Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbona Nyaga Mawalla kajiua kule Kenya tena?

Discussion in 'Kenyan News' started by Ab-Titchaz, Mar 25, 2013.

 1. Ab-Titchaz

  Ab-Titchaz Moderator Staff Member

  #1
  Mar 25, 2013
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 16,212
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 0
  Lawyer commits suicide in hospital

  By Cyrus Ombati

  Nairobi, Kenya: A prominent Tanzanian Lawyer cum businessman Mr Nyaga Mawalla committed suicide at the Nairobi Hospital.

  Mawalla had been admitted at the hospital before he jumped to his death from the first floor ward on Saturday, police and the hospital officials said.


  It is not clear what caused him to commit suicide but police said they are investigating the incident.
  "We are informed he is a lawyer based in Arusha but we are yet to get more details on what may have led to the incident," said Nairobi head of police Benson Kibue.

  Officials said his firm handles corporate legal services to dozens of local and international tourists, real estate and mining companies.

  Standard Digital News - Kenya : Kenya : Lawyer commits suicide in hospital
   
 2. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #2
  Mar 27, 2013
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,767
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 38
  Nimesoma mwananchi! dah...Arusha. Utata umegubika mazishi ya Wakili maarufu nchini, Nyaga Mawalla baada ya wakili wa kujitegemea ambaye pia ni mtoto wa Rais wa zamani wa Zanzibar, Fatma Karume kuwasilisha wasia wa marehemu kwa wazazi wake ambao alitaka azikwe kwenye shamba lake la Momela, wilayani Arumeru, mkoani Arusha.Hata hivyo, wasia huo unadaiwa kupingwa vikali na baba mzazi wa marehemu, Juma Mawalla huku akitoa sharti la kutohudhuria mazishi ya mwanaye iwapo akizikwa sehemu tofauti na Kijiji cha Marangu.Mawalla, alifariki hivi karibuni baada ya kujirusha kutoka ghorofani akiwa Nairobi, Kenya alipokwenda kutibiwa. Taarifa za awali zinasema kwamba Mawalla aliamua kujiua kutokana na kusumbuliwa na msongo wa mawazo, inadaiwa enzi zake za uhai alikuwa na uhusiano mbaya na baba yake.Kwa mujibu wa vyanzo vya habari kutoka kwa mmoja wa mawakili wa kujitegemea mjini hapa, siku chache baada ya kifo cha wakili huyo, Karume alifika Kilimanjaro kuwasilisha wasia alioucha marehemu.Ilidaiwa binti huyo ambaye anatajwa kuwa karibu na marehemu enzi za uhai wake, alikutana na baba yake mzazi na kuusoma.Hata hivyo, chanzo hicho kilidai kuwa pendekezo hilo la marehemu lilipingwa vikali na baba yake na kusema iwapo mtoto wake atazikwa Momela, hatahudhuria mazishi hayo.Imeelezwa kipindi cha miaka miwili, wakili huyo hakuweza kuongea na baba yake hadi alipofariki, kutokana na uhusiano mbaya waliokuwa nao.Hata hivyo, wakili huyo alisisitiza kuwa, chanzo cha uhusiano mbaya baina yao ni kutokana na mzee Mawalla kumwonya mwanaye kuhusu biashara anazofanya baada kupokea malalamiko mbalimbali kutoka kwa watu, maofisa usalama na baadhi ya polisi nchini waliokuwa wakifika kijijini mara kwa mara kumsemea. Mmoja wa mawakili wa Kampuni ya Mawalla Advocates, Lemy Bartholomew alipoulizwa kwa njia ya simu na gazeti hili kuhusiana na taratibu za mazishi, alisema ni mapema kuzungumzia suala hilo kwa sababu kuna vikao vya familia vinaendelea.Wakili huyo alisema baada ya vikao hivyo, ndipo uamuzi utakapojulikana iwapo atapozikwa shambani kwake au nyumbani kwao kijijini Marangu.Imeandikwa na Moses Mashalla na Peter Saramba .
   
 3. cacico

  cacico JF-Expert Member

  #3
  Mar 27, 2013
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 8,391
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 38
  rip nyaga! aachwe sasa apumzike panapomstahili......! huyo baba naye hata maiti nayo ya kuiziria?? angesamehe yaishe sasa, kha!
   
 4. bucho

  bucho JF-Expert Member

  #4
  Mar 27, 2013
  Joined: Jul 13, 2010
  Messages: 4,372
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 48
  kama amesema azikwe momela sioni kwanini baba yake ang'ang'anie kumzika marangu .
   
 5. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #5
  Mar 27, 2013
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,940
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 38
  Ukizingatia mtu ashakufa..Anasusia maiti!!?
   
 6. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #6
  Mar 27, 2013
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 7,333
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 63
  kuna info za chini ya kapeti zinasema jamaa alijiua kwa bastola huku arusha ndio akapelekwa nairobi na kutangazwa kuwa kajirusha gorofani!
   
 7. g

  gakato JF-Expert Member

  #7
  Mar 27, 2013
  Joined: Sep 4, 2012
  Messages: 834
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 18
  RIP Mawalla; ila tujifunze tuliobaki kuwa dhuluma mwisho wake mahuti...
   
 8. M

  Mshangai JF-Expert Member

  #8
  Mar 27, 2013
  Joined: Feb 16, 2008
  Messages: 204
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 16
  Nilidhani msongo wa mawazo ni wa sisi tuliosheni dhiki kumbe hata wenye nazo?
   
 9. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #9
  Mar 27, 2013
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 58,043
  Likes Received: 4,004
  Trophy Points: 113
  The will of the decedent almost always prevails.

  Sasa huyo baba atapingaje?

  Naye ndo tunaambiwa ni mwanasheria?
   
 10. l

  lasix JF-Expert Member

  #10
  Mar 27, 2013
  Joined: Mar 13, 2011
  Messages: 347
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 18
  Sioni sababu yoyote ya kudanganya kuhusiana na aina ya kifo alichokufa.kujipiga risasi na kujirusha ghorofani vyote ni kujiua tu hakuna tofauti.
   
 11. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #11
  Mar 27, 2013
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 12,478
  Likes Received: 525
  Trophy Points: 113
  Sasa mbona hii dogo dogo binti karume anatoa siri za ndani za mteja mshikaji?
   
 12. B

  BASIASI JF-Expert Member

  #12
  Mar 27, 2013
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 2,384
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 38
  Nafilkir na mali zake apewe huyo mtoto wa karume jaman amekuwa nae karibu mno msi;wache kwenye kaufalme chenu cha mgao
   
 13. G

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #13
  Mar 27, 2013
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 9,728
  Likes Received: 1,104
  Trophy Points: 113
  RIP Advocate Mawalla, ur generosity will ever remain in our hearts...
   
 14. G

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #14
  Mar 27, 2013
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 9,728
  Likes Received: 1,104
  Trophy Points: 113
  RIP Advocate Mawalla, ur generosity will ever remain in our hearts...
   
 15. G

  G4-Pune Member

  #15
  Mar 28, 2013
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nyaga alikwenda kwa matibabu na sio kujiuwa kama inavyosemekana hapa na msongo wa mawazo sio tatizo kwake kiasi cha kijiua. Utata mkubwa kuhusiana na kifo chake tusubiri ripoti ya polisi kenya kwani ghorofa ya kwanza ni pafupi sana kwa mtu kuvunjika kiasi hicho alivyo sasa hivi. Ugomvi wake na mzee wake haukuwa namna hio kama majirani tunavyo fahamu.
   
 16. M

  Mwathirika JF-Expert Member

  #16
  Mar 28, 2013
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 125
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hakuna siri, huo ni wosia wa marehemu na ameenda kuusoma kwa wazazi wake. Wosia siyo siri.
   
 17. tofali

  tofali JF-Expert Member

  #17
  Mar 28, 2013
  Joined: Mar 27, 2013
  Messages: 2,691
  Likes Received: 161
  Trophy Points: 63
  Hizo ni laana za kugombana na mzazi..ht km mzazi wako kakufanyeje yapasa kumsamehe..huyo ndo Mungu wa duniani..km alikua anafanya biashara haramu asikanywe.? Kisa
   
 18. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #18
  Mar 28, 2013
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,067
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 48
  msongo wa mawazo hata kwa wenye nazo...nadhani mimi utingo tu ndiye mwenye msongo wa mawazo maana hata kula yangu shida mpaka nipige jeki mara kibao
   
 19. Dhuks

  Dhuks JF-Expert Member

  #19
  Mar 28, 2013
  Joined: Mar 15, 2012
  Messages: 1,730
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 38
  Mmmmm, mimi nafikiria ni deceased
   
 20. Bubu Msemaovyo

  Bubu Msemaovyo JF-Expert Member

  #20
  Mar 28, 2013
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 3,489
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 38
  Kwa kweli inasikitisha sana kwani ni habari ya kusikitisha sana na imekuwa kama ghafla. Kumekuwepo na kutoelewana kati ya wazazi na watoto wao kwa kipindi kirefu sasa tangu tuwe katika mambo huria namaanisha tulipobwaga mila zetu tukazifuata hizi za kuletewa. Enzi hizo haya yangemalizwa kwa mila na desturi zetu. Mtoto akijikwaa alikuwa akiitiwa wazee na kuonywa, leo hii akijikwaa anakuletea Mwanasheria Uonywe Wewe Mzazi wake. Tukumbuke Imeandikwa; "Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na BWANA, Mungu wako."........Mungu alimaanisha hayo.

  Asanteni.
   

Share This Page