Elections 2010 Mbowe Afanyiwa Fujo Kubwa Hai

Mkuu Kamende ameleta habari, imejadiliwa. Inaonekana mambo si shwari. Sasa tusubiri taarifa ya Gen. Emeritus Shimbo. Prof. Kinana na Dr. Makamba kwa upande mmoja na ya Ndugu Baregu na Mabere Marando kwa upande mwingine. Bado natafakari
 
ACID tumia akili yako kufikiri. Supposedly kwenye mikutano ya kampeni kuna walinzi je katika maelezo hapo juu umeaona role yao? Usianze tu kuamua kuwa Mbowe angeenda kufuata utaratibu wa sheria wakati mazingira yaliokuwepo pale ujayajua. Si ni Green Guard ndio walikwenda kwenye mkutano wa CHADEMA kwa hiyo uchunguzi unaosema ni kuonyesha labda CHADEMA ndio walianza uchokozi siyo? Use your common sense!
 
vijana wa green guard hawana akili na Fuya ameshashindwa, walicofanya hakina maana... lakini mbowe ameonyesha upuuzi mkubwa kama mwenyekiti wa chama kushindwa kumalizia mkutano na kufuata utaratibu wa sheria (ambao yeye kwa wilaya ya hai ana priviledge hiyo kubwa tu na anaijua) kumtoa kijana wake

Kama tunalaani violence, basi tuifanye kwa vitendo... kwa kwenda kufanya mambo ya tambaza nimesikitika sana

siamini mtu mwenye staha anaweza kuvunja mkutano kwenda kuokoa kwa staili ya kibohehe, mringa au tambaza

angetuma vijana

Nimesikitishwa na green guards lakini nimesikitishwa zaidi na mbowe

ukifanya ya kipumbavu na mpumbavu, watu hawatajua tofauti yenu

Mmmmmh,we naweeeee
 
Inasikitisha sana.

Vitendo hivi vya kutumia nguvu ni vya hatari sana. Kama kawaida hakuna hata kemeo moja kutoka serikalini hii inamaanisha kuwa serikali inavipalilia vitendo hivi vya kihuni na jinai. Kikwete na CCM jukwaani wanahubiri amani lakini matendo yanayofanywa na watu wao yanatuambia vingine.

Ni lazima kila mtu kulaani vitendo hivi kwani kama vikiachiwa hatutakuwa na nchi bali jehanamu. Ni lazima watu wote wenye mapenzi mema na nchi yetu tukemee kwa nguvu vitendo vya vijana hawa wa kihuni na kudai mara moja kuvunjwa kwa vikundi vyote vya ubabe na uhuni kama green guard. Jeshi la Polisi ni lazima lisimamie hili mara moja bila kujivuta au kutuambia kuwa linaunda timu ya uchunguzi. Vyama na watu wote wanastahili ulinzi na usalama katika kipindi hiki.

Mimi kama Mtanzania na mzalendo wa nchi yangu ninalaani kwa nguvu zote vitendo hivi vya vijana hawa wa Green Guard na ninalitaka Jeshi la Polisi kuwashika na kuwafungulia mashtaka wote waliohusika na vitendo hivi ikiwa ni pamoja na viongozi na makamanda wao wa uovu.
 
Viongozi wote (I don't care mnatoka chama gani) mliopewa dhamana na wananchi, mnayaona haya mnanyamaza tu. Mahakama inayoshughulika na kesi kama hizi iko nchi mwetu (Arusha), hatuhitaji kufungua nyingine. Uchaguzi ukimalizika na mashitaka nayo yanafunguliwa. Kuweni makini katika utendaji kazi wenu.
 
Mamaaaaaaa,tunaenda wapi huku?????
Kwani hawa walinzi wa kijani wana umuhimu gani?????
Inamaana polisi wooooote wanao watumia waha toshi hadi watumie green guard????

Naona hao GREEN GUARD ni kama wale MUNGIKI wa Kenya, inakuwa vipi nchi yenye utawala wa sheria inaruhusu haya mambo?!!
 
