'Mboni Yangu': Big Up! Bongo Celebrities Lakini..........

Mzalendowetu

Member
May 22, 2012
87
34
Pongezi Bongo Celebrities kwa wimbo wa ‘Mboni Yangu’ ambaO ni maalum kwa msanii Sajuki anayesumbuliwa na ugonjwa. Hongera wote mlioshiriki kwa namna moja au nyingine katika kufanikisha wimbo huu, hasa Waheshimiwa Makamba, Zitto, Mdee, Kamata na Bulaya kwa kuonyesha uwakilishi halisi wa vijana. Licha ya majukumu ya kitaifa mmeungana na kushirikiana na vijana wenzenu katika kutayarisha wimbo huu. Tunaamini hata mtakaposhika nafasi za juu zaidi serikalini bila shaka mtaendelea kuwa wawakilishi wazuri. Kwa ujumbe wake, wimbo huu utaendelea kutumika katika kukusanya juhudi zetu za hali na mali katika kutatua matatizo yanayowakumba watanzania wenzetu.
Lakini licha ya maudhui mazuri ya wimbo, kasoro kubwa iliyojitokeza ni pale video inapokuwa haendani na maudhui. Kuna baadhi ya washiriki wameonyesha sura za tabasamu na wengine hata kucheka na kugangeana (Mfano Prof. Jay, Mwana FA, Wema na Barnaba). Ukiangalia vitendo hivyo ni tofauti kabisa na maudhui ya majonzi, masikitiko, picha ya huzuni ya msanii Sajuki na Wastara iliyopo kwenye video na hata sauti za hudhuni zinazoonyeshwa na baadhi ya waimbaji kama Ditto, Ally Kiba, Mh. Mdee n.k. Iliwezekana kabisa hata kwa kuigiza kuwa na sura za huzuni ili ziendane na maudhui ya wimbo.
 
Hivi yule wa milioni 10 hajachangia ktk kumnurusu sajuki ila anasubiria akifa ndo akachangie?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom