Mbowe awa kiongozi wa upinzani bungeni, Zitto naibu , Lissu chief whip

Status
Not open for further replies.
wasisahau kile kichwa cha CUF - Hamad Rashid.

Kama upinzani ungekuwa makini zaidi huyu Mh. Hamad Rashid ndiye angefaa kugombea kiti cha uspika. Naamini upinzani ungekamilika lakini kumweka mh Mabere Marando? wamechemsha, hawezi kupewa kura.Nadhani wamempa nafasi agombee ili kumfurahisha huku wakijua hapati kitu. Bunge lingekuwa moto wa kuotea mbali; wabunge wengi CCM, wabunge wengi wa upinzani bara-Chadema,visiwani- draw. Raisi-CCM,Spika- CUF hapo ingekuwa ni kazi tu hakuna kulala.
 
CUF wametoa vice president, wanategemea kutoa baadhi ya mawaziri (uko ZNZ) unafikiri wanaweza kuwa wapinzani kweli, uku wako kwenye payroll ya serikali?

I second your arguments. Huwezi kusema mdio na hapana kwa wakati mmoja. Ukiweza lazima uwe mnafiki kwa upande mmoja.
 
Zitto Kabwe ana uzoefu mkubwa wa bunge, ameshiriki kwenye kamati nyeti ya kurekebisha sheria ya madini. Ametoa changamoto kubwa ndani ya bunge lililopita mpaka akasimamishwa. Ni mpiganaji zaidi ya Mbowe.
Pili Mbowe ni mwenyekiti ana majukumu mazito ya chama. Zitto anakaribia kuwa mwanasiasa mkongwe.
 
Fuatilia michango mingine utaona maamuzi yaliyofikiwa ndani ya vikao vya chama
 
Zitto Kabwe ana uzoefu mkubwa wa bunge, ameshiriki kwenye kamati nyeti ya kurekebisha sheria ya madini. Ametoa changamoto kubwa ndani ya bunge lililopita mpaka akasimamishwa. Ni mpiganaji zaidi ya Mbowe.
Pili Mbowe ni mwenyekiti ana majukumu mazito ya chama. Zitto anakaribia kuwa mwanasiasa mkongwe.

Acha majungu yasiyokuwa na tija kwa taifa hili. It is quite natural ukiwa na wakubwa wako katika kila mazingira wanapewa nafasi kama viongozi. Na hayo unayoyasema Zitto kafanya ni kwa mtazamo wako na si wa kila mtu. Kama wewe si CCM, acha kabisa otherwise kama ni CCM unaweza kuendelea kwaajili ya kupata malipo yako.
 
Unampaje madaraka ya uongozi wa bunge melevi mbwa kama mbowe!!!!! Tuache ushabiki tundu lissu au zito lilikua chaguo sahihi.... Mbowe hana ubavu na hana data za kujadiliana face to face na pinda mule ndani na kuna situations ambazo hakutokua na muda wa kumuuliza mtu pembeni..... Ukabila ulaaniwe zitto usiwe na shaka muda bado upo na utafanya makubwa waache hao wachaga wakubanie na wataaabika mjengoni

Punguza hasira mkuu,
hapa ni watu makini wanafanya mambo yao tuu..
This time, hakuna pa kupumulia! Mtaondoka
 
Nilifikiri hiyo post itaongozwa na NONE CHAGGA kumbe baado

Hivi mtu unayezungumza ukabila wakati huu je wewe kweli unaipenda nchi yetu? Je una ugomvi gani na Wachagga. Mimi ningeunga mkono hoja ya kuonyesha udhaifu au makosa ya mtu yanayomfanya asifae kutuongoza. Hakuna mwanadamu aliyepiga kura kuzaliwa kabila au rangi fulani hivyo kama una chuki binafsi na Wachagga sema lakini usituletee siasa za ubaguzi wa kikabila. Kuzungumzia siasa za chuki na ukabila imekuwa ni kampeni ya kudumu ya CCM dhidi ya wagombea wote wa ushindani. Kampeni chafu kama hizo alifanyiwa Mrema, Lipumba, Mbowe na Dr. Slaa. Kama kweli una dhamira hai na unamjua Mungu naomba ukatubu dhambi hii chafu kwani inaonyesha kuwa huelewi historia na madhara ya siasa hizi chafu.
 
Safi sana,timu nzuri, tunaomba mungu Marando apate Uspika na hapo kutakuwa hakuna kuficha jambo hata hivyo bado hata awe spika wa kupandikizwa bado wananchi ndiyo wenye sauti ya mwisho, watanzania wengi wamebadilika na kwakweli hii ni generation nyingine ya viajana wengi wenye mitazamo ya kisasa na si rahisi kuwadanganya.

Mapinduzi ya technologia ya habari na mawasiliano imeongeza uwelewa wa watu kwa kasi ya ajabu,na hivyo imekuwa rahisi kujua mbichi na mbivu sio kama zama za kale.
 
Wewe mzee ndo huna busara kabisa, Zitto bado ana issue nyingi tu za kutu assure hata sisi moderate citzens who are leaning chadema amekuwa too contravesial recently huyu kijana , hivyo ni bora kuwa na safe choice kwa sasa kuliko kubahatisha, hata hivyo ni msaidizi wa wa kiongozi wa upinzani hiyo post inamtosha wakati tuna evaluate nyendo zake, is too risky hivi sasa majukumu mazito ya chama kukabidhi kwa kijana kama zitto ambae anakuwa kama kinyonga wakati flani, kwani vitta na CCM ilijaa tamaa na hujuma nyingi inahitaji jemedali mwenye msimamo thabiti kama mbowe!

Na watu walio amua uongozi huo uwe hivyo ni caucus ya wabunge wote wa chadema, hivyo wanajuwa nini wanachotaka na ni uamuzi sahihi kabisa, Napata mashaka na wewe Bwana Technology inawezekana hukitakii mema chadema au una agenda ya siri lakini kwa mtu yoyote mwenye kutakia mema chadema atafurahia na uchaguzi huu, CCM wenyewe hawampendi Mbowe kutokana na misimamo yake ambayo inaimarisha chama, sasa unataka kuniambia wabunge wote hao wa chadema waliochagua hao viongozi ni wachaga? au wote wanatoka Kilimanjaro, mbona unakuwa unreasonable na shutuma zako hazima facts?

Kumezuka hili kundi ambalo linaleta siasa ya Maji Taka Tanzania, jee wewe una uhakika kagani kwamba Zitto ni CCM? Unajua Zitto ameweka maisha yake kwenye line kiasi gani? Tusiwe washabiki, huyu mtu anabishana na watu hatari ambao wanaweza hata kutoa roho yake, wewe na mimi ni wale ambao tumekaa pembeni kuangalia wale watakao kufa kwa maendeleo yangu, yako na vizazi vyetu.

Tuwe na fadhira, na sio kuvisha watu kofia sababu tumetofautiana nao agenda moja au mbili. Ni sababu zipi zinazokufanya uamini kwamba Zitto ni CCM? Sababu ni rafiki na JK? Mboe and JK ni marafiki pia, but political they have a huge difference. Hivi sio vita, bali ni kutofautiana kwa policies ndio kunako sababisha wengine wanakuwa upinzani na wengine chama tawala.

Leo hii ni wangapi wanaweza simama wakasema Rostam mwizi? au Lowassa vile? Mimi na wewe tunapiga kelele nyuma ya PC zetu
 
Zitto Kabwe ana uzoefu mkubwa wa bunge, ameshiriki kwenye kamati nyeti ya kurekebisha sheria ya madini. Ametoa changamoto kubwa ndani ya bunge lililopita mpaka akasimamishwa. Ni mpiganaji zaidi ya Mbowe.
Pili Mbowe ni mwenyekiti ana majukumu mazito ya chama. Zitto anakaribia kuwa mwanasiasa mkongwe.

Sio Kosa lako, Ni kama Jogoo liloingia mjini usiku linawika likidhani mchana kumbe mwanga wa umeme, fuatilia post humu ndani kwanza ndio upost zako.
 