Hivi mtu akimkamata Mkeo na kuanza "Kumuwowa" mbele yako. Anakuja mwanao anachukua kibano kutoka kwa rafiki zake. Wee Mwanamume mzima na msuli kama wa Sokwe Mtu na Bastola yako kiunoni, utaanza kutumia busara za kwenda kituo cha Polisi kwenda kuriport?

Sijui hadi ukija kurudi na POLISI hao, Mkeo na Binti yako watakuwa "wamewolewa" mara ngapi.

Eti hii ndiyo busara aliyotakiwa MBOWE aifuate.

Ningelijuwa wake zenu, ningelikuja niwawowe mbele yenu na nione mnavyoenda POLISI kuriport.

Waongo wakubwa nyie, mngeniweka kabali ya mbao hadi nikachafua kufuli.

Minafiki mikubwa nyie. Anakushinda hata huyu hapa chini, loooohhh...

chimpanzee-glock.jpg
 
Ulichotoa hapo, na walichotoa wana ccm (kadogoo na Anfaal) vina tofauti gani? nimetumia neno spin za wanaccm, kama hii inakufanya wewe mwanaccm so be it.

Ngoja nikukumbushe jambo moja, miaka fulani iliyopita wakati mkapa akiwa preziii. CUF walifanya mkutano kigamboni (au temeke) kama sikosei. Polisi kama ilivyokuwa kawaida yao wakati wa uongozi wa mkapa, wakaenda wakatoa kipigo cha nguvu sana. Watu wengi sana waliumizwa na kupelekwa polisi. I know this kwa sababu nilikuwepo kwenye mkutano huo.

Mkutano uliofuatia, CUF wakampeleka Lipumba akasaidie kwenye kampeni. Polisi kama kawaida yao, wakatoa dozi kwa wafuasi wa CUF (this time wakampiga Lipumba). Lipumba akaumizwa mkono kutokana na kipigo. Kwa kuonesha solidarity kwa wanachama wake, Lipumba "akalizimisha" kukamatwa pia na polisi. Vyombo vya habari vikachukua picha... the next thing we know, picha zinaoneshwa kwenye TV na kwenye magazeti Lipumba akiwa kafungwa bandage akielekea kwenye tinga tinga la polisi.

Hiyo publicity ilikuwa too much for Mkapa to handle. Since then, polisi walianza kuwa na adabu kwenye mikutano ya CUF. Kama Lipumba angeingia mtini na kuacha wanachama wake, nadhani risasi za moto zingetumika kuwafagilia mbali.

Katika kampeni za upinzani, polisi wanatoa "heshima kidogo" kwa viongozi wa kitaifa. Wanachama wengine ni sisimizi tu wasio na thamani yoyote ile.
haijalishi maneno amngapi unaandika... mbowe amejastifai lengo la chama cha mafisadi
 
Mkuu Kamende ameleta habari, imejadiliwa. Inaonekana mambo si shwari. Sasa tusubiri taarifa ya Gen. Emeritus Shimbo. Prof. Kinana na Dr. Makamba kwa upande mmoja na ya Ndugu Baregu na Mabere Marando kwa upande mwingine. Bado natafakari

Upande mmoja Gen. Shimbo, Dr. Sheikh Yahya, Dr. J. Kikwete, Dr. Manyaunyau, Dr. Bibigula, Prof. Rostam, Prof. Lowasa, Prof. Majimarefu.... Na kwa upande mwingine Ndugu Slaa, Ndugu Mbowe, Ndugu Baregu, Ndugu watanzania wazalendo wote.
 
Mbowe alitaka kumwaga damu watu? huyu jamaa ni mtu hatari sana hasa kwenye maswala ya maslahi yake anaweza mtoa uhai wa mtu...

Huyu hawezi pata ubunge hai, anakubalika kwao tu Machame pekee ndiko anakokubalika,swala la ubunge kwa kipindi hiki asahau kwa kweli ..
usidandie treni kwa mbele..

CCM walitaka damu imwagike through green guards, aka interahamwe... bahati mbaya mbowe akashindwa kuvumilia akareact, na ndicho walichotaka akina kinana

kila mtu anajua wamwagaji damu ni ccm... umesahau ya zanzibar?? umesahau ya mwembechai? umesahau ya nyamongo?? umesahau ya geita???

namuomba mbowe asiingie mtego wa ccm
 
Safi sana Kamanda Mbowe... sasa hakuna haja ya kuzuia na kujikinga ... full scale vita ni vita tu... Police, Green mgambo, TISS, JWTZ, na JK Family wote lao moja tu kuhakikisha Mafisadi wako salama...
 
