Mbona hawa wengine hatuwasikii...?

deny_all

JF-Expert Member
Feb 24, 2008
431
30
i68_ViongoziChadema.JPG

Naomba kuuliiza Chadema kuna makamu mwenyekiti - visiwani(Mzee Said Mzee) ambaye mwenza alikuwa Marehemu Chacha Wangwe na naibu katibu mkuu - visiwani (Hamad Mussa Yusuf) mwenza wake akiwa Mh. Zitto Kabwe.

Lakini mbona hatuwasikii hawa mabwana Mzee Said Mzee na Hamad Mussa Yusuf kila siku ni Mbowe, Dr. Slaa, Zitto .....wanakuwa kama picha tu hapo Chadema na kama wapo hawapo au ndio ule msemo watu wanasemaga chama kina wenyewe, au ni protokali ya chama ndivyo inataka hivyo naomba kueleweshwa....au ni ni watu wa kufanya majukumu maalumu?
 
Attachments

  • Viongozi Chadema.JPG
    Viongozi Chadema.JPG
    38.6 KB · Views: 119
Mkuu deny_all, labda wamekubaliana kuwa wale wa bara ndio tu wawe wanasikika na sio wa visiwani
(haya ni maoni yangu tu).
 
Kwani hata huko ccm si Makamba na JK na Chiligati? Kwa upande wa Zanzibar upinzani wenye nguvu ni CUF....So mustakabali wa siasa za Zanzibar mara zote unawashirikisha CUF, Ni politics za upinzani...Za ccm ni lazima mara nyingine ziwashirikishe viongozi wake kwenye habari kwasababu ni chama tawala...Na trust me kama ccm wakipigwa chini the story could be the same kwasababu ni wazi kuwa ccm ya bara na ya Zanzibar ni ccm za tofauti kabisa.
 
Lakini nafasi walizonazo ni za kitaifa......sio nafasi za kuzungumzia tu Zanzibar ndani ya Chadema au Tanzania. Kwa maana hiyo inabidi wajitahidi kuyajua mambo ya upande mwingine wa Muungano(bara) vile vile.

Kwa mtazamo wangu naona si vyema kwa Chadema kama chama kuiga kila kitu kinachofanywa na CCM inabidi wawe tofauti kwenye mambo mengi.
 
ccm zenji na bara wanazungumzia issue za kitaifa kwa mitizamo inayofanana?
Huu muungano wenyewe kasheshe..Mmesahahu mambo ya mgombea mwenza?
Politics za Muungano ni zile zile na namna ya kudili na issue hii inategemeana na msimamo wa chama kuhusiana na Muungano.
 
deny_all, hao hata mimi sijawahi kuwasikia kabisa....aiseee hivi CHADEMA na huko Zanzibar ni moto kama ilivyo bara?? au kule ni Maalimu Seif na CUF yake ndio wanatimua vumbi tu?
 
Kwani hata huko ccm si Makamba na JK na Chiligati? Kwa upande wa Zanzibar upinzani wenye nguvu ni CUF....So mustakabali wa siasa za Zanzibar mara zote unawashirikisha CUF, Ni politics za upinzani...Za ccm ni lazima mara nyingine ziwashirikishe viongozi wake kwenye habari kwasababu ni chama tawala...Na trust me kama ccm wakipigwa chini the story could be the same kwasababu ni wazi kuwa ccm ya bara na ya Zanzibar ni ccm za tofauti kabisa.
ina maana hata tukiwapa nchi chadema mambo yao yatakuwa yale yale wanayofanya ccm?
 
Huwezi kuwasikia kwani dawa ya moto ni moto au kwa kiswaili kingine Jogoo la la shamba haliwiki mjini hivyo hawa wa kutoka Unguja huwezi kuwasikia wakiwika Upande wa pili hata Nyerere alikuwa haendi Tanga na akienda anakwenda kwa ufunguzi tu ,humuoni kuwika ,na ukiangalia zaidi Mawaziri karibu wote wa Muungano ni kutoka Bara hivyo kuwavaa watu hawa inabidi ipatikane mipini kutoka huko huko bara na ndio maana ukaona Maalim Seif huivalia njuga CCM Wahafidhina na kuwapigisha mchakamchaka hufika kuwaita wapumbavu kwa maana ya maamuzi yafanywayo na Wahafidhina. Hawezi kuja bara na kumwita au kusema Kikwete au mwengine yeyote ni mpumbavu atampa sifa yeyote ile kwani jini likujualo halikuli likakwisha. Lakini tunaona akina Mbowe na wenziwe wakiwabofya akina Kikwete na mambo yanaendelea kama kawaida...watu wanafahamiana kwenye sms au ulaji hivyo wacha waitane vya kuitana lakini wanajuana kwa vilemba.
 
Mimi nadhani kwa kiasi fulani inaonyesha udhaifu wa Chedema au wahusika wenyewe. Kuna wakati tunaona press releases zimesainiwa na Mnyika kwa niaba ya mwenyekiti, wakati kuna makamu mwenyekiti(znz) na naibu katibu mkuu(znz)......au wao muda wote wapo Zanzibar tu?

Nadhani ili chama kiwe na umoja wa kweli ni vizuri kwa wahusika kutok znz kuyajua vizuri ya Tanzania bara and vice-versa.
 
Back
Top Bottom