Mbona Tukiweke Issue za Wazanzibari wanavyoina Bara Moderator anaziondoa?

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
Tumeweka Makala kadhaa kuhusu Wazanzibari jinsi wanvyoukataa muungano na Bara wanaita ni wa kichawi, wakila maneno mabaya; lakini Moderator hapa anaiondoa kuna sababu? Au tunatakiwa kuongelea tu tofauti Kati ya CCM na Chadema na sio matatizo mengine? Mimi naota tatizo kubwa kwetu ni huu muungano tunahitaji kuujadili kwa ufasaha wakati katiba mpya inatakiwa.

Chini ni makala kuhusu Muungano jinsi wazanzibari wanavyouona jinsi ulivyo...

• MAFUTA YETU HATUTOI NG’O!
Na: Malik Nabwa
Kama kuna kitu kilichopangwa na kushuhulikiwa kwa umakini mkubwa hapa nchini ni Muunagano wa Tanzania na Zanzibar. Yaani kila kitu ambacho bara wanakifanya juu ya Muungano basi huwa ‘’very strategic’’ kiasi ambacho mikakati hiyo inavyopangwa kwa umakini mkubwa laiti ingekuwa inatumiwa kuleta maendeleo ya Taifa basi Taifa hili lingekuwa mbali kimaendeleo.
Mara kadhaa tumejaribu kuonesha kuwa muungano wa Zanzibar na Tanganyika haukufanywa hata kwa chembe moja ya nia njema. Naufananisha kabisa na mungano wetu na chama cha wachawi huko Ging’ingi. Kwa anaewafahamu wachawi vizuri basi umoja wao huwa hauko katika nyoyo zao bali hamu na matakwa ya nafsi zao tu. Wachawi hawana chembe ya nia njema wala upendo kati yao na walivyonavyo kwa mfano watoto wao au hata familia zao. Hivi ndivyo ulivyo Muungano kwa wenzetu wa bara dhidi yetu.Ni chama cha wachawi tu kila mtu ana lengo lake tena leno baya dhidi ya mwenzake.
Tumeona kuwa msingi wa kuungana kwetu ulikuwa wa magube matupu. Kwanza hakukuwa na ulazima wa kuungana kwani ukiungana na mchawi lazima siku moja atakuliza tu au kukutia wanja jicho moja, tumulize shekh Karume kama tunataka ushahidi juu ya hili. Pili, mara tu baada ya Muungano tulishuhuduia mambo kadhaa ya kuipora Zanzibar kuwa nchi na kujitegemea kwake. Tuakunganisha vyama na kila kitu. Ikafika wakati lazima kila kitu kiamuliwe bara. Hii ndio taswira halisi ya Muunagno wa kinafiki sawa na muungano wa Kichawi. Muungano usio na nia njema siku zote hukimbilia msihipa ya kuvutia pumzi ya mwenza wake na kuidhibiti. Ikishafanya hivyo mwenye kuzibwa pumzi lazima atii amri na akishindwa basi hana hiari ila ni kufa au kukosa kila kitu kabwi na mtindi. Muungano wetu sisi Wazanzibari umetufikisha hapa.
Si vibaya tukijikumbusha kidogo ajenda za siri za Muungano kutuchagulia viongozi wa juu kama moja ya mbinu yao ya kuendelea kututawala na kuimaliza mirija michache ya kuvutia pumzi iliyobaki tuanzie na Raisi wa Kwanza. Raisi Karume alipokuja tanabahi tu kuwa kujiingiza katika Muungano lilikuwa kosa la jinai akataka kujitoa pale alipoanza kubwatuka hadharani; ‘’muungano mwisho Chumbe’’ huku akisahau kuwa ukishaingia uchawini huwezi kutoka. Yaliyomkuta ndio yale. Mauaji yake yalikuwa hayahitaji uchunguzi wa CIA,FBI, KVB, wala Scotland Yard.
Nini kilitokea baada ya kikwazo cha kuendeleza Ubabe wa kutaka kuung’oa Muungano kuondoka yaani baada ya kifo cha Sheikh ‘’K’’. Dodoma ilipanga nani ni mtu wao atakaeweza kutimiza azma yao ya kuidhibiti mirija muhimu ya kuvutia pumzi ya Zanzibar na kuiweka chini ya himaya ya Muungano. Akaletwa Jumbeambae alikuwa mwenzao badala ya Sefu BAKARI alietakiwa na Baraza la Mapinduzi lenyewe. Kwa upande mmoja ilikuwa shufaa kuwekwa Jumbe kuliko Sefu Bakari maana japo Seifu alikuwa hana malengo na Muungano lakini alikuwa kichwa maji kuliko hata Karume kwa hiyo hata angewekwa yeye tusingepata shufaka yoyote. Afadahali huyo Jumbe ni anagalau afadhali ya kung’twa na nge ukakoswa na tandu, wala si afadhali kitu maana mchawi ni mbaya tu hata awe vipi.
Muungano ulifanikisha azma yake kwa kumuweka Jumbe. Baada ya kupandikiza mtu wao huyu wakajichukulia hatua moja muhimu ya kuudhibiti mshipa mkuu wa pumzi wa Zanzibar. Nao ni pale Jumbe alipokubali Kuunganisha vyama na Nyerere mwaka 1977. Katika kosa kubwa katika historia ya Zanzibar ni hili alilolifanya Jumbe (The grave mistake over Zanzibar future stake in the Union). Kwa kuunganisha Chama ndio alijimaliza yeye mwenyewe kama Rais kamili wa Zanzibar na pia ikawa kashaiondolea kinga dola ya Zanzibar. Kuanzia hapo ndio Zanzibar ikawa ni sehemu tu ya Jamhuri ya Muunagano.
Kama nilivyotangulia kusema hapo awali kuwa ngoma ya kichawi haina mwisho mwema. Mwema wako leo kesho ndie mbaya wako wa mwisho. Jumbe akawa amejitia kitanzi mwenyewe na bila kinga wala hifadhi akatolewa kikoa katika hali ya aibu kabisa na idhilali. Haya ndio malipo ya kushirikiana na watu wabaya. Tukumbuke kuwa Nyerere alimtimua Jumbe baada ya kuhakikisha ameshashikilia maeneo muhimu ya Zanzibar. Kwa mfano kama Jumbe hakuunganisha vyama Nyerere angepata nguvu wapi ya Kumfukuza? Lengo lake ikawa limefanikiwa.Kinachofuata sasa ni kung’atuka maana ‘’mission accomplished’’.
 
Naona umejieleza sana - lakini hujapendekeza strategy za kuiondoa Zanzibar kutoka kwenye muungano. Kwa kweli mkiondoka mimi nitafurahi maana kwa kweli Zanzibar umekuwa mzigo kwetu.
 
zanzibar inabidi iwe mkoa,sio nchi .hakuna cha rais wala baraza la wawakilishi.
 
mods hawafundiswi na vilaza ...... hii thread sio mahali pake ...hoja mchanganyiko
 
nngu007, Pamoja na kwamba sijasikia wabara wakizungumzia hayo mafuta ya zenji, ningetegemea uzungumzie namna gani zenji itajiondoa kwenye huu unaouita muungano dhalimu. Kwa malalamiko ya jinsi hii naamini mtaendelea ku-enjoy matunda ya muungano.
 
Znz mnasubiri nn kujitenga najua mtaondoka na CUF yenu japo tupunguze chama kimoja cha wanafiki maana najua muungano ukivunjika na CUF imekufa Bara
 
Wazanzibar
1.tunaburuzwa kwenye muungano
2.Tunachaguliwa rais wa zanzibar (kimkakati kwani CCM inawapitishia wagombea urais)
3. Dai jipya: TUMECHEZEWA RAFU MATOKEO YA FORM FOUR 2010 (wanataka baraza lao la mitihani)na malalamiko kibao.TUJITOE KWENYE MUUNGANO

BARA:tudumishe muungano jamani na misemo kibao ya Mwalimu.

My take:Tuwaachie zanzibar yao waone watafika wapi na siasa zao zisizo na hoja wala mashiko bali visasi vya kihistoria mara HANGA,ushiriki wa SEIF kumdhalilisha JUMBE,sijui mara Sultan alifanyaje yaan ajabu bin ajabu.

Vijana wa BARA tunataka siasaleo (sio siasahistoria ya CUF+-CCM)inayochipua hoja bila woga kwa maslahi ya taifa.Tumeingia kwenye ulingo mwingine wa kuikomboa nchi kutoka kwa Mafisadi.
 
Nahisi sasa wakati umefika... mfumo wa huu muungano uangaliwe upya na tukikosa muafaka kuuhusu basi tuuvunje kila watu waende kivyao!!
 
Back
Top Bottom