Mbowe avuka lengo kuchangia msikiti, asisitiza amani, upendo na mshikamano

Hakuna hata siku moja harambee ya kuchangia radio Iiman bali kuna kila mwenye swadaka yake katika kuboresha na kukuza coverage ya Radio hiyo basi na atoe pasi na kujinadi ametoa kiasi gani.

Lakin cha msingi ni kuwa Radio Iman kuanzia taarih 15 Dec 2011, inaingizwa katika satellite na kuweza kusikika dunia nzima kwa njia ya mtandao. Inaunganisha na Satellite ya http://www.lyngsat.com/intel906.

Hongera sana Nahdi kwa maendeleo makubwa ya radio hiyo

umeona watu wasio na gubu kama wewe??!!
wao wanataka maendeleo tu..........harambee imefanyika na msikiti unajengwa, watu wataswali humo na maisha yataendelea.

vijana watajipanga kupandisha watalii mlima kilimanjaro, watapata mihela, na maisha yataendelea

miti itapandwa, mazingira yataboreka, na maisha yataendelea.

Wewe kalia hadith tu na extremism.
 
how old are u Sheikh?
 
umesema yote, sina la kuongeza
 
kama mbowe anawajali waislam.tutamuona uwanja wa taifa 18/12/2011 katika uchangaiji wa TV mpya ya kiislam. yaani TV imani.vyenginevyo tutaamini wamekatazwa na cdu

Una maana kila tukio la uchangiaji huduma za Kiislamu Mbowe lazima ajipeleke bila kuombwa na wahusika? Huko alikofanya harambee ni jimboni kwake, ni himaya yake kwa wapiga kura wake. Hayo ya kuchangia radio Imani wameyapangilia wahusika kwa utaratibu wao, na kama watamwalika aende kuendesha hiyo harambee hilo ni jambo jingine lakini si kujipeleka bila kuombwa au kuelekezwa na wahusika.
 
kama mbowe anawajali waislam.tutamuona uwanja wa taifa 18/12/2011 katika uchangaiji wa TV mpya ya kiislam. yaani TV imani.vyenginevyo tutaamini wamekatazwa na cdu

Zitto Kabwe naye alikuwa kwenye harambee ya kuchangia kanisa sikumbuki vizuri nadhani maeneo ya mkoa wa Dar au Pwani, na huko hakujipeleka, aliombwa au kuelekezwa na wahusika na mradi huo. Hatutaki watu wenye mwono finyu kama huu kwa sababu utaifa haujengi matabaka ya kidini, kikabila nk. Kumbuka tofauti za kiitikadi katika siasa ni kichocheo cha maendeleo na usitawi wa taifa.
 
Inatia shaka! Huyu mshikaji na msikiti wapi na wapi?!!!

Jeuri ya CCM mfukoni, maana makamanda sasa kila kona wanashambulia kama nyuki kwa kubadili mbinu kila kukicha. Pia makamanda kuombwa katika hafla mbalimbali sasa hivi ni mwendelezo usiokoma, maana huko ndiko chimbuko la wapiga kura na ninafasi ya kujitangaza kisiasa. Hii nimeipenda hadi Tanzania tukomae kwa siasa za kupinduana kwenye masanduku ya kura vinginevyo usahii huu chama kimoja kushika dola miaka nenda rudi unazidi kudidimiza nchi.
 
Usipende KUKURUPUKA mjomba,soma line kwa line,neno kwa neno.Mtoa mada mwishoni kabisa amesema source ni IPP MEDIA,sasa Majira imetoka wapi?Au Majira inatoka Ipp siku hizi?
Usipende KUKURUPUKA mjomba. Mwanzisha uzi alitaja source: majira. Baada ya kuamshwa kutoka usingizini ndipo akaedit. Akabadili kuwa Nipashe. Fatilia vizuri kabla ya kulaumu.
 
Mbowe ataka siasa za amani, upendo zitawale

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amesema siasa za amani, upendo, mshikamano na zenye hofu ya kumuogopa Mungu, ndizo zinazohitajika Tanzania. Mbowe aliyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Jimbo lake la Hai kwenye harambee ya kuchangia ujenzi wa Msikiti wa Lambo uliopo jimboni humo.

