Mbona mzee Mwinyi hashiriki kampeni za CCM?

Landala

JF-Expert Member
Dec 24, 2010
997
473
Jamani watanzania wenzangu mbona chama cha matusi aka chama cha majaji hakijawahi kumteua rais mstaafu Ally Hassan Mwinyi kushiriki kwenye kampeni za kumnadi mgombea wa CCM kwenye chaguzi ndogo kama mzee Mkapa,mwenye kujua sababu atujuze.
 
Mwinyi ni mtu mwenye heshima zake, anaheshimika sana TZ hii na hawezi kujivunjia heshima hasa katika kipindi hiki cha DOT.COM, we ukamtukane mwinyi kwenye hadhara ya watu ustaarabu kweli! mwacheni apumzike.
 
Busara zake zinamzuia kuchanganyika na wasema hovyo wakina Lusinde, Mwigulu na Nape!!
 
Ni mtaratibu mno, af'wanaogopa anaweza kuchapwa kibao na mwanaM4C ikawaharibia muvi..
 
Kwanza hana kashfa kama Ben, kwa hiyo hawawezi kumlazimisha. Wakati wa Ben uchumi ulikuwa afadhali
 
Sio kwamba Mkapa anapenda kushiriki katika kampeni. Ni kama kapewa adhabu na Kikwete siunajua ukiwa na makosa lazima unyenyekee ili usije ukaumbuliwa ndio haya yanayomsibu Mkapa. Mkapa ana issue ya ufisadi akiwa rais ivyo hawezi kukataa chochote kile ambacho ataambiwa na mwenyekiti wake. Anaogopa wasije wakaanza kumuulizia kiwira. Mwinyi alikuwa rais wa watanzania hivyo hawezi piga kampeni kwa chama kimoja wakati analipiwa gharama na watanzania wote bila kujali vyama.
 
Back
Top Bottom