Zitto Kabwe ana uzoefu mkubwa wa bunge, ameshiriki kwenye kamati nyeti ya kurekebisha sheria ya madini. Ametoa changamoto kubwa ndani ya bunge lililopita mpaka akasimamishwa. Ni mpiganaji zaidi ya Mbowe.
Pili Mbowe ni mwenyekiti ana majukumu mazito ya chama. Zitto anakaribia kuwa mwanasiasa mkongwe.

Tatizo la kulala Mchana. Hata ukiamka saa 12 jioni unadhani ni asubuhi.

Karibu jamvini mjomba.

Sasa hivi wenzio tunajadili 6 kuhamia Chadema.
 
Nachelea kusifia tungije utekelezaji wa masuala muhimu yanayogusa mwananchi wa kawaida maana wahishimiwa sometimes hujisahau sana wakiingia mjengoni
 
cuf kushirikishwa na chadema siioni mantiki hapa na swala la kulipa fadhila kwa kuwa bunge lililopita chadema walishirikishwa na cuf ni fikra potofu na mgando kwani cuf ya kipindi kile na sasa ni tofauti cuf ya sasa ni ccm katika vazi la upinzani.
 
Congrats CHADEMA and I'm very happy because you always surprise your enemies. Ngoja sasa tuone watakuja na Santuri ipi

Hawakosi sababu hao! Sisi ni furaha kujenga ngome imara kwa 2015

attachment.php
 
Ni kweli Zitto ana record nzuri, isipokuwa binafsi moja ya jambo lililonifanya nianze kumtilia mashaka kidogo ni pale alipotaka tununue mitambo ya wale matapeli wa DOWANS.
Hiyo ilinishock na kunipunguzia imani kwake kwa asilimia nyingi sana, kwa sababu kwa upeo wa Zitto, mpaka leo sijaelewa alipata wapi ujasiri ule (hiyo yaweza kuwa siri yake). ingawa baadaye nadhani baada ya watu wengi kumshitukia, akasema kile tulichomtegemea akiseme (i.e kuitaifisha).
Nadhani nafasi aliyoipata inafaa, na naomba aitumie vizuri kwa sababu kauli yake ilituumiza mioyo wengi tuliokuwa tumemwamini sana.
 
Tatizo la kulala Mchana. Hata ukiamka saa 12 jioni unadhani ni asubuhi.

Karibu jamvini mjomba.

Sasa hivi wenzio tunajadili 6 kuhamia Chadema.

Mkuu nimekuappriciate, uko makini. teh teh teh teh!!!!!!!!!!!! nimecheka kama JK.
 
Kama upinzani ungekuwa makini zaidi huyu Mh. Hamad Rashid ndiye angefaa kugombea kiti cha uspika. Naamini upinzani ungekamilika lakini kumweka mh Mabere Marando? wamechemsha, hawezi kupewa kura.Nadhani wamempa nafasi agombee ili kumfurahisha huku wakijua hapati kitu. Bunge lingekuwa moto wa kuotea mbali; wabunge wengi CCM, wabunge wengi wa upinzani bara-Chadema,visiwani- draw. Raisi-CCM,Spika- CUF hapo ingekuwa ni kazi tu hakuna kulala.

Huyo mpemba wako kamzuia nani kugombea uspika? una maana hakupata mtu wa kumweleza form za kugombea zinapatikana wapi hapo dodoma baada ya kuwasili kutoka nchi jirani ya zanzibar? wewe furahia ukombozi wa chadema, hakuna tena viongozi wa upinzani wapemba ambao hawajui chochote kuhusu tanganyika. wanatakiwa watu wanaozijua na kuzilinda raslimali zetu. Hiyo CUF siyo chama cha upinzani tena kwa sababu kimeunda serkali ya muafaka na ccm. Katibu mkuu na mwasisi wake ndiye raisi msaidizi wa serkali huko zanzibar, huwezi kuwa na rais serkalini halafu bado ukabakia mpinzani wa hiyo serkali. Kama ungelijua hilo ungefuta hayo matongotongo machoni pako..... LOL
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom