Mbowe aelezea mauaji ya mkenya ITV

AMARIDONG

JF-Expert Member
Jun 24, 2010
2,502
180
Wakuu nilikuwa nimetoka kidogo kurudi namkuta muheshimiwa Aikaeli Freeman Mbowe anaeleza kitu kuhusu mauajiya mkenya juzi kule Arusha aliyeipata hiyo taarifa kikamilifu tafadhali atueleze Mkuu wetu anasemaje??
 
MTAWALA jitahidi kutpostia Thread zenye kicha na miguu sasa unaposema nimekuta eti:
"kurudi namkuta muheshimiwa Aikaeli Freeman Mbowe anaeleza kitu kuhusu mauajiya mkenya juzi kule Arusha" naona km vile umeona mkia unaishia sasa hujui ni paka au mbwa.

Bora usubiri upate uhakika wa jambo siyo kukurupuka kurusha vitu robo robo humu.

Ahsante
 
Ni hivi kati ya wale waliouwawa na polisi juzi mmoja ni raia ya wa kenya aneitwa paul njuguna anatoka kajiado,polisi wakambatiza jina george mwita waitara,
so cdm wameligundua na ushahidi upo
 
wameua wawekezaji wao ha ha ha sijui tutaenda wapi kuomba msaada..............jamani habari za mwanzo niliambiwa na makambah ameuwawa wajumbe kuna ukweli wowote?
 
kujua ni mkenya au mtanzania sio tija. tija ni kuwa alishiriki maandamano yaliyopigwa marufuku. Mbowe na Slaa wawajibike kwa umma kwa nini hawakutii amri ya IGP ambayo ndio amri ya serikali halali..
 
Kagumyeto,Igp hana mamlaka kisheria kuzuia maandamano,mwenye mamlaka ni rpc,lakini pia cdm wana barua halali kutoka kwa rpc ya kupanga njia ya maandamno ya tarehe 4,na siku hiyo usiku igp anapiga marufuku tena kwenye vyombo vya habari bila kuwaandikia au kumwamuru rpc kuwaandikia cdm,sasa hapa wa kuwajibika ni cdm au igp,rpc,na ocd?na wengi wa hawa waliouwawa ni raia wa kawaida wasiokuwa wanacdm,na walikuwa kwenye pita zao,na je polisi kupiga watu kwenye eneo la mkutano ni halali?pia kuna fundi garage aliuwawa akiwa gerji kwake kwa kisingizio cha kutaka kuchoma kituo moto,,,huu ni uhuni na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu,lakini iwe kwa damu au vinginevyo lazima kupigania na kutetea haki na ukombozi
 
mtu aliyeuwawa na polisi kwa kupigwa risasi tumboni walimtambulisha kwa jina la george Waitara cdm wamefukunyua wakajua jina lake ni njuguna na passport yake wameipata wanaendelea kuuhakikishia umma wa watz kuwa polisi waliuwa wananchi ambao hawakuwa kwenye zoezi la kuchoma vituo vya polisi vya polisi bali waliua watu ambao walikuwa kwenye shughuli zao . Ukiangalia raia wa kenya ataandamana kudai uchaguzi wa meya kwa maslahi gani ?
 
MTAWALA jitahidi kutpostia Thread zenye kicha na miguu sasa unaposema nimekuta eti:
"kurudi namkuta muheshimiwa Aikaeli Freeman Mbowe anaeleza kitu kuhusu mauajiya mkenya juzi kule Arusha" naona km vile umeona mkia unaishia sasa hujui ni paka au mbwa.

Bora usubiri upate uhakika wa jambo siyo kukurupuka kurusha vitu robo robo humu.

Ahsante

au nyoka
 
wameua wawekezaji wao ha ha ha sijui tutaenda wapi kuomba msaada..............jamani habari za mwanzo niliambiwa na makambah ameuwawa wajumbe kuna ukweli wowote?

na kenya ndio nchi ya pili kwa uwekezaji hapa tanzania baada ya uingereza
 
msaada wa binafsi mimi nahisi niaomba mnisaidie wana wema wenzangu wapi naingia ili sasa nami niweze kutuma post zangu
 
kujua ni mkenya au mtanzania sio tija. tija ni kuwa alishiriki maandamano yaliyopigwa marufuku. Mbowe na Slaa wawajibike kwa umma kwa nini hawakutii amri ya IGP ambayo ndio amri ya serikali halali..

Alikuambia kuwa anaenda kuandamana? au unafikiri watu wote waliokuwa Arusha siku ile walikuwa wanaandamanaji? huyo atakuwa alikuwa anaendeleana kazi zake za uwezekaji huwezi jua risasi ikapigwa katikati ya watu ikampata bahati mbaya au wewe unafikiri zile risasi zimeambiwa ziue waandamanaji tu?

hawa nao walikuwa wanaandamana sio????
01.jpg
 
kujua ni mkenya au mtanzania sio tija. tija ni kuwa alishiriki maandamano yaliyopigwa marufuku. Mbowe na Slaa wawajibike kwa umma kwa nini hawakutii amri ya IGP ambayo ndio amri ya serikali halali..

kwani adhabu ya kupuuza amri ya halali ya IGP ni kifo?polisi walishindwa kuwakamata bila risasi za moto?unataka kuniambia vile vitambaa vyeupe walivyokuwanavyo waandamanaji ni 'Vitanzi' ambavyo vingeweza kuwanyonga polisi ?
Fikiria kwanza kabla ya kupost pumba zako.
 
msaada wa binafsi mimi nahisi niaomba mnisaidie wana wema wenzangu wapi naingia ili sasa nami niweze kutuma post zangu

click click forum unayotaka mfano jukwa la siasa hapo juu. Scroll down the page (of threads) na mwisho utakuta icon ya post new topic.
Ingia, andika title then endelea na contents za thread yako
 
msaada wa binafsi mimi nahisi niaomba mnisaidie wana wema wenzangu wapi naingia ili sasa nami niweze kutuma post zangu

i like your stance... you are very civilised..... shule haiishi hapa duniani...kuuliza si ujinga.... kula tano yangu instantly
 
Back
Top Bottom