Aidha, alisisistiza suala la wananchi kujitoa katika shughuli za maendeleo ya kijamii pasipo kujali itikadi za kisiasa na kiimani.
Mbowe, ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani bungeni, alisema yeye kama kiongozi wa wananchi anapendezwa sana na siasa za amani na daima atahubiri amani na mshikamano. Alifafanua kuwa maendeleo ni suala muhimu linalomgusa kila mwananchi, hivyo inapofikia wakati wa kuangalia itikadi za kidini na vyama, itakuwa ni ngumu kuleta maendeleo ya wananchi pale inapohitajika suala la kuchangia au kushiriki katika shughuli za ujenzi wa taifa.

Katika harambee hiyo, Mbowe alichangia Shilingi milioni tano na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, aliahidi kukamilisha paa la msikiti huo pamoja na mazulia yenye thamani ya Sh. milioni 4.5 na kufanikisha kupatikana kiasi cha Sh. milioni 30 kiwango ambacho kilivuka lengo la kukusanya Sh. milioni 15. Awali, kabla ya harambee hiyo, Mbowe alifungua ofisi ya shirika lisilo la kiserikali la Hai Kilimanjaro Development Initiative (Hakidi) ambayo ilianzishwa kwa lengo la kutoa ajira kwa vijana kupitia sekta ya utalii.
Akizungumza na wakazi wa mji huo wakati wa kupanda miti 10,000 na kufanya usafi katika maeneo hayo, Mbowe aliwataka wananchi hao kufanya usafi katika makazi yao na kupanda miti ili kusaidia upatikanaji wa maji.

Katika risala yake, Meneja wa shirika hilo, Mohamed Mbowe, alisema shirika lake linakusudia kuajiri vijana takribani 5,000 ambapo kwa kuanza watoa ajira kwa vijana 145 katika sekta ya utalii na wanakusudia kupanda miti milioni tatu kwa kipindi cha miaka minne ijayo.
Katika uzinduzi huo, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama, alitakiwa kuwa mgeni rasmi, lakini hakutokea kutokana na kwenda kulipokea kundi lililoshuka kutoka Mlima Kilimanjaro.

Source: IPPMedia

Nafikiri hapa siasa inachukua mkondo wake.

Iweje aje Zitto kumsindikiza Mbowe kwenye harambee wakti kuna Ndesamburo na Yule wa Rombo? au ndio shoka haliwezi kukata miti mpaka litiwe kipande cha mti(mpini).

Na nazidi kuunga mkono maneno ya FF. Msikiti huo uitwa masjid al Bilicanas. Na kibla yake iangalie kule Bilicanas ilipo Dar.

Habari hii ni wizi wa mchana na uzushi mkubwa,mleta mada amesema source ni majira wakati mi ninalo gazeti hilo apa mkononi habari hiyo haipo,na ninayo magazeti ya majira ya tangu jumamosi. jamani mbona jamii forum inazidi kupoteza dira na mwelekeo?

vilaza utawajua tu, hebu soma hyo habari mpaka mwisho wapi wamekuambia majira, as a source, mie nimeona ippmedia. na ukiclick on the link inakuonesha source nipashe. acha uvivu.
 
Hakuna hata siku moja harambee ya kuchangia radio Iiman bali kuna kila mwenye swadaka yake katika kuboresha na kukuza coverage ya Radio hiyo basi na atoe pasi na kujinadi ametoa kiasi gani.

Lakin cha msingi ni kuwa Radio Iman kuanzia taarih 15 Dec 2011, inaingizwa katika satellite na kuweza kusikika dunia nzima kwa njia ya mtandao. Inaunganisha na Satellite ya http://www.lyngsat.com/intel906.

Hongera sana Nahdi kwa maendeleo makubwa ya radio hiyo

Kweli elimu ni muhimu sana, kwani hiyo sadaka unatoa matope au pesa? mwombe ALLAH basi ashushe mabati na cement kutoka mbinguni.
 
Kamanda umetoa ujumbe mzuri juu ya utofauti wa udini na siasa,swala kumpata kiongozi bora ili atuletee maendeleo na si udini.Hongera sana waislamu wa Hai kwa kuofungwa kifikra na mambo ya udini!
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom