Mbona Papii nguza nae alikua na miaka 17 vipi lulu?

harakat

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
2,888
1,347
wakati kesi inayomkabili msanii lulu ikiendelea angalia hivi vifungu jinsi vilivyomiminika hapa
mawakili wanadai mteja wao yuko chini ya umri kwa hiyo kesi ihamie mahakama ya watoto
mbona Papii nguza haikua hivyo?

Fungamtama alisema Kifungu cha 4 cha Sheria ya Mtoto ya mwaka 2009 Kipengele namba 21, kinatamka wazi kuwa mtoto ni yule aliye na umri chini ya miaka 18. Wakili huyo aliendelea kunukuu vifungu mbalimbali vya Sheria ya Mtoto kama 98 (i) na 114 (ii), ambavyo alidai kuwa vyote vinawapa nguvu ya kuwasilisha maombi yao hayo ya kuihamisha kesi hiyo. “Hata katika suala la Mahakama, vifungu vyote vya sheria hii vimefafanua, hivyo tunawasilisha maombi yetu kwamba mteja wetu ana umri wa miaka 17 na shauri hili lingepaswa kusikilizwa Mahakama ya Watoto,” alidai.

Kwa upande wake, Wakili wa Serikali, Elizabeth Kaganda aliomba wapewe muda zaidi kwa sababu bado wanaendelea na upelelezi wa kesi hiyo. “Kesi hii imekuja mahakamani hapa kama ya mauaji na upelelezi bado haujakamilika. Tunaposema haujakamilika, tunapeleleza kila kitu, likiwamo suala la umri,” alieleza Kaganda. Alisema hata jina linaloonekana katika cheti cha kuzaliwa kilichowasilishwa mahakamani hapo, linasomeka Diana Elizabeth wakati mshtakiwa ametajwa mahakamani hapo, kwa jina la Elizabeth Michael. “Tunaomba muda tuweze kuchunguza kuhusu umri wa mshtakiwa kwa sababu aliwaeleza polisi kwamba ana umri wa miaka 18 halafu mawakili wake wanakuja kueleza hapa mahakamani kwamba ana umri wa miaka 17,” alidai Kaganda. Wakili huyo wa Serikali alidai kuwa kutokana na mvuto wa kesi hiyo katika jamii, wanaomba wapewe muda zaidi kufanya upelelezi ili kumtendea haki mshtakiwa huyo.

Kuhusu cheti hicho kusomeka Diana Elizabeth, Wakili Fungamtama alikiri na kudai kuwa ni jambo la kawaida hasa kwa Wakristo kuwa na majina mawili. Fungamtama alidai kuwa hawana pingamizi na maombi ya upande wa mashtaka kwamba wapewe muda zaidi wa kufuatilia cheti cha kuzaliwa cha mshtakiwa, ingawa alidai kuwa suala hilo halina ugumu. Akitoa uamuzi baada ya kusikiliza hoja za pande zote, Hakimu Mkazi Augustina Mbando alisema: “Mahakama imesikiliza maombi yaliyoletwa na Fungamtama na Kaganda na imeona kesi iliyopo hapa ni ya mauaji na jinsi kesi hii ilivyo, hatuwezi kufanya hoja yoyote hadi upelelezi utakapokamilika.”

“Kama defence (upande wa utetezi) wana maombi yoyote wanaweza kufanya hivyo kupitia Mahakama Kuu,”
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Mei 21, mwaka huu itakapotajwa tena. Inadaiwa kuwa Aprili 7, mwaka huu katika eneo la Sinza Vatican, Dar es Salaam msanii huyo wa kike, alimuua Kanumba. Jana Lulu alifikishwa mahakamani hapo saa 2:50 asubuhi akiwa peke yake kwenye gari linalobeba mahabusu, huku akisindikizwa na magari mengine mawili.

Alipoingia mahakamani alikuwa amezingirwa na askari Magereza na Polisi zaidi ya 10 na kuufanya umati mkubwa wa watu uliofurika mahakamani hapo kushindwa kumwona. Miongoni mwa watu waliofika mahakamani hapo jana ni baba mzazi wa msanii huyo, Michael Kimemeta na ndugu zake wengine kadhaa.
 
Tofauti hii hapa. 1. Papii Nguza ilikula kwake kutokana na mzee wake (mzee nguza), kutafuna "ngozi" ya mh. sana. Mh. Sana ni mtu wa visasi sana, si mtu wakusamehe hata siku moja. Hata hii ishu ilimkuta Amatus Liyumba.... 2. Lulu alikuwa analiwa na mtoto wa mh. sana, sasa kwa sababu wao ndio "wamiliki wa hii nchi", lolote watakalo wanaweza kufanya, in short "wao ndio mpango mzima"...
 
Lulu kiumri ni mdogo lkn matendo yake wajameni yamezidi ya bibi zake! Ktk umri huo anamiliki nyumba kubwa tu Kimara etc. Shule hakakumaliza kwa kujiingiza kwenye mambo yaliyomzidi umri. Nilishuhudia interview yake na Salama kwenye kipindi chake cha Mikasi, akaulizwa umri wake na proudly akajibu "nina miaka 18!". Leo ana miaka 17! Haya yetu macho. Mimi ninaamini hata kama angekuwa na miaka 40 na kama hakuhusika na kifo cha Kanumba, sheria itamlinda tu na hakuna haja ya kutafuta sababu za kusave kesi kama kweli hahusiki.
Wazazi wa Lulu wanapaswa pia kulaumiwa kwa kutomlinda mtoto wao, wangemsimamia amalize shule na si kufurahia pesa alizokuw akiwapa (maana mama yake yake aliwahi kutamka kuwa Lulu ndiye tegemeo lao na anawatunza. Binti bado mdogo sana kwakweli kutwishwa majukumu hayo. Namuombea sheria ichukue mkondo wake ili kama hajahusika aachiwe huru k maana atakuwa amejifunza na kuwa binti mwema.
 
aliyekuwa na miaka 17 ni fransis nguza!! walikuja kumuachia baada ya miaka kadhaa...
 
Tofauti hii hapa. 1. Papii Nguza ilikula kwake kutokana na mzee wake (mzee nguza), kutafuna "ngozi" ya mh. sana. Mh. Sana ni mtu wa visasi sana, si mtu wakusamehe hata siku moja. Hata hii ishu ilimkuta Amatus Liyumba.... 2. Lulu alikuwa analiwa na mtoto wa mh. sana, sasa kwa sababu wao ndio "wamiliki wa hii nchi", lolote watakalo wanaweza kufanya, in short "wao ndio mpango mzima"...

Acha wewe kuongea nadharia zisizo na mashiko, wewe ulisaidia kushika hiyo 'ngozi' wakati ikitafunwa na huyo 'mh. Sana'?
 
Kwa umri kweli Lulu ni mdogo sana. Lakini kwenye masuala ya Ngono/Ndoa Lulu ni USED kuliko hata mama aliye kwenye ndoa kwa miaka 20 na mwenye watoto 3. Believe it or not.

Lul* ni used inayokaribia Scrapper.
 
Kesi ya nguza ilihusu watoto wadogo na hivyo na ilisikilizwa kwa kuzingatia hilo. Hivyo kulikuwa hakuna point tena kuhusu umri wa Papii katika kusikiliza kesi hiyo kwa kuwa tayari mazingira ya kesi yenyewe (kuhusu watoto) yalitaka isikilizwe privately (in camera)! Hivyo sio sawa kulinganisha kesi ile na hii ya Lulu.
 
Back
Top Bottom