Mbowe aunda Baraza la Mawaziri Vivuli - ni la CHADEMA

Teheheeeee, yaani nimefurahi, kwa hiyo rais kivuli ni Dr. wa ukweli Wilbroad Slaa.

Natamani kila mwisho wa Mwezi Dk Kikwete akitoa hotuba yake Dr Slaa naye atoe ya kwake ambayo ni kivuli.
 
Shibuda ni kada wa CCM na hana uchungu na CDM na pia ana mawasiliano ya karibu na mafisadi akiwemo Makamba na Jk

Kama mlijua ni kada wa CCM ilikuaje mkampokea? CHADEMA wamekuwa kama kapu la mama anaenunua chakula sokoni! hutumbukiza kila kitu humo! ndizi, nyanya, mchicha, tangawizi na mwisho shubiri ambae ndio huyo SHIBUDA!!!!
Kuendelea kumkubali SHIBUDA kuwa Mbunge wao huku wakijua kuwa ni Kada wa CCM, basi CDM inaonyesha kuwa ni chama dhaifu kisicho kuwa na msimamo!
 
MSemaji ofisi ya Raisi: Freeman Mbowe, Msaidizi: Silinde David
Uwekezaji na Uwezeshaji: Matiko
Ofisi ya Waziri Mkuu: Vicent Kiboko
Ofisi ya Raisi: Said
Ofisi ya Raisi & Utawala Bora: Mch Nakse wa Karatu
Ofisi ya Makamu wa Raisi: Gekulu
Ofisi ya Raisi & Mazingira: Leticia Nyerere
OFisi ya Fedha: Zitto Kabwe Msaidizi: Christina Lissu
Mambo ya Ndani: Lema
Katiba ya Sheria: Tindu Lissu
Kimataifa: Wenje
Jeshi la Ulinzi: Seladhini
Mawasiliano: prof Kayili
Makazi: Mdee
Maliasili: Mch Peter Msigwa
Nishat na Madini: Mnyika
Ujenzi: Machemli
Uchukuzi: Mhonga Said
Viwanda: Olenywa
Elimu na Mfunzo: Mtinda
Afya: Dr Gilbert Mbasa
Maendeleo ya Jamii: Naomi Kaiula
Vijana na michezo: Mbilinyi Mr Two
Kilimo: Meshack Obulugwa
Maji: Haines Kiwia

Hawa ndio MAWAZIRI KIVULI WA UPINZANI

UDINI MTUPU!!!!!!!!!!!:angry:
 
wana jamii forum naombeni mwongozo juu ya kuandika new topic, nimejitahidi nimeshindwa hata kuchakachua pia imegoma, nipeni utaratibu ukoje.
 
Kwa ujumla, ni baraza makini. Ila nadhani Mbowe amenoa kwenye uteuzi huu:

John Mnyika - Nishati na Madini?!

Tundu Lissu - Sheria na Katiba


Sawa, Tundu Lissu ni mwanasheria aliyebobea. Lakini wizara ingemfaa zaidi ni Nishati na Madini kuliko wizara ya sheria. Huku ana uzoefu mkubwa wa tafiti nyingi alizofanya akiwa LEAT na pia angetumia vyema utaalamu wake wa sheria kufumua mikataba ya wizi ya kwenye madini na umeme.

Mnyika hana uzoefu wa mambo ya nishati na madini ingawa ni mwanasiasa makini. Lissu angetoa mchango mkubwa zaidi kwenye hii wizara nyeti.

Kikwete amekuwa hajui umuhimu na unyeti wa wizara hii ndiyo maana siku zote anateuwa mawaziri wasio na uwezo unaotakiwa kwenye wizara ya madini, kama William Ngeleja, wa sasa.

Inasikitisha kuona Mbowe naye amenoa kwenye wizara hii kama Kikwete.

The Following User Says Thank You to Fareed For This Useful Post:

Mwita Maranya (Today)​
 
.


fareed nakubaliana na wewe,lakini hiyo haimzuii kushirikiana na mnyika kufanikisha malengo yao,kumbuka prof. Salungi alikuwa ni daktari bingwa wa mifupa lkn alipewa wizara ya ulinzi,najua kazi itakwenda vizuri tu!otherwise nimekupa senkyu
 
Timu imekaa vizuri , cha msingi wajipange kutoa Shadow budgets ambao zitaonekana zinaualisia na watu waone dira ya wapambanaji wa CDM the time tunaamua kuwapa nchi 2015.


Nimependa nafasi anayohold mnyika na zito wamefiti katika nafasi hizo.


We wish you all the best.
 
Polisi walikunywa uji wa mgonjwa wakijua atakufa, sasa mgonjwa amepona wasuburie. Amekuwa boss wao, yeye na Vuai Naodha ndo watakaa kupitisha bajeti ya mishahara yao.
 
MSemaji ofisi ya Raisi: Freeman Mbowe, Msaidizi: Silinde David
Uwekezaji na Uwezeshaji: Matiko
Ofisi ya Waziri Mkuu: Vicent Kiboko
Ofisi ya Raisi: Said
Ofisi ya Raisi & Utawala Bora: Mch Nakse wa Karatu
Ofisi ya Makamu wa Raisi: Gekulu
Ofisi ya Raisi & Mazingira: Leticia Nyerere
OFisi ya Fedha: Zitto Kabwe Msaidizi: Christina Lissu
Mambo ya Ndani: Lema
Katiba ya Sheria: Tindu Lissu
Kimataifa: Wenje
Jeshi la Ulinzi: Seladhini
Mawasiliano: prof Kayili
Makazi: Mdee
Maliasili: Mch Peter Msigwa
Nishat na Madini: Mnyika
Ujenzi: Machemli
Uchukuzi: Mhonga Said
Viwanda: Olenywa
Elimu na Mfunzo: Mtinda
Afya: Dr Gilbert Mbasa
Maendeleo ya Jamii: Naomi Kaiula
Vijana na michezo: Mbilinyi Mr Two
Kilimo: Meshack Obulugwa
Maji: Haines Kiwia

Hawa ndio MAWAZIRI KIVULI WA UPINZANI


Saaaafi sana hiii............BARAZA MAKINI NA 'CLEAN'
Natamani angeanza na 'Rais wetu' kabisa juu paleee, then wanafuata makamanda....! maana 'rais wa hao wengine' yupo hoi, hawajui hata wale 'anaotafuna rasilimali zetu' nao meza moja, ilimaanisha, keshafeli zamani hata kabla ya kuanza utawala wake uliotokana na ufisadi na uchakachuaji wa haki na chaguo la umma!
 
wana jamii forum naombeni mwongozo juu ya kuandika new topic, nimejitahidi nimeshindwa hata kuchakachua pia imegoma, nipeni utaratibu ukoje.

Rudi nyuma kwenye icon ya Forum: 'Jukwaa la Siasa' (au jukwaa lolote ulipo).
Chini yake kuna icon ya 'Post new topic'.
Ingia hapo, andika title yako, endelea na text kwenye jedwali.
 
Kauli yako imekaa kichochezi zaidi. Nani alikuambia kuwa ilikuwa ni lazima kwa Shibuda kuwa waziri kivuli? Halafu kwani wabunge wote wa CHADEMA wamepatiwa nafasi ya waziri kivuli? Kama sivyo sasa inakuwaje wewe unaibuka na hoja nyepesi kama hii?
 
Back
Top Bottom