Mbunge wa CCM
JF-Expert Member
- Nov 13, 2009
- 475
- 22
Rejea maoni yangu ya jana kuhusu hoja iliyoanzishwa na kishoka ya ama kuwa na uchaguzi mwakani au la. Binafsi, sikubaliani na wazo la Mbowe kugombea ubunge huko Hai. Huyu ndiye aliyekuwa mgombea halisi mshindani kwenye nafasi ya urais wa JMT mwaka 2005, na sera mbadala za chama chake hadi leo zimeshika hatamu kwenye majukwaa ya siasa za Tanzania.
Najua kuna wana Chadema wengi wanaoweza, lakini kujitosa kwa Mbowe ili achujwe ndani ya chama chake, kutaletea ushindani wa kweli ndani ya Chadema na nje yake dhidi ya mgombea wa Makamba, JK.
Uzoefu unaonyesha kuwa kwa Tanzania, usiposimamisha mgombea urais, basi hupati hata mbunge! (Japo si lazima kupata mbunge ukisimamisha mgombea urais). Hivyo, nina wasiwasi kuwa endapo Chadema haitasimamisha mgombea urais, itapungukiwa idadi ya wabunge, na ndio utakaokuwa mwisho wa "vita dhidi ya ufisadi."
Hata kama si Mbowe, tuombe Mungu Chadema waweke mtu makini zaidi, lakini wasifanye kosa la kuingia uchaguzi mkuu bila mgombea urais!
Tujadili...