Mbowe kuiuza CHADEMA kwa mafisadi

Umejibu hovyo kabisa,Usiniponde mimi mimi sijatunga hiyo habari,napenda kujua kama ni ya kichochezi au vp


Katika My Take nataka kujua kuhusu habari hii,mtuambie nyie wanachama na viongozi wa Chama chenye nguvu kama hii habari ni ya kweli sio unaniponda mimi.

ni habari ya kidaku... na hakuna kiongozi wa CDM atakayekuthibitishia hilo, halafu usiwe unakurupuka kupost habari bila kuwa na source za uhakika maana hilo gazeti hata layout yake siijui..
 
Naona umetaka maoni ya viogozi wakubwa wa CDM. Mimi nafikiri japo mimi siyo kiongozi unayemtaka wewe, Lakini ninaomba nikuulize maswali kwanza kabla hujawasumbua akina Slaa na Mbowe.

Mosi hili gazeti ni la fisadi lililokubuhu. Kwa hiyo si gazeti la kusoma. Kazi yao kubwa ni kupambana na CDM kwa proganda za uwonga. Let that stick to your mind first.

Pili, siyo rahisi kumhonga mbowe kwa sababu mbowe ni tofauti na hao wa vyama vibaraka wa ccm wanao hongeka kirahisi. Amezoea pesa toka akiwa mtoto. Do not forget that, Mbowe anatumia fedha zake binafsi bila kumsahau Ndesapesa na wengineo kusaidia Chadema. Acha uwongo.

Tatu, Chadema siyo TLP, NCCR nk, ni taasisi, siyo NGO ya mtu binafsi kama vyama vingine. That being the case, unaiuzaje? Kwani yeye mbowe alinunua TSH ngapi? kutoka kwa nani? Mimi na wenzangu tulimpitisha kwa kura za Kishindo. Get that as well.
Nne, nina wasiwasi na wewe mlete hoja, umewezaje kulipia internet ukaingia jamii forums lakini huna pesa ya kununua gazeti hilo ili upate habari kamili? Badala yake unaleta udaku wa kichwa cha hapbari? Halafu unataka great thinkers wajadili hoja isiyokamilika?
Pamoja na kuwa mimi ni kiongozi mdogo sana CDM na siyo msemaji rasmi wa Chadema, majibu hayo yanakutosha kwa sasa. Acha Akina Mbowe, Slaa na Ndesamburo wachape kazi ya kuwakomboa watanzania.
Thank you.
 
Jamani... JF naona vichaa wanaongezeka kila siku, hivi ni ugumu wa maisha au ni ugumu wao wa kuelewa chanzo cha shida zilizowafanya warukwe na akili?

Tatizo ni hofu kwa mafisadi, hawaamini kinachoendelea sasa, wanakosa mlango wa kutokea.
 
Ni sehemo mojawapo ya choko choko za CCM kutaka kuhamishia mashaibu ndani ya chama chao kuja CHADEMA ili nako kuwepo na mgogoro kama kwao. Ipuuzeni habari hii kwa staili inayostahili.

Asiyejua kwamba MAFISADI nchini wameweweseka kupita kiasi na kuendelea kupapasa kila sehemu wapate pa kutokea ni nani?? Mara usikie eti wana mpango huu na Zitto, kesho ni ule na yule basi taabu tu kwa mfa maji huyu.

Tulieni; sote tunajua tumetoka wapi, hadi sasa tumefanikiwa kiasi gani na kwamba vita mbele tumejiandaa vijana kiasi gani. Usiogo hizo nyoka zilizokufa na mpango wetu wa kufa mtu na kusonga mbele zaidi i karibu.
 
Hiithread yako haina haja ya kujibiwa na viongozi wakubwa unaowataka wewe. Kiogozi wa chini kabisa wa Chadema anaweza akakujibu.

Mosi, Mbowe hana tabia hiyo na ana akili, kwa hiyo usimzushie. kwani mbowe alinunua kwa Tsh ngapi hadi aiuze, Kwani yeye kauziwa na nani?

Pili, Sorce of your information is not credible. Ni gazeti la mafisadi. Kwa hiyo, usiwapotezee viongozi wa kitaifa kuthibitisha udaku wa magazeti ya mafisadi.

Tatu CHADEMA siyo TLP , NCCR nk ambavyo ni vyama vilivyoko katika mifuko ya watu. Viongozi wao wa juu ndo kila kitu. Hapana. Chadema ni taasisi na inaendeshwa na vikao halali vya kikatiba.

Mwisho, wewe kama ulikuwa na nia njema kwanini ulishindwa kununua gazeti hilo badala yake unaleta taarifa za uwongo za kuchafua chama chetu?