Sheria ya Vyama vya Siasa inakataza vyama kuwa na vikosi vya kijeshi. Green Guards wa CCM ni "militia" ambao ni sawa na wanajeshi.

Je, kwa hili, CCM haiendi kinyume na Sheria? Kwa nini CCM isichukuliwe hatua za kisheria?

CHADEMA, NCCR, CUF, TLP, UDP, DP, UPDP, PPPT na wengineo wangekuwa na MILITIA zao, Tendwa angekawia kuwachukulia hatua?

Tuache unafiki. Damu isimwagike nchini kwa kutaka kuingia Ikulu.
 
ambalo ni lipi?
wapinzani wagomvi.... mie nimekulia uswazi na najua visa vya jirani

ccm hawana sera na walijua udhaifu wa mbowe... mbona hawakwenda kwa zitto? mbona tarime hawakumchanganya mgombea?
 
Wakuu naona sasa tumebase zaidi kwenye tafsiri kuliko facts. But what I see is another Zimbabwe in the making. Nilikuwa sifikirii kwamba mambo kama haya yanaweza kutokea Tanzania.
 
Ulichotoa hapo, na walichotoa wana ccm (kadogoo na Anfaal) vina tofauti gani? nimetumia neno spin za wanaccm, kama hii inakufanya wewe mwanaccm so be it.

Ngoja nikukumbushe jambo moja, miaka fulani iliyopita wakati mkapa akiwa preziii. CUF walifanya mkutano kigamboni (au temeke) kama sikosei. Polisi kama ilivyokuwa kawaida yao wakati wa uongozi wa mkapa, wakaenda wakatoa kipigo cha nguvu sana. Watu wengi sana waliumizwa na kupelekwa polisi. I know this kwa sababu nilikuwepo kwenye mkutano huo.

Mkutano uliofuatia, CUF wakampeleka Lipumba akasaidie kwenye kampeni. Polisi kama kawaida yao, wakatoa dozi kwa wafuasi wa CUF (this time wakampiga Lipumba). Lipumba akaumizwa mkono kutokana na kipigo. Kwa kuonesha solidarity kwa wanachama wake, Lipumba "akalizimisha" kukamatwa pia na polisi. Vyombo vya habari vikachukua picha... the next thing we know, picha zinaoneshwa kwenye TV na kwenye magazeti Lipumba akiwa kafungwa bandage akielekea kwenye tinga tinga la polisi.

Hiyo publicity ilikuwa too much for Mkapa to handle. Since then, polisi walianza kuwa na adabu kwenye mikutano ya CUF. Kama Lipumba angeingia mtini na kuacha wanachama wake, nadhani risasi za moto zingetumika kuwafagilia mbali.

Katika kampeni za upinzani, polisi wanatoa "heshima kidogo" kwa viongozi wa kitaifa. Wanachama wengine ni sisimizi tu wasio na thamani yoyote ile.

jibu zuri.
 
Hawa Green Guard ni nani hasa? Kwanini serikali ya CCM wamekosa uungwana..kwanini wanatumia dola vibaya kwa kuwavika mamluki sanda ya kijani kutishia na kumwaga damu zisizo na hatia?..kwanini wanakua waumini wa amani wasiyoiamini? Ifike mahali sasa watumie kiasi kidogo cha utu waliosalia nao baada ya kutaabisha wananchi kwa miaka yote pasi na ahueni kuelekea madhabahuni na misikitini kutubu dhambi zao kabla kiama chao hakijafika! 2010 Watanzania wameamka!
 
wapinzani wagomvi.... mie nimekulia uswazi na najua visa vya jirani

ccm hawana sera na walijua udhaifu wa mbowe... mbona hawakwenda kwa zitto? mbona tarime hawakumchanganya mgombea?

walikwenda musoma wakakata watu mapanga, hujasikia hilo?
Tarime hawawezi kwenda maana wanajua watapokea kipigo cha mbwa mwizi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom