Mbowe anavyojiosha Bungeni...

tumemsikia mkuu akijiosha kwa muheshimiwa, eti wao ndio huwa wanawaziwia wanainchi wasiandamane, anachekesha kweli!!!!
kumbe wao ndo wanatuchelewesha makusudi wakati wakija kwetu wanatuambia tupo pamoja tusubiri kidogo kuna mambo wanafatilia kabla hatujaingia mtaani. Duh,wanakatisha tamaa la umeme nilipania sana!
 
Katika kipindi cha maswali na majibu kwa waziri Mkuu leo bungeni, Mbowe alisema viongozi wa upinzani wanajitahidi sana kuzuia watu kufanya maandamano kwa ajili ya umeme.

Kuna ukweli jamani, wakati chadema inajulikana kwa maandamano?
tatizo lako umesoma chini ya mbuyu, we suala la umeme unalionaje ni furaha kwako? Chama cha siasa ni nani? We unadhani kama CDM wanaandama kwa mambo ya kipuuzi Halaiki ya watu ingewakubali kihivyo?

watu wamechoka na usanii huu kila mara wanaambiwa mipango ya muda mrefu mfupi mwembamba mnene mweusi ila ile muda kitalaam hawana
 
CHADEMA wamemfata nan nyumban kwake il wakaandamane???? Jarbu kufkria kwa kutumia Ubongo sio utumie UTI WA MGONGO
 
CHADEMA wamemfata nan nyumban kwake il wakaandamane???? Jarbu kufkria kwa kutumia Ubongo sio utumie UTI WA MGONGO

Na wale waliouliwa Arusha? Viongozi wa Chadema walifata nini kule au wote kule ndio kwao?
 
tatizo lako umesoma chini ya mbuyu, we suala la umeme unalionaje ni furaha kwako? Chama cha siasa ni nani? We unadhani kama CDM wanaandama kwa mambo ya kipuuzi Halaiki ya watu ingewakubali kihivyo?

watu wamechoka na usanii huu kila mara wanaambiwa mipango ya muda mrefu mfupi mwembamba mnene mweusi ila ile muda kitalaam hawana

Suala la umeme linajulikana kuwa tatizo lake ni kuwa waliopita hawakutegemea kama kutakuwa na mfumuko wa maendeleo ambao utahitaji umeme mwingi kama tunaoutumia sasa na mahitaji yetu ya sasa ni zaidi ya mara 5 kuliko alivyoyaacha Mkapa na ya kila mwaka yanaongezeka maradufu.

Hakuna awamu iliyoongeza na iliyosaini mikataba mikubwa ya umee zaidi ya hii. Au7 unabisha kwa hilo? Leo hii tumeona mtambo ukiingia na mingine miwili iko njiani, na tumeona mikataba ya kufua umeme wa mkaa wa mawe ikisainiwa unanini wewe, kama ni rahisi si cdm ingeleta tu mitambo ioneshe uhodari wao badala ya kulalama kila saa.
 
Wengi humu ndani wanaongea crap tu hata hawatumii akili kufikiri hata kidogo,na mnaotetea kuhusu swala la umeme basi nyinyi hamna mgao ndio maana,watu biashara zinalala na hawaingizi kipato inabidi tuwaangalie na wenyewe pia......
 
Katika kipindi cha maswali na majibu kwa waziri Mkuu leo bungeni, Mbowe alisema viongozi wa upinzani wanajitahidi sana kuzuia watu kufanya maandamano kwa ajili ya umeme.

Kuna ukweli jamani, wakati chadema inajulikana kwa maandamano?

Mkuu mimi niliwahi kuandamana kwenda Bungeni viwanja vya Karimjee kudai Demokrasia zaidi wakati ule wa mwanzo kabisa wa vuguvugu la vyama vingi. Baada ya vyama vingi kuruhusiwa na kuandikishwa sijaandamana tena ILA KWA HILI LA UMEME HATA NIKIITWA SASA HIVI NIKAANDAMANE NITAENDA KUANDAMANA
 
Hivi maandamano ndio yataleta umeme?

Nawashangaa vyama vya upinzani, kuhusu hili la umeme, hii ilikuwa turufu kwao, kuongea na wafadhili wao wa nje wawaletee mitambo ya umeme haraka haraka, wawaoneshe wananchi kuwa wao wanaweza walichoshindwa Serikali, badili yake wanahaha kwa makelele yasio na tija.

Sheria zimebadilishwa na yeyote awezae kuzalisha umeme na alete, au hilo hawalijui? Kama wanalijua wanangoja nini? Au wamejaribu wakaona pagumu?

Mkuu serikali ina wajibu wa kutupatia umeme. Kama imeshindwa ikae kando waingie wenye uwezo wa kuleta umeme. Hili suala linanikera hasa nikiona wale wenye dhamana ya kuleta umeme wakiwa kwenye vilabu vya pombe wamelewa chakari!!
 
Back
Top Bottom