 
Umejibu hovyo kabisa,Usiniponde mimi mimi sijatunga hiyo habari,napenda kujua kama ni ya kichochezi au vp


Katika My Take nataka kujua kuhusu habari hii,mtuambie nyie wanachama na viongozi wa Chama chenye nguvu kama hii habari ni ya kweli sio unaniponda mimi.
....kwa hapo ulipogusa mmmh! sijui kama utapata majibu ya kujitosheleza humu ndani! Labda waje wenyewe wenye chama chao!!
ukisikia TETESI - KANUSHA!
ukiwa na HOJA - ISIMAMIE NA KUITETEA!
ukisingiziwa - KANA na TOA USHAHIDI
ukisifiwa - USILEWE SIFA, GANGAMALA!
ukitusiwa - USITUKANE watu wakashindwa KUKUTOFAUTiSHA!
na... na.... na.....
J
 
Soma vichwa vya habari vya AlNur
hapo ndipo nafurahia wafikiriaji wapevu wa hapa jamvini!!

tunajiita: "Les grands penseus!!!!!" then majibu yetu yanashindwa kutoa majawabu.... wala atujiulizi tunafikiriwaje na tunaowajibu! hatupaswi kujisifu kwa vile tusivyokuwa!
tunapaswa kuwa "weledi" na kuwajali "wateja" na ikiwa hatuwajali wateja wetu je tunaamini sisi ni wengi kuliko wao? Je ikiwa majibu yetu ni ya aina hii basi TWADHANI kwamba TUNAJITOSHELEZA? na je si kwamba kwa majibu haya TUNAFUKUZA wateja wapya.....

na kama hivi ndivyo basi "HERI SISI TUSIO WANACHAMA WA VYAMA VYENU" Kwa maana HATUKERWI WALA HATUNA TUNACHOPOTEZA... (tutavipiga kumbo vyama vyenu mfu kwa kuweka MGOMBEA BINAFSI- kwanini sisi ni wengi kuliko ninyi!

ninapomjibu mtu nahitaji apate muda wa kufikiria majibu yangu na si upuuzi nilioufanya. ninapojibu nahitaji hata kama jibu hilo litaonekana halina thamani kwa sasa lakini muda ujao liwe na maana (hii ndio historia)
 
Umejibu hovyo kabisa,Usiniponde mimi mimi sijatunga hiyo habari,napenda kujua kama ni ya kichochezi au vp


Katika My Take nataka kujua kuhusu habari hii,mtuambie nyie wanachama na viongozi wa Chama chenye nguvu kama hii habari ni ya kweli sio unaniponda mimi.

ukitaka taharifa kuwa makini na vyanzo vya habari hzo ...msiwe wepesi wa kuhoji ..nikuulize, labda ww ulijaribu kujiuliza kwanza na ulipata jbu gani? be self- analytical on issues
 
Katika kupitia vichwa vya habari vya magazeti mbalimbali leo hii,nimejionea kichwa kimoja cha habari katika gazeti moja.

Gazeti hilo linadadavua mpango wa Mwenyekiti wa CHADEMA Mh. Freeman Mbowe(Mb) wa kuiuza CHADEMA kwa mafisadi nchini Tanzania na vikao vinaendelea mjini Arusha,Tanzania.(Source : SautiHuru)

My Take: Wale viongozi wa Chadema na wakereketwa waliopo humu JF watuthibitishie hii habari kama ni kweli.

Chaggas Development Manifesto (CHADEMA) ni chama cha wapenda hela , sintoona ajabu Mbowe akiwauza hawa jamaa
 
Chaggas Development Manifesto (CHADEMA) ni chama cha wapenda hela , sintoona ajabu Mbowe akiwauza hawa jamaa

kuna watu wakisikia CHADEMA tuu... hata kama walikua chooni au gesti watakurupuka tuu......
 
Umejibu hovyo kabisa,Usiniponde mimi mimi sijatunga hiyo habari,napenda kujua kama ni ya kichochezi au vp


Katika My Take nataka kujua kuhusu habari hii,mtuambie nyie wanachama na viongozi wa Chama chenye nguvu kama hii habari ni ya kweli sio unaniponda mimi.

Wala hajajibu hovyo.. alitaka kukuhabarisha kuwa mara nyingi haya magazeti ya kifisadi yanaweka vichwa vya habari vya kuvutia lakini ukilinunua ukalisoma ndani unakuta habari yenyewe inatofautiana na kichwa cha habari. Kwastaili hiyo hata viongozi wa cdm hawawezi kukujibu maana wenzio wameisoma.
 
nadhani unajua fika vichwa vya habari siku hizi havikupi mwanga wa habari, ili upate jibu zuri la kueleweka, kutokana na swali lako, please scan, au retype hio habari hapa ndio wataalamu watakuambia kama kuna ukweli au ni yale mambo yetu ya kawaida.

(kama usipoitoa watajua kwamba na wewe ni mmoja wao)

nimeshaweka update ya habari nzima ,pitia na uisome kwa makini
 
Soma vichwa vya habari vya AlNur

Jamani Alnur halisomwi na watu wenye akili timamu! Ni uchochezi mtupu, bora kusoma udaku maana katuni zipo utacheka hata ukikosa habari ya maana, japo pia udaku nazo zimeingiza uchochezi wa kidini kama SANI!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom