunge wa kawe na Mh. Halima Mdee kaisi kwamba hata kesi bado hataki kuifuta.

Hapo knye red hicho chama bado hakijasjiliwa

Njaa inamsumbua naona anafikiria mivinyo kwa sana kuliko kutetea maslahi ya waganga njaa wa bongo

huyo mbunge anaitwa machali.halafu nccr inawabunge vijana sana na machachari kama kafulila na mkosamali.

Kitendo hiki cha wabunge wa CHADEMA na NCCR-MAGEUZI kuwa pamoja bungeni kimenipa faraja kubwa.Tunawaomba waheshimiwa muendelee hivyohivyo.NCCR akiondoka Mbatia tu basi,upiganaji utakuwa mzuri.Kila la kheri!!1

Kitendo hiki cha wabunge wa CHADEMA na NCCR-MAGEUZI kuwa pamoja bungeni kimenipa faraja kubwa.Tunawaomba waheshimiwa muendelee hivyohivyo.NCCR akiondoka Mbatia tu basi,upiganaji utakuwa mzuri.Kila la kheri!!1

ye nyumbai

wabunge chadema na NCCR MAGEUZI ndio watetezi wetu cc wananchi hivyo itapendeza zaidi endapo wataungana pa1 kulichukua jimbo Igunga ila wenzetu wa CUF ndio hivyo tena, wameshaolewa na CCM hivyo hawafurukuti chochote

Safi sn NCCR- na CHADEMA kwa ushirikiano muliouonesha jana Bungeni, nina imani tukiungana kuwa kitu kimoja tutaweza kuwadhibiti mafisadi wa CCM,naomba kazeni msuli muweze kutukomboa sisi wananchi wanyonge.

Hii nimeifurahia kama wao wapinzania wanajua ni lazima washughulike pamoja wakati mwingine na itasaidia wao kwenda juu

Freeman Mbowe-Kiongozi wa Upinzani Bungeni Ujumbe huu ukufikie.

Kila siku tunashuhudia hali inazidi kwenda kombo Bungeni.
Tumeshuhudia madudu ya wabunge wa CCM kuzomea,kupiga meza hovyo,kulala,kukejeli na kudharau wabunge wa upinzani na upendeleo kwa wabunge wa ccm unaofanywa na spika wao.
Tumeshuhudia ushahidi mbali unaowasilishwa kwa spika hausomwi hadharani matokeo ya kuiacha jamii ikiwa na maswali mengi kuliko majibu.
Tumeshuhudia spika akitumia madaraka na kanuni vibaya na kuleta upendeleo wa wazi kwa wabunge wa ccm.
Jana imeanza tabia ya kuwatoa wabunge wa Chadema nje ya bunge huku mwenyekiti akionekana wazi kuipendelea ccm, leo tena wamemtoa Lema,Lissu na Msigwa.
Binafsi nachukizwa sana na huu upendelen unaoletwa na spika na naibu wake na hali hii ndio inayofanya wabunge wa ccm wajione wapo juu ya sheria na kanuni.
Hivi kama wabunge wetu tuliowachagua wakatuwakilishe wanatolewa nje kwa kuwa tu wanapaza sauti zao kututetea wanyonge je ni wapi kilio chetu kitasikika?

Sheria nyingi na kanuni za Bunge zimewekwa kuipendelea CCM na kwa kuwa spika anatoka ktk chama chao ni dhahiri watatumia nafasi hiyo kuwakandamiza.
Sioni sababu ya kuendelea kuukubali mfumo huu kwa bunge la vyama vingi halafu spika atoke cha tawala hii ni hatari kwa demokrasia tunayoipigania kila kukicha na ni kustawisha upendeleo na kujaribu kufunika maovu ya serikali kama hivi tunavyoona sasa.

Nimepoteza imani na spika na naibu wake na kama ilivyo Tume ya Taifa ya uchaguz watumishi wake hawaruhusiwi kuwa na vyama vya siasa lakini kila uchaguz wanaonyesha upendeleo wa wazi kwa chama tawala sembuse huyu spika ambae ana kadi kabisa na ni mkereketwa wa ccm!

Rai yangu mkakati wa haraka unahitajika kufanya mabadiliko ipigwe kura ya wapinzani kutokua na imani na spika ikiwezekana achaguliwe spika mwingine ambaye hatatoka na chama cha siasa ili kuondoa ubaguzi na upendeleo wa wazi uliopo.
Hatakama katiba inakataa hilo na kulinda uovu huu ni wakati sasa katiba hiyo nayo ifutwe maana kifungu chochote cha katiba yoyote kinachokwenda kinyume na haki hakifai.

Anzeni sasa kuitafuta haki ya kweli hapo bungeni. Wananchi tupo nyuma yenu.
Najua siku zote mwanzo mgumu lakini tukiamu tunaweza.
Wananchi ndio cha mamlaka yote ktk serikali

Nawasilisha.

Mbona hujazungumzia uwezo wa Mbowe ku-scan atmosphere na kutumia uwezo wake kama kiongozi wa upinzani bungeni kuweka mambo sawa! kwani wapenzani nao kwa ujumla wao wanaweza kuepukana na malumbano yasiyo ya lazima na ku-deal na hoja.

Back
Top Bottom