Mbona msiba wa Jeremia Sumari haupewi attention kama wa Regia?

AMARIDONG

JF-Expert Member
Jun 24, 2010
2,502
180
HATA MAGAMBA WENYEWE MMEPOOZA?MPENI UZITO MZEE YULE SI ALIKUWA WAZIRI JAMANI EEEEHH MSIFANYE HIVYO

NIMESIKIA SPIKA ANAFIKIRIA JUU YA KUAGWA KWA SUMARI KAMA WAMUAGIE KARIMJEE AU POPOTE JAMANI

AU KWA SABABU ALIKUWA HAJAAPISHWAAAAA??SASA KAMA NI iSSUE MSISEMA MBUNGE,SEMENI MBUNGE MTEULIWA AU WAZIRI WA ZAMANI
 
inategemea hapewi eataim wapi. Hapa jf hatuna uhakika kama alikuwa memba. Regia alikuwa memba mwenzetu
 
HATA MAGAMBA WENYEWE MMEPOOZA?MPENI UZITO MZEE YULE SI ALIKUWA WAZIRI JAMANI EEEEHH MSIFANYE HIVYO

NIMESIKIA SPIKA ANAFIKIRIA JUU YA KUAGWA KWA SUMARI KAMA WAMUAGIE KARIMJEE AU POPOTE JAMANI

AU KWA SABABU ALIKUWA HAJAAPISHWAAAAA??SASA KAMA NI iSSUE MSISEMA MBUNGE,SEMENI MBUNGE MTEULIWA AU WAZIRI WA ZAMANI

Kila msiba una mwenyewe...
Bahati ya mwenzako usiilalie mlango wazi...
Ukiona vyaelea vimeundwa...
Ganda la muwa la jana Chungu kaona kivuno...
Angenda juu kipungu hafikirii mbinguni...
Pema usijapo pema ukipema si pema tena...
Kila ndege huruka kwa ubawa wake...
Tenda wema wende zako...

Kila tukio mkuu huwa linakuwa habari pale linapotokea kwa mara ya kwanza. Leo hii ukiamka ukasikia X ambaye ulikuwa naye jana kuwa amefariki utashituka sana, lakini ukiambiwa Y ambaye alikuwa anaumwa kwa muda mrefu amefariki utasikitisa sana na kupata mshituko pia ila hautakuwa kama wa yule mtu ambaye hukuwa umejityuni kuwa anaweza kututoka.

Ukitaka kuleta siasa za misiba utachanganyikiwa sana maana tukio la Msiba wa JK Nyerere mwaka 1999 ambao ulishitua wengi sana na tukafanya maombolezo ya mwezi mzima na kila mtu kulia hata kama alikuwa hataki kwa kuangalia waliokuwa wanalia kwenye maombolezo ya TV. Utajiuliza Mbona Simba wa vita (RM Kawawa) alipofariki hatukufanya hivyo?. And the list goes on, kwa hiyo ushauri wangu tuache siasa za misiba, maana Kifo si tukio la kushabikia japo ni wajibu. Ni tukio linalotunganisha na wale tuwapendao ama kwa kuwaacha duniani au kuwatanguliza akhera.

Tuache watu waomboleze kifo cha mpendwa wao Sumari anything cha kufananisha na kingine ni kama kuwasimanga. I believe all human are equal mbele ya mwenyezimungu. Ukizikwa na mtu mmoja au laki moja hajalishi kitu kama katika maisha yako hukuwa mtenda mema na mcha mungu. Ni amali pekee ndiyo itakayokuwa ngao ya mwanadamu pindi maisha yake yanapokoma na si namba ya wanaomlilia au kuomboleza.

Rest in peace Sumari
 
1.MH Regia alikuwa member wa jf na alitumia jina lake halisi. Sijuwi baba wa nancy kama alikuwa member hapa.
2.UMRI.mh Regia alikuwa mdada na mbunge kijana na machachari sana,ameishi kipindi kifupi ukilinganisha na Jeremiah sumari.
3.AINA YA KIFO KILIVYOTOKEA. Mh.Regia ajali ya gari ghafla {unexpected occarence} Sumari ameugua sana tangu mwaka 2010 na hakuapishwa.
4.SHUGHULI: MH.Regia aliainisha mambo aliyofanya na aliyotaka kufanya tofauti na mh.sumari mimi binafs cjuwi.
5.UMAARUFU:mh.regia alikuwa maarufu sana kuliko mh. Sumari.
6.KARIBA:mh.regia alikuwa Kiongozi na mh. Sumari alikuwa Mtawala
7.TULIO WENGI wetu humu jf ni vijana sana mh.regia ni kama alikuwa mwenzetu wakati mh.sumar kama babu yetu.
8.MH.regia chama na jinsia vimembeba wakati mh.sumari umri,chama na jinsia vimemwangusha.
NIKOSOLEWE KAMA NIMEKOSEA NINAMAPUNGUFU YANGU Nawakilisha.
 
Wanabodi,
Nimepata nafasi kuhudhuria msiba hapa nyumbani kwa Jeremia Sumari.

Kama ilivyo kwa Regia, hapa kwa Sumari ni vivyo hivyo, viongozi wa vyama vya upinzani wameungana na viongozi wa CCM na waombolezaji wengine kuwafariji wafiwa.

Jioni hii, Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe akiongozana na Naibu Katibu Zitto Kabwe wameungana na Mwenyekiti wa UDP Mzew John Cheyo wapo kwa pamoja na mawaziri kadhaa wa serikali ya JK wakiongozwa na Mawaziri Wakuu Wastaafu Mhe. Edward Ngoyai Lowassa!. na Fredrick Tuluway Sumaye!

Jana rais Jakaya Kikwete na Katibu Mkuu wa Chadema Dr. Wilbrod Slaa wakifika nyumbani hapa kuwafariji wafiwa!.

Mawaziri Wasira, Nchimbi, wabunge wakiongozwa na Katibu wa Bunge Dr Kashilila etc pia wapo!

Ni jambo jema na la kupendeza uonapo ndugu wakikaa pamoja kwa upendo wakati wa shida na raha. Huu ni uthibitisho kuwa licha ya tofauti za kiitikadi, Watanzania tu wamoja kwa upendo na mshikamano miongoni mwetu!.

"Mahali ni Pazuri..Ndugu Wanapokaa...

My Take:
Wanabodi hivi kama ushirikiano, upendo, amani na mshikamano unaofanyika misibani kama ungepelekwa mpaka Bungeni Dodoma, Jee Tanzania tungekuwa wapi?.

Rip Jerry Solomon Sumari!.Thanks kwa Upendo, Amani, Ushirikiano na Mshikamano!

Pasco.
Update:
Ratiba imetolewa.
1. Misa kesho saa 2:00 Msasani Lutheran
2. Saa 5 Mwili kupelekwa Karimjee
kuagwa kitaifa.
3. Mwili kurudi kulala nyumbani.
4. Jumapili asubuhi kusafirishwa kwa ndege kwenda Arusha.
5. Maziko Jumatatu.
 
I totally agree with you 500 percent!!

Back
Top Bottom