Mbolea feki tani 1000 yakamatwa Mbozi!!

white wizard

JF-Expert Member
May 18, 2011
8,307
13,269
Wakulima poleni sana, jitihada zenu zinakwamishwa na mfumo wa kifisadi uliopo nchini na hawana nia nzuri na nyie. Haiwezekani mtu anajipinda kulima kwa muda mrefu anakwenda kununua anapewa mbolea iliyochanganywa na majivu, matokeo yake haambulii chochote! jamani mwogopeni Mungu, kuna mbolea tani elfu moja imekamatwa leo katika ghala moja huko wilayani Mbozi na mkurugenzi wa kitengo cha ukaguzi wa ubora wa mbolea, na wanachofanya eti ni kumnyang'anya leseni! tu kweli hii ni adhabu tosha? wakiwa jukwaani ohoo kilimo kwanza kwa staili hii! nchi hii tumelogwa na nani jamani? waziri Malima anasema hayupo ofisinI hawezi kulizungumzia kwani hana uhakika nalo!

source.TBC taifa.
 
Dah! Arv feki, madawa ya kuua wadudu feki, mbolea feki!
Sijui tunaponea wapi maskini!
 
This is a genuine fake land!
Wananchi na wenyenchi wote tuko kama taa za disko, ukitubonyeza tunabadilika rangi tu.
 
Dahh.. Niende kluishi wapi kabla sijapata shinikizo la damu au magonjwa ya akili? Tanzania hii kila kitu ni bandia. Mungu wangu!!
 
Inaumiza sana! lakin hii yote ni kutojua nn maana ya maisha, kukosa utu na uzalendo kwa maslahi binafsi bila kujali adhali kwa mtu mmoja mmoja na kwa taifa zima kwa ujumla lililo kubwa ni kupunguza tamaa na kudhaminiana hatutorudishana nyuma kiuchumi kiasi hicho kama ilivyo kwa taifa letu kilimo kilimo kilimo si pa kupafanyia hivyo hapo!
 
Duh!!!!!!!!!!!! kwa nini waziri mwenye dhamana asiachie ngazi? la sivyo tuone hatua madhubuti atakazochukua kwa waliokamatwa. hivi kitendo hiki si kinaashiria kuwa huyu mtu anataka Tanzania iwe na njaa, na kwa maana hiyo anataka kuua watanzania? kwanini asihukumiwe kunyongwa hadi kufa kama zoezi la kumtwanga risasi hadharani lina ugumu?
 
Ilo la mbolea litapita tuu ila ARV fake ndo walikomaa nalo bse wakubwa linawahusu